Ndugu yangu nimemtafutia kazi mshahara laki 3, anaikwepa, nimefowadiwa meseji zake anadai ninamnyanyasa. Nifanye nini?

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,014
Kamaliza chuo mwaka juzi ila hadi sasa hana shughuli, alikuja hapa mjini pasaka mwaka jana ila nikamwambia abaki baki ajiskie huru hasa ukizingatia nyumbani kwangu kuna vyumba vya nje kwa hio haikuwa taabu kumuhifadhi.

Sina ubaya wala hila, mimi kila wiki huwa nampa 50 kwajili ya matumizi, sifanyagi hivi kwa ndugu wengine ila kwa kuwa yeye mama yake alikuwa akinisaidia mara kwa mara kiuchumi nilipokuwa chuoni, basi huwa ni kama narudisha fadhila tu na hata hiyo 50 haijawahi kunipa mawazo kumpa.

Alikuwa ananiambia ana apply kazi serikalini lakini kwa hali ilivyo nilimwambia ajira zilekuwa ngumu hivyo nimtaftie, ni kama mara 2 hivi nilitaka kumsaidia mchongo ila alikuwa anakazia kwamba kuna interview anakaribia kuitwa.

Basi mimi nikaamua nimtaftie kazi sehemu ya mtu tunaejuana, tuna undugu kwa mbali, sehemu ile kazi huwa ni jumatatu hadi ijumaa saa 1 na nusu hadi saa 12 jioni.. na jumamosi huwa ni saa tatu hadi saa saba hivi.

Mshahara ni kama laki 3 na elf 30 hivi, pia kila jumamosi kuna posho ya weekend, nadhani itakuwa kati ya elf 10 hadi 15..kuhusu chakula cha mchana na maji kipo, kinapikwa nyumbani gari inaleta ofisini.. kasoro jumamosi tu.

Hii ni fursa nzuri kwake hasa ukizingatia atakuwa na uhuru wa kutosha akijipangia sehemu yake, hasa ukizingatia bado ni kijana,.mfano hapa kwangu ni marufuku kuingiza binti, saa moja geti linafungwa, n.k.

Sasa nilipompa hii habari ni kama hajaichukulia vizuri, alipoanza kuniambia nisubiri subiri kuna interview anaisikilizia nikamwambia wala asiwe na hofu, akiitwa kwenye interiew ataenda ila hii kazi inabidi aianze, kiukweli kwa jinsi alivyochukulia hisi suala ni wazi kabisa ni kama vile haitaki.

Jana ndio nimefowadiwa meseji screenshot analalamika kwamba namfanyia manyanyaso kwamba kazi ina muda kidogo wa kupumzika, malipo kidogo, n.k.
 
Anza kumpa elf 10 mwambie mambo hayajakaa vizuri na usimuulize kitu chochote, na ukitaka asikuulize mpe asubuhi wakati unatoka haraka haraka unampa na kuondoka, na ukirudi usimpe nafasi yakujadili kitu atanyooka tu.
 
kamaliza chuo mwaka juzi ila hadi sasa hana shughuli, alikuja hapa mjini pasaka mwaka jana ila nikamwambia abaki baki ajiskie huru hasa ukizingatia nyumbani kwangu kuna vyumba vya nje kwa hio haikuwa taabu kumuhifadhi. sina ubaya wala hila, mimi kila wiki huwa nampa 50 kwajili ya matumizi

alikuwa ananiambia ana apply kazi serikalini lakini kwa hali ilivyo nilimwambia ajira ziekuwa ngumu hivyo nimtaftie, ni kama mara 2 hivi nilitaka kumsaidia mchongo ila alikuwa anakazia kwamba kuna interview anakaribia kuitwa.

Basi mimi nikaamua nimtaftie kazi sehemu ya mtu tunaejuana (connection) ila pia tuna undugu pia kwa mbali, sehemu ile kazi huwa ni jumatatu hadi ijumaa saa 1 na nusu hadi saa 12 jioni.. na jumamosi huwa ni saa tatu hadi saa nane hivi.

Mshahara ni laki 3 na kitu ila haujazidi 350k.

Sasa nilipompa hii habari ni kama hajaichukulia vizuri, alipoanza kuniambia nisubiri subiri kuna interview anaisikilizia nikamwambia wala asiwe na hofu, akiitwa kwenye interiew ataenda ila hii kazi inabidi aianze,, kiukweli kwa jinsi alivyochukulia hisi suala ni wazi kabisa ni kama vile haitaki.

Jana ndio nimefowadiwa mesej screenshot analalamika kwamba namfanyia manyanyaso kwamba kazi ina mda kidogo wa kupumzika, malipo kidogo, n.k.
Mkuu ruhusu pm tafadhali
 
15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom