Ndugulile: WhatsApp call zimeathiri simu za nje

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia, Dkt. Faustine Ndugulile amesema ukiangalia simu zinazopigwa kwenda nje au kuingia kutoka nje zimepungua.

Amesema watu huzungumza na watu wa nje kupitia mitandao kama whatsapp, skype nk hivyo ni lazima serikali ichukue hatua kurekebisha hilo.

Waziri Ndugulile amesema pia wanaangalia mfumo wa kuwawezesha kujua yanayozungumzwa katika mtandao ili kubaini matusi kejeli na utapeli unaoendelea kwa njia ya simu na meseji.

Aidha mifumo mingine ni ya kuchuja ili mtu akiweka neno tofauti inaweza kulizuia ili kama ni sms isimfikie mlengwa.

 
Badala ya kufikiria na wao waalike wataalamu wa kutengeneza mfumo wa simu za bei chee wao wanawaza wapi pa kupata hela.

Dunia nzima inafurahia kila kukicha wabunifu walete ahueni kwa wananchi ila kwetu ni tofauti kabisa.

Hawa viongozi wangewekewa malengo kwa mwaka wameongeza nini kwa kuongeza ajira badala ya kuleta bla bla.
 
Hizi taasisi zimejaa wazee wenye mawazo ya miaka ya 47. Hovyo kabisa ndio maana mpaka leo hata vitu muhimu kama paypal yanazuia. Majinga majinga tu.

Yaanacha kuwaza mambo ya maana ya kuturahisishia maisha yenyewe kazi yao kutia ugumu.
 
Nadhani mpaka hapo tumeshaelewana,

Lengo la Serikali ya wanyonge ni kuhakikisha inaongeza wanyonge zaidi, haitaki watu wapate urahisi sehemu yoyote,

Hakika siku ikisikia wanyonge wengi wameanza kula Milo mitatu kwa siku lazima ije na lake jambo hata kama ni kuleta nzige ili tu kuhakikisha wanyonge wa kugawiwa T-shirt na kuhudhuria mikutano yao wapo wa kutosha.
 
Mafanikio ya viongozi wetu Ni kuona watanzania wanaumia.
Ni kiongozi yupi amebuni kitu kilichofanya Maisha yetu yakawa nafuu?
Kwenye DStv hatuoni itv
Nyumba za Kimara Mbezi
Mishahara imeongezeka
Uchaguzi ulikua wa wazi na haki
Mahindi yanauzika
Korosho usiseme
 
Kuna mambo ya kitaifa ya msingi ya kujadili kama Kutafuta soko la mahindi wanajadili WhatsApp!!

Sent from my SM-G955F using JamiiForums mobile app

Ndio hapo sasa,inashangaza kiongozi anashindwa kuongelea masuala ya maendeleo kwa jamii badala yake anabaki kuongelea teknolojia za zilizobuniwa na kuanzishwa na nchi za wenzetu.

Eti na hapo wanataka maendeleo kupitia technolojia hizo.

Ubinafsi utafika mwisho tu.
 
Binafsi namuona huyu Waziri kama mshamba, kiherehere na Mwenye kujipendekeza tu. Hana msaada wowote wa kitaalam ktk Wizara.
Yy ni kudhibiti tu. Haongelei Kasi ya Internet, connection ya Mkonga wa Taifa wa mawasiliano ktk familia (kama Kenya), nk.

Isitoshe kupiga au kupokea Whatsapp Call/Video lazima uwe na Bando. Kwa akili yake fupi sijui bando ni bure? "Eti mapato yameshuka" Yaani kwake mapato ni bora kuliko Tanzanians Welbeing. Nchi zote zina pambana kushusha gharama za maisha kwa raia wake.

Issue kubwa hapa ni mitandao zina mu expose Mkubwa! Ni namna tu ya kuzidi kudhibiti watu.
 
Hizi taasisi zimejaa wazee wenye mawazo ya miaka ya 47. Hovyo kabisa ndio maana mpaka leo hata vitu muhimu kama paypal yanazuia. Majinga majinga tu.

Yaanacha kuwaza mambo ya maana ya kuturahisishia maisha yenyewe kazi yao kutia ugumu.

Yote hayo yana mwisho wake.
 
Back
Top Bottom