Fool me once shame on you, Fool me twice shame on me, Nimemkamata binti wa dukani kaniibia kwa mbinu aliyoniibia mwanzo, Kazi hana mshahara umekwenda

Uncle bright

JF-Expert Member
Feb 9, 2023
1,040
4,080
Ukinitapeli mara ya kwanza aibu iwe kwako unaenifanyia hayo mabaya, lakini ukinipiga mara ya pili kwa style ile ile nikiwa na utimamu wa kujua kinachoweza kutokea basi aibu iwe kwangu, Niliapa sitoweza kuangukia kwenye mtego wa jaribio la kwanza kwa mara ya pili.

Niliweka binti wa kazi alinitandika shilingi laki 3 mwezi mwanzoni na nikadhani may be ni kosa langu but hadi kuamua kufikia hayo maamuzi ni baada ya kuona kwamba labda pengine ni uzembe wangu wa kutokutunza kumbukumbu vizuri, pia alilia sana machozi kwahio nikasema acha nifunike kombe mwanaharamu apite maisha yaendelee.

Lakini sikuwa mjinga kusamehe na kusahau, nilishaweka countereasures za kutoangukia mtego maana hilo tukio nilikuwa nalikumbuka halikupotea kichwani.

Siku ya jumatatu baada ya kumlipa mshahra wake nashangaa tena leo nimekula short ya laki na 30 flani , HELL NOOO !!!

Yeye hakujua kwamba nilianza kutunza rekodi za withdrawals kila siku kisirisiri na niliweka camera ya siri ofisini so nikavua koti kuanza nifatilie, kila kitu kilichorekodiwa pindi nikiwa sipo mpaka duka linapofungwa.

Nimemdaka live bila chenga kaingia ofisini na kuchomoa pesa, Binti ni mafia aisee!! kumbe na yeye ana funguo spare sehemu nayotunza pesa, kweli alikuwa kajipanga.

Nilivuta pumzi na kuongea kwa sauti, FOOL ME ONCE SHAME ON YOU, FOOL ME TWICE SHAME ON ME !! yeye akasema bosi kuna nini, nikarudia tena FOOL ME ONCE SHAME ON YOU, FOOL ME TWICE SHAME ON ME !! akawa kimya akinishangaa nikamwita kwa majina yake matatu mara mbili na kumwambia HOW DARE YOU , hasira nilizozipata nusu nimzabue mikofi ziga zaga ya bila mpangilio ovyo ovyo, Ila nikashusha pumzi nikamwambia hebu njoo uone huku kwenye screen, alipojiona akaanza kupiga magoti ohh boss nisamehe, nilikuwa na shida ya pesa, mshahara haukutosha, n.k. nilibaki kumshangaa nikamuuliza mshahara wako tuliokubaliana nimewahi kukuchelewa, akabaki hana jibu maana sijawahi kumcheleweshea, nikamuuliza tena day allowance yako nimewahi kukunyima, akasema hapana maana ni kweli kila siku akifika tu ana haki ya kuchukua elf 3.

Nilichofanya ni kumwambia naenda kumwambia polisi na ndugu zake, Network yake ni kama ilikata, nikamwambia option pekee aliyonayo anirudishie laki 3 aliyonipiga mwanzo na laki 1 aliyonipiga jana na kisha aondoke.

Uzuri nilikuwa napajua kwao na alinisihi sana nisioneshe video kwa watu wake naowajua, kijana toka asubuhi saa tatu ndio karudi muda huu na pesa laki 3 na elf 70 inaelekea kahenya sana huko,

Shughuli ndipo imeishia hapo kazi hakuna tena na nimemfanyia kwa huruma sana maana evidence clealy inaonyesha anavyoiba
 
ni mzuri? ungemkula tu kwa kweli na hela akulipe. kama mzuri nipe namba yake nimtibu tatizo la udokozi nimpe na kazi.
Watu wengine ni kama mmejulia haya mambo utu uzimani, basi mnakuwa kama walevi wa vilabuni mliozoea chimpumu mkishika pesa za ghafla za kuweza kumudu bia za bar basi inakuwa fujo ni mpaka tone la mwisho la kila chupa.

Ni vitu vya kawaida sana hivyo na wala havina thamani na hatari unazoweza kuingizwa nazo iwe kwenye biashara, kiafya, kazi, n.k.
 
😂😂Mkuu we uliyewajulia utotoni mbn wanakupiga za uso mpaka unaongea ngeli kama unaigiza bongo movie
Anaekukomoa kwa wizi nae mkomoe kimafia arudishe alichokiiba iwe cash, mwizi anaweza kuwa jinsia yoyote.

Mambo ya kufidia pesa kwa puzi hapana aisee, hayo mambo kama umezoea since upo 15 huko yanapungua value kulingana na baadhi ya mazingira.
 
Ukitaka ubadili wafanyakazi mpaka uchanganyikiwe weka camera sehemu ya biashara kisha ajili mtu,Jamanii sisi ngozi nyeusi tunashida mahali si bure.
Kuna mdau humu kafungua uzi kajenga lodge yake, kagharamika sana kuweka camera za kuchunguza idadi ya wateja wanaokodi vyumba lakini mhudumu akawa anavuruga mifumo ya camera makasudi,

Baada ya kumfukuza na mapato yameongezeka, watu wanakuja kwako kwa la kukupiga sio kujenga biashara yako
 
MTU AKIKU FOOL MARA MOJA UNAWEZA KUWA MWELEWA UKAMSAMEHE, ILA KWELI MARA NYENGINE TENA !! YANI INAONESHA KAKUONA ZUZU LA KUJIPIGIA TENA NA TENA NA TENA
Inatia hasira sana, mie kuna mdg angu nakaa nae hapa, anasoma form 2 sahivi.

Sasa mie na tabia ya kuweka hela sehem mbali mbali ktk kabati, juu ya meza etc bila kujua ni kias gani exactly nilichoweka (natupiaga tu chenchi chenchi au buku buku zinazobaki ktk mfuko).

Sasa juzi kati nachungulia kabatini naona hela kama zimepungua nachek ktk meza nakutana na jero tu.. mhh..

Nikatafuta kibox flan hivi.. nikawa naweka hela humo zote ila nakiset mtu akifungua nijue.. bado dogo akawa anafungua anaiba.

Nikamweleza siku moja usiwe unaniibia hizi hela.. akakana, mwendo ni ule ule.

Nikaona huu ujinga, nikaandika kikaratasi kabisa " Endelea kuiba hizi hela ".

Bado akawa anaiba.

Nikasema huyu kashashindikana, nimemrudisha kwa wazee akakae nao maana akili zangu mbili ntampa ngumi za kifua niue.
 
Umasikini ama dhiki yoyote haimfanyi mtu aibe, hivyo huyo kijana ni mwizi ki tabia na hauwezi kumrekebisha.
 
Inatia hasira sana, mie kuna mdg angu nakaa nae hapa, anasoma form 2 sahivi.

Sasa mie na tabia ya kuweka hela sehem mbali mbali ktk kabati, juu ya meza etc bila kujua ni kias gani exactly nilichoweka (natupiaga tu chenchi chenchi au buku buku zinazobaki ktk mfuko).

Sasa juzi kati nachungulia kabatini naona hela kama zimepungua nachek ktk meza nakutana na jero tu.. mhh..

Nikatafuta kibox flan hivi.. nikawa naweka hela humo zote ila nakiset mtu akifungua nijue.. bado dogo akawa anafungua anaiba.

Nikamweleza siku moja usiwe unaniibia hizi hela.. akakana, mwendo ni ule ule.

Nikaona huu ujinga, nikaandika kikaratasi kabisa " Endelea kuiba hizi hela ".

Bado akawa anaiba.

Nikasema huyu kashashindikana, nimemrudisha kwa wazee akakae nao maana akili zangu mbili ntampa ngumi za kifua niue.
ungemleta kwa babu njunju nina tiba yao hao maandazi watu
 
Mbona ngona na ujinga wa aina zake imekuwa overrated sana? Yaani aibe hela yangu halafu atumie tundu la haja ndogo kama honey trap!!!!😖.
Hiiiiii bagosha
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom