Ni ipi maana halisi ya kumkomboa Mwanamke?

Ni ipi maana halisi ya kumkomboa Mwanamke?

Hivi unajua kuna mila ambazo hadi leo zinakeketa wanawake?
Unajua kuna maeneo hadi leo mwanamke ruhusiwi kusoma na anaozwa akiwa na miaka 6 kwa lizee la miaka 50?
Unajua kuwa wanawake wangapi wapo kwenye ndoa lakini wananyanyasika? Mume haachi matumizi akirudi kalewa anapiga kwanzia mke hadi watoto?

Hayo ni machache, msiwe mnajadili mambo ambayo hamyajui .
kuna wanaume wanauawa na kurogwa na wake zao,wanabambikiwa watoto.hao nao wanahitaji ukombozi[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Asante
kuna wanaume wanauawa na kurogwa na wake zao,wanabambikiwa watoto.hao nao wanahitaji ukombozi[emoji3][emoji3][emoji3]
mkuu kwa kukumbusha hilo.

Sisi mbona hatuna harakati za kukomboa wanaobambikiwa mimba? Au kulea watoto wasio wao🤪
 
Sasa hii isifanye uone kwamba wanawake wote wanafanya hivyo wapo baadhi wanafanya hivyo lakini kuna baadhi bado wanasimama kwenye asili yao
Ni sawa ila pia tambua ubongo wa binaadamu unakumbuka baya kirahisi kuliko jema. Hivyo huenda wapo wachache ila ndio wanawaharibia wengi.
 
Ni sawa ila pia tambua ubongo wa binaadamu unakumbuka baya kirahisi kuliko jema. Hivyo huenda wapo wachache ila ndio wanawaharibia wengi.
Ni kweli, ila ni lazima tujifunze kuwaza chanya la sivyo kila jambo tutakifanya kwa wasiwasi with negative thoughts, cha msingi ni kuweka misingi ya kuongoza familia yako tangu mwanzo hata kama mke amekuzidi elimu na mshahara kama kuna misingi mizuri ya ndoa basi ataisimamia, ila sasa wewe ukishindwa kujua nafasi yako kama mume obvious mke atachukua nafasi yako na wewe utachukua nafasi yake

Jiamini
 
Hio misingi ya ndoa nyie kama akina mama mna wajibu wa kuwaelimisha mabinti zenu mapema maana uzembe wenu ndio umepelekea kizazi kibovu sana cha mabinti wasio na nidhamu na maisha na afya zao.
 
Hili naungana na wewe. Bahati nzuri mimi natembea sana maeneo tofauti tofauti kutokana na shughuli zangu hivyo nimejionea kwa macho sio kusimuliwa.

Binafsi ni muumini wa haki sawa na sijawahi pata shida yoyote kwwnye familia yangu.
Haki sawa ukimaanisha 50-50?
 
Miongoni mwa hasara zinazotokana na hizi harakati zenu ni mwanamke kufanywa kama bidhaa, na kuonekaa si kolote si chochote zaidi ya kupata maslahi kuputia yeye, huku thamani na heshima yake ikishuka.

Kadhalika mwanamke anaona njia ys kupita iki afanikiwe ni mpaka ajilinginishe na sisi. Hapa tunasema amefanywa mjinga na kuminywa katika uwanda wa kufikiri na kutatua matatizo yake.

Tena hakufundishwa ya kuwa anapata faida moja kwa hasara mia moja, hajui kulea watoto na kuwakuza katika maadili mema.
za wewe kuogopa utashindwa kumnyanyasa akiweza kujitambua?
Haya ndiyo matatizo ya kuwa na wakimu wenu vipofu. Hakuna mwanamke mwenye kujitambua akashindana na Mwanaume, sisi tumeoa na tunaishi na wake zetu wanajitambua hasa.

Sijawahi kuwaza kushindana na mwanamke, sababu najua majukumu yangu. Sishindani na kiumbe ambaye asili na sheria zinanitaka mimi nimsamie na nimuhudumie na kuhakikisha ya kuwa haki zake anazipata.

