Wadada mlio na mnaoingia kwenye ndoa jifunzeni hapa

Holly Star

JF-Expert Member
Aug 25, 2018
3,118
5,475
*MAJUTO NI MJUKUU*

Dada zangu kuna kitu cha kujifunza hapa

Niliolewa na mwanaume mpole sanaaaaaa miaka mitano iliyopita, yani nikisema mpole ni mpole mno, hakunifatilia hata sikumoja, hakuniuliza nini wala nini, alinpa uhuru wa kutosha, nikiaga naenda mahali anasema nenda, hata kama narudi saa nane usuku atanifata tu maana hakuwa akipenda niendeshe gari usiku hata sikumoja, nikirud na tax ananifokea sana,,,, gari mafuta niliwekewa kila safari, vocha niliwekewa, alinikuta fresh from collage so hata kazi sikuwa nayo, akanitafutia kazi,baada ya ndoa, nikapata, na nikaanza, kuna kipindi akawa ananiambia niache gari anafeele proud kutembea na mimi kwenye gari, kifupi alinijali sana, sana sana,,,,,,,, sasa ile care yake ndio ninayoikumbuka hadi leo hii, wamama, wadada, wanandoa, kama una mwanaume anakujal mshikilie vizuri sana.

Si kwamba alikuwa hanithamini, alikuwa ananithamini sana tu, sikuwah kumfumania hata mara moja, ana likuwa muwazi sana kwangu, yani muwaz sanaaa, ofisn kwao walinijua, alipenda kunitambulisha kila kona,,,, kuna kipindi alienda south kikazi ikawa kila weekend ananitumia nauli naenda, siku zingine anakuja yeye hadi aliporudishwa huku, ni upendo wa ajabu,,

Nilichofaidi kwake tu ni kwamba alikwenda kwetu akapaona palivyo, akasema atanisaidia kujenga, alivunja nyumba ile na kumjengea mama yangu kijumba kidogo cha kumtosha mwenyewe, akamuwekea mashamba, hadi leo namkumbuka, kwao yye kazaliwa peke yake, mama yake alifariki wakati amemzaa tuu, akasema anamlea mama yangu kama mama yake, hana dada wala kaka wa kuzaliwa tumbo moja, wako wa ndugu wengine tu

NATHIBITISHA KWA KINYWA CHANGU, COMPANY ULIYONAYO INAWEZA KUBADILI MSIMAMO NA KUSHUSHA AU KUZIDISHA HESHIMA YAKO,,, company niliyokuwa nayo mimi ilikuwa ni ya kupunguza heshima kwangu na ndio iliyoniponza, staki kuiongelea sana hilo maana wengi rafiki zangu wako humu, ila kifupi tu, nilifanya ujinga mno, naujutia hadi kesho,

Nikiwa na rafiki zangu tuliandaa mtoko kwenda bagamoyo kutembea lakini tukapanga tusiwaambie waume zetu ukweli, tudanganye maana wengi wasingekubali tukapanga safari tukasema uongo kwamba ni safari za kiofisi,( mme wangu hakuwa akinifatilia oficn kabisa) basi nikamwambia ni safar ya kikazi tunaenda bagamoyo, yeye oficn kwake ni boss, so anaweza kuondoka muda wowote bila swali, basi akasema nitakufata, sitawasumbua nitakaa hotelini tu, wewe ukimaliza kikao chenu utanikuta chumbani, nakumbuka siku hiyo nilichukia sanaaa, yani sanaaaa nilichukia nikamwambia hapana tunalala wawili wawili, akasema basi sawa nenda,

Alinipa hela ya kutosha nikaenda na rafiki zangu tulikuwa group ya watu wanne tu, watatu tumeolewa mmoja bado, basi kufika bagamoyo tuli have fun sana almost three days, nikiwa kule nikakutana na kijana mmoja ambae alinipenda sana (admin naficha jina,,,, ila tumpe KELVIN) basi alikuwa kaja na marafiki zake wengine nafikir nao kuhv fun,,

Sasa kila jioni tukiiniga buffet tunakutana nae, akaanza kunitongoza nikagoma, akamfata mmoja wa rafiki zangu akaomba namba akapewa, nashangaaa usiku akanipigia simu, nikakataaa, rafiki zangu walinisisitiza sana nimkubali, kijana mzuri, handsome, nikasema no, ninae mme wangu, simtaki huyu,,,,,

Siku naondoka akaja na diary moja nzuri sana kwenye gari yetu, akaniambia unaondoka nikasema ndio unataka nini, akasema don’t be dry like this akanipa diary yake niichukue kama kumbukumbu, nikakataa nilipofika mjin mr alinifata, akanipokea akaniambia tu mke wangu toka toka uende huko, nimekuwa mpweke sana,, wkati huo sikujua kama alipiga simu ofisn kuconfirm kama ni kweli niliondoka,,, akaambiwa nimejaza AD na sio kwamba nimesafiri kikazi,,, kumbe ukweli aliujua, nashangaa mwanaume huyu hakuniuliza chochote akakaa kimya tu, ila aniliona changez, coz tulipokuwa kweny gari alinikuwa ananiangalia sanaaaaaaaa,,, nikimtazama na mimi anageuka anaangalia pembeni,
Nikamuuliza vipi, akasema nilikumiss tu mke wangu,,,, tukafika home nikaoga nilikuwa nimechoka kesho asubuh tukaondoka, kila mtu na gari yake, kufika ofic hro hakuniambia chochote kama aliwasiliana na mme wangu aliniuliza tu, umepona? Nikasema ndio akasema karibu tena, basi kazi ikaendelea,,,,,,

Baada ya siku nne tu akaja yule kaka hado oficn kwangu na alielekezwa na mmoja wa hao best zangu, alipofika nilishangaa nikamuuliza nini kimekuleta hapa akasema tuongee kwenye gari, basi nikaingia, jamani ni kama nililogwa naweza sema kweli tena, kama hamtaamin basi ila naamini ALINIROGA HUYU KAKA, maana alivyokwua akiongea nikaanza kumpenda,,, nilizidi kumpenda kupita kiasi nikaanzak uona uzuri wkae, nikaanza kumcompare na franco wangu, naona huyu amemzidi kila kitu,
baadae aliniaga akasepa, tokea pale nikaanza kumpenda kupita maelezo

KUMBUKENI CHA KWANZA FRANCO KUGUNDUA KUWA SIO MWAMINIFU ILIKUWA NI KUSEMA NAENDA BAGAMOYO KIKAZI, WAKATI OFIS HAIJUI NA NILIAGA NAUMWA,, SO HII ILIKUWA YA KWANZA ALIGUNDUA NA HAKUSEMA KITU:

Niliporud home mr akasema anaomba tutumie gari moja tu, moja tupaki, atakuwa ananipeleka kisha ananirudisha, nilimkasirikia sna nikamwambia sitaki, maana ya kuwa na magari mawili ni nini alininunulia la nini wakati alijua anaweza kunipitia, akasema nimeamua tu, mke wangu nini shida kwani, wewe nakupeleka nakurudisha kama una issue zako nitakupeleka nakuacha ufanye mimi naondoka badae nakufata nikakataa akasema sawa

Mahusiano yangu mabest zangu waliyajua vizuri sana, siku ya bithdday yangu nilipotoka nikamkuta kelvin ananisubiri nje akanichukuwa kunipeleka hotel moja hivi iko sinza, nzuri sana nikakaa kama nusu saa wakaja mabest zanu na keki,,,,

Nilibaki nashagaa, nikiwa hapo mme wangu alinipigia simu kuuliza niko wapi,, nikakimbilia chooni kupokea simu, akauliza uko wapi mama, nikasema muhimbili nimekuja kumuona mama yake rafiki yangu aanaumwa, akasema mbona sauti ina mwangwi, na kumetulia hivyo, nikasema niko chooni nakojoa, akasema mbona hukuaga, nikasema sory, ilikuwa urgently,… alichosema ni kimoja tu,,,
KUWA MAKINI NA MAAMUZI UNAYOTAKA KUYAFANYA, akakata simu

Nilikaa hapo bila hofu kabisa mbaya Zaidi nikisema nawahi nyumbani kwa mr, wananiuliza unamnyonyesha? Kaa ule raha hapa,,,, nilikaa kweli hadi saaa mbili, nikiwa hoi, akawa ameanza kunipa pombe ninywe, nilishindwa kwakweli nikaanza kunywa wine tu ambazo nazo sikuwa nikitumia zamani,

Nafika home tu namkuta mme wangu kakaa kibarazan ila kaka wa getin wakat anafungua aliniambia tu dada leo shemej ana hasira hasira sana sijui kwanini, (kijana wa getini ni ndugu yangu so yuko huru kwangu sana ) nikamuuliza kakuulizaje akasem alisema tu ikifika saa nne hujaja nisifungue geti atakuja kukufungulia yeye,,,

Tumejenga nyumba ya ghorofa basi ile naingia naongea na mlinzi kumbe yuko ghorofan ananiangalia atu mie sikumuona maaan niusiku na amekaa kwenye kono, badae ndio kaka akaniambia umeona anavyokuangalia yule kule juu, ndio nikamuona, alipoona nimemuona tu akarudi ndani,,,,,, naingia seblen tu nae aanshuka ngazi, akanifuata akanikumbatia akasema nikupokeee hand bag,,,,, kisha twende dining kuna gift yako,,,, tukaenda hadi dining, nikakuta kuna keki, akamuita dada aandae sahani alete cha champaigne, basi nikajikausha kama sio mie nikafurahi ili awe na Amani, nikashangaa mbona hasira nilizoambiwa anazo sizioni tena,,,, basi tukakata keki tukala, akaniiimbia wote na kina dada na kaka wa mlangoni kisha wakasambaa, tukapanda juu kulala, ile nafika juu tu akaniambia nina gift yako ingine,,,,,, njoo tukae hapa tuongee kidog nikupatie zawad,,, tukae sebule ya juu, ambayo inatazamana na chumba chetu,,,,, nikamwambia nisubiri basi nakuja,

Bas niliiingia ndani nikachkua simu nikamusms kelvin asinipigie maan nimefika nyumbani, hakujibu chochote kile, mme wangu akasema mbona hukuniaga ulipoenda na sio kawaida yako??? Akasema mbona hukuniambia wakati huwa unaaga, nikamwambia mgonjwa alizidiwa nikachanganyikiwa akasmea,,, KUWA MAKINI NA HAYO UNAYOTAKA KUYAFANYA, akanifata akaniambia nakupenda sana,,, jitahidi uniheshimu, usiniumize,,,nikasema sawa, akaniambia, chukuwa zawadi yako pale kwenye kikabati cha vitabu,,,, nikaenda nikakuta simu nzuriiii ya HTC ONE rangi ya gold, Niliruka sanaaaa sana nikamkumbatia.
usiku nikashangaa saa nane usiku naamka niende washroom mr hayupo kitandani, nikastuka, nikaenda washrum hayupo, nikatoka sebule ya juu hayupo, nikaja kumchungulia namuona sebul ya chini amekaa anaangalia movie, amevaa tauro tu,,,, nikashuka hadi chini, nikamuuliza unashida gani usiku huu watu wamelala wewe unaangali tv, akasema niache sina usingizi, kucheki pembeni yuko na simu yangu,,, moyo ukafanya paaaaaaaaaaaaaaa
Nikamwambia mbona umekaa na simu yangu, akasema SINA MIPAKA JUU YA SIMU YAKO MKE WANGU,,,,, nikataka kuichukuwa kwan nguvu akasema usitupende kutumia nguvu, sana utamumia,,, chukuwa simu hii hapa nenda kalale, nikakuta anakunywa wine ,, alikuwa anaangalia CD moja ambayo nilitamani kila mtu angekuwa nayo inaitwa FIND A SECRET,,, nzuri san asana sana,,,,,,,,,

Nikamwambia okay uliichukuwa yanini, akasema nilipizie basi nenda nayo yakwangu
Sikumjibu nikarudi ndani, nikaanza kupekua sms, sikukuta sms hata moja, nikajipa moyo sikujua kumbe kelvin alikuwa alirudisha majibu na alinisifia Sanaa tuliposex, mme wangu akajifowadia sms ile maana siku ananiacha kanisani aliionyesha na akasema anazo sms zote maana alienda (mtandao kampuni by admin) AKAPRINTIWA SMS NA RAFIKI YAKE, ambazo tulikuwa tunatumiana, basi nilipojiridhisha tu nikalala usingizi hauji nikaseam au katuona?

Nilipitiwa na usingizi nikalala, hali ilianza kubadilika hapo, simuelewi kabisa mwenzangu, anauchuna tu, haniuliz chochote ni kama ndani ya miezi sita niko na kelvin mambo moto moto,,

Kuna siku akanimbia mke wangu nataka kukutoa
nikamwambia wapi? Akasema nahitaji kuongea na wewe omba ruhusa kazini WAAMBIE UNAUMWA TENA,,,, nahitaji kwenda na wewe Zanzibar,,, mh nikastuka hiyo tena imetoka wapi? Nikamuuliza niwaambie tena kwani nishawahi kuomba ruhusa ya kuumwa, akasmea ah nilikosea kuongea tu, don’t mind, we omba ruhusa, niliomba tukaenda hadi zanziba, tukafikia hotelini, lakini safari ile ilikuwa ni kuongea tu,,,,,,, ananisii nitulie, kama kuna shida niseme, kama kuna tatizo tuongeee ananipenda sana,, yani aliongea kupita kiasi, nikasema sema kwani kuna nini, najikausha akasema ah moyo tu hauna amani, tukaenjoy kidogo akaninunulia madraya ya mkono ya kutumia mwenyewe nisiende salon, yani kila kitu hao tukarudi dar, kufika tu ugomvi ukaanza na kelvin kwa simu, anasema kwanini niliondoka bila kumwambia, nikamwambia nilikuwa na mme awngu, na ilikuwa ghafla, na nilikuwa so tight nisingeweza kabisa kuongea na simu, akachukia akaanzak kutuma sms za ajabu ajabu
tukiwa tumekaa seblen niko busy na simu, yangu, sina hili wala lile, franco akasema wife,,,, SIKU NIKIGUNDUA UNANIDANGANYA, NITAKACHOKUFANYA HUTOSAHAU MAISHANI KWAKO,,,, nikamwambia kwani nini, basi nikazuga hapo kimoyo moyo nikasema ntakuwa makini zaidi,

Tulikaa kama miezi miwili Amani ikiwepo kabisa nyumbani kwangu, japo sio sana, tukawa tumepanga twende kwa mama yangu, tukamsalimie yuko kigoma, tukaenda na mmewangu hadi kigoma nashangaa nimefika kigoma kelvin ananipigia simu nae yuko kigoma eti alinifanya nikasema siwezi kukuona aksema no, lazima tuonane, basi nikadanganya kuwa naenda kwa dada yangu mkubwa, mr aniruhus niende tu, akasema mie nimekuja kwenu,,,, wewe ndio mwenyej wangu, unaniacha na huyu mama naongea nae nini?

Kuna mipaka mimi kwenda kwa ndugu zako hadi uende peke yako? Nikasema hakuna, nilichokaa maana nilikuwa nimemuelekeza kelvin aje maeneo hayo, namimi huku mr akniabana twende wote ikabidi nimwambie kelvin asije,,,,,,,,
sijui hadi leo, mme wangu aliisomaje ile smsms maana nilikuwa nikituma tu naifuta, wakati tunarudi dar akaniuliza vipi, mbona ulimzuia mwenzio, kuja kwa dada yako, nikasema nani? Akasema ah, ACHANA NAYO HAYO, NIKASEMA NO, NIAMBIE UNAMAANISHA NINI? AKASEMA yaache tuendelee na mengine,,,, akaanza kuongea mengine, nilistuka kidoog ila mwenzn
angu akawa sawa tu,

Tulipofika dar, ugomvi ukaanza na kelvin kwanini nilimzimia simu, ugomvi mkubwa sana,,, nikaaendelea kuchelewa nyumbani,
kuna siku nilipigiwa simu na mama akanaimbai suz una nini nyumani kwako? Maana mumeo kaniambia niongee na wewe, nikamuuliza kuhus nini kasema wewe UNAJUA NIONGEE NA WEWE, nikamwambia mama hakuna kitu acha nitayamaliza kama yapo,,,, usiku nikamuuliza mme wangu uliongea na mama akasema yes nilikuwa namsalimia tu namjulia hali nilikosea? Akasema no hukukosea KABISA UKO SAWA

KUNA SIKU INGINE TENA NILIKUWA NIMELALA.......MIDA KAMA YA SAA NANE HIV USIKU NIKASTUKA NINI.SIJUI NIKAKUTA MWENZANGU HAYUPO KITANDANI..
NIKASTUKA NIKAINUKA NIKAAA. SASA JUU HUKU KWETU MADIRISHA YAKE NI MAKUBWA SANAAAAAAA NA HUWA SITUMII AC MAANA UPEPO WAKE MKUBWA SANAAA BAS HUWA NAKUNJA PAZIA TU KWAHIYO.MWANGA HUPENYA NDANI NIKAONA KWENYE KONA KABISA MME WANGU AMEKA JUU YASOFA KAINAMISHA KICHWA CHINI

NILIINUKA NIKAWASHA TAAA NIKAMFATA NIKAMUULIZA ANA NINI.MBONA SIMUELEWI....KABLA HAJAJIB.MACHOZ YAKAANGUKA NIKASTUKA NIKASEMA MH...FRANCO....AR YOU CRYING????KUCHEKI KOCH LIMELOWA KWA MACHOZ NA MAFUA ANALIA BILA KUTOA SAUTI.....NIKAMUINUA KICHWA NIKAONA MACH YAMEMVIMBA NI KAMA MTU.ALIEANZA KULIA ZAMAN SANA
NIKAMSOGELEA NIKAMUULIZA UNA NINI BABA???

PLEASE TELL HAKUJIBU KITU CHOCHOTE AKANISUKUMA AKASHUKA NGAZ KWRNDA CHINI..
NIKAWA NAMFATA AKANIGEUKIA AKANIONYESHA KIDOLE TU.....ISHARA NISIMFATE.......NIKABAKI NIMESIMAMA
HAKUNIJIBU AKATAKA KUNISUKUMA NIKAMWAMBIA NO....KAMA KUNA KITU TUONGEEE PLEASE KULIA SIO SOLUTION..AKASEMA HIV...NIJIBU MASWAL NITAKAYOKUULIZA...NIKASEM SAWA

AKAANZA...KWANN UNATEBEA NJE YA NDOA?,,
BAS NIKARUD JUU NIKAKAA USINGIZ UKAKATA KABISA......

NIKASEMA NO....NAMFATA NIKATOKA NIKAENDA SEBLEN CHIN NIKAKUTA HAYUPI ILA MLANGO UKO WAZI..NIKASHUKA HARAKA NIKATOKA NJE NIKAMKUTA AMEKAA ANALIA HUKU AMENG'ATA KIDOLE...NIKAMFATA NIKAMKUMBATIA..NIKAMWAMBIA NAKUPENDA
MOYO UAFANYA PAAAAAA NIKAJIAUSH NIKASEM NINI WEWE? AKASEMA SIRUDII SWALI HATABMOJA MAAN UMESIKIA.......

LA PILI.. NIPE SABABU ZA KUFANYA HIVYO...NA TATU NFANYE NINI UMUACHE KELVIN..WAKAT HUO ANAONGEA ALIKUWA NA HASIRA SANA....MACHO MEKUNDU SANAAA MISHIPA KICHWANI IMESIMAMA ANANG'ATA MENO..ANAJIPIGAVKICHWANI.......AKASEMA NIPE MAJIBUBYA MASWA YANGU HUKU ANANITAZAMA USONI
NIKASEMA HAYO NI MAWAZO YAKO..SINA MTU MIMI.......KWAMARA YA KWANZA TOKA NIOLEWE ALINIZABUA KIBAO KIMOJA KIKALI..AKASEM KWANN UNATEMBEA NJE YA NDOA..KWANN HURIDHIKI..WHAT ISBSO SPECIAL KWAHUYO JAMAA YAKO..AKANIZABU KINGINE..NIKAKIMBILIA NDANI NIKAPANDA NGAZ HARAKA MAANA ALIKUWA ANANIKIMBIZA

Nilipofika ndani nikapanda ngaz harakaharaka akanifata.mie napanda moja moja yeye mbilimbili kabla sijafika hata mlangon akanivuta akanishusha chini akasema leo nakuuwa........siwez penda mwanamke nikampa kila kitu anachotaka kisha anisaliti alinipiga sana pale chin..salama yangu ni kijana wa getin kuja kuniokoa maana nilipiga kelele kama nimekalia moto.......

Hakuongea aliponipiga nikaokolewa akaenda kwenye wine space akakaa huko akaanza kunywa wine...huku analia sana.....nikaingia chumban nikaanza kulia asbh kufika nikamkuta kalala palepale juu ya meza ya wine sikumsemesha kitu nilivaa nikaondoka kwenda kazin....sijui aliamka sangap..ila mida ya mchana akanipigia simu sikupokea..akapiga nikakata akatuma sms pokea simu mke wangu sikupkkea

Niliporud jion kaka wa getin akasema shem nae kaondoka sasa hiv toka asbh alikuwa analia tu. Kaja rafiki yake wameondoka ....sikujibu kitu nikafika......kidogo ikaingia sms kwamba nimfate samakisamaki kule mliman city nikasema siji....sijakaa sawa akamtuma mtu anifate nikaenda kufika akaniomba radhi sana mbele ya rafiki xake kwa kunipiga...yeye mwenyeer anajutia kwann alinipiga aliomba radhi sanaaaaaa nilimshangaaa kukuta nakunywa pombe wakat alikuwa hanywi nikamuuliza franco..when did you start this....yesterday.......and its becouse of you...bas aliomba radhi na wenzie wakanisihi nimsamehe tukarud home.....that day alinitia vze...lkn bado niseme kweli kelvin aliniroga jaman..

Za mwiz zilifika ambazo had leo sijui aliijuaje hotel niliyokuwa nimeenda kulala na kelvin....nawaza had leo nakaribia miaka miwil toka nimeachika sijui alijuaje franco

Ilikuwa jimamos kelvin akaniambia kuwa ameninunulia kiwanja mkuranga niende akanikabidhi....hakusema kama nitalala huko sikujipanga kuaga chochote ..nikamwambia franco naenda kwenye kikao huko mbagala akasema sawa nenda.....nikaondoka kufika huko tukakaa baa moja hiv tukala..akaenda kunionyeaha hicho kiwanja nikakitazama

Tulipomaliza kukiona akasema twende kwenye kituo chake kimoja cha mafuta mbele ya mkuranga. Wakat huo ilikuwa saa 12 jion......nikamwambia si unajua natakiwa kurud home akasema yes hatukai sana....tulipaki gar yangu nyumban kwake kawe tukaondoka na gar yake.

I was confortable coz ilikuwa full tinted ukisema uchungulie ndan unajiona sura yako unavyochungulia ndan huon kitu
Kufik huko tukatembelea kituo chake nikapaona....kelvi. alikuwa hajaoa kabisa so nilikuwa free kwake..akani introduce kwa wafanyakaz wake kama mkewe mtarajiwa..bad enough nilikuwa nikikutana na kelvin tu ananiambia toa mapete yako..na kuna siku alitaka kuzitupa alisema hazipendi ikawa ugomvi bas nikawa nazivua....

Baada ya hapo akaniambia anafeel joto nimsindikize kuna hotel moja hiv na akasema azini nami hawezi niacha nami kumuonesha ushirikiano wa kiwanja kile nikaenda ila kwa makubaliano tukimaliza tunarud nyumbani ..siku nzima sikuwa nimeongea na wale mabest zangu hata mmoja... tukaenda hotelin hukohuko mkuranga

Tukiwa hoteln pale timeshazini akaniambia leo huondoki..simu hii hapa mpigie mmeo sema unavyosema leo tunalala wote.nikalia sanaaaa akanipokonya funguo za mlangon..akasema siku nikisikia mme wako kafa ntafurah sana..hana hadhi ya kumiliki mtoto mzur kama wewe.......nililia aniruhus akagoma.....

Bas mida ya saa mbil sim ikaita kucheki ni mme wangu.......nikafungua madirisha ili mwangwi utoke nikapokea nikamwambia nimepitia msibani kuna rafiki yangu kafiwa ........akachekaaaaa akasema okay kwahiyo hurud?nikasema naweza kuchelewa sana..akasema haya mke wangu. Nakupenda nikamwamvbia nakupenda pia. Akakata simu.. hapo nilikuwa na hofu sanaaaa

Nikiwa hapo tulikuwa tumeagiza kuku wa kuchoma nje. Nikasema hatuendi kula nje walete chumbani..basi nilikaa ndani kama saaa moja baada ya kuongea na Franco akapiga tena akasa nipo hapa ulipo naomba nikuone Mara moja... Nikaastuka akasema tena unakuja au Mimi nine?.....saut ile ilikuwa kama MTU Analia.......pemben nasikia MTU anamwambia Franco utaharibu sasa....nikakata simu

Nikamuuliza klevin Franco anasema yupo hapa nilipo kuna MTU yyte ulimwambia tutakuwa hapa Leo? Kelvin akasema bwege huyo muongo anakutishia tu..mie sikumwambia MTU ila niliongea na na rachel asbh nikamwambia Leo nakuja kukupa KIWANJA ila sikusema nitakuja hapa
Simu ikaita tena nikapokea akasema Mke WANGU.

