Ndoa yangu ipo ICU !dah

Ndoa yangu ipo ICU !dah

HUYO ANATAKA KULA UJANA GIVE HER A LOT OF SPACE MPE HATA MWAKA.
AKIIJUA THAMANI YAKO ATARUDI SAIVI ANA MTU WANAONANA.

ATAKAPORUDI ANALIA NDO MDA WA KUMFUNZA SOMO.
 
Nionacho mimi, UNAMPENDA SANA MKEO NA UNAMUAMINI SANA!!

Bro in family mwanaume unatakiwa uwe dikteta, mambo ya kumpa uhuru mwanamke atakuonea mpk utaonekana umepewa limbwata. Kumbuka wewe ni kichwa! A head controls the body.

Lazima umuwekee mipaka, issue za kumbembeleza sijui uzungu zungu wa outing ni mlango wa kuharibu ndoa, huko ndo anaenda kujifunza utaahira wa kukudharau.

Yes, ulimpa kipigo ila hakukoma, do u know pychological torture? Hii ndo dawa kwa wamama wasiojielewa.

Halafuuu! We only live once, sasa kwa nini upate stress sijui mateso daily? Set yo things, hakikisha moyo umekuruhusu, chukua watoto, kawalee kwa upendo then ule monde!

Hivi ukiwa unasafiri kwenda Dodoma uko kwa bus umesinzia, mara umeamka unastukia gari ni la Arusha, utaendelea na safari? Mwenye busara anashuka anatafuta la Dom safari inaendelea.

Pole sana, sientertain kuivunja ndoa yako, but ukiona maji yamezidi unga using'ang'anie kunywa uji!

Kumbuka: Asilimia 60 ya ndoa ulimwenguni huishia break-up!
 
Cha msingi achana nae angalia maisha yako na usipokuwa makini ipo siku atakuwekea hata sumu kwani inaonyesha ameishakuchoka
 
Ni ukweli mchungu ila pls usiite uboya, yamkini yalishakukuta ama yanaweza kukufika hata wewe siku moja! Pia kumbuka huyu wa jamaa ni mke sio hawara!
Vyovyote utakavyochukulia.. Nina experience kubwa sana na welfare za mahusiano kitaaluma n.k


Nasema hivi , msimamo wangu ni ule ule. Unapoona dalili za kuumizwa na mwanamke tafuta mikakati ya kujinasua either

1. Kumpiga chini
2. Kuendelea kuwa nae ila potezea na vumilia kila Kitu (Ni wanaume wachache wanaweza hii)


Kinyume na hapo utakufa na kuacha wanao wanateseka bure huku mkeo akiendelea kuliwa uroda na mabazazi. Ifike muda nyeusi tuseme nyeusi tusipake rangi. Wanaume tunajitfutia vifo kwa mikono yetu.



Hakuna maamuzi magumu yasiyokuja na maumivu. Apige moyo konde atapata mtu sahihi. Sio kuendelea kulialia huo sio uanaume. Uanaume ni maamuzi magumu. Maamuzi magumu sio kuruka sarakasi ubungo mpaka chanika pekee. Kuwa imara kwa nyakati kama hizi kunapima "Uanaume" pia.


Please mkuu nikuombe tena kwa Ustawi Wa maisha yako achana na huyo mke kabla hali haijawa mbali. Kama MTU hakutaki anashindwaje kukuwekea hata sumu ?? Angalia hili kwa jicho la tatu. Unaweza kuishi na simba lakini sio Mke au Mme asiekutaka. Ni kujitafutia mabalaa tu.




Najua maumivu anayopitia Mkuu ila siku zote lazima uhalisia Wa mambo ndio uakisi maamuzi. Kama anaona hali anazopitia anaweza kuendelea na Mke wake , namuomba aendelee na Mke wake. Mimi macho na masikio Yangu natega Redion na habari za magazetini.
 
Mtoa mada pole sana, ila kabla sijakushauri naomba nkuulize..kumbuka kipindi kile ndo unamtongoza mkeo kwa mara ya kwanza, alikusumbua sana kwa mda mrefu ndo ukampata? Kama alikusumbua kwa mda mrefu alikusumbua kwa mda mrefu kiasi gani? Au ulimpata kirahisi.

