DOKEZO Tumeachishwa kazi kihuni na Global Publishers, wanataka kutudhulumu haki zetu, tufanye nini?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Boran Jakutay

Senior Member
Apr 8, 2023
110
255
Habari zenu, kwanza nianze kwa kuwapa hongera wale wote walio kwenye mfungo wa KWARESMA na RAMADHANI, MUNGU WA MBINGUNI awaongoze salama hadi mwisho.

Leo nimekuja mbele yenu nataka ushauri, nifanye nini au tufanye nini sisi wafanyakazi wa Kampuni ya Global Publishers inayomilikiwa na Mbunge wa Buchosa, ERIC SHIGONGO ili tupate haki yetu?

Stori nzima ipo hivi; Februari 12, 2024, Meneja Mkuu wa Global Publishers (Abdallah Mrisho) aliwapa taarifa wahariri wa magazeti ya michezo ya CHAMPIONI na SPOTI XTRA kwamba ofisi imesitisha kuchapisha magazeti kutokana na hasara inayopatikana.

Baada ya hapo, hakukuwa na kauli rasmi ya uongozi kwenda kwa wafanyakazi wote kwa maana ya waandishi waliokuwa wakiandikia magazeti hayo na hata wasanifu kurasa hawakupewa tamko rasmi nini kitafuatia baada ya hapo.

Cha kushangaza, baada ya siku mbili kutoka Februari 12 hadi 14, ikaundwa timu ya watu sita (6) yenye wahariri wawili (2), waandishi wawili (2) na wasanifu kurasa wawili (2) ili kuendelea na kazi ya kuyaandaa magazeti mawili yanayotoka mtandaoni kwa wiki (CHAMPIONI IJUMAA na CHAMPIONI JUMATATU).

Kumbuka wale wahariri waliopewa taarifa ya kusitishwa uchapishaji magazeti, walikuja kwa waandishi na wasanifu kurasa kufikisha taarifa hizo, sisi tulitarajia baada ya hapo uongozi utatoa tamko rasmi lakini imekuwa kimya mpaka leo hii.

Hata hivyo, taarifa zilieleza baada ya kusitishwa uchapishaji magazeti, zitatolewa barua kwa wafanyakazi ili kuonesha mikataba imesitishwa na kila mmoja afahamu stahiki zake na atazipataje, ukizingatia wapo waliokuwa kazini kwa zaidi ya miaka nane (8), lakini hakuna barua yoyote iliyotoka, hivyo ni kama tumeachishwa kazi KIHUNI.

Kila mara tunapoomba tukutane na Mkurugenzi Mkuu (Eric Shigongo) ambaye ni MBUNGE WA BUCHOSA ili tuzungumze naye, kumekuwa na ugumu kwani naye anawarushia mpira viongozi wa chini ndio wasikilize vilio vyetu.

Sisi tumekuwa tukitaka kuonana na SHIGONGO kwa sababu viongozi wa chini yake tumekaa nao vikao vingi, lakini majibu yao hayaridhishi, wakati mwingine hawana kabisa majibu ya maswali yetu, wanatoa ahadi ambazo hazitimizwi, hivyo basi tunapofanya juhudi ya kutaka kuonana na mmiliki wa kampuni, anatukwepa.

Tunajiuliza, Mbunge ambaye ana jukumu la kuongoza wananchi, anawakwepaje wananchi wake wa ofisini, je huko jimboni kwake matatizo yakitokea anayatatuaje au pia anayakimbia?

Ushauri wenu ni muhimu sana, tufanye nini ili tupate haki yetu kwa sababu siku zinazidi kwenda, hatujui hatma yetu na tupo nyumbani tangu tulivyositishiwa ajira zetu KIHUNI, tunaona tunakwenda kudhulumiwa.

Tunaidai ofisi hela nyingi sana ikiwemo mishahara ya takribani miezi 11, tumefanya kazi kuanzia Aprili 2023 hadi Februari 2024 bila ya kulipwa mshahara. Tunaishije na tuna familia zinatutegemea.
 
Habari zenu, kwanza nianze kwa kuwapa hongera wale wote walio kwenye mfungo wa KWARESMA na RAMADHANI, MUNGU WA MBINGUNI awaongoze salama hadi mwisho...
Mleta mada pole sana kwa mazila, zahama na sintofaham mnayopitia. Uonevu, usaliti na dhulma mnayopitia naelewa kabisa inavyouma. Mnaonewa hivihivi kwenye haki yenu na kudhulumiwa. Pia isikute mnasalitiwa ma wakubwa wenu ama mawakilishi.

Bwana awape uvumilivu na Allah awafanyie wepesi kwenye harakati zenu za kupata haki.
 
Nendeni wizara ya kazi kitengo Cha ajira binafsi naamini watawap maelezo wap pa kuanzia

Kuna wapishi walifutwa kazi,wakaenda huko wakapat haki Yao na mafao Yao walillipwa yote

Goodluck
 
Habari zenu, kwanza nianze kwa kuwapa hongera wale wote walio kwenye mfungo wa KWARESMA na RAMADHANI, MUNGU WA MBINGUNI awaongoze salama hadi mwisho.

Leo nimekuja mbele yenu nataka ushauri, nifanye nini au tufanye nini sisi wafanyakazi wa Kampuni ya Global Publishers inayomilikiwa na Mbunge wa Buchosa, ERIC SHIGONGO ili tupate haki yetu?

Stori nzima ipo hivi; Februari 12, 2024, Meneja Mkuu wa Global Publishers (Abdallah Mrisho) aliwapa taarifa wahariri wa magazeti ya michezo ya CHAMPIONI na SPOTI XTRA kwamba ofisi imesitisha kuchapisha magazeti kutokana na hasara inayopatikana.

Baada ya hapo, hakukuwa na kauli rasmi ya uongozi kwenda kwa wafanyakazi wote kwa maana ya waandishi waliokuwa wakiandikia magazeti hayo na hata wasanifu kurasa hawakupewa tamko rasmi nini kitafuatia baada ya hapo.

Cha kushangaza, baada ya siku mbili kutoka Februari 12 hadi 14, ikaundwa timu ya watu sita (6) yenye wahariri wawili (2), waandishi wawili (2) na wasanifu kurasa wawili (2) ili kuendelea na kazi ya kuyaandaa magazeti mawili yanayotoka mtandaoni kwa wiki (CHAMPIONI IJUMAA na CHAMPIONI JUMATATU).

Kumbuka wale wahariri waliopewa taarifa ya kusitishwa uchapishaji magazeti, walikuja kwa waandishi na wasanifu kurasa kufikisha taarifa hizo, sisi tulitarajia baada ya hapo uongozi utatoa tamko rasmi lakini imekuwa kimya mpaka leo hii.

Hata hivyo, taarifa zilieleza baada ya kusitishwa uchapishaji magazeti, zitatolewa barua kwa wafanyakazi ili kuonesha mikataba imesitishwa na kila mmoja afahamu stahiki zake na atazipataje, ukizingatia wapo waliokuwa kazini kwa zaidi ya miaka nane (8), lakini hakuna barua yoyote iliyotoka, hivyo ni kama tumeachishwa kazi KIHUNI.

Kila mara tunapoomba tukutane na Mkurugenzi Mkuu (Eric Shigongo) ambaye ni MBUNGE WA BUCHOSA ili tuzungumze naye, kumekuwa na ugumu kwani naye anawarushia mpira viongozi wa chini ndio wasikilize vilio vyetu.

Sisi tumekuwa tukitaka kuonana na SHIGONGO kwa sababu viongozi wa chini yake tumekaa nao vikao vingi, lakini majibu yao hayaridhishi, wakati mwingine hawana kabisa majibu ya maswali yetu, wanatoa ahadi ambazo hazitimizwi, hivyo basi tunapofanya juhudi ya kutaka kuonana na mmiliki wa kampuni, anatukwepa.

Tunajiuliza, Mbunge ambaye ana jukumu la kuongoza wananchi, anawakwepaje wananchi wake wa ofisini, je huko jimboni kwake matatizo yakitokea anayatatuaje au pia anayakimbia?

Ushauri wenu ni muhimu sana, tufanye nini ili tupate haki yetu kwa sababu siku zinazidi kwenda, hatujui hatma yetu na tupo nyumbani tangu tulivyositishiwa ajira zetu KIHUNI, tunaona tunakwenda kudhulumiwa.

Tunaidai ofisi hela nyingi sana ikiwemo mishahara ya takribani miezi 11, tumefanya kazi kuanzia Aprili 2023 hadi Februari 2024 bila ya kulipwa mshahara. Tunaishije na tuna familia zinatutegemea.
Ushauri wangu ni huu,mfanyakazi anapokuwa kazini na taratibu za kazi zikikiukwa ikiwemo kutolipwa mshahara anapaswa kumfikisha mwajiri wake katika mahakama yan usuluhishi wa kazi na kuomba mahakama hiyo imsaidie kupata hizo haki na pia kulinda ajira yake kama mikataba unavyoeleza.

Na ikiwa Mfanyakazi ataondolewa kazini Kwa namna yoyote na akakosa kupata stahiki zake,pia anapaswa kwenda mahakama ya kazi CMA,kuomba mwajiri alazimishwe kulipa hizo stahiki.

Muda wa kisheria wa kufungua madai ni Kati ya siku 1-60,Kuna mazingira ya madai halali kupokewa ndani ya siku 30 na Kuna mazingira ya madai halali kupokewa baada ya siku 30 na isizidi 60.

Ninyi mpo ndani ya mazingira hayo Kwa hatua ya kwanza mnaweza kupeleka madai yenu ya kulipwa stahiki zenu za kazi mkiwa ni waajiriwa wa Global mpaka wakati huu

Na ikiwa mtapewa barua rasmi ya kuachishwa kazi basi mtafungua shauri katika mazingira hayo.

Kuendelea kumsubiri mwajiri au kupeleka malalamiko maeneo mengine kutawaondolea fursa ya kisheria(muda) wa kufungua madai na hii itaathiri haki zenu zote

Nimewashauri hivi nikiwa ni Mwandishi mwenzetu ambaye nilifanikiwa kupata stahiki zangu Kwa kufuata taratibu hizo nilizoandika hapo juu
 
Kafungueni lalamiko CMA si bado mpo ndani ya siku 60 toka tatizo litokee
 
Ndio tatizo la magazeti kuwa na mrengo wa kuimba mapambio kwa watu fulani, halafu wakiondoka, ndio kwisha habari yake

cc musiba
 
Habari zenu, kwanza nianze kwa kuwapa hongera wale wote walio kwenye mfungo wa KWARESMA na RAMADHANI, MUNGU WA MBINGUNI awaongoze salama hadi mwisho.

Leo nimekuja mbele yenu nataka ushauri, nifanye nini au tufanye nini sisi wafanyakazi wa Kampuni ya Global Publishers inayomilikiwa na Mbunge wa Buchosa, ERIC SHIGONGO ili tupate haki yetu?

Stori nzima ipo hivi; Februari 12, 2024, Meneja Mkuu wa Global Publishers (Abdallah Mrisho) aliwapa taarifa wahariri wa magazeti ya michezo ya CHAMPIONI na SPOTI XTRA kwamba ofisi imesitisha kuchapisha magazeti kutokana na hasara inayopatikana.

Baada ya hapo, hakukuwa na kauli rasmi ya uongozi kwenda kwa wafanyakazi wote kwa maana ya waandishi waliokuwa wakiandikia magazeti hayo na hata wasanifu kurasa hawakupewa tamko rasmi nini kitafuatia baada ya hapo.

Cha kushangaza, baada ya siku mbili kutoka Februari 12 hadi 14, ikaundwa timu ya watu sita (6) yenye wahariri wawili (2), waandishi wawili (2) na wasanifu kurasa wawili (2) ili kuendelea na kazi ya kuyaandaa magazeti mawili yanayotoka mtandaoni kwa wiki (CHAMPIONI IJUMAA na CHAMPIONI JUMATATU).

Kumbuka wale wahariri waliopewa taarifa ya kusitishwa uchapishaji magazeti, walikuja kwa waandishi na wasanifu kurasa kufikisha taarifa hizo, sisi tulitarajia baada ya hapo uongozi utatoa tamko rasmi lakini imekuwa kimya mpaka leo hii.

Hata hivyo, taarifa zilieleza baada ya kusitishwa uchapishaji magazeti, zitatolewa barua kwa wafanyakazi ili kuonesha mikataba imesitishwa na kila mmoja afahamu stahiki zake na atazipataje, ukizingatia wapo waliokuwa kazini kwa zaidi ya miaka nane (8), lakini hakuna barua yoyote iliyotoka, hivyo ni kama tumeachishwa kazi KIHUNI.

Kila mara tunapoomba tukutane na Mkurugenzi Mkuu (Eric Shigongo) ambaye ni MBUNGE WA BUCHOSA ili tuzungumze naye, kumekuwa na ugumu kwani naye anawarushia mpira viongozi wa chini ndio wasikilize vilio vyetu.

Sisi tumekuwa tukitaka kuonana na SHIGONGO kwa sababu viongozi wa chini yake tumekaa nao vikao vingi, lakini majibu yao hayaridhishi, wakati mwingine hawana kabisa majibu ya maswali yetu, wanatoa ahadi ambazo hazitimizwi, hivyo basi tunapofanya juhudi ya kutaka kuonana na mmiliki wa kampuni, anatukwepa.

Tunajiuliza, Mbunge ambaye ana jukumu la kuongoza wananchi, anawakwepaje wananchi wake wa ofisini, je huko jimboni kwake matatizo yakitokea anayatatuaje au pia anayakimbia?

Ushauri wenu ni muhimu sana, tufanye nini ili tupate haki yetu kwa sababu siku zinazidi kwenda, hatujui hatma yetu na tupo nyumbani tangu tulivyositishiwa ajira zetu KIHUNI, tunaona tunakwenda kudhulumiwa.

Tunaidai ofisi hela nyingi sana ikiwemo mishahara ya takribani miezi 11, tumefanya kazi kuanzia Aprili 2023 hadi Februari 2024 bila ya kulipwa mshahara. Tunaishije na tuna familia zinatutegemea.
Mna mikataba lakini? Isijekuwa mlikuwa mnafanyishwa kazi za deiwaka! Chukueni huo ushauri wa kwenda CMA mkafungue mashauri yenu pale. Tafuteni mwanasheria mzuri awasaidie hili la kwenda CMA.
 
Back
Top Bottom