Ndugu yangu nimemtafutia kazi mshahara laki 3, anaikwepa, nimefowadiwa meseji zake anadai ninamnyanyasa. Nifanye nini?

Rudisha kijijini hiyo ng'ombe ilienda chuoni kukua! Vijana wa siku hizi kazi hawawezi aisee! Kwani mkuu ni kazi gani hiyo? Na mimi napita changamoto kama yako, nina toto la sister kichwani hazimo eti linataka nilitafutie kazi za ofisini. Nikaliambia ujinga sifanyi shule ulichemka mwenyewe hizo kazi za ofisini utaweza? Nikalipeleka VETA limesomea ufundi wa umeme sasa hivi tena halitaki kufanya kazi za kuongeza ujuzi kwa kujishikiza kwa mafundi linasubiri interview za kwenye miradi. Hizi mkuu ni ng'ombe
Mjomba maneno gani ya kashfa unayoingea hata mjomba ni mama kwahyo wewe ni mama kuwa na huruma basi
 
Kamaliza chuo mwaka juzi ila hadi sasa hana shughuli, alikuja hapa mjini pasaka mwaka jana ila nikamwambia abaki baki ajiskie huru hasa ukizingatia nyumbani kwangu kuna vyumba vya nje kwa hio haikuwa taabu kumuhifadhi.

Sina ubaya wala hila, mimi kila wiki huwa nampa 50 kwajili ya matumizi, sifanyagi hivi kwa ndugu wengine ila kwa kuwa yeye mama yake alikuwa akinisaidia mara kwa mara kiuchumi nilipokuwa chuoni, basi huwa ni kama narudisha fadhila tu na hata hiyo 50 haijawahi kunipa mawazo kumpa.

Alikuwa ananiambia ana apply kazi serikalini lakini kwa hali ilivyo nilimwambia ajira zilekuwa ngumu hivyo nimtaftie, ni kama mara 2 hivi nilitaka kumsaidia mchongo ila alikuwa anakazia kwamba kuna interview anakaribia kuitwa.

Basi mimi nikaamua nimtaftie kazi sehemu ya mtu tunaejuana, tuna undugu kwa mbali, sehemu ile kazi huwa ni jumatatu hadi ijumaa saa 1 na nusu hadi saa 12 jioni.. na jumamosi huwa ni saa tatu hadi saa saba hivi.

Mshahara ni kama laki 3 na elf 30 hivi, pia kila jumamosi kuna posho ya weekend, nadhani itakuwa kati ya elf 10 hadi 15..kuhusu chakula cha mchana na maji kipo, kinapikwa nyumbani gari inaleta ofisini.. kasoro jumamosi tu.

Hii ni fursa nzuri kwake hasa ukizingatia atakuwa na uhuru wa kutosha akijipangia sehemu yake, hasa ukizingatia bado ni kijana,.mfano hapa kwangu ni marufuku kuingiza binti, saa moja geti linafungwa, n.k.

Sasa nilipompa hii habari ni kama hajaichukulia vizuri, alipoanza kuniambia nisubiri subiri kuna interview anaisikilizia nikamwambia wala asiwe na hofu, akiitwa kwenye interiew ataenda ila hii kazi inabidi aianze, kiukweli kwa jinsi alivyochukulia hisi suala ni wazi kabisa ni kama vile haitaki.

Jana ndio nimefowadiwa meseji screenshot analalamika kwamba namfanyia manyanyaso kwamba kazi ina muda kidogo wa kupumzika, malipo kidogo, n.k.
Mtoe hapo nyumbani

Atakuletea mikosi tu
 
Mjomba maneno gani ya kashfa unayoingea hata mjomba ni mama kwahyo wewe ni mama kuwa na huruma basi
Kwani mpwa hujui unavyonipa changamoto? Wewe no ng'ombe nilikupeleka chuoni kukua! Rudi kwenu ukapambane na babako kijijini!😁😁😁😂😂😂
 
Yani elfu 50K kwa week unakaa tu nyumbani unakula maishaa alafu uniambie nikafanye kazi nilipwe 75k si bora niendelee kulalaa nikisubiri mchongo wa maana maana hela ipo 😃 😃 😃 Ukitaka aanze kazi chap USIMPE HATA 100 YA VOCHA ale na kulala bure tu.
 