Kwenye mwanzo mahusiano yenu kabla hamjaoana, huyo mkeo alikuwa na tabia ya kukuomba pesa hovyo bila mpangilio? Hata kama mizinga yake ilikuwa haikukeri, au Midogo, specify kiasi cha pesa alchokuwa anakuomba. simon baker
mkuu kuanzia uhusiano wetu yeye ndo alikomaa tuwe serious(kipind hiko alikua anatoka kwenye uhusiano na mimi nilikua nipo nipo tu)nilikua namkwepesha nakuwa nae karibu sana kwasabab nilielewa maybe ni maumivu aliyotokea nayo..basi kiutani utani kweli niliamua kudate nae maana nilikua nampenda pia -nilimpenda awali nikajenga ukaribu nae nilivyogundua anapitia a break up nikapunguza mazoea apite salama ila yeye akazidisha eventually tukadate
Kwenye mahusiano alikua sio mtu wa vizinga
Yani huyu mwanamke hela sio kipaumbele ila ana ujana nahisi hajafanya bado ndo anapigania sana afanye kwa sasa
 
Mtoa mada pole sana, ila kabla sijakushauri naomba nkuulize..kumbuka kipindi kile ndo unamtongoza mkeo kwa mara ya kwanza, alikusumbua sana kwa mda mrefu ndo ukampata? Kama alikusumbua kwa mda mrefu alikusumbua kwa mda mrefu kiasi gani? Au ulimpata kirahisi.

Kwenye mwanzo mahusiano yenu kabla hamjaoana, huyo mkeo alikuwa na tabia ya kukuomba pesa hovyo bila mpangilio? Hata kama mizinga yake ilikuwa haikukeri, au Midogo, specify kiasi cha pesa alchokuwa anakuomba. simon baker
mkuu kuanzia uhusiano wetu yeye ndo alikomaa tuwe serious(kipind hiko alikua anatoka kwenye uhusiano na mimi nilikua nipo nipo tu)nilikua namkwepesha nakuwa nae karibu sana kwasabab nilielewa maybe ni maumivu aliyotokea nayo..basi kiutani utani kweli niliamua kudate nae maana nilikua nampenda pia -nilimpenda awali nikajenga ukaribu nae nilivyogundua anapitia a break up nikapunguza mazoea apite salama ila yeye akazidisha eventually tukadate
Kwenye mahusiano alikua sio mtu wa vizinga
Yani huyu mwanamke hela sio kipaumbele ila ana ujana nahisi hajafanya bado ndo anapigania sana afanye kwa
 
Wakati naoa niliwahi kumwambia aliye mke wangu, tukioanana nisingependa kutokea kuachana. lakini ikatokea tukatengana. "I feel your pain". nakushauri jifunze taratibu kupenda bila kuwa naye.Jua kuwa wewe ndiyo unayependa si vinginevyo.Usijenge hisia za kutompenda kwa sababu ulizozisema kwa kuwa yeye bado ni binadamu na bado safari ni ndefu. Kanuni ya kumpenda adui yako, ukiitafakari na ukaielewa vizuri itakusaidia sana, hasa kwa kuwa una watoto naye.
Jawabu madhubuti ya wana "ndoa" wenye watoto linatakiwa lipatikane ndani yao katika hisia zote (kimwili(body), kiakili(mind) na kiroho(heart)).Ndugu, marafiki na jumuia ni washereheshaji. Fanya hayo kwa ajili ya maono yako na ustawi wa familia na watoto wako.
 
Duuuh kazi kweli. Kila mmoja kwenye maisha ana kanuni zenye kumuongoza. Moja ya kanuni zangu kwenye maisha ni hii,"Sikuzaliwa ili kuwa kero kwa jamii bali fahari kwa jamii". Kwenye mahusiano yako na mkeo wewe tayari ni kero, ili uwe fahari unatakiwa kumuacha. Sehemu ndoa yenu ilipofikia twaweza sema ni "Point of no return".
Hakuna kitu kinauma kama kuona mtu uliemwamini na kujenga msingi wa maisha yako kwake akikusaliti.Ni simanzi, ni majonzi. Mbele hakuendeki, nyuma hakutamaniki.
Ushauri wangu kwako, jambo lolote ili ulishinde ni muhimu kutumia maarifa. Tafuta kitabu kiitwacho," BIKRA YANGU" mwandishi wa kitabu Prvatus Karugendo. Kisome ukiwa umetulia, naamini kitakusaidia.
 
hapo inabidi uamue bila hata kufikiria mangapi mazur mmefanya maana inakoelekea utakuja kujuta zaid kwa kuchelewa leo mkutoa uamuzi huyo sahv roho yake haipo kwako ,, mpe anachotaka na utapona na haya masaibu kuliko kuendelea nae utalia kila siku
 
Pole brother ,Mungu akiwa upande wetu ni Nani aliye juu yetu,Bibilia inasema Hakuna.
Brother,endelea kuwa mpole na kuendelea kufanya majukumu Kama baba wa Familia.
Note.Endelea kumpenda mke wako vizuri kabisa mwisho wa siku,Mungu atamrejesha na huo uovu wake.
Kitu ambacho unateseka nacho ktk kipindi hichi unapoona mwanamke Hana utii Maana wanaume wengi wanapenda utii kutoka kwa wake zake.

Turudi kwenye maandiko ya Neno la Mungu kidogo.
23 Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili.
24 Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo.
25 Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake;
26 ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno;
27 apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa.
28 Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe.
29 Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake po pote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye anavyolitendea Kanisa.
30 Kwa kuwa tu viungo vya mwili wake.
31 Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja.
Efeso5:------
Mkuu i am a very emotional person yani nasoma hii huku dah...asante sana mkuu
I believe Mungu anasikia sana kilio changu japo ni mtihani huu anataka nifaulu vyema...najijua moyo wangu nikimtupia kisogo sitaweza kumsamehe hata anifufulie wazazi wangu..ndo mana nawaza mda mwingine ila naamini pia ntakua nakosea but niombe Mungu anizidishiwe wepes moyoni
 
Binafsi nipo kwenye ndoa takribani miaka mine na tumebarikiwa watoto wawili. Changamoto zilianza mke alipohamishwa kikazi mwaka juzi kutoka Dar kwenda Morogoro.

Kutokana na ukaribu nikawa najituma sana kutwa kwenda halafu isitoshe huyu mtoto wa pili alikua mwaka mmoja. Umbali ukasababisha mimi niwe mnywaji kidogo kuondoa upweke kuliko niwe nachepuka. Nikawa napunguza safari za kwenda weekend na yeye akazidisha mahusiano ya simu na mfanyakazi mwenzie(sijui kama walitembea ila nilijua wana uhusiano baada ya kunasa chat maana ilifika kipindi anajua weekend nalala ndo anakua busy kwa simu wakiongea na huyo mpaka nilivyombana na chats aka admit wanamahusiano via simu na huyo mtu yupo Dar).

Siku moja nikaenda Moro ghafla nikakuta anachat nae bado na isitoshe kuna mwingine wa Moro; nilimdunda hatari. Tukasuluhishwa na familia baada ya hapo kila tukikwaruzana kidogo anakimbilia kusisitiza tuachane yaani ndo ukawa wimbo.

Sasa nikaona kuondoa usumbufu na yeye kuhamia Dar aligoma kwa kusema maisha nafuu Moro nikatafuta kazi Moro nikahamia(nilipata kazi half the pay ya Dar) ila nilimweleza la msingi tuwe pamoja tuweze nusuru ndoa.

Sasa tangu tumeamua kukaa pamoja mambo hayajawa mepesi. Mimi na-cover basic needs kama kawaida yangu na napambana na biashara ila mwenzangu amekuwa amepotea kabisa kimapenzi. Tangu mwaka huu tunaweza kuwa tumesex si zaida ya mara 15 am sure maana mwenzangu hayupo kabisa anaona nimembana sana.

Kila kitu anatupia lawama nivomdundaga na matatizo ya nyuma. Nimejitahid kumpa space sana ila naona kitu kidogo anakimbilia kutaka talaka.

Sasa kilichonipelekea kuandika uzi huu ni majuzi nilimwambia naenda Dar maana alikua yupo moody sikujua ni sababu yangu au lah. Nikamwambia tu nina safari ya Dar week nzima; aisee alifurahii sana.

Safari ilikuwa ya siku mbili nikarejea jioni nikamtafuta kwenye simu akawa hapokei alivyotoka kibaruani. Jirani yetu ni mfanyakaz mwenzie akarudi tukapishana nikamuuliza vipi shoga yako akasema tumeachana amesema anapita sokoni mara moja (nikaona very rare kutorudi na shoga yake).

Wife akanitumia meseji akasema ametoka outing na shoga zake. Nikasema fine mimi nikanyuti nje mtaa wa pili kuona nani angerudi nae.

Kuna gari ikaja ikapaki kwa jirani ikakaa dakika kama 15 akashuka halafu gari ikaondoka. Alivyoingia ndani nami nikamfwata kwa nyuma
akashtuka sana. Nikamuuliza nani akasema rafiki yake tu walienda pata wine.

Nikamwambia naomba uwe makini tu kuna maradhi. Kama tumefikia huko naomba basi uwe na amani ufanye yako na si hapa kwangu na isitoshe tuna watoto wadogo usilete jazba kwenye haya mambo(maana tulivoingia ndani akaanza kuwaka kama simuamini alivyosema yupo outing nikamweleza outing sio issue ishu umetoka huko mkaweka kambi kwenye gari mie nawaona tu mnapiga story hamkumaliza huko outing)

Nimegundua hana mapenz kwa sasa na nimevumilia sana vituko vyake ila nawaza niwashirikishe wazazi wake na wadhamini wetu nataka niwachukue wanangu nirudi Dar nimpe nafasi tu.

Mkewangu ananiuma sana kila nikikumbuka nilivyompata, mahusiano yetu nk. Yeye ndo alikuwa kipaumbele kunitia sana moyo pale nilipokwama au kusita jambo(hii naandika kwa majonzi sana)

Umri wake haujazidi 30 bado na kuna muda naamini alingia ndoani akiwa mdogo sijui kuna mambo hajafanya? Ila mimi ni mtu wa kuwa huru sana namwambiaga nishirikishe nikupe kibali sina hiyana wala nini cha msingi ni imani tu kwamba hatavuka mipaka.

Suala la uwezo sijalitilia uzito maana yeye binafsi ana kazi na mshahara wake kwakweli huwa simgusiagi hata kidogo anafanya atakavyo. Mimi nina nyumba Dar ndo nimepangisha kuja kuishi naye huku. In short majukumu yangu nayajua na nayamudu.

Suala la kitandani lilikuwa zuri tu sote tunafurahi nk. Mwaka huu lilianza kususasua penzi la kubembeleza yeye ata enjoy ila mpaka nimemuandaa nimemconvince mbona shughuli.

Kwa upande wangu sio mnywaji sana na anajua. Nikinywa tu wine nikiwa nae ntajitahid kumueleza kiu yangu juu ya mambo ambayo hanitimizii hapo nae atarukia "si uniache"bas mkibishana atasema mlevi tatizo.

Weekend ndo tunakaa na kujadili mambo ila mara chache sana maana katikati ya wiki akirudi home yeye kachoka ni kula kulala tu.

Mimi ni mwanadamu pia naweza kuwa na mapungufuyangu ila all i know kuachilia mbali kila jambo nimekuwa nikijitahid kuomba msamaha ninapokosea nk.

Ndugu zangu ndo wanaona nimekamatwa kwelikweli ila nakuwa najitahid niishi ki maadili maana mke mwenyewe mmoja.

Nimesali sana mpaka nimeona kama ni watoto hata nikisema nimpotezee nitahitaji kuwaona wanangu ambapo itapelekea nimwone labda na yeye kitu ambacho mda mwingi kinaniwia ngumu kuvunja familia. Ila nikisema nibebe watoto(namjua kwa sasa majibu yake atasema nenda nao tu la msingi tuachaneee nk) nitabeba ila nataka niombe nisingependa kusikia pua yake na wakwe ndo watakua gia ya kuwaona. Ninataka full right ya wanangu nina uwezo wa kuwalea vizuri. Yani naumia sana ila naona ndo best option kwa sasa.

Naomba ushauri wenu wakuu
Omba waihamishie wodi nyingine hata ya watoto
 
Vyovyote utakavyochukulia.. Nina experience kubwa sana na welfare za mahusiano kitaaluma n.k


Nasema hivi , msimamo wangu ni ule ule. Unapoona dalili za kuumizwa na mwanamke tafuta mikakati ya kujinasua either

1. Kumpiga chini
2. Kuendelea kuwa nae ila potezea na vumilia kila Kitu (Ni wanaume wachache wanaweza hii)


Kinyume na hapo utakufa na kuacha wanao wanateseka bure huku mkeo akiendelea kuliwa uroda na mabazazi. Ifike muda nyeusi tuseme nyeusi tusipake rangi. Wanaume tunajitfutia vifo kwa mikono yetu.



Hakuna maamuzi magumu yasiyokuja na maumivu. Apige moyo konde atapata mtu sahihi. Sio kuendelea kulialia huo sio uanaume. Uanaume ni maamuzi magumu. Maamuzi magumu sio kuruka sarakasi ubungo mpaka chanika pekee. Kuwa imara kwa nyakati kama hizi kunapima "Uanaume" pia.


Please mkuu nikuombe tena kwa Ustawi Wa maisha yako achana na huyo mke kabla hali haijawa mbali. Kama MTU hakutaki anashindwaje kukuwekea hata sumu ?? Angalia hili kwa jicho la tatu. Unaweza kuishi na simba lakini sio Mke au Mme asiekutaka. Ni kujitafutia mabalaa tu.




Najua maumivu anayopitia