Ndugulile: WhatsApp call zimeathiri simu za nje

Ndugulile: WhatsApp call zimeathiri simu za nje

Binafsi namuona huyu Waziri kama mshamba, kiherehere na Mwenye kujipendekeza tu. Hana msaada wowote wa kitaalam ktk Wizara.
Yy ni kudhibiti tuu. Haongelei Kasi ya Internet, connection ya Mkonga wa Taifa wa mawasiliano ktk familia (kama Kenya), nk.

Isitoshe kupiga au kupokea Whatsapp Call/Video lazima uwe na Bando. Kwa akili yake fupi sijui bando ni bure? "Eti mapato yameshuka" Yaani kwake mapato ni bora kuliko Tanzanians Welbeing. Nchi zote zina pambana kushusha gharama za maisha kwa raia wake.

Issue kubwa hapa ni mitandao zina mu expose Mkubwa! Ni namna tu ya kuzidi kudhibiti watu.
 
Hivi hili habari ya Mh Waziri inatouti na hii?

Haina tofauti sana ila sababu wazo limetolewa na mbongo basi halina maana ila wangesema mizungu lingekua la maana.
 
Ndio hapo sasa,inashangaza kiongozi anashindwa kuongelea masuala ya maendeleo kwa jamii badala yake anabaki kuongelea teknolojia za zilizobuniwa na kuanzishwa na nchi za wenzetu.

Eti na hapo wanataka maendeleo kupitia technolojia hizo.

Ubinafsi utafika mwisho tu.
Sasa wewe hushangai gari atengeneze Mjapani na huko unalininua kwa dola 3000 au 4000 ukuliingiza utalia kwa kodi watakayokubandika, utadhani wametengeneza wao.
 
Ndungulile hili amekosea sana innovation and technology watu wanabuni ili kupunguza gharama za huduma vilevile kuongeza ufanisi sasa unavyozuia innovation binafsi nashindwa kumuelewa kabisa. Huenda hafahamu yupo kwenye wizara gani
 
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia, Dkt. Faustine Ndugulile amesema ukiangalia simu zinazopigwa kwenda nje au kuingia kutoka nje zimepungua...

Serikali inataka kuweka mfumo wa kutoza kodi simu za whatsapp zinazokwenda na kutoka nje ya nchi. Waziri Ndugulile amesema siku hizi watu wakitaka kuwasiliana na ndugu/jamaa zao nje ya nchi wanatumia whatsapp call badala ya simu za kawaida na hivyo kuikosesha serikali mapato.

Kwa mfano mtu akiunga bundle la internet la TZS 1,000/= anaweza kupigia ndugu zake wengi waliopo nje ya nchi na bado akabaki na bundle la kuperuzi mitandaoni. Lakini akitumia TZS 1,000/= kupiga simu za kawaida nje ya nchi hataweza kuwasiliana hata na mtu mmoja. Kwahiyo Ndugulile anaona dawa ni kuanza kutoza kodi simu za whatsapp.

My Take:
1. Kazi ya serikali ni kuboresha huduma kwa wananchi. Kwa hiyo wananchi wanapopata unafuu wa huduma serikali inatakiwa kufurahi. Serikali iliyosikitika kuona watu wanatumia gharama nafuu kuwasiliana na ndugu zao nje ya nchi ni serikali ya ajabu.

2. Serikali iache kuchuma mahali ambapo haijapanda. Whatsapp sio product ya serikali. Mark Zukerberg ameinvest teknolojia, ubunifu na fedha nyingi, lakini ameruhusu watu wapige simu bila kulipia kodi. Serikali ambayo haijakuwekea hata profile picture inataka kukutoza kodi. Upuuzi.
Ni kama serikali imeanza kuzoea kuchuma mahali ambapo haijapanda. Hata ukiagiza gari nje ya nchi unaweza kulipia $5,000 kwa Mjapani aliyetumia muda wake, nguvu na teknolojia kubuni gari hilo. Lakini likifika bongo serikali ambayo haijachangia hata tairi moja inakudai kodi 15M.

3. Serikali isijaribu kushindana na teknolojia. Hakuna aliyewahi kushindana na teknolojia akashinda. Serikali ikitaka watu walipie kodi simu za Whatsapp, watu watatumia application zingine kupigia simu ndugu zao, kama vile Viber, Talkhome, Yola, Dingtone, TalkU etc. Na bado kila siku zinabuniwa nyingine mpya. Serikali haiwezi kutoza kodi zote.

4. Serikali iache kutafuta vyanzo rahisi vya mapato vinavyomuumiza mwananchi. Mauritius inaingiza Trilioni 10 kupitia utalii wa fukwe peke yake, sisi tunaingiza Trilioni 1.7 kwa utalii wote kuanzia mbugani, mlima, hadi fukwe. Kwanini tusiwekeze zaidi kupata pato kubwa badala ya kuhangaika kutoza kodi simu za whatsapp?

Malisa GJ.
 
Huu ni ukosefu wa maarifa au kutafutana ubaya!

Screenshot_20210310_234723.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unapofosi kiungo kingine tofauti na kichwa kitumike kufikiri matokeo yake ndio haya. No offense.
 
kwa serikali ya ambayo imeshindwa kutengeneza au kuunda vitega uchumi vyake au kiwanda cha kufuma toilet paper na kutatua changamoto za maji na umeme kwa miaka 60.

Kamwe haitoweza kupambana na technology eidha wakubali au wakatae watu wataendelea kutumia data kwa mawasiliano na hawatoweza kudhibiti technology ambayo inakuwa kila siku ukichangia sio ya kwao.

Sasa Badala ya kuboresha maisha ya mwananchi kwa kuboresha huduma za mawasiliano wao ndio wanakaza kwa kisingizio cha kodi.
Ukikaba huduma za mawasiliano utapata hasara mara mbili kwenye sekta mbalimbali sababu mawasiliano ndio kila kitu kwenye ulimwengu wa sasa.
Kila kitu kinahitaji mawasiliano.

Na huo mfumo watakaoweka ndio mapato yatapungua mara mbili zaidi sababu wananchi watatafuta njia nyingine.

Hawa politicians huwa wanafikiria kwa kutumia nini mbona wanafanya mambo ya ajabu na ya kitoto kama nchini wanaishi peke yao na familia zao?

Huu ni mfano hai kwanini africans ni watu wa hovyo na masikini.
Haya mambo yanatia hasira sana.
 
Roho mbaya tena za kutisha zimewatala sana.
Mh hajiulizi kwanini gharama za kupiga simu Tz kutokan nje ni kubwa kuliko EAC na SADC kwa ujumla

Kwanini Watanzania wanendekeza roho za korosho kama hizi, yaani anaona kulipia bundle haitoshi lazima yawepo mapato mengine kwa maana gharama zaidi kwa watumiaji.

Mambo kama haya yanafanya kila taasisi, shirika au kampuni inayokuja EAC kuweka kambi Nairobi.

Tunakuwa vituko tuu duniani kila siku na kila nyanja

JokaKuu
 
Back
Top Bottom