Nimekosana na rafiki yangu baada ya kumdai pesa niliyomkopesha

Jobless_Billionaire

JF-Expert Member
Aug 9, 2022
1,812
4,920
Wasalaaam, naamini mu wazima wa afya. Wale mnaojiandaa na sikukuu basi ikawe njema kwenu.

Niende moja kwa moja kwenye mada. Wiki kama mbili nyuma kuna rafiki yangu ambae tumefahamiana kutokana na kazi tunazofanya kuwa za kufanana na muda mwingine kupeana deals mbalimbali zinapotokea alipatwa na changamoto ambayo aliniomba kama nina kiasi kadhaa cha pesa nimsaidie ili aweze kutayua changamoto yake.

Kwa jinsi alivyokuwa akinieleza, inaonyesha kabisa ilikuwa ni issue serious na alitakiwa kuisolve ndani ya muda mfupi sababu aliharibu gari ya mtu na alipeleza pesa ya ku-repair. Alitoa na ahadi baada ya wiki atanirudishia pesa yangu.

Nilimueleza sina ila alinishawishi nikaona ngoja tu nimsaidie. Nikamuuliza tena, una uhakika utanirejeshea ndani ya wiki kama unavyodai? Maana mie mwenyewe nina mambo mengi ya kukamilisha yanayohitaji pesa na kuzingatia ni msimu wa sikukuu. Akala na viapo vyote unavyovifahamu. Ikabidi nimsaidie.

Baada ya week kuisha, nilijua angefanya uaminifu kunirejeshea lakini kukawa kimya. Siku ya tisa nikampigia simu, ikaita lakini haikupokelewa. Nikatuma na ujumbe wa kumkumbusha in case simu hakuisikia basi asome ajue.

Ikapita kimya siku hiyo. Siku iliyofuata nikatuma ujumbe haukujibiwa, nikapiga simu ikaita halafu ikakatwa. Nikapiga tena ikawa haipatikani, muda huo nahitaji pesa pia nifanye mambo yangu na maandalizi ya sikukuu.

Cha ajabu hakuonyesha hata uungwana wa kutuma sms kuonyesha labda alikuwa busy au muda nnaompigia labda anakuwa hayupo na simu. Nikaendelea kupambana kumpigia bila mafanikio. Nikitumia namba ngeni anapokea, ila akijua tu ni mimi anakata na kuzima kabisa simu. Nikamaindi kabisa na kumtumia sms kali ila hakujibu.

Jana katika mihangaiko ya hapa na pale tukakutana, kaanza kuleta sababu eti alikuwa anaumwa halafu hana kifurushi chochote kile ndio maana hajanitafuta. Nikamuuliza sasa mbona hata nikikupigia hupokei? Anasema huwa anakuwa kalala. Nikaona upuuzi huu. Afanye kuniambia saa ngapi nimfuate kwake nikachukue hela maana nmekwama pia, akasema jioni atanipigia. Nikaona poa.

Jioni kimya, nikapiga mara nne hajapokea. Nikafunga safari kwenda kwake, sikumkuta. Hasira zikanipanda, nikaondoka. Leo nimemfata kimya kimya nikamkuta akaanza kuleta Kiswahili chake. Nikamwambia nahitaji hela yangu, ulikuja vizuri nikakusaidia, mbona unakuwa mhuni tena? Kama hunilipi niambie tu niache kujisumbua pasipo na matumaini, nitajua cha kufanya. Kasema saa kumi uhakika kabisa leo. Ulipofika muda nikamcheki tena hayupo. Simu ikaita akazima.

Nikamwandikia sms kumwambia huenda hajanijua. Ustaarabu nmetumia, nmejifanya mpuuzi ili nipate pesa yangu kaona ananimudu. Kaja kujibu anadai fanya chochote sina hela.

Waliosema ukitaka uonekane mbaya udai chako walikuwa na maana kubwa. Urafiki umekufa huu. Nitapotezea sababu siwezi kwenda kushtaki popote sababu hakuna ushahidi, tulipeana juujuu tu.

