Kama kweli Dr. Balali amefariki,Kikwete na Serikali yake walikuwa wanalingoja hilo ili watoe Hadharani Ripoti ya E&Y.Bado Hakuna Ukweli kuhusu habari za Kifo cha Dr.Balali,walio karibu nae wanatafuta Ukweli wa habari hizo.Lakini haiingii akilini kuona kwamba Ripoti ilikuwa Tayari toka Mid-November,kwa nini ichukue karibu miezi miwili ndio tuambiwe matokeo?.Kikwete na watu wake wanatufanya Watanzania wajinga,ni wazi kwamba siri zao zitawaumbua,kwa sababu Taarifa yake kwa vyombo vya Habari imeweka maswali Mengi,na ni wazi kuwa watu kama Spika Sita ni lazima wawajibike kutokana na kauli zao,kufuatia kukanusha habari hizi za Ufisadi zilipotolewa Bungeni na Dr.Slaa.Tunalisubiri Bunge la 29/Jan/08 litaanza na mambo makubwa,kwani bado ya Buzwagi na Richmond tutayasikia huko!!!