Kamaliza chuo mwaka juzi ila hadi sasa hana shughuli, alikuja hapa mjini pasaka mwaka jana ila nikamwambia abaki baki ajiskie huru hasa ukizingatia nyumbani kwangu kuna vyumba vya nje kwa hio haikuwa taabu kumuhifadhi.

Sina ubaya wala hila, mimi kila wiki huwa nampa 50 kwajili ya matumizi, sifanyagi hivi kwa ndugu wengine ila kwa kuwa yeye mama yake alikuwa akinisaidia mara kwa mara kiuchumi nilipokuwa chuoni, basi huwa ni kama narudisha fadhila tu na hata hiyo 50 haijawahi kunipa mawazo kumpa.

Alikuwa ananiambia ana apply kazi serikalini lakini kwa hali ilivyo nilimwambia ajira zilekuwa ngumu hivyo nimtaftie, ni kama mara 2 hivi nilitaka kumsaidia mchongo ila alikuwa anakazia kwamba kuna interview anakaribia kuitwa.

Basi mimi nikaamua nimtaftie kazi sehemu ya mtu tunaejuana, tuna undugu kwa mbali, sehemu ile kazi huwa ni jumatatu hadi ijumaa saa 1 na nusu hadi saa 12 jioni.. na jumamosi huwa ni saa tatu hadi saa saba hivi.

Mshahara ni kama laki 3 na elf 30 hivi, pia kila jumamosi kuna posho ya weekend, nadhani itakuwa kati ya elf 10 hadi 15..kuhusu chakula cha mchana na maji kipo, kinapikwa nyumbani gari inaleta ofisini.. kasoro jumamosi tu.

Hii ni fursa nzuri kwake hasa ukizingatia atakuwa na uhuru wa kutosha akijipangia sehemu yake, hasa ukizingatia bado ni kijana,.mfano hapa kwangu ni marufuku kuingiza binti, saa moja geti linafungwa, n.k.

Sasa nilipompa hii habari ni kama hajaichukulia vizuri, alipoanza kuniambia nisubiri subiri kuna interview anaisikilizia nikamwambia wala asiwe na hofu, akiitwa kwenye interiew ataenda ila hii kazi inabidi aianze, kiukweli kwa jinsi alivyochukulia hisi suala ni wazi kabisa ni kama vile haitaki.

Jana ndio nimefowadiwa meseji screenshot analalamika kwamba namfanyia manyanyaso kwamba kazi ina muda kidogo wa kupumzika, malipo kidogo, n.k.
Nilicho-expirience kwa sasa! Baadhi ya vijana hawataki kufanya kazi hasa wale ambao wanaishi kwa watu wenye uwezo kiuchumi.

Kwa jinsi maisha yalivyo kasi, habari ya mjini ni kutafuta hela tu, na si vinginevyo!

Ndugu kama hao wasikuumize kichwa na wala wasiwe chanzo cha kuacha kuwasaidia wengine.

Cha kufanya, mkamate kwa nguvu mpeleke huko kazini, kama kushindwa ashindwe mwenyewe. Hakuna kubembelezana. Kuna watu hujifunza kwa vitendo na siyo maneno.

Huko mbeleni akikaa miaka 5 bila kupata kazi serikalini ndio atakukumbuka.

Kwanza, umefanya kosa kubwa sana la kuwa unampa hela kila wiki. Hapo unamlemaza.

Kijana apewe nyavu akavue samaki, na siyo kumpa samaki.

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom