Ndugulile: WhatsApp call zimeathiri simu za nje

Ndugulile: WhatsApp call zimeathiri simu za nje

Binafsi namuona huyu Waziri kama mshamba, kiherehere na Mwenye kujipendekeza tu. Hana msaada wowote wa kitaalam ktk Wizara.
Yy ni kudhibiti tu. Haongelei Kasi ya Internet, connection ya Mkonga wa Taifa wa mawasiliano ktk familia (kama Kenya), nk.

Isitoshe kupiga au kupokea Whatsapp Call/Video lazima uwe na Bando. Kwa akili yake fupi sijui bando ni bure? "Eti mapato yameshuka" Yaani kwake mapato ni bora kuliko Tanzanians Welbeing. Nchi zote zina pambana kushusha gharama za maisha kwa raia wake.

Issue kubwa hapa ni mitandao zina mu expose Mkubwa! Ni namna tu ya kuzidi kudhibiti watu.
Jamaa Ni mchimbachumvi tu .

Anadhani huko WhatsApp tunapiga bure wakati tunanuna bando

Au anadhani bando Ni kuchat na kubrauzi

Anaongea bila reasoning Wala logic .
 
Kuna watu hawastahili kupewa madaraka makubwa wanastahili kupewa nafasi za kawaida .

Maana wakipewa madaraka makubwa huaribu kwa kujitafutia ujiko maana hawana leadership skillz
 
na sim zimeharibu kabisa masanduku ya posta, tuzifungie!
 
Google walikubali na wako kwenye mazungumzo (possibly wamemshakubaliana) na kampuni za habari Australia wawalipe. FB walitingisha kiberiti waka backoff.

Nadhani waliona local innovation na innovators wengine wanachukua soko wakaona heri wakubali shari iishe.
Hii lakini ni issue nyengine na Serikali wapo sahihi.

Mfano Google unasearch lyrics pale pale kwenye search results wanakuletea matokeo ya lyrics mzima (wamecopy kwa mtu) wewe kama mtumiaji unasoma hujatembelea website ya mhusika aliehangaika kuziweka na wala humfaidishi kivyovyote mhusika, Google anafaidika hapa kwa kitu kisicho chake.

So wanachofanya Hawa jamaa iwe kwa Google News ama means nyengine wanatoa habari, na huduma nyengine bila kutolea jasho hivyo vitu then Wana bypass means za serikali kukusanya mapato kwao pamoja na kutowalipa wahusika.

Australia wameanza tu wengine soon watafuatia.
 
Hawa chalii yaani hawataki technology kabisa duh.

Paypal wamepiga chini
Youtube wamefanya maisha yawe magumu
Bloggers nao maisha magumu
Wablock sites kma Twitter na Tele
Sasa wanataka kumonitor WhatsApp calls

Wanataka kuwa kma china lakini hawana hzo hela wala allies wa kuwa support. Haya mambo yote yaliyoendelea hapa karibuni huwezi shawishi investor yoyote wa company ya tech kma Google or Facebook kuwekeza hapa hata siku moja.
 
Hii lakini ni issue nyengine na Serikali wapo sahihi.

Mfano Google unasearch lyrics pale pale kwenye search results wanakuletea matokeo ya lyrics mzima (wamecopy kwa mtu) wewe kama mtumiaji unasoma hujatembelea website ya mhusika aliehangaika kuziweka na wala humfaidishi kivyovyote mhusika, Google anafaidika hapa kwa kitu kisicho chake.

So wanachofanya Hawa jamaa iwe kwa Google News ama means nyengine wanatoa habari, na huduma nyengine bila kutolea jasho hivyo vitu then Wana bypass means za serikali kukusanya mapato kwao pamoja na kutowalipa wahusika.

Australia wameanza tu wengine soon watafuatia.
Uko sahihi. Nilikuwa namsahihisha mdau niliyemnukuu. Hizi Big Tech zimekuwa na nguvu na zipo mikononi mwa walevi wa madaraka. Kusipokuwa na regulation kwao zitageuka kuwa balaa na kutishia usalama wa nchi
 
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia, Dkt. Faustine Ndugulile amesema ukiangalia simu zinazopigwa kwenda nje au kuingia kutoka nje zimepungua.

Amesema watu huzungumza na watu wa nje kupitia mitandao kama whatsapp, skype nk hivyo ni lazima serikali ichukue hatua kurekebisha hilo.

Waziri Ndugulile amesema pia wanaangalia mfumo wa kuwawezesha kujua yanayozungumzwa katika mtandao ili kubaini matusi kejeli na utapeli unaoendelea kwa njia ya simu na meseji.

Aidha mifumo mingine ni ya kuchuja ili mtu akiweka neno tofauti inaweza kulizuia ili kama ni sms isimfikie mlengwa.

Inachekesha! Matusi, kejeli, utapeli unaoendelea unawahusu nini serikali? Waziri hana kazi kabisa!
 
Badala ya kufikiria na wao waalike wataalamu wa kutengeneza mfumo wa simu za bei chee wao wanawaza wapi pa kupata hela.

Dunia nzima inafurahia kila kukicha wabunifu walete ahueni kwa wananchi ila kwetu ni tofauti kabisa.

Hawa viongozi wangewekewa malengo kwa mwaka wameongeza nini kwa kuongeza ajira badala ya kuleta bla bla.
Sera ya mgombea kwa wapigie kura wake ni waishi kama mashetani! Unategemea nini?
Nchi zilizoendelea sera ni kurahisisha, kuboresha, kuwapa ahueni ya maisha ya kila siku katika kila nyanja!
 
Mbona viongozi waandamizi tena wasomi wanakuwa horrible kiasi hiki? Alitaka mtu atumie 50k kuwasiliana na ndugu yake badala ya kuweka bundle la 1000? Hawajui teknolojia ipo kuboresha na kurahisisha maisha ya watu.
 
Hivi unaweza kusema simu za mkononi sms zifungwe sababu shirika la posta haliingizi pesa watu hawatumi barua.

Hivi unaweza sema mabasi ya mikoani marufuku ili watu wapande train serikali iingize pesa.

Kuna kiongozi mmoja sikumbuki alikuwa waziri kipindi flani kidogo atake ku propose mambo ya M-PESA Yasiwepo maana benk zinakosa hela.

dunia inakwenda kasi sana lazima serikali ikubali mabadiliko na kukumbana nayo huwezi kuzuiya maendeleo ya watu kwa kiganja cha mkono.Busara ingetumika kama mtu akipiga whatsup charge iweje sio kuifunga.Wakumbuke kufanya hivyo watao athirika sio watanzani pekee hata watu wa nje ya nchi na serikali yenyewe ikiwemo.

Kabla ya kutoa uamuzi huu wajaribu kuchunguza nchi za wenzetu jirani na mataifa makubwa wao wanafanyaje
 
Baada ya leo taerhe 2-4-2021 Makampuni ya Simu yakiwa na nia ovu kupandisha bei za vifurushi na kufuta ofa zote.

Insemekana watu wanahamia kupiga simu kwa watsup, nako huko waziri anafanya mchakato watusp voice call ifungiwe hapa Tanganyika.

Magu alisema tutamkumbuka, nafikiri kuanzia leo tumeanza kumkumbuka.

MATAGA wameloa , maana hawaamini, walijua wapinzani pekee ndio wataadhirika na kupanda kwa bei.

Hii imechagizwa na agzo la Mh Hassan aliposema waziri wa fedha akakusanye trilioni 2 kwa mwezi, sasa mzigo unapelekwa kwenye simu, tukishazuiwa kupiga simu kwa watsup, itatulazimu kununua dakika kwa bei ghali, yaani karibuni tutarudi kuandikiana barua.

Makundi ya wasap ya umbea yanakwenda kufa soon, MITANO TENA.
 
Baada ya leo taerhe 2-4-2021 Makampuni ya Simu yakiwa na nia ovu kupandisha bei za vifurushi na kufuta ofa zote.

Insemekana watu wanahamia kupiga simu kwa watsup, nako huko waziri anafanya mchakato watusp voice call ifungiwe hapa Tanganyika.

Magu alisema tutamkumbuka, nafikiri kuanzia leo tumeanza kumkumbuka.

MATAGA wameloa , maana hawaamini, walijua wapinzani pekee ndio wataadhirika na kupanda kwa bei.
Mataga wanataka kuturudisha kwenye zama za ujima, sijawahi kuona daktari wa ajabu kama ndungulile, huyu alitakiwa awe mganga wa kienyeji
 
Back
Top Bottom