Ndugu yangu nimemtafutia kazi mshahara laki 3, anaikwepa, nimefowadiwa meseji zake anadai ninamnyanyasa. Nifanye nini?

Tatizo ni kwenye hiyo 50k unayompa kila wiki, ghetto la kujiachia na msosi wa uhakika, afanye kazi ya nini tena

Kazi ni kweli ndogo, muda mrefu wa kufanya kazi lakini sioni mantiki ya yeye kuona unamnyanyasa pasipo kuangalia jitihada unazoziweka ili aishi vizuri

Mkuu kama upande wako hauna tatizo lolote, usimpe chaguo, muambie aende huko ili akajue dunia inaendaje la sivyo utampoteza mazima
 
kamaliza chuo mwaka juzi ila hadi sasa hana shughuli, alikuja hapa mjini pasaka mwaka jana ila nikamwambia abaki baki ajiskie huru hasa ukizingatia nyumbani kwangu kuna vyumba vya nje kwa hio haikuwa taabu kumuhifadhi. sina ubaya wala hila, mimi kila wiki huwa nampa 50 kwajili ya matumizi, kuna kipindi nikiwa chuoni mwaka wa mwisho nilikosa kabisa ada kama laki 6 hivi, mama yake aliniokoa, hivyo mama yake ana mchango mkubwa.

alikuwa ananiambia ana apply kazi serikalini lakini kwa hali ilivyo nilimwambia ajira ziekuwa ngumu hivyo nimtaftie, ni kama mara 2 hivi nilitaka kumsaidia mchongo ila alikuwa anakazia kwamba kuna interview anakaribia kuitwa.

Basi mimi nikaamua nimtaftie kazi sehemu ya mtu tunaejuana (connection) ila pia tuna undugu pia kwa mbali, sehemu ile kazi huwa ni jumatatu hadi ijumaa saa 1 na nusu hadi saa 12 jioni.. na jumamosi huwa ni saa tatu hadi saa nane hivi.

Mshahara ni laki 3 na kitu ila haujazidi 350k.

Sasa nilipompa hii habari ni kama hajaichukulia vizuri, alipoanza kuniambia nisubiri subiri kuna interview anaisikilizia nikamwambia wala asiwe na hofu, akiitwa kwenye interiew ataenda ila hii kazi inabidi aianze,, kiukweli kwa jinsi alivyochukulia hisi suala ni wazi kabisa ni kama vile haitaki.

Jana ndio nimefowadiwa mesej screenshot analalamika kwamba namfanyia manyanyaso kwamba kazi ina mda kidogo wa kupumzika, malipo kidogo, n.k.
Mwache.
 
Unampa kila week 50,000, anakula na kulala bure hana stress in short, kama ni wewe ni me na yeye ni me jiandae atanawiri sana na atakugongea hata mkeo.
 
Back
Top Bottom