News Alert:balali Is No Longer??

Gembe

JF-Expert Member
Sep 25, 2007
2,483
159
Heshima Mbele.Kuna Taarifa ambazo nimezipata kutoka kwa Afisa mmoja Mwandamizi wa Usalama,Kaniambia Ndugu yetu Daud Balali Amefariki Dunia.Nimejaribu kuwasiliana na Mzee Mwanakijiji kasema ataweka News Update ila kakataa kuthibithisha hilo.Je ni kweli.Je hizi habari kuna mtu mwingine anaweza kuzithibitisha?
 
Gembe,
Hiyo ni wishful thinking ya afisa huyo mwandamizi. By the grace of God Balali is well and alive.
 
Balali mzima.. walianza kumchuria wiki kadhaa zilizopita. Wao waendelee kuombea kwenye ule Mbuyu wa Oysterbay pale ili afe, so far mizimu ya kwao kina balali (sijui mtu wa wapi) naona inawazidi nguvu. Ni mzima anapata nafuu tu.. hali ikibadilika taarifa zitasikika..
 
Naona wanataka kudivert issues. Uzima wa Balali ni kitu muhimu kuliko suala lingine lolote kwa wakati huu tunapotaka kujua ni nani hasa wahusika wa ufisadi. Kwani uzima wake utatusaidia sana kujua mafisadi na wahujumu uchumi; ambao kimsingi wanawayumbisha sana wasomi wetu na watumishi waadilifu wa serikali yetu.
 
Prez" amemtengua Balali kama Gavana Mkuu Kuruhusu Uchunguzi wa kina kuhusu Ubadhilifu uliogunduliwa kwnye uchunguzi uliokuw aunafanyika.Hilo ni tangu 8/01/08
 
Basi bwana kama kweli kafa, Tanzania ni kiboko. Mafisadi wametupiga tena bao la kisigino, mchana kweupeee!
 
Oh!masikini, pumzika kwa amani japo wahenga husema ni vibaya kumdai marehemu, lakini umeondoka na taarifa muhimu za mafisadi wa hela zetu, sijui kama ulipata nafasi ya kuacha wosia na vielelezo vyako!
 
nilikua nataka kuibandika nikakuta tayari...nasikia ni asubuhi ..yaani usiku kwa muda wa kule....kwa maana hiyo ..muungwana aliipata taarifa leo midnight...

kama kweli ndivyo nitaamuona muungwana wa ajabu sana kuwahi kuitisha mkutano wa kumfukuza kazi ..mtu ambaye is no more...masikini magazeti ya mchana ambayo hayajui kitu...yameandika kwa ushabiki...BALALI AFUKUZWA KAZI!!!!!...Thats what jk wants..aliona akimbilie kubreak kwanza habari ya kumfukuza kazi...ili kesho wakitangaza waseme ..aliyekuwa gavana wa ame....

lakini kichekesho kingine kama si kulinda umaarufu usiporomoke...barua yake ya kujiuzulu si alishaandika mapema tangu alipotoka ICU ...salva akasema mzee yupo mapumzikoni na nanii mpya ...so kwa sasa hawezi kushuhulikia lolote kama haligusi usalama wa taifa.....matokeo ya uvivu wake mkuu ndio yamepelekea leo kukimbizana na muda kumfukuza kazi mtu ambaye tayari....

du umaarufu tunaulinda hata kwa gharama ya kutimua mtu no more...muda wote ulikuwa wapi tulipokuwa tunaomba uchukue hatua nayeye akiwa hapahapa.....au ulikuwa ukingojea ushahidi uzame naye chini.....
 
Ebwana hizi habari ni KWELI? kama kweli unavyosema mkuu Muungwana alijua na kamfukuza mtu aliefariki.....hii ni akili kweli?

Alafu hili sakata jamani naona Balali anaonekana kama ndio alikuwa kinara.INAMAANA KIPINDI CHOOTE CHA UBADHIRIFU HUU JK ALIKUWA HAPATI MZUNGUKO MZIMA NDANI YA BOT? Na kama hapati nini kazi yake jamaa huyu JK.....Pilot?
 
Kama hii habari ni ya kweli, ninamuombea marehemu apumzike huko anapokwenda,japokuwa mapumziko yake hayatakuwa na amani. Huwezi kulitumbukiza taifa katika hujuma kubwa namna hii halafu ukapumzika kwa amani kuzimu. Ama kweli mbio za sakafuni huishia ukingoni.

Si bora tu angeita waandishi wa habari akatoboa kila kitu hata kama na yeye alihusika pengine hii ingeweza kuwa fundisho kwa next governors and presidents. Jamani hizi pesa tutaziacha hapahapa duniani. Ni vyema tukawaachia mazingira mazuri walio hai hapa tanzania.

Waandishi wa habari hebu jaribuni kuongea na mke wake mama muganda, huenda anaweza kuwamegea kidogo.

Ndio maana mimi sina imani na benno hata kama ni mtaalamu aliyetukuka katika elimu ya uchumi. Kesho na kesho kutwa atarudia yaleyale ya balali, maana waliokuwa wanashirikiana na balali bado wapo hai na wamekamata sukani. Sasa benno achague kusuka ama kunyoa.

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom