Habari ya mwaka mpya wana jamii forum.
wanaccm kila wanapoangalia madarasa haya mapya ya sekondary hasira dhidi ya Ndugai zinaongezeka na kumuona kama msaliti
Ndugulile akikagua baadhi ya madarasa ya kiwango cha juu kabisa aliyoyasimamia yeye mwenyewe kwa fedha zilizotolewa na mh rais wetu.

FB_IMG_16408844806970802.jpg
 
Hawamu ya tano kilikuwa kipindi kigumu, waulize wafanyabiashara, wakulima wa mahindi, mbaazi, korosho, wafanyabiashara biashara maduka ya fedha, wanasiasa nje ya CCM na ndani, pia tambua kipindi kigumu ni jinsi kinavyo adhiri makundi mengi!
Mbona unawasemea watu ? Sema biashara hewa na magumashi ndio zilipata tabu Ila biashara zote za haki mambo yalikuwa poa

Awamu ya tano iliwaumiza wapigaji, wale ambao wanawafanya kazi hewa kila idara
 
Kama huna bando ni hivi, Ndugai aliupata Uspika kwa fitna dhidi ya Mama Anne Makinda, Ndugai alitibiwa kwa mamilioni ya fedha ughaibuni na hajapona Bado, Ndugai ana tabia ya kuwachapa bakora wapinzani wake....
Ndugai alipitishwa na vikao vyote vya CCM tena kwa kupigiwa kura na kuibuka mshindi ndipi jina lake likaenda kupigiwa kura na wabunge wote ambapo aliibuka kidedea kwa kuwashinda wagombea wenzake.

Huyo anayesema Ndugai alimshinda Makinda kwa fitina ni zaidi y kipofu kwa sababu kama ni lawama angezielekeza kwa wajumbe wa vikao vya CCM waliompigia kura Ndugai.

Tafuteni fursa za uteuzi kwa akili basi sio kujitoa ufahanu kwa arguments za kitoto.
 
Ndugai alipitishwa na vikao vyote vya CCM tena kwa kupigiwa kura na kuibuka mshindi ndipi jina lake likaenda kupigiwa kura na wabunge wote ambapo aliibuka kidedea kwa kuwashinda wagombea wenzake...
Ngoja yaendelee kuparuana yenyewe, yamezorotesha upinzani. Sasa hakuna kwa kupeleka kelele zao ni bora tu yaparuane tuone mikwaruza yao. Ni likundi linalojifikiria lenyewe kama vile hakuna watu wengine. Na sisi tumezidisha ujinga na uoga. Ubatili mtupu.
 
Ndugai alipitishwa na vikao vyote vya CCM tena kwa kupigiwa kura na kuibuka mshindi ndipi jina lake likaenda kupigiwa kura na wabunge wote ambapo aliibuka kidedea kwa kuwashinda wagombea wenzake. Huyo anayesema Ndugai alimshinda Makinda kwa fitina ni zaidi y kipofu kwa sababu kama ni lawama angezielekeza kwa wajumbe wa vikao vya CCM waliompigia kura Ndugai.

Tafuteni fursa za uteuzi kwa akili basi sio kujitoa ufahanu kwa arguments za kitoto.
Mambo ya CCM hayo mtajuana wenyewe dadeeeeki
 
We una roho na nafsi ya kichawi kabisa, ulitaka aende kwa sangoma au mganga wa kienyeji au ulitaka afe???
ndio, aende sangoma na kwa waganga wa kienyeji kama hizo ndio options za matibabu zilizopo kwa mamilioni ya Watanzania wengine

wanatakiwa watumie fedha zetu kuongoza ujenzi wa miundombinu ya afya ya kutunufaisha sote, sio kwenda kutibiwa wao nje ya nchi. Ndo maana Pombe Magufuli aliamua kufia kwenye hospitali tunazofia sisi badala ya John Hopkins wanapotibiwa kina Kikwete.

uhai wa Nduli Ndugai, Sitta, Kikwete, Nyerere, Mkuchika, Salim Salim na wengine wote waliotumia mabilioni yetu kutibiwa nje, uhai wao sio muhimu kuliko wa mwananchi mwingine.

Lakini sasa tutaanza kupiga hatua, Spika anahoji madeni ya hovyo ya Rais, Mwenezi wa mkoa CCM anahoji uvunjaji katiba wa Spika wa CCM, Mbunge wa Taifa CCM anakemea wahuni ndani ya CCM, Rais anashika mic kujibu hoja ya Spika hadharani...

Ndio hizi haki za kuhoji na kuwajibishana ambazo kina Lissu wametandikwa risasi wakizipigania
 
Hahaha vipi kuhusu kibajaji na msukuma??
Msukuma na Kibajaji wanna IQ kubwa Sana wale....ni tofauti kabisa na huyu galasa na mnywa ulanzi wa Njombe....hovyo kabisa huyu mwenezi....huwezi kuwasilisha hoja kihivyo....
 
Kufuatia kauli ya Ndugai kupinga serikali kukopa pesa kwaajili ya kumalizia miradi mikubwa iliyoasisiwa na hayati Magufuli, chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa njombe kimeipinga vikali kauli hiyo ya Ndugai ambaye ni spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Akizungumza wakati wa kukagua miradi ya maendeleo ikiwemo madarasa yanayojengwa kwa pesa za UVIKO-19, katibu wa siasa na uenezi mkoa wa njombe, bw Erasto Ngole amemtaka spika Ndugai kuwa na adabu kwani hata katika awamu ya tano serikali ilikopa lakini yeye kama spika hakuwahi kuhoji chochote kuhusu mikopo hiyo na kuwa Tanzania sio nchi pekee inayokopa duniani hivyo aiache serikali ifanye kazi ya kuwaletea wananchi maendeleo.

Kada huyo nguli amemtaka spika Ndugai kama ana hoja za msingi za kushauri aziwasilishe kwenye vikao vya juu vya chama kwa kufuata utaratibu la sivyo chama kitamshughulikia.

Aidha, kada huyo ameendelea kuwatahadharisha wabunge kuwa makini na spika Ndugai huku akidai kuwa alipata uspika mara mbili kwa kubebwa japokuwa hafai

"Ninawaomba wabunge mumwangalie sana huyu spika wetu, ameingia kwenye uspika mara mbili kwa kubebwa, hakuna asiyejua na tunajua jinsi ulivyoingia kwa kumwondoa makinda mpaka yuko nje tunajua" alisema kada huyo na kuongeza.

Mbali na kashifa ya kumwondoa Makinda kwenye nafasi ya uspika kwa zengwe, kada huyo amemtaka Jobu Ndugai kurudi nchini India alikokuwa akipatiwa matibabu kupima akili yake kama bado inafanya kazi sawa sawa.

" ulienda India ukatibiwa kwa zaidi ya bilioni mbili za watanzania na inawezekana hujapona ndio maana unaropoka ropoka, inawezekana akili yako bado imeruzi, rudi India wakakucheki tena kama hicho kichwa chako kinafanya kazi sawa sawa".

Katika hatua nyingine, kada huyo kutokea njombe amemtaka spika Ndugai kuacha tabia ya kuchapa viboko watu wanaompinga au kumwambia ukweli

" umezoea wanaokusema kwenye ukweli unawapiga viboko, ulimpiga viboko mgombea mwenzako kule kongwa sasa mimi ni mpigaji mwenzako kama unataka kupiga njoo ukutane na mimi".

Pia, kada huyo amehoji juu ya uwepo wa wabunge 19 bungeni ambao hawana vyama ambapo amedai kwamba ni ishara kuwa spika hana uwezo na hafai kuongoza bunge isipokuwa anatumia ubabe.
 
Back
Top Bottom