Nimejiapiza hata aje mtu anataka kufia miguuni mwangu nimkopeshe haitokaa itokee nikamkopesha hata kama pesa ninayo ya kutosha kiasi gani. Bora afe kabisa. Ntachomshauri ni kwamba aende kwenye ofisi za mikopo huko watamsaidia ila mimi, NEVER EVER.

Wish You A Marry Christmas.
 
Kwaiyo ilo biti ilkua kuja kushtaki humu ..haya Mshana Jr Rakims mpeni uyu kijana mbinu za anga za upambanaji
Mkuu, mtu akiamua kuacha tu jambo lipite haimaanishi hana cha kufanya. Miaka ya nyuma kabisa nilikuwa sitaki upuuzi kabisa. Niliwahi kumpasua jicho mtu sababu alinisumbua kunilipa. Nilishatia watu hasara sababu nawadai. Niliishia kufungwa tu. Niliamua kubadilika na kuwa mtu wa tofauti ila kumbe dunia haitaki watu wa aina ambayo nimekuwa mimi. Napotezea, sihitaji kurudi kule mkuu. Nimeamua kutosaidia mtu tu kivyovyote vile.
 
Ukiwa huna mke Ndugu na jamaa wanafurahi sana sababu unakuwa mwepesi kwao. Lakini ukishaoa wanajua meneja wa benki yupo nyumbani ile hela ya kijinga haitoki tena, ndio maana ndugu hawa wapendi wake za jamaa zao. Wakijua meneja wa benki hataki masihara na hela ya mumewe.
 
Mm nlikuwa na marafiki ambao Kwa kiasi flan tulikua tunajuana japo sio kiivo, wakiwa na shida wananambia niwasaidie wakipata wanarudisha mwanzon haikua shida baadae wakabadilika wakichukua Hela kubwa wanarudisha ila hzo fifte fote thate wakawa wanapuuzia nliwakataa kimtindo kila Moja nlimuomba Hela ambayo na uhakakika hana na hawezi nipa.......ikawa ndo baba jeni mama jeni byeeeee
 
Juzi kati kuna jamaa angu mmoja alinipigia simu kwa huruma sana anataka nimkopeshe hela huku akiahid baada ya wiki moja atarudisha nilimwambia siko vizur, ila kwa kua alisisitiza atarudisha nikaona ngoja nimkopeshe.

Ile kumkopa ilipita wiki hata simu yake sijaiona nikaona ngoja nimtafute mimi. Nampigia simu anaanza ooh naumwa nikapeleleza kumbe haumwi muongo ni kaona huyu dawa ni kumkaushia tu.

Nikapata funzo mtu hata aje kwa style gani siwez kukopesha hela labda nimpe tu km zawadi.
 
Dah! Usinikumbushe mkuu,
Uyu jamaa Hapa chini ananisumbua balaa
829540848.jpg
 
Wasalaaam, naamini mu wazima wa afya. Wale mnaojiandaa na sikukuu basi ikawe njema kwenu.

Niende moja kwa moja kwenye mada. Wiki kama mbili nyuma kuna rafiki yangu ambae tumefahamiana kutokana na kazi tunazofanya kuwa za kufanana na muda mwingine kupeana deals mbalimbali zinapotokea alipatwa na changamoto ambayo aliniomba kama nina kiasi kadhaa cha pesa nimsaidie ili aweze kutayua changamoto yake.

Kwa jinsi alivyokuwa akinieleza, inaonyesha kabisa ilikuwa ni issue serious na alitakiwa kuisolve ndani ya muda mfupi sababu aliharibu gari ya mtu na alipeleza pesa ya ku-repair. Alitoa na ahadi baada ya wiki atanirudishia pesa yangu.

Nilimueleza sina ila alinishawishi nikaona ngoja tu nimsaidie. Nikamuuliza tena, una uhakika utanirejeshea ndani ya wiki kama unavyodai? Maana mie mwenyewe nina mambo mengi ya kukamilisha yanayohitaji pesa na kuzingatia ni msimu wa sikukuu. Akala na viapo vyote unavyovifahamu. Ikabidi nimsaidie.

