Ndugu yangu nimemtafutia kazi mshahara laki 3, anaikwepa, nimefowadiwa meseji zake anadai ninamnyanyasa. Nifanye nini?

kamaliza chuo mwaka juzi ila hadi sasa hana shughuli, alikuja hapa mjini pasaka mwaka jana ila nikamwambia abaki baki ajiskie huru hasa ukizingatia nyumbani kwangu kuna vyumba vya nje kwa hio haikuwa taabu kumuhifadhi. sina ubaya wala hila, mimi kila wiki huwa nampa 50 kwajili ya matumizi, mama yake ana mchango mkubwa kwangu, kuna kipindi nikiwa chuoni nikitikisika kiuchumu mama yake alikuwa ni msaada kwakweli, kwahio ni kama narudisha fadhila tu, hata hio 50 hainipi mawazo nikianza kumfikiria mama yake.

alikuwa ananiambia ana apply kazi serikalini lakini kwa hali ilivyo nilimwambia ajira ziekuwa ngumu hivyo nimtaftie, ni kama mara 2 hivi nilitaka kumsaidia mchongo ila alikuwa anakazia kwamba kuna interview anakaribia kuitwa.

Basi mimi nikaamua nimtaftie kazi sehemu ya mtu tunaejuana, tuna undugu kwa mbali, sehemu ile kazi huwa ni jumatatu hadi ijumaa saa 1 na nusu hadi saa 12 jioni.. na jumamosi huwa ni saa tatu hadi saa saba hivi.

Mshahara ni laki 3 na kitu ila haujazidi 350k, kila jumamosi kuna posho ya weekend, nadhani itakuwa kti ya elf 10 hadi 15

Sasa nilipompa hii habari ni kama hajaichukulia vizuri, alipoanza kuniambia nisubiri subiri kuna interview anaisikilizia nikamwambia wala asiwe na hofu, akiitwa kwenye interiew ataenda ila hii kazi inabidi aianze,, kiukweli kwa jinsi alivyochukulia hisi suala ni wazi kabisa ni kama vile haitaki.

Jana ndio nimefowadiwa mesej screenshot analalamika kwamba namfanyia manyanyaso kwamba kazi ina mda kidogo wa kupumzika, malipo kidogo, n.k.
Mrudishe kijijini kwanza mpaka akili ikae sawa. Unampa laki 2 kwa mwezi, ndio màna anakataa kazi ya laki3
 
Huyo ndugu yako kaona kheri apate laki 2(50 kila wiki unayompa) kwa mwezi bila kuitolea jasho kuliko laki 3 ya kuienyea huku akisubiria interviews zake. Hivi unadhani husingekua unampa hiyo 50 kila wiki angekuringia?
 
Tatizo limeanzia kwenye hiyo 50 ya wiki. Yaani hiyo ni uhakika, halipii kodi, umeme, maji, nauli, chakula nk.
Ana uhakika wa 200k ambayo hata anayepokea 500k kwa mwezi anaweza kushindwa kubaki nayo (kama anajitegemea)

Jaribu kumwekea vikwazo vya kiuchumi apate akili.
 
Wewe unampa elfu 50 kila wiki unategemea awe na njaa ya laki 3. Huyo haukutakiwa kumpa hela kila wiki,ungemuonyesha maisha yalivyo magumu
 
Inauma ila no way, asubuhi ya leo rafiki yangu anaomba hata nikisikia kazi za ulinzi wa nyumba ya mtu halafu ni mdada dah nilijisikia vibaya sana

Halafu kuna kakiumbe kamoja kanakataa kazi, world is not fair anymore
Huyo dada leo ana bahati,em njoo pm tuupange mchongo wa yeye kuajiriwa 'MAHALA"
 
Kamaliza chuo mwaka juzi ila hadi sasa hana shughuli, alikuja hapa mjini pasaka mwaka jana ila nikamwambia abaki baki ajiskie huru hasa ukizingatia nyumbani kwangu kuna vyumba vya nje kwa hio haikuwa taabu kumuhifadhi. Sina ubaya w
Rudisha kijijini hiyo ng'ombe ilienda chuoni kukua! Vijana wa siku hizi kazi hawawezi aisee! Kwani mkuu ni kazi gani hiyo? Na mimi napita changamoto kama yako, nina toto la sister kichwani hazimo eti linataka nilitafutie kazi za ofisini. Nikaliambia ujinga sifanyi shule ulichemka mwenyewe hizo kazi za ofisini utaweza?

Nikalipeleka VETA limesomea ufundi wa umeme sasa hivi tena halitaki kufanya kazi za kuongeza ujuzi kwa kujishikiza kwa mafundi linasubiri interview za kwenye miradi. Hizi mkuu ni ng'ombe
 
Rudisha kijijini hiyo ng'ombe ilienda chuoni kukua! Vijana wa siku hizi kazi hawawezi aisee! Kwani mkuu ni kazi gani hiyo? Na mimi napita changamoto kama yako, nina toto la sister kichwani hazimo eti linataka nilitafutie kazi za ofisini. Nikaliambia ujinga sifanyi shule ulichemka mwenyewe hizo kazi za ofisini utaweza? Nikalipeleka VETA limesomea ufundi wa umeme sasa hivi tena halitaki kufanya kazi za kuongeza ujuzi kwa kujishikiza kwa mafundi linasubiri interview za kwenye miradi. Hizi mkuu ni ng'ombe
Pole sana
 
Kamaliza chuo mwaka juzi ila hadi sasa hana shughuli, alikuja hapa mjini pasaka mwaka jana ila nikamwambia abaki baki ajiskie huru hasa ukizingatia nyumbani kwangu kuna vyumba vya nje kwa hio haikuwa taabu kumuhifadhi. Sina ubaya wala hila, mimi kila wiki huwa nampa 50 kwajili ya matumizi, sifanyagi hivi kwa ndugu wengine ila kwa kuwa yeye mama yake alikuwa akinisaidia mara kwa mara kiuchumi nilipokuwa chuoni, basi huwa ni kama narudisha fadhila tu na hata hiyo 50 haijawahi kunipa mawazo kumpa.

Alikuwa ananiambia ana apply kazi serikalini lakini kwa hali ilivyo nilimwambia ajira zilekuwa ngumu hivyo nimtaftie, ni kama mara 2 hivi nilitaka kumsaidia mchongo ila alikuwa anakazia kwamba kuna interview anakaribia kuitwa.

Basi mimi nikaamua nimtaftie kazi sehemu ya mtu tunaejuana, tuna undugu kwa mbali, sehemu ile kazi huwa ni jumatatu hadi ijumaa saa 1 na nusu hadi saa 12 jioni.. na jumamosi huwa ni saa tatu hadi saa saba hivi.

Mshahara ni laki 3 na kitu ila haujazidi 350k, kila jumamosi kuna posho ya weekend, nadhani itakuwa kati ya elf 10 hadi 15

Sasa nilipompa hii habari ni kama hajaichukulia vizuri, alipoanza kuniambia nisubiri subiri kuna interview anaisikilizia nikamwambia wala asiwe na hofu, akiitwa kwenye interiew ataenda ila hii kazi inabidi aianze, kiukweli kwa jinsi alivyochukulia hisi suala ni wazi kabisa ni kama vile haitaki.

Jana ndio nimefowadiwa meseji screenshot analalamika kwamba namfanyia manyanyaso kwamba kazi ina muda kidogo wa kupumzika, malipo kidogo, n.k.

Hapo unajenga CV yako, unajenga connections, ubobezi.

Ni rahisi kupata kazi nyingine nzuri ukiwa kazini. Bora kuliko kukaa nyumbani.
 
Back
Top Bottom