Nipo nje.....unakuja au nije? Ila saut yake kama anabana kilio....nikakata simu bila kujibu... Jaman sitakaaakusahau Siku hiiiii huwa nalia sanaaaaa hapa pia nalia ..nimekumbuka mbali

Ghafla simu ya chumban kwetu ikaita.....wote tukaogopa kupokea.........kidogo mlango wa chumban ukagongwa
Mlango ulipogongwa kelvin akauliza nani? Wakat huo Mimi Niko hoi jasho linanitoka..mail unaishiwa nguvu..nikaombaaaaaa nikasema Mungu wa uzima nitetee kwenye hili naahid nikitoka salama sitakutenda dhambi tena

Kama mnakumbuka nilikuwa kwenye purukushan za kutaka kumkimbia kelvin tulipofika..moyo haukuwa na amani kabisa Siku hiyo hiyo kelvin aliuchukua ufunguo ili nisitoroke akawa nao mlangon kukabaki hakuna kitu chochote cha kuzuia ufunguo mwingine kupita....tukasikia sauti ya muhudumu ikisema Mimi mhudumu fungua mlango
Kelvin akamfokea....kwann unasumbua wateja?.... In sharia ya wapi hii ya kumuarisha muhudum afungue mlango?...hakujibiwa...nikasikia nyayo zikitembea kama zinaondoka vile moyo ukarelax
Baada ya dk tano tu nikasikia mlangp unafunguliwa ndio nikaju kumbe na hotel huwa wana funguo spare....oh pssaaa naumia zaid mazingira niloyokutwa Nayo violet I'm crying kila ninapokumbuka haya mwenzenu roho inaniuma sana mimi

Nikiwa uchi kabisa nimekaa kwenye kona ya kitanda nimeshikilia MTO..kelvin akiwa m2pu kabisa ameganda kona ya kitanda hajui afanye ninii akashika simu anaach anainuka anakaaa anaangalia pa kukimbilia....mwisho akasema niingie uvungu wa kitanda.....rum tulochukua INA vitanda vya box vile vikubwa sana havina uvungu akatoa godoro ili niingie kupotia chaga za kitanda..

Ndipo mlango ulipofunguliwa nikiwa nimesimama natafuta pa kuitetea ndo yangu
Alianza kuingia shemej yangu ambae in askari ila alivaa kiraia badae akafata Mme WANGU mpenzi Franco.....ambae alipofika mlangon aliganda tu.... Alishikilia mlango tu akinitazama Mimi na kelvin..huku machoz yanamtoka..kamasi zinamwagika.....akaniangalia...shemej akanitazama akasema hapa ndio msibani? Kabla sijajibu kitu Shem alinipiga kibao kimoja kupitia Kitano cha bastola yake nikakwepa kikanichana mgongon juu ya bega. Nikakimbilia kwenye godoro
Juuu kwenyw kona ya kitanda nikakaaa

Shem akamvamia kelvin akaaanza kumpiga vichwa yule manager wa hotel akaa za kuzuia huku akiniambia mama vaaa tauro.......wakat huo Franco amesimama tu mlangoni anatetemeka had I unaona kabiaa anatetemeka...jasho linamtoka..badae akavua sandals alizokuwa amevaaa akasimama pale pale..muda wote huo ananitazama Mimi tu

Yule muhudum na meneja walifanikiwa kumtuliza shemej yangu...Shem akanifata akaniita KWA jina langu Mimi ............(admin wa TT plsss hide the name) akaniuliza umefanya nini? Mbona familia yetu ilikuamini na kukupenda sana.....imekuwaje umefanya hivi?....kilikupata ninii shemej yangu. Shem nae anaongea kwa kuliaa kabisa..akasema unataka ummalize Franco ukoo wake ufe?maaana kabaki peke yake..hana dada wala kaka (shem ni Mtoto wa babake mkubwa Franco)

Ghafla nilianza kuishiwa nguvu....kuanzia miguuun ganzi ikaaanza kupanda kuja mapajan badae kwenye vidole na mikono.mwisho nikasikia kizunguzungu nikakosa nguvu nikalegea kabisa na kuangukia kita ndani style ya ubavu KWA kulala..nasikia ...naona. Lkn sijui nilipatwa na kitu gani sikuweza kunyanyua mdomo..sikuweza kutikisa hata kidole kimoja mapigo ya moyo yalibadilika nalia machozi hayatoki kabisa yamekata ila jasho linanimwagika kama maji

Namuona kelvin anavaaa nguo lkn damu zinavuja puani sana badae muhudumu namuoana anavyonifunika taulo shemej anaongea kilugha na Franco kumsihi asiwe vile alivyo nikasikia akimwambia tamka chochote moyo upumue..usiwe hivyo utakufa? Ongea chochote maana toka ameniona pale alisimama mlangon hakutamka neno lolote lile na analia tu machoz na kamasi zinamtoka mimi niipo naona lkin siwez Fanya lolote.........sina nguvu na ulimi kama umekatwa...sikuwah kupata mstuko wa aina hii toka nimezaliwa..ingekuwa sio faham kuwepo naona ningekuwa nimekufa
Nakumbuka Franco alisogea mbele akanitazama KWA upole akaniambia sikustahil haya WANGU........sina nilipokosea make WANGU kustahili adhabu hii......naaapia kama niliwah kutembea nje ya ndoa toka nimekuoa BA's nice kifo cha mateso.............kwann uliamua kufanya hivi......nini kilikusibu WANGU.......akalia sanaaaaaaa kisha akasema UTANIKUMBUKA........AKakainuka akatoka shem akanitazama akasema weweeee....bahat yako.......haya endeleeni wakatoka wakatufungia mlango

