Ndoa yangu ipo ICU !dah

Ndoa yangu ipo ICU !dah

Kweli mpenzi mnapitia mengi halafu nyie mnajua kuvumilia shida hizi bila hata kutoa chozi ila mnaumia ndani kwa ndani..
Huko nje bidada kashakolezwa Na hisia kwa mume zimeisha. Amuache tu


Ukute mke wa mtoa mada analiwa tigo na wajanja huko nje, hlf hatoi tigo kwa mumewe Mzigua90
 
Pole mkuu Kwa changamoto hizo, mi naona hapo mapenzi yameisha, nakushauri utafute kazi tena dar, urudi na watoto wote, hamishia upendo wote Kwa watoto, kuwa busy na kazi na kusali. Punguza kunywa kwa ajili ya kumuwaza mkeo, pia tafuta mchepuko wa kupunguzia protein usije kuanza kupiga puchu!
 
mkuu to be honesy kila nikifikiria hii road naumiaga sana na niombe niwe imara kwa hili
Kuna siku nilikuta vyakujipimia ngoma anavyo..niliishiwa pozi kumuuliza nilisubir tupo outing tukiwa tume refresh nikamuuliza angependa tukapime sote maana nilikuta kachukua hatua mwenyew maana sijajua kama either mimi nilisababishia ahofie au yeye tu mwenyewe aliniuliza umeaza lin kupekua vitu vyangu..nikachoka
Kweli mkuu inaonekana una moyo wa upendo sana na familia yako ila huyo mkewako anachanganywa na ulimbukeni wa dunia tu. Mpe likizo kwanza means achana nae kwanza kwa mda ili dunia imfunze.
 
SULUHISHO MUDA MFUPI CONT...
2.Endelea Kumwombe Mwenzi Wako Na Umsemeshe Kwa Upole Hata Kama Unaumia,shetani Hapendi Amani Na Umoja Usually Ndoa Ni Vita Against Temptations And Evils! Usisahau Kuomba Toba Kwa Ajili Yako, Yake Na Familia Yako! Ombea Upendo,umoja Na Usemi Wenu!
3. Hakikisha Umempa Nafasi Ya Kutosha Usimbane,there's A Time People Act The Way They Do As A Reaction To The External Forces!
4. Wajibu Wako Kama Mume Ni Kumpenda Mkeo Na Kutumia Akili Ku Navigate Mahusiano Yenu.
5. Watoto Wasiwe Sehemu Ya Ugomvi Wenu.
6. Onyesha Upendo Kwake Hata Baada Ya Kuondoka, Ni Upendo Tu Utakaowarudisha Pamoja Na Kumfuatilia Au Kupigana!
7. Tafuta Marriage Conseller Au Mentor Akusaidie Na Changamoto Kwenye Kipindi Hiki Cha Mpito.
8. Usimwache Mkeo,huyo Sio Mwanamke Tu,ananafasi Tofauti Na Wanawake Wengine. The Best Gift You Can Ever Give Your Kids Is To Love Their Mum Unconditionally!

If You Want More Personal Advice Let Me Know Bro!
May God Hold Your Family Together!
 
Mkeo anaitwa nani;
Kw
Binafsi nipo kwenye ndoa takribani miaka mine na tumebarikiwa watoto wawili. Changamoto zilianza mke alipohamishwa kikazi mwaka juzi kutoka Dar kwenda Morogoro.

Kutokana na ukaribu nikawa najituma sana kutwa kwenda halafu isitoshe huyu mtoto wa pili alikua mwaka mmoja. Umbali ukasababisha mimi niwe mnywaji kidogo kuondoa upweke kuliko niwe nachepuka. Nikawa napunguza safari za kwenda weekend na yeye akazidisha mahusiano ya simu na mfanyakazi mwenzie(sijui kama walitembea ila nilijua wana uhusiano baada ya kunasa chat maana ilifika kipindi anajua weekend nalala ndo anakua busy kwa simu wakiongea na huyo mpaka nilivyombana na chats aka admit wanamahusiano via simu na huyo mtu yupo Dar).

Siku moja nikaenda Moro ghafla nikakuta anachat nae bado na isitoshe kuna mwingine wa Moro; nilimdunda hatari. Tukasuluhishwa na familia baada ya hapo kila tukikwaruzana kidogo anakimbilia kusisitiza tuachane yaani ndo ukawa wimbo.

Sasa nikaona kuondoa usumbufu na yeye kuhamia Dar aligoma kwa kusema maisha nafuu Moro nikatafuta kazi Moro nikahamia(nilipata kazi half the pay ya Dar) ila nilimweleza la msingi tuwe pamoja tuweze nusuru ndoa.

Sasa tangu tumeamua kukaa pamoja mambo hayajawa mepesi. Mimi na-cover basic needs kama kawaida yangu na napambana na biashara ila mwenzangu amekuwa amepotea kabisa kimapenzi. Tangu mwaka huu tunaweza kuwa tumesex si zaida ya mara 15 am sure maana mwenzangu hayupo kabisa anaona nimembana sana.

Kila kitu anatupia lawama nivomdundaga na matatizo ya nyuma. Nimejitahid kumpa space sana ila naona kitu kidogo anakimbilia kutaka talaka.

Sasa kilichonipelekea kuandika uzi huu ni majuzi nilimwambia naenda Dar maana alikua yupo moody sikujua ni sababu yangu au lah. Nikamwambia tu nina safari ya Dar week nzima; aisee alifurahii sana.

Safari ilikuwa ya siku mbili nikarejea jioni nikamtafuta kwenye simu akawa hapokei alivyotoka kibaruani. Jirani yetu ni mfanyakaz mwenzie akarudi tukapishana nikamuuliza vipi shoga yako akasema tumeachana amesema anapita sokoni mara moja (nikaona very rare kutorudi na shoga yake).

Wife akanitumia meseji akasema ametoka outing na shoga zake. Nikasema fine mimi nikanyuti nje mtaa wa pili kuona nani angerudi nae.

Kuna gari ikaja ikapaki kwa jirani ikakaa dakika kama 15 akashuka halafu gari ikaondoka. Alivyoingia ndani nami nikamfwata kwa nyuma
akashtuka sana. Nikamuuliza nani akasema rafiki yake tu walienda pata wine.

Nikamwambia naomba uwe makini tu kuna maradhi. Kama tumefikia huko naomba basi uwe na amani ufanye yako na si hapa kwangu na isitoshe tuna watoto wadogo usilete jazba kwenye haya mambo(maana tulivoingia ndani akaanza kuwaka kama simuamini alivyosema yupo outing nikamweleza outing sio issue ishu umetoka huko mkaweka kambi kwenye gari mie nawaona tu mnapiga story hamkumaliza huko outing)

Nimegundua hana mapenz kwa sasa na nimevumilia sana vituko vyake ila nawaza niwashirikishe wazazi wake na wadhamini wetu nataka niwachukue wanangu nirudi Dar nimpe nafasi tu.

Mkewangu ananiuma sana kila nikikumbuka nilivyompata, mahusiano yetu nk. Yeye ndo alikuwa kipaumbele kunitia sana moyo pale nilipokwama au kusita jambo(hii naandika kwa majonzi sana)

Umri wake haujazidi 30 bado na kuna muda naamini alingia ndoani akiwa mdogo sijui kuna mambo hajafanya? Ila mimi ni mtu wa kuwa huru sana namwambiaga nishirikishe nikupe kibali sina hiyana wala nini cha msingi ni imani tu kwamba hatavuka mipaka.

Suala la uwezo sijalitilia uzito maana yeye binafsi ana kazi na mshahara wake kwakweli huwa simgusiagi hata kidogo anafanya atakavyo. Mimi nina nyumba Dar ndo nimepangisha kuja kuishi naye huku. In short majukumu yangu nayajua na nayamudu.

Suala la kitandani lilikuwa zuri tu sote tunafurahi nk. Mwaka huu lilianza kususasua penzi la kubembeleza yeye ata enjoy ila mpaka nimemuandaa nimemconvince mbona shughuli.

Kwa upande wangu sio mnywaji sana na anajua. Nikinywa tu wine nikiwa nae ntajitahid kumueleza kiu yangu juu ya mambo ambayo hanitimizii hapo nae atarukia "si uniache"bas mkibishana atasema mlevi tatizo.

Weekend ndo tunakaa na kujadili mambo ila mara chache sana maana katikati ya wiki akirudi home yeye kachoka ni kula kulala tu.

Mimi ni mwanadamu pia naweza kuwa na mapungufuyangu ila all i know kuachilia mbali kila jambo nimekuwa nikijitahid kuomba msamaha ninapokosea nk.

Ndugu zangu ndo wanaona nimekamatwa kwelikweli ila nakuwa najitahid niishi ki maadili maana mke mwenyewe mmoja.

Nimesali sana mpaka nimeona kama ni watoto hata nikisema nimpotezee nitahitaji kuwaona wanangu ambapo itapelekea nimwone labda na yeye kitu ambacho mda mwingi kinaniwia ngumu kuvunja familia. Ila nikisema nibebe watoto(namjua kwa sasa majibu yake atasema nenda nao tu la msingi tuachaneee nk) nitabeba ila nataka niombe nisingependa kusikia pua yake na wakwe ndo watakua gia ya kuwaona. Ninataka full right ya wanangu nina uwezo wa kuwalea vizuri. Yani naumia sana ila naona ndo best option kwa sasa.

Naomba ushauri wenu wakuu[/QUOT
Kwa maelezo yenu mnahitaji kuonana na Mariage Counselor kwa sababu naona kabisa kuwa ndo inataka kuvunijika na hakuna anayetaka kuinusuru so inabidi mtafute mtu akaewaonesha umuhimu wa ninyi kuwa pamoja OVA.Nipigia kwa +255222820024 Naweza kukupa ushauri mzuri
 
Duh,pole sana.Huyo mke wako inaonekana kabisa hajatulia,unajua shida ya wanawake wengi wa sasa wanahitaji tu kuolewa na si mume,na akisha olewa kinachofuata ni kuendelea na mambo yake bila ya kujali kuwa yeye ni mke wa mtu..
 
...kiukweli simon umenitoa machozi ndugu yangu. Nimesoma ulichoandika mara tatu tatu, nikaanza kuhisi pengine labda mimi ndio niliandika huu uzi jana usiku, ila kutokana na mawenge ya strees pamoja na usingizi,, nimejikuta nimesahau. Maana kiukweli ulichokiandika chote, kama kilivyo...ndio hali halisi niliyonayo mwenzako hivi sasa, mpaka nimeisi pengine umeniibia story.

Kiukweli haya maisha ya mahusiano, tuyaache tu kama yalivyo...."mtu mwema ukutana na bedui na bedui ukutana na mwema" sio fair hata kidogo.

Nikupe tu pole ndugu yangu, maana natamani niandike zaidi ya pole lakini nawaza...nitaandika nini, wakati me na wewe tupo kwenye boti moja.

Ila Mungu yupo....tumuachie yeye.
 
Pole sana! Fanya maombi ya kufunga kwa siku 3 ukiomba Mungu akuwezeshe kufanya maamuzi sahihi. Baada ya hapo fuata kile kitakachokupa amani ya moyo. Yawezakuwa kubaki na huyo mwanamke au kumwacha.
Naomba nilifanyie kazi hili
Huku nikianza na sala ya toba
 
...kiukweli simon umenitoa machozi ndugu yangu. Nimesoma ulichoandika mara tatu tatu, nikaanza kuhisi pengine labda mimi ndio niliandika huu uzi jana usiku, ila kutokana na mawenge ya strees pamoja na usingizi,, nimejikuta nimesahau. Maana kiukweli ulichokiandika chote, kama kilivyo...ndio hali halisi niliyonayo mwenzako hivi sasa, mpaka nimeisi pengine umeniibia story.

Kiukweli haya maisha ya mahusiano, tuyaache tu kama yalivyo...."mtu mwema ukutana na bedui na bedui ukutana na mwema" sio fair hata kidogo.

Nikupe tu pole ndugu yangu, maana natamani niandike zaidi ya pole lakini nawaza...nitaandika nini, wakati me na wewe tupo kwenye boti moja.

Ila Mungu yupo....tumuachie yeye.
Pole sana kaka!
Hayo ni maumivu ya muda yatapita tu, endeleeni kumtumainia Mungu ipo siku atawafuta machozi.
 
Wewe ni mwanaume mzuri. Unampenda mke wako na ndoa yako kiasi cha kuamua kujikana na kuacha kazi na nyumba Dar ili kuinusuru ndoa yako. Wengi wanakuona bwege lakini wanaojua maana ya kujitoa na kuwajibika wanaelewa kuwa uamuzi wako ulikuwa sahihi. Sasa hapa ulipofikia ukiendelea kutokufanya uamuzi wowote utazidi kuumia. Maisha ni yako na moyo wako unao wewe. Sisi huku tutakushauri kulingana na uzoefu wetu na machungu na visasi vyetu. Amua moja na Mungu akutie nguvu kupokea na kukabiliana na matokeo ya uamuzi wowote utakaochukua. Yaliyokupata ni ya kawaida kwa binadamu wote na halitakudhuru kama hutaogopa. Mambo yote (mema na mabaya) hutokea kwa faida ya mtu. Kuwa na imani, chukua somo uendelee na maisha.
 
Mkuu je mama yako yuko hai?
Na mtoto wa pili ana umri gani?
Nakushauri usilazimishe kuishi na mtu asiye na mapenzi na Wewe tambua wewe ni binadamu iko siku atakufanyia kituko ili tu akuvunje moyo muachane na wewe ukashindwa kuvumilia ukachukua maamuzi magumu halafu watoto wataabike na kubaki yatima...
Nakushauri mtoto mkubwa mpeleke shule boarding..
Huyo mdogo Kama umri mdogo zaidi mpeleke kwa bibi yake yaan mama yako akikua kidogo naye mpeleke boarding..

Usilazimishe kuishi na joka ndani ya nyumba iko siku litakudhuru
Wazaz wangu wamdhafariki mkuu
Asante kwa ushauri
Huyu mdogo miwil sasa
 
Watu wa mbeya
Pole sana Simon, siku zote umuhimu wa mtu/kitu huonekana kikiwa hakipo ,kama ukifanikiwa kumove on,ndyo atakuja kukumbuka mno na itakua late tayari,
Mi nakushauri umove on tu inauma ila utazoea, watoto unaweza mwachia mpk wakifikisha umri (7yrs) nadhani utaweza kuwachukua ukawalea mwenyewe ,ila mnawasababishia watoto kuanza kulelewa na single parent jamani arrgh. afu huyo Dada aache kutuharibia CV watu wa Mbeya. Siye hatupo hivoo.
 
Back
Top Bottom