Deogratius Ndejembi ateuliwa kuwa Makamu wa Rais

Deogratius Ndejembi ateuliwa kuwa Makamu wa Rais

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
27,978
Reaction score
63,812
Hongera kwa Deo.

Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imependekeza na kupitisha jina la Waziri wa Nishati, Deogratius John Ndejembi, kuwa mgombea wa nafasi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ndejembi anapendekezwa kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, ambaye amejiuzulu
b92030882d85c3d75a9c65a6f11db29d (1).jpeg

Je, Deogratius Ndejembi ni nani?

Deogratius John Ndejembi ni mwanasiasa wa Tanzania wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mbunge wa Jimbo la Chamwino, Dodoma.

Deogratius John Ndejembi alizaliwa tarehe 12 Julai 1983.

Elimu:
Alisoma shule ya msingi 1988–1995: Cannon Andrea Mwaka, Primary School — CPEE

kisha 1996–1998: Kigurunyembe Secondary School — CSEE/Jamhuri Secondary na

2002–2004: Merton College — ACSEE

Baadaye alisoma International Relations katika University of Lincoln na kupata Advanced Diploma kutoka Institute of Administrative Management[alisoma International Relations – University of Lincoln (2006–2009) na Advanced Diploma in Administrative Management (2009–2012)]

Siasa:
Ni mwanachama wa CCM na anaiwakilisha Chamwino Bungeni.

Tarehe 07 Julai, 2016 Hayati Magufuli alimteua Bw. Deogratius John Ndejembi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma.

Katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020 alipita bila kupingwa kwani wapinzani wake wote wa vyama vingine waliemguliwa.

Katika kura za maoni ndani ya CCM za kuwania ubunge mwaka 2020, Deogratius (Deo) Ndejembi alipata kura 422 katika Jimbo la Chamwino (wakati huo likiitwa Chilonwa). Alimshinda aliyekuwa Mbunge Joel Mwaka aliyepata kura 99.

Mwaka 2021 Samia aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI

Machi 31, 2024: Samia Suluhu Hassan alimhamisha kutoka Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu)

Tarehe 21 Julai 2024, Ndejembi aliteuliwa kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , katika mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yaliyofanywa na Samia Suluhu Hassan. Alimrithi Jerry Silaa.

Mnamo Novemba 17, 2025, Samia Suluhu Hassan, alimteua Deogratius Ndejembi kuwa Waziri wa Nishati. Kabla ya kuwa Waziri, alikuwa Naibu Waziri wa TAMISEMI.


MY TAKE;
Pipa na mfuniko.
 
Huyo Deogratius Ndejembi ni haramu kama alivyokuwa Nchimbi.

Kuanzia Samuya ,Nchimbi na sasa huyo Ndejembi ni haramu.

Siku watanzania wakifanya uchaguzi mkuu huru na wa haki ndio watapata viongozi halali hao ni wateule wa jaji Mwambengele yeye na tume yake ndio waliwapigia kura na hili hata jaji Warioba alisema tume ya Mwambengele ndio iliandaa kiitwacho uchaguzi na ikafyatua kura milioni 31 na kujitangazia matokeo.

Haramu haitakiwi kupongezwa.
 
Hongera kwa Deogratius Ndejembi
View attachment 3657631
Je, Deogratius Ndejembi ni nani?

Deogratius John Ndejembi ni mwanasiasa wa Tanzania wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mbunge wa Jimbo la Chamwino, Dodoma.

Elimu:
Alisoma shule ya msingi Cannon Andrea Mwaka, kisha Kigurunyembe/Jamhuri Secondary na Merton College.

Baadaye alisoma International Relations katika University of Lincoln na kupata Advanced Diploma kutoka Institute of Administrative Management.

Siasa:
Ni mwanachama wa CCM na amekuwa akiwakilisha Chamwino Bungeni.

Serikalini:
Kabla ya kuwa Waziri, alikuwa Naibu Waziri wa TAMISEMI.

Machi 2024:
Rais Samia Suluhu Hassan alimteua kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu).

MY TAKE;
Pipa na mfuniko.
Sawa! Inapendeza
 
Back
Top Bottom