Ndugu alisomeshwa sekondari hadi chuo na kusaidiwa kupata kazi kakata mawasiliano kabisa na familia iliyomsaidia na kumjali, ni sawa?

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,033
Bamkubwa wangu aliweza kumsomesha ndugu yake aliekuja nyumbani kwake kutoka kijijini, aliweza kumsomesha form 1 hadi chuo na kumtaftia kazi.

kijana huyo aliweza kupokelewa vizuri na kuwa sehemu ya familia, yani kuanzia bamkubwa, mke wake, watoto wao watano na wengine kwenye nyumba waliishi nae vizuri sana, walikiwa marafiki sana na mtoto mojawapo wa kiume wa bamkubwa, walisoma shule moja form 1 hadi form 6 kasoro chuoni, walikuwa mabesti sana.

sasa baada ya kumaliza chuo bamkubwa alimtaftia connection ya kazi huyo ndugu sambamba na mtoto wake, ni kazi walifanya kama miaka miwili hivi huku urafiki ukiwa safi tu, kipindi hiki bamkubwa aliwapa wote nyumba za kuishi sababu bamkubwa huwa anajenga nyumba na kuzikodisha.

sasa ikatokea ile kazi ikaisha, bamkubea akampigia connection yule ndugu yake kupata kazi shirika flan la serikali kile kipindi cha Kikwete 2015 kazi za connection, alikuwa anavuta 1.8 milion baada ya makato kila mwezi na posho si haba, kwa sasa kapandishwa daraja mshahara utakuwa mkubwa zaidi.

Kwa huyu mtoto wa bamkubwa akasema yeye ajira hataki, alianza biashara kwa kusua sua kwa miaka ile miwili ila akawa mzoefu na comnection za mzee zikamsaidia, 2019 niliweza kujiridhisha kwenye vitabu vyake na financial statements anapata faida ya milioni 30 kila mwezi baada ya kulipa mishahara, kodi na matumizi mengine, kwa sasa sijaweza kuona vitabu vyake ila sina shaka itakuwa hata 60, kwakweli biashara yake imepanuka sana na hata wafanyakazi mishahara wameongezewa si kama zamani.

kilichotokea ni kwamba tangu mwaka 2017 huyo ndugu hataki kabisa mawasiliano, hata kwenye misiba haonekani wala sherehe, kwa sasa yupo zaidi na ndugu zake wale wa kijijini.

Yeye bamkubwa alishasema hakusaidia kungoja shukrani ama kunyenyekewa, anapenda mtu awe huru, watoto nao kawaasa sana wasimjengee chuki yoyote wala kumzungumzia vibaya na ndio maana hata kwenye sherehe bado wanamualika (lakini haji)
 
Poti kila kiumbe kina serikali yake permanent na fantasy zake. Nafkiri serikali yake imeamua kujipambanua na kuonesha asili yake.

Watu hawa a dili ila wanakuonesha vile walivyo kutoka kwenye yale unayoyajua na kuyazoea kisha kupewa mapya.

Yakale yamekwisha tazama Mapya.
 
Wafadhilaka wapundaka..

BInadami sisi ni wepesi saana kusahau, nakumbuka bimkubwa wake kwa uwezo wake mdogo, huenda tungepata maishA mazuri zaidi ya tuliyopata, lakini watoto wa ndugu zake walikuwa wengi home, kinapikwa chakula as if kuna shughuli ndogo,wengine shule kawapeleka, wengine wadogo zake kabisa, sasa hivi kila mtu ana maisha yake. Hata kupiga simu tu kazi, akilalamika namwambia kuwa mpole, ulitenda kwa upendo, basi malipo yako bora yapo kwa mungu.

Ukitenda wema/ubaya unajitendea mwenyewe.
mwambie mzee avunge tu, ye alitenda wema malipo bora yapo kwa mungu, huyo aliyemsaidia hawezi kumlipa kile mungu atamlipa, ikitokea huyo aliyesaidiwa nae akotenda wema nae kajitendea mwenyewe, na anavyomlingia(ubaya) anajitendea mwenyewe na malipo yake atayakuta.


Tukitoa tusitegemee lulipwa na binadamu, sababu hata nae akikutendea mema still mungu atakulipa, hata asipokutendea mema still kwa mungu malipo yapp pale pale.


Hiyo ni kwa mujibu wa IMANI yangu.
 
Bamkubwa wangu aliweza kumsomesha ndugu yake aliekuja nyumbani kwake kutoka kijijini, aliweza kumsomesha form 1 hadi chuo na kumtaftia kazi.


Moral obligation ni personal issue, ni sawa, labda kama palikuwa na mkataba.

Nimewafanyia wema watu wengi kwenye maisha yangu, wema kweli kweli, but Men, a Human? Nisikufuru.

Take care of your Children, zikizidi katoe sadaka etc kwa watu ambao hautajisikia vibaya siku wa na kudelete.

Muangalie huyo mtu mnyonge unayemsaidia, unyonge, upole na bidii ni kwa sababu ana shida tu.
 
Moral obligation ni personal issue, ni sawa, labda kama palikuwa na mkataba.

Nimewafanyia wema watu wengi kwenye maisha yangu, wema kweli kweli, but Men, a Human? Nisikufuru.

Take care of your Children, zikizidi katoe sadaka etc kwa watu ambao hautajisikia vibaya siku wa na kudelete.

Muangalie huyo mtu mnyonge unayemsaidia, unyonge, upole na bidii ni kwa sababu ana shida tu.


Mkuu ulisema unajiondoa jamii forums mbona BADO upo?
 
Ukingoja shukrani, utakuja chelewa. 🎵🎶
Yaani tulio wasaidia waliturudia kwa mabaya zaidi,Mtoa mada hajui kwamba kama anategemea shukrani ategemee kurudiwa kwa mabaya kwa yule aliyemtendea WEMA na hiyo ndio Dunia 🤷🏼‍♀️
 
Sikiliza hiyo poem, unaweza ukapata majibu ya swali ulilouliza.
 
Kulikuw na makubaliano ya kumlipa fadhila kabla ya kumsomesha.tuanzie hapo lakini angalizo kwa ndugu wazaz na rafiki tuache tabia ya kutegemea msaada mara baada ya kusomesha watoto wetu kwasabab huo n wajibu wa mzazi,wewe ndugu na mzaz tafuta kwa juhud hasa ukiwa kijana ili uzeeni ufanye yako kwa raha na sio kulia misaada ya fedha hasa kwa wale uliowasaidia..
 
Siku zote huwa Sipendi kutoa ushauri au Maamuzi kwa Kusikiliza upande mmoja Ila Navyohisi mimi kutakuw na Tatizo mahali ambapo Mtoa mada Hajaamua kuliweka wazi.

Inawezekan kuna kitu kidog sana ambcho ht wew mtoa mada hujakichukulia uzito au kuhisi kam kinawez kutunza chuki ya kudumu kwenu kutok kw huyo Ndugu yenu ila ndo hvyo watu hutofautiana.
 
Back
Top Bottom