Lingine ni hili, kama mnaona kusoma na kuwa na mali mwaname hanyanyaswi huku ni kujiongopea sababu mapenzi si mali tu.
yaani na sasa hiv hamna kitu kinarudisha maendeleo ya mwanamke nyuma kama mwanaume mwenye insecurity jaman, mmoja ameoa tu mke wake akapata kazi kwenye NGO ya UN eti anamwambia aache hiyo kazi sababu atamshinda mshahara asubiri apate serikalini ili wafanane, kweli? unaona ni sawa?
Nyinyi mmefanywa vipofu, wakimu wenu waongo na nyinyi pia mmekuwa waongo, na mpaka sasa mmeshindwa uwezo mpaka na wanyama, wanyama ambao hawako radhi kuona familia hasa watoto wao wanapotea kisa kutafuta chakula au mfano wake, tazama maisha ya nyuki na viumbe wengine katika Hayawani, kila mdudu na mnyama ana majukumu yake kukingana na maumbile na silika yake.

Mwanamke asili yake ni akae nyumbani ikitokea ametoka basi iwe dharura na dharura ikiondoka anarudi nyumbani. Kila mtu akae nafasi yake.

Madhara ya mwanamke kutoka nje ya nyumba yake ni makubwa kuliko mwanamke akikaa nyumbani, hii ni kwa wale wanao jitambua na kujua majukumu yao.

Hiyi sababu ya huyi mwanaume kuhofia kushindwa mshahara ni sababu mufkisi, Mwanaume timamu hamkatazi mke wake kufanya kazi kisa atamshinds kwa kadha, bali anamkataza asifanye kazi kwa sababu jukumu la kulea, kulisha,kuvisha,kusomesha ba kumtunza mke ni letu sisi, bali akae nyumbani alee watoto na kusimamia nyumba na mali za zetu sisi.

Sasa mnapofikia hatua mnashindwa utendaji mpaka na Hayawani mjue mna hali mbaya, yaani mpo gizani.
 
Huenda wewe una mtazamo tofauti ila kinachoonekana kwenye Campaigns za ukombozi wa mwanamke ni kama revenge plans.

Kwamba kundi la sasa la wanawake wawe empowered ili nao wawe kama wanaume meaning wawe equipped kielimu na kichumi ili wachague either kutii mamlaka ya mume au kupuuza.

Kuna msemo niliona kuna mdada kapost kwenye status yake unasomeka,,,"The more i can pay my own bills the more that i find a man more useless"...
Utaona kwa picha halisi kuwa kadri mwanamke anavyopata mamlaka ndio kadri ambavyo anakua na mentallity ya kumchukulia poa mwanaume..Mtajenga familia gani hapo?
Nikweli mkuu leo hii utawaskia wakiambizana kwamba silaha ya kumfanya mwanaume umtawale ni kumzidi kipato na kielimu.

"The more i can pay my own bills the more that i find a man more useless".hiyo quote ina maana kubwa sana
 
Asilimia kadhaa ya waliozaliwa wanaume wamefanya transition kuwa na mwonekano wa kike. Hawa wanaitwa Trans women. Ukikutana nao utadhani wanawake kabisa.

Lakni watu kama nyie mna lalamika ni sisi tunataka kujifananisha na nyie. Haya hamyaoni?
sijaona mantiki ya hoja yako iko wapi maana hao wanaobadilisha jinsia wengi wanakuwa wana hormones nyingi za kike.

Kimwili unaonekana ni mwanaume ila kihisia ni kinyume na ndio maana wanaamua kubadili jinsia kufata hisia zao
 
Hio misingi ya ndoa nyie kama akina mama mna wajibu wa kuwaelimisha mabinti zenu mapema maana uzembe wenu ndio umepelekea kizazi kibovu sana cha mabinti wasio na nidhamu na maisha na afya zao.
Asilimia 98 ya tabia ya mtoto inatokans na wazazi wote wawili, kile mnachofanya ndio mtoto anachoiga, ifike mahali wazazi wote tuwe responsible kuhakikisha aina ya maisha tunayoishi haitamletea mtoto madhara negative in future