Baada ya week kuisha, nilijua angefanya uaminifu kunirejeshea lakini kukawa kimya. Siku ya tisa nikampigia simu, ikaita lakini haikupokelewa. Nikatuma na ujumbe wa kumkumbusha in case simu hakuisikia basi asome ajue.

Ikapita kimya siku hiyo. Siku iliyofuata nikatuma ujumbe haukujibiwa, nikapiga simu ikaita halafu ikakatwa. Nikapiga tena ikawa haipatikani, muda huo nahitaji pesa pia nifanye mambo yangu na maandalizi ya sikukuu.

Cha ajabu hakuonyesha hata uungwana wa kutuma sms kuonyesha labda alikuwa busy au muda nnaompigia labda anakuwa hayupo na simu. Nikaendelea kupambana kumpigia bila mafanikio. Nikitumia namba ngeni anapokea, ila akijua tu ni mimi anakata na kuzima kabisa simu. Nikamaindi kabisa na kumtumia sms kali ila hakujibu.

Jana katika mihangaiko ya hapa na pale tukakutana, kaanza kuleta sababu eti alikuwa anaumwa halafu hana kifurushi chochote kile ndio maana hajanitafuta. Nikamuuliza sasa mbona hata nikikupigia hupokei? Anasema huwa anakuwa kalala. Nikaona upuuzi huu. Afanye kuniambia saa ngapi nimfuate kwake nikachukue hela maana nmekwama pia, akasema jioni atanipigia. Nikaona poa.

Jioni kimya, nikapiga mara nne hajapokea. Nikafunga safari kwenda kwake, sikumkuta. Hasira zikanipanda, nikaondoka. Leo nimemfata kimya kimya nikamkuta akaanza kuleta Kiswahili chake. Nikamwambia nahitaji hela yangu, ulikuja vizuri nikakusaidia, mbona unakuwa mhuni tena? Kama hunilipi niambie tu niache kujisumbua pasipo na matumaini, nitajua cha kufanya. Kasema saa kumi uhakika kabisa leo. Ulipofika muda nikamcheki tena hayupo. Simu ikaita akazima.

Nikamwandikia sms kumwambia huenda hajanijua. Ustaarabu nmetumia, nmejifanya mpuuzi ili nipate pesa yangu kaona ananimudu. Kaja kujibu anadai fanya chochote sina hela.

Waliosema ukitaka uonekane mbaya udai chako walikuwa na maana kubwa. Urafiki umekufa huu. Nitapotezea sababu siwezi kwenda kushtaki popote sababu hakuna ushahidi, tulipeana juujuu tu.

Nimejiapiza hata aje mtu anataka kufia miguuni mwangu nimkopeshe haitokaa itokee nikamkopesha hata kama pesa ninayo ya kutosha kiasi gani. Bora afe kabisa. Ntachomshauri ni kwamba aende kwenye ofisi za mikopo huko watamsaidia ila mimi, NEVER EVER.

Wish You A Marry Christmas.
Huyo sio rafiki ako, alafu ondoa mentality ya kwamba ukiwa unamdai mtu ni kama unammiliki yeye mzima,kwamba inabid ajieleze asipopatkana,apokee simu yako,awe mpole et tu kwasababu ya wewe unamdai, wewe ukiona hakupi ushirikiano jua anamambo yake na yeye binafsi yamekwamisha sio lazma aanze kujielezea.

Endelea na mipango mingine, siku akipata ataleta hata ikipita mwaka, la pendekeza kumtumia sms kwamba kama mambo hayajakaa sawa asijal itanipa ukipata, alafu unaleta story zingine za maisha.

Hîi tabia ya kujifanya kupunguza marafiki ,kwa kuona wanashindwa kulipa kwa wakati , na kuwaona waswahili ni tabia ya umaskini sana, wenye akili za kitajiri hawana kabisa hii.
 
Back
Top Bottom