sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,408
- 19,033
Ni ndugu yangu mwenye miaka 26, kamaliza chuo mwaka juzi.
Hapo zamani mara kwa mara alikuwa akiniomba pesa za kutatua shida zake, hizi elfu 20 nimemtumia sana.
Nikaona isiwe taabu, kitu anachoomba ni kama samaki naowavua basi nayeye nimpe ndoano awe anajivulia, Tulikaa chini pamoja nikamuuliza kama yupo tayari kufanya biashara, hili ndio lilikuwa swali la msingi zaidi maana asije kuwa na mambo yake yatayomtinga, akasema yupo tayari. Swali la pili nikamwambia aende kujitafakari vizuri anataka kufanya biashara ipi ya mtaji wa milioni 4 za kununulia mzigo jibu anipe baada ya wiki, biashara aliyochagua ni nzuri tu sikuwa na shaka nayo.
Katika maandalizi ya kumfungulia duka niligharamika takribani milioni 1 na nusu ya ziada kulipia kodi ya miezi 6 ya fremu, mafundi wa mbao, makufuli imara, kabati la bidhaa, kusajili biashara, leseni ya biashara, kupata tin ya eneo la biashara, tax clearance, n.k.
Biashara akaanza rasmi nami nilipata furaha mno kuona ndugu yangu nae kaanza safari ya kujitegemea kama mwanaume kamili.
Ajabu ni kwamba baada ya miezi kadhaa akaanza upya kuniomba hizi 10 mara 20, n.k.
Baada ya uchunguzi nimekuja kujua kwamba alianza kutumia pesa kuzidi faida anayoingiza, strarehe !
Undugu wetu upo pale pale, wala hatujavunja undugu, wala simdai hata shilingi 50, naumia kuona tu kwamba ndugu yangu pamoja na usomi wake nilitegemea atachangamkia hii fursa ili na yeye aanze kufaidi maokoto yake ila imekuwa ndivyo sivyo, Malengo yangu yalikuwa kwamba huyu akianza kujitegemea nisaidie wengine na pengine nae awe msaada kwa wengine ila ndio hivyo tena !! Ile milioni 5.5 inaweza kuwa ndogo kama unajijali peke yako lakini kiasi hiki kinaweza kusaidia watu wenye shida nayo, mfano nina baadhi ya ndugu kijijini wanachota maji mbali, ingetumika kuchimba kisima ingekuwa msaada mkubwa, muda wa kwenda kuchota maji watu wangetumia kupata kufanya shughuli zingine, hatari za kwenda kuchota maji umbali mrefu zingekwepeka, n.k.
Hana mshipa wa aibu??