Nina rafiki yangu yeye mume wake huwa anarudi nyumbani asubuhi au anaweza asirudi hata siku tatu na wakati mwingine akirudi amelewa anamtolea mama maneno makali na matusi juu, watoto wamekua sasa, binti yupo form six na kijana yupo form four na kipindi choote mama akmekua akipambana mwenyewe kuhakikisha watoto wanasoma na kupata mahitaji muhimu

Yule binti kuna siku alimwwambia mama yake kwamba yeye akikua mkubwa hataki kuja kuolewa kwa sababu wanaume ni wanyanyasaji na atasimama kuwatetea wamama wote wanaonyanyaswa na waume zao kama anavyofanyiwa mama yake

Yule kijana wao wa form four akisikia tu baba amegonga geti anakaa mlangoni na baba akianza tu kutukana kijana anasogea karubu anamwambia mzee naomba uingie upumzike, umekuta amani hapa tunaomba usiivuruge

Baba kwa kutokujua kwamba ile hali imewaathiri watoto, anaanza kumlaumu mama kwamba anawafunza ujeuri watoto

Back to your point, unadhani huyu binti hata akiolewa atakuwa na imani na wanaume? Kwa sababu hakuwahi kuona upendo wa baba tangu mdogo na imejengeka akilini mwake kwamba wanaume ni wanyanyasaji
 
sijataka kusoma comment za wengine ngoja na mimi niweke mawazo yangu.
juzi nimesoma article BBC inazungumzia jinsi watoto wa kike wanavyoozeshwa kipindi hiki cha COVID kwa sababu hawaendi shule, na imeonekana barani Africa wasichana wengi wanaozeshwa sana kipindi hiki. Mind you hao ni watoto wadogo. Nadhani kimjini mjini hizi harakati za kumkomboa mtoto wa kike inaonekana hazina maana kwa sababu baadhi ya watu wameshatoka kwenye malengo, sasa imekua ni fashion.
Ila tusizibeze zimetutoa mbali sana na bado kuna watoto wanahitaji kukombolewa kutoka kwenye mila potofu hasa hasa kwenye hizi nchi zetu maskini.
Naanzia hapa, hao watoto wanaolewa wakiwa na umri gani ? Wamebalehe au hawajabalehe ?

Kama wamebalehe shida iko wapi ?

Ushawahi kusikia katika BBC wakikemea suala la mwanamke kufanywa kama bidhaa, yaani leo hii club haifanyi kazi bila wanawake kuwa kama kivutio, milio ya simu kadhalika, na katika matangazoya biashara kadhalika ? Au kwa sababu huko kuna malipo na posho ? Sasa tukisema Wanaharakati na wanawake wote wenhe mlengo huo wote mazwazwa, wamekuwa kama mshumaa, mnawanufaisha watu kwa mwanga huku ukiisha na kutokomea. Leo hii mwaamke haogopewi kabisa wala aheshimiki ile heshima ya kweli.

Ndiyo maana tunasema hivi nyinyi mnashindana na sisi, lazima muumie na mtaumia sana mpaka siku mkija kujitambua na kurudi katika mstari.

Sisi ambao tunawataka mkae nyumbani tunawajali sana na kuwaheshimu mno na kuwapenda mno,kuliko hao wale walio watoa nje na kuwafanya kuwa ma "Secretary" huko maofisini na mfano wake.

Rudini kwenye asili, na hakuna jambo rahisi kama kurudi kwenye asili.
 
Nawaamkia kwa maamkizi wote watoto na wavyele.

Huu ni muendelezo wa pale nilipoishia katika mada zangu kuwahusu hawa wenzetu, wenzetu ambao ni mama zetu, dada zetu, jirani zetu, watoto wetu na wake zetu pia.

Kila siku tunasikia mikutano, matamasha, makongamano na sherehe pia ya kuwa Mwanamke amekombelewa kutoka katika dhiki na manyanyaso au anaendelea kukombolewa.

Swali langu amekombelewa toka wapi na sasa yuko wapi na ipi faida ya kukombolewa Mwanamke na hasara zake ni zipi?

Tanbihi: Hamasa hasi na mihemko hapa si mahala pake, bali hoja na bayana na upole na uadilifu hapa ndiyo mahala pake.

Karibuni sana.
Ngoja nijibu hoja zako sasa maana maoni yangu ya awali yalitokana na baadhi ya maoni ya wachangiaji.
Maana halisi ya kumkomboa mwanamke ni kumtoa kwenye mila na desturi zinazomkandamiza, zinazomnyima haki yake ya msingi kama binadamu. mfano haki ya kupata elimu, kumiliki mali,kupiga kura,kuchaguliwa kuwa kiongozi n.k

amekombolewa toka wapi? Zamani wanawake walikua hawahesabiwi kwenye sense, walikua hawapigi au kupigiwa kura, walikua hawasomi,hawamiliki mali, hawaruhusiwi kutoa maoni yao.

Sasa yuko wapi? Sasa hivi mwanamke anahesabika ni mwananchi kama wananchi wengine, yuko huru kusoma kwa ngazi zote anazotaka na kusoma masomo yote anayoyataka, yuko huru kugombea nafasi yeyote ya uongozi, yuko huru kuchagua viongozi wake,yuko huru kufanya kazi zozote halali za kumuingizia kipato, yuko huru kumiliki mali zozote anazotaka,yuko huru kutoa maoni yake popote pale anapohitaji kutoa. Kwa kifupi mwanamke wa sasa ana haki zote za kibinadamu.

Faida ndiyo nilizoeleza alipo sasa hivi.

Hasara; Nadhani kuna sehemu mwanamke anasahau yale majukumu yake ya msingi aliyopewa kuanzia mwanzo hayo kwangu mimi nadhani hayana mjadala mwanamke ni mke na ni mama.

Nadhani mwanamke aendelee kukumbushwa majukumu yake ya msingi aliyopewa na Mungu wakati huu ambapo yuko huru kuishi kama binadamu wengine.
 
jibu swali acha risala, unaona ni sawa huyo dada aache kazi kisa atamshinda mume mshahara? jibu hapo tu. kama ni dhaifu anaogopa nini kupitwa mshahara na mtu dhaifu?

Hapana sio sawa mwanaume kumwambia mke aache kazi sababu ya kuzidiwa kipato , wanaume kama hao ndio wanaochafua wanaume wote
 
Upo sahihi kabisa.

Ila hizi kampeni zinafanyika vijijini sema haionekani kwa sababu hawana smartphone wa post.

Kijijini kwetu hizi semina zilikuwa zinafika sana, hata nakumbuka kipindi nipo primary walikuwa wanakuja hadi shuleni wasichana wote tunaitwa tunafundishwa mambo kuhusu kukataa kufanyiwa vitendo vibaya kama kukeketwa, kubakwa na kukaa kimya(maana mabinti wengine wanabakwa hadi na baba zao na hawajui kama ni vibaya kufanyiwa hivyo), ukifanyiwa kitendo kama hicho inabidi useme nk.

Kwahiyo zinafanyika ni vile hazifanywi na watu maarufu ambao watakuja kupost kwenye pages zao za instagram watu waone. Ila zinafanyika sana na kwa asilimia kubwa wamefanikiwa.
Semina zilizofika kijijini ni kuhusu ukeketaji, haki elimu, na katazo la ndoa za utotoni na hizi kweli ni haki yenu kupata

Ila hii dhana ya usawa 50/50 sio tu kijijini kwamba haipo bali hata mjini huikuti na mara nyingi hii inapiganiwa na wanaharakati wa mitandaoni tu
 
Wanaume kuna mahali tumekwama au kuteleza kutimiza wajibu wetu kama viongozi wa hawa wanawake kwa mujibu wa maumbile ndio maana tumefikia hapa.....

Dunia haiwezi kubakia salama ikiwa msimamizi anataka kusimamiwa na msimamiwa.......
 
