Ni ipi maana halisi ya kumkomboa Mwanamke?

Ni ipi maana halisi ya kumkomboa Mwanamke?

Mwanamke ni mwanamke na mwanaume ni mwanaume.

Mwanamke hawezi kuwa mwanaume na mwanaume hawezi kuwa mwanamke.

Tutaendelea kubishana lakini huo ndio uhalisia na haubadiliki unless Mungu aumbe ulimwengu mpya.
Ni kweli kabisa na kwa kweli hakuna anayetaka kuwa mwanaume but tuacheni na sisi tutimize ndoto zetu duniani tumeumbwa kwa kusudi na Mungu.
Ukiona mkeo ana uwezo wa kufanya kitu Cha mafanikio msupport kwa faida yake, ya familia kwa ujumla nakuapia atakupenda na kukutiii mnooo, kuliko kumgandamiza kwa uoga wa kukupita, ataigiza tu kwa muda ila siku akipata chance ndo wanakuwaga nyoka
 
Anakombolewa kutoka katika sheria kandamizi za kiutamaduni na kidini, ambazo zinamnyika haki yake mfano kwenye urithi watoto wote ni sawa kwanini mwanaume achukue kingi kuliko mwanamke, mfano wa tabia kama hizi lazima zifike mwisho

Mwanaume akichukua kingi anapeleka kwa mke wake na watoto sasa tuambieni ukweli mwanamke akipata kingi anapeleka wapi zaidi ya mnafanya kampeni mwanamke akiwa na kingi akimbie na watoto akajitawale mmeingiwa na ushetani mliorithi kutoka kwa bibi Hawa , wanaume halisi tunajua babu yetu Adam alidanyika kutoka kwa mkewe Hawa , akina Adam wa sasa hasa wa Africa hatufanganyiki , tunawaona vituko tu tutawasapoti na mambo ya msingi tu kama mpate elimu nzuri zaidi muwe vizuri kiuchumi na kimaadili ili mjenge familia hayo mnayoyaka umiliki na mjitawale , mtangongaminika

Mpaka Yesu anarudi hamtafanikiwa, Mheshimiwa Mama Samia kawapa za uso kwamba mumuogope Mungu endeleenj na shingo ngumu zenu na ibada zenu za kifreemasons na ki mamons kamwe hamtafanikiwa mtajifariji na vijisenti vyenu na mahawara zenu mbaya zaidi mnaharibu jamii hasa kwa watoto wenu kukosa malezi ya baba na mama watoto wenu wengi wanaishia kulelewa na step parent kwa ubinafsi wenu mnaona sawa HAIKUBALIKI , eti mke nae arithi ardhi ili iweje

Sio uninafsi kwa nini msiseme mume na mke warithi kwa pamoja na siku hizi serikali
Inaruhusu hati za ardhi kumilikiwa
Kwa pamoja
Mme na mke ?
 
Ni kweli kabisa na kwa kweli hakuna anayetaka kuwa mwanaume but tuacheni na sisi tutimize ndoto zetu duniani tumeumbwa kwa kusudi na Mungu.
Ukiona mkeo ana uwezo wa kufanya kitu Cha mafanikio msupport kwa faida yake, ya familia kwa ujumla nakuapia atakupenda na kukutiii mnooo, kuliko kumgandamiza kwa uoga wa kukupita, ataigiza tu kwa muda ila siku akipata chance ndo wanakuwaga nyoka
Hatukatai mwanamke kujituma lakini hizi motto zenu ni za kupeana vichwa na kiburi na kuona hakuna umuhimu wa wanaume kwenu. Ni hatari sana ukishakuwa na mawazo hayo ndani ya nyumba
 
Ni kweli kabisa na kwa kweli hakuna anayetaka kuwa mwanaume but tuacheni na sisi tutimize ndoto zetu duniani tumeumbwa kwa kusudi na Mungu.
Ukiona mkeo ana uwezo wa kufanya kitu Cha mafanikio msupport kwa faida yake, ya familia kwa ujumla nakuapia atakupenda na kukutiii mnooo, kuliko kumgandamiza kwa uoga wa kukupita, ataigiza tu kwa muda ila siku akipata chance ndo wanakuwaga nyoka
Wewe Umefanya nini?
 
Hivi unajua kuna mila ambazo hadi leo zinakeketa wanawake?
Unajua kuna maeneo hadi leo mwanamke ruhusiwi kusoma na anaozwa akiwa na miaka 6 kwa lizee la miaka 50?
Unajua kuwa wanawake wangapi wapo kwenye ndoa lakini wananyanyasika? Mume haachi matumizi akirudi kalewa anapiga kwanzia mke hadi watoto?

Hayo ni machache, msiwe mnajadili mambo ambayo hamyajui .
Kuna mada fulani ilikuja hukusu kuuzwa kwa watumwa ,ikaonekana machifu ndio walikuwa wanawauza watumwa kwa sababu walipewa zawadi ndogo ndogo, mm naomba kuuliza je kuna ngariba wa kiume ambae anakeketa wanawake? Je ktk swala zima la kukutwa na anahusika zaid kati ya kamati ya kikeni na kamati na kiumeni? Ukweli halisi wanawake ndio huwakeketa wanawake wenzio na wao ndio chanzo cha haya yooote. Kinachotakiwa hapa ni kwamba iyanzishwe elimu ya jitambue ifundishwe mashuleni ambayo itamfanya mwanamke ajitmbue yeye ni nani anatakiwa afanye nn akinyimwa uhuru wa kuendelea kimasomo afanye nn nk, lkn hawa wanaharakati wanaotaka kujikomboa wengi ni watu wazima, wengi wameshamaliza elimu ,wengi washazalishwa,wengi wanataka uhuru wa kumiliki mali sawa na mwanaume,

Tunapozungumzia mwanamke tambua ww ndio mama yetu unajukumu la kutulea na kuelimisha lkn sio kupotosha hata ufanye nn ni ngumu kuwa sawa na mwanaume kwa maaana kubwa sanaaaaaaaa. Nafikili kila mtu angekuwa ktk imani ya dini yake mambo meeengi yangekaa sawa bila kikwazo chochote, napenda kuwasilisha hoja kwenu wajumbe.
 
Ni kweli kabisa na kwa kweli hakuna anayetaka kuwa mwanaume but tuacheni na sisi tutimize ndoto zetu duniani tumeumbwa kwa kusudi na Mungu.
Ukiona mkeo ana uwezo wa kufanya kitu Cha mafanikio msupport kwa faida yake, ya familia kwa ujumla nakuapia atakupenda na kukutiii mnooo, kuliko kumgandamiza kwa uoga wa kukupita, ataigiza tu kwa muda ila siku akipata chance ndo wanakuwaga nyoka

Malalamiko yenu makuu ni mfumo wa maisha una mkandamiza mwanamke , mnasema dini , mila na desturi zinamkandamiza mwanamke na kumpendelea mwanaume . Pamoja na yote mipango yote ya kumnasua mwanamke na huo ukandamizi umuimarishe mwanamke kuwa mama bora katika familia yake , wazungu waanzilishi wa hii mipango wamefanikiwa kumkomboa mwanamke kielimu , kiuchumi na nafasi ya mwanamke katika jamii walichoshindwa ni kuyatumia maendeleo hayo mapya kwa wanawake wanayoyaita ukombozi kulinganisha na awali kuyatumia kuimarisha ndoa zao.

Dola duniani imeshikwa na wanaume na ndio hao hao wanaume wanao ongoza serikali nyingi duniani ndio wameshika mpini wa haya mabadiriko lakini ajabu facilitators wengi mnakosea katika uhamasishaji mnatakiwa mrekebishe walichokosea wenzenu wazungu ambao ndio wafadhili na waratibu wakuu kimtandao wanachowaelekeza changanyeni akili za kuambiwa na zenu ...mlete matokea chanya yaani jitahidini kuimarisha umoja wa mwanamke na mwanaume pingeni utengano kwa gharama yoyote ile .

Yapo mabadiliko mengi wanaume wanaunga mkono mfano mwanamke kukeketwa, kunyimwa elimu , kuolewa umri mdogo , nafasi za uongozi mabadiliko hata serikali ya Tanzania inatekeleza na matokeo yanaonekana , sasa mnapoanza kuhoji ya dini huko mnaanza kwenda mbali , Mungu alikuwa na sababu zake kwa nini alimuumba mwanaume kwanza halafu mwanamke akafuata , Mungu alipanga mwanamke ndie abebe mimba ya mume wake enzi za akina Sara kuzaa nje ya ndoa ilikuwa issue kubwa siku hizi kwa harakati zenu mmeshahalalisha . Facilitators sasa hivi nendeni mkawasaidie wanawake hasa wa vijijini tupo pamoja na ninyi lakini katika kujenga sio kubomoa .
 
Kinachotakiwa hapa ni kwamba iyanzishwe elimu ya jitambue ifundishwe mashuleni ambayo itamfanya mwanamke ajitmbue yeye ni nani anatakiwa afanye nn akinyimwa uhuru wa kuendelea kimasomo afanye nn nk,

Aiseee.
Sasa kwani hizo campeni dhumuni lake ni nini kama siyo hiyo? Na sio shuleni tu na mtaani pia maana wengine hawajapewa nafasi ya kwenda shule.
 
Mwanamke ni mwanamke na mwanaume ni mwanaume.

Mwanamke hawezi kuwa mwanaume na mwanaume hawezi kuwa mwanamke.

Tutaendelea kubishana lakini huo ndio uhalisia na haubadiliki unless Mungu aumbe ulimwengu mpya.
Hivi unaelewa unachoandika?
 
Kuna mwanazuon mmoja alisema eti unamkomboaje mwanamke ambaye ni lecturer then anapata uteuzi wa ubunge viti maalum eti hapo umemkomboa au umempiga teke chura ? Yulewalimu alikuwa ana vikembe vya chini chini hihihihihihi
 
Jamii inaanzia kwenye uimara wa ndoa , jamii iliyojaa ndoa zilizosambaratika zinazalisha tabaka ovu lenye mchango duni kwa jamii na taifa . Hata hapa Tanzania jamii za wahindi na waarabu na wapemba zenye kujali sana uimara wa ndoa hata kimaendeleo zipo mbele ya jamii za makabila mengine yote hapa Tz , kama unabisha itisha kongamano la wanawake wa kipemba , waarabu na wahindi halafu uwaletee huo upuuzi wa kumkomboa mwanamke ipo lugha hata Zanzibar sasa hivi inatumika na inaeleweka kauli mbiu kama usimnyanyase na kumzalilisha, kubaka mwanamke hata uarubuni wazungu waliopelekq mabadiriko huko wanatumia
Lugha nyepesi mfano sio vizuri kumkataza mwanamke kuendesha gari nk hutasikia etu uhuru wa mwanamke wa kumiliki . Uhuru ni kuleta ubinafsi , matengano mwishoe mifarakano isiyo na muafaka SEMENI MAENDELEO KWA MWANAMKE KWA FAIDA YA FAMILIA YAKE MUME WAKE NA WATOTO kwani mtapungikiwa nini ? Hata kama inatokea mwanamke ana kipato zaidi ya mwanaume kwa dunia ya sasa si amechuma akiwa akiwa ndani ya ndoa si inakuwa heri kwa mustakabali wao na watoto ? . Kuhusu manyanyaso , ulevi , uashareti ,matumizi ,
Mabaya ya vipato dawa sio mwanamke apate mali ili
Na yeye amnyanyase mwanaume ndio mafunzo ya yasiotakiwa hayo . HIVI EMAU MBONA WAKO KIMYA SANA SIKU HIZI EMAU YA AKINA MAMA KUNDYA ?;

E- Elimu
MA-Malezi
U- Umma

~Elimu ya malezi bora ya umma
 
Wanawake
3df7b43b518c4e68808883492781843d.jpeg
 
Hivi unajua kuna mila ambazo hadi leo zinakeketa wanawake?
Unajua kuna maeneo hadi leo mwanamke ruhusiwi kusoma na anaozwa akiwa na miaka 6 kwa lizee la miaka 50?
Unajua kuwa wanawake wangapi wapo kwenye ndoa lakini wananyanyasika? Mume haachi matumizi akirudi kalewa anapiga kwanzia mke hadi watoto?

Hayo ni machache, msiwe mnajadili mambo ambayo hamyajui .
Hivi n kweli wañaume hawanyanyaswi?
 
Matatizo ya unyanyasaji yapo kijijini wanaoenda kwy matasha/semina/wars ya wapo mjini wanashinda kwy viyoyozi! Ndio maana huo ukombozi ni porojo tu za wapigaji.
 
Huwa nawashangaa sana nyie watu na sijui kwanini si wakweli.

Hivi mnataka kutuambia hakuna hasara yoyote katika jamii kutokana na hizi harakati za kumkomboa Mwanamke zinazo fanywa kila uchwao ? Kama zipo kwanini hamzitaji ? Hamuoni ndiyo mnazidi kumkandamiza zaidi huyo Mwanamke kwa kumuonyesha faida ndogo sana katika hasara kubwa zaidi ?
 
Unajua kuwa wanawake wangapi wapo kwenye ndoa lakini wananyanyasika? Mume haachi matumizi akirudi kalewa anapiga kwanzia mke hadi watoto?
Hili la kunyanyasika si hoja ya msingi, sababu mwanamke anayo haki ya kuomba talaka na kuachika, akiona hili ni haki yake aoombe talaka. Kadhalika nijuavo mimi Mwanamke hawezi kuishi sehemu yenye manyayaso.
 
Hivi unajua kuna mila ambazo hadi leo zinakeketa wanawake?
Kwahiyo majibu ya kumtoa katika huu mtihani ndiyo kumfundisha ajilinganishe na sisi ?

Maana haya matatizo yake huwa mwishoni utatuzi wake mnaona ni kumfanya mwanamke awe sawa na sisi.

Swali la msingi ni je,ni kweli mwanamke hawezi kupata hadhi au heshima bila kumshindanisha na Mwanaume au kufanana na Mwanaume ?
 
Back
Top Bottom