Alipoondoka kelvin alinitazama alikua amwchanika mdomo na jicho moja lilikuwa jekundu sanaaaaaaa akaniambia pole......sikuweza kujibu alivaaa yeye akanivalisha nikiwa kitandani badae akampigia simu rafiki yangu mmoja aje yeye pia aliogopa KWA hali niliyokuwa Nayo' maaana mie sijui nini kilibishika nikawa nimepooza

Badae walikuja wawil wakaanxa kuninyoosha KWA kunipia piga misuli KWA mbaliii nikahisi ufahamu ila koo lilikuwa linauma na ulimi bado haukua ukinyanyuka vzr......wakanibeba had kwenye gari KWA kujikongoja nguv zimeisha kabisaaaa tukaenda hadi kwa rafiki yangu ilala.....nguv zikaaanza kuja taratibu sana nikaweza kuongea macho yakaaanza kutoka sasa nalia kama nimefiwa nawaza narudije kqa Franco niliumia sana
Badae Kelvin alituacha kwenda hsptl akatibiwe majeraha badae alipiga simu nipelekwe wakanicheki na Mimi nikapelekwa wakanishona nyuzi NNE tukarudi nyumbani KWA rachel wakawa wananifariji.....

Ilipita Siku mbili nikamfata aunt yangu anipeleke kwangu
Nikamueleza kila kitu.......alinisema sanaaaaaa nimewatia aibu...ila tukasema nisimwambie mama kwanza tukaenda wawil kufika tukaingia tukamkuta amelala anaangalia movie seblen akatupokea vzr tu .........akamkaribisha aunt akampa juice namimi akanimiminia akanikaribisha ..nilipata faraja sana badae akasema anataka kutoka so tuseme tulichofata...aunt akajieleza sanaaaaaaaa lkn Franco alianza kulia akasema shangaz niko tofaut na baadhi ya wanaume..Mimi ni mpumbavu kuliko woote ndio maana bint yako ameweza kunichezea hivi...mama yangu alikufa nilipozaliwa .nimekosa upendo wa mama nikaweka upendo WANGU woote KWA mke WANGU......nilimpa kila anachotaka mke WANGU...alinibadilikia ghafla .. Muongo..msiri.. Sijui alikosa nini..akashindwa kulinda upendo WANGU....

Alieleza mengiiii jinsi alivyokuwa akinifatilia anasema pale alielekezwa KWA njia ya simu. Alisaidiwa na best friend wake yuko mtandao wa.................... .(jina kapuni)......pia yule Shem WANGU alisaidia kujua niko wapi kwa system yao wanayotumia huko kazin kwao ndio MANA walifika anasema yeye aligundua siku nying nachepuka na hakutaka kuambiwa alikuwa akinionya tu labda nitaacha mwisho akasema hataniacha had athibitishe so Hata nisamehe kamwe
Alieleza sana jins inavyotumika kukukamata kama wakihitaji na imlicost sanaaaaa. Basi alisema nikiendelea kumuona hapa ntazid kuumia nitamfanya kitu kibaya hatasau mtanipa kesi.. Shangaz kama mmemchoka Mtoto wenu mwachen hapa ila kama mnampenda naomba nenden nae
Alikataaa kabisa nikamfata kwa magot akagoma akasema ana hasira niondoke zikiisha ataniita..tukaondoka na aunt........

Kesho yake nikapigiwa simu na mchungaj wa kanisani tulikokuwa tunaabudu niende ofcn kwake.....nilienda nikiwa mpole nimevimba macho KWA kuliaa nikamkuta Franco nae yupo huko na yule shem WANGU askari aliekuja nae mkuranga
Akaelekea KWA mchungaj kisha akasema nilimchukulia hapa...mkatubarikia hapa....namuachia hapa...tukitoka hapa atafute pa kwenda.... Kama kutakuwepo na anachodai aende mahakamani nitakutana nae huko na nitamlipa anavyodai.... Nguo zake nimeshusha KWA mama aggy ( ni mama anaefanyaga USAF kanisan na ofcn KWA pasta).akanidai funguo za gar yake...badae akasema ah gari nakuachia vingine atafanya kelvin..kama tulisaidiana nae vingine bas na huduma achangie..nwambie akutafutie pa kuishi..akujengee.......ukija nyumban utatoka maiti
Pasta alimsihi sanaaa Franco aliondoka bila kujibu chochote....pasta akasema hana jins ila atazid kuongea nae lkn pia kwa sheria za kanisan kwetu lazima nitengwe nipewe adhab KWA dhambi ya uzinzi

Nilirud kwa shangaz akasema tumpigie mama simu tumueleze mama alilia sanaaaaaaaaaaaa Alinisema sana akampigia Franco aongee nae Franco alikataa aa akamwambia mama too late and sorry sihitaj maongez juu yake

Mama alikuja toka kwake tukaenda KWA Franco......tukaambiwa kachukua likizo kaenda kupumzika south Africa.. Na hiyo safar ilikuwa twende wote na yeye alikuwaga ameniambia nifanye research tufikie hotel gani nzur..ameenda peke yake..nikaaanza kulia

Ulipita mwaka ..mzima nikiwa na kelvin baaada ya Franco kunikataaa.... Mungu akaniadhibu tena kelvin alienda kuoa UK na alioa kwa siri....nilijua baada ya ndoa yake.......nilikuwa kama kichaaaa

Nilisikia kuna mdogo wake franko amefariki ......nikaenda msibani na rafiki zangu nikaonywshwa msichana anaeishi na Franco kwa sasa... Franco kanisan kahama sijui anasali wapi kifupi haeleweki maaana nilijua nitamuona kanisan tu...mbaya zaid bint huyo nilikuwa namjua alikuwa jiran yetu na alikujaga kumasaidia aunt yake vikazi vya ndani baada ya kutoka kijijin nikasema poor franco......ameenda kukachukua kasichana kadogo kias hiki?? Aliponiona msiban alistuka ila hakunisemesha lolote ndugu baadhi walinipokea wengine walinichunit a
Najipa moyo iko Sikh nitarud kwa franco WANGU tu!

HIVI NDIVY NILIVYOACHWA NA FRANCO....admin wa TT PLSSSS WAAMBIE WASHEE ILA MAENEO MUHIMU YAFICHE KABISA KWA USALAMA WANGU..ITAWASAIDIA..KAMA MME WAKO ANAKUPENDA ...MUHESHIMU

MIE HAPA NIMEPOTEZA DIRA YA MAISHA YANGU.. FAMILIA NZIMA IMENIDHARAU MAMA KILA AKINIONA ANANISEMA....KIWANJA CHA FRANVO KIPO TU..NIMEPANGA NYUMBA YANGU NAISHI. NAKULA....LAKIN BADO SIJAKIDHI HAJA YA MOYO WANGU NAJIULIZA IKO SIKU FRANCO ATARUDI KWANGU?????? MUNGU ANAJUA

Waruhusu watumie ushuhuda huuu wajiFunze kupitia Mimi. Kama umeolewa na unaheshimiwa...

Sent using Jamii Forums mobile app
 

funzadume

JF-Expert Member
Jan 28, 2010
13,057
19,193
Najua hii story ni ya kutunga ila ina mafunzo makubwa ndani yake.

Kuna kitu nilijiapiza katika Maisha yangu kuwa sitokuja kutembea na mke wa mtu. Imenitokea mara chache kutembea na mke wa mtu ambapo roho yangu uwa inaumia sana. Sifa ya demu nayetembea nae ya kwanza ni awe single. Sitaki maumivu ya usaliti niyapeleke kwa mwanaume mwenzangu kwa kuwa mimi binafsi sitaki yanikute.

Halafu kwa wanawake wote, msiziamini hizi simu ni rahisi sana kugundulika kwa kupitia simu. Hakuna siri kwenye simu. Mbaya Zaidi kutokana na njaa zao watu wa kampuni za simu ukimpa laki 2 tu anakupa gazeti lote la mawasiliano. Najua kuchepuka kupo toka Enzi kabla ya Yesu ila mwanaume akigundua madhara yake ni makubwa sana. Wanaume uwa tuna mioyo tofauti hatusamehi kirahisi rahisi
 

SK2016

JF-Expert Member
Apr 6, 2017
7,980
13,479
Hatimaye wanaume wapole tumeonesha makali yetu.
Wanawake wengi ndiyo maana wanapenda kuolewa na wanaume wapole ili wawe huru zaidi kufanya upuuzi wao.

Pia mwanamke ukipata bahati ya kuolewa, tulia mjenge maisha na mumewe. Mtaka mengi kwa pupa, hukosa yote.

Pia ukishaolewa, hakuna mwanaume atayekupenda sana ila wanataka wapige tu wasepe maana wanajua madhara hayatawakuta bali yatamkuta mumeo tu.

Hii story nzuri sana na inafundisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

TUMBOO

JF-Expert Member
Jun 27, 2014
3,825
2,004
Ila tuongee ukweli japokua story ni yakutunga aya mambo mengi hutukuta wanawake sababu ya marafik utakuta mwanamke alikua akiwasimulia mashost zake habari za uyo franco na sisi wanawake tuna wivu mbaya sana hapo ni dili lilichezeka kuharibu ndoa....anyway ndoa nyingi za sikuiz zinashindikana sababu wanawake tunapenda kutoa maelezo yandoa zetu kwa mashost na ni kitu sio kizuri..wanawake tujifunze kua na siri hata kwa ndugu zetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 

heartbeats

JF-Expert Member
Feb 10, 2014
4,565
6,054
Ukikosea sana hapo alipokugusia mwende wote mwanaume yoyote mwenye akili timamu lazima alarm iwake kichwani mwake lazima afuatilie,anyway pole hukuwa na nia mbaya ila ulikosa uaminifu

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Chaliifrancisco

JF-Expert Member
Jan 17, 2015
21,290
61,018
Kwa ujinga huu sijui kama ntaoa. Siwezi kuvumilia upuuzi huu kama Franco ningeshatimua siku mingi sana.
 

Similar Discussions

11 Reactions
Reply
Top Bottom