Maana halisi ya kumkomboa mwanamke ni kumtoa kwenye mila na desturi zinazomkandamiza, zinazomnyima haki yake ya msingi kama binadamu. mfano haki ya kupata elimu, kumiliki mali,kupiga kura,kuchaguliwa kuwa kiongozi n.k
Hii si maana halisi ya kumkomboa Mwanamke. Maana halisi ya kumkomboa Mwanamke ni kumuweka mahala anapostahiki.

Hivi mwanamke hawezi kumiliki mali bila kutoka kwenda maofisini au kuchanganyika na mambo mengine ?

Kupiga kura si hoja ya msingi, sababu mnaweza kupiga kura na kisiwe chochote. Mfano mimi sijawahi kupiga kura na sitakuja kupiga kura mpaka nakufa,kadhalika Wake zangu hawapigagi kura wala hawajawahi kufanya hivyo na hii si haki, sababu upigaji kura si njia sahihi ya kuchagua kiongozi.

Umeongelea kuhusu elimu, hapa bila shaka unakusudia elimu ya shule, akishasoma lengo aekimike au atafute hela ? Je wenye hela wote wamesoma mpaka hapo walipo ?

Nukta nyingine dhaifu ni hii ya kuwa kiongozi, swali je ni lazima uwe kiongozi wewe ? Je usipokuwa kiongozi mambo hayataenda na yapi yataharibika pindi ukiwa kiongozi ? Mwanamke ni kiongozi wa nyumbani kwake na watoto wake na mali za mumewe, ila si kiongozi wa jamii na watu kwa ujumla, bali yeye ni tegemeo katika kutengeneza jamii bora akiwa yuko nyumbani.
 
Ngoja nijibu hoja zako sasa maana maoni yangu ya awali yalitokana na baadhi ya maoni ya wachangiaji.
Maana halisi ya kumkomboa mwanamke ni kumtoa kwenye mila na desturi zinazomkandamiza, zinazomnyima haki yake ya msingi kama binadamu. mfano haki ya kupata elimu, kumiliki mali,kupiga kura,kuchaguliwa kuwa kiongozi n.k

amekombolewa toka wapi? Zamani wanawake walikua hawahesabiwi kwenye sense, walikua hawapigi au kupigiwa kura, walikua hawasomi,hawamiliki mali, hawaruhusiwi kutoa maoni yao.

Sasa yuko wapi? Sasa hivi mwanamke anahesabika ni mwananchi kama wananchi wengine, yuko huru kusoma kwa ngazi zote anazotaka na kusoma masomo yote anayoyataka, yuko huru kugombea nafasi yeyote ya uongozi, yuko huru kuchagua viongozi wake,yuko huru kufanya kazi zozote halali za kumuingizia kipato, yuko huru kumiliki mali zozote anazotaka,yuko huru kutoa maoni yake popote pale anapohitaji kutoa. Kwa kifupi mwanamke wa sasa ana haki zote za kibinadamu.

Faida ndiyo nilizoeleza alipo sasa hivi.

Hasara; Nadhani kuna sehemu mwanamke anasahau yale majukumu yake ya msingi aliyopewa kuanzia mwanzo hayo kwangu mimi nadhani hayana mjadala mwanamke ni mke na ni mama.

Nadhani mwanamke aendelee kukumbushwa majukumu yake ya msingi aliyopewa na Mungu wakati huu ambapo yuko huru kuishi kama binadamu wengine.
nakuabaliana na wewe kwamba hivyo vyote ulivyovitaja ni haki yake kupata as long as dhana ya usawa 50/50 haitahusika
 
Wanaume kuna mahali tumekwama au kuteleza kutimiza wajibu wetu kama viongozi wa hawa wanawake kwa mujibu wa maumbile ndio maana tumefikia hapa.....

Dunia haiwezi kubakia salama ikiwa msimamizi anataka kusimamiwa na msimamiwa.......
Lakini wanao kosea wanatakiwa warudi kwenye mstari, na sio wanawake nao wakosee kama tunavyokosea sisi. Hapa ndipo kuna hoja ya msingi.
 
Back
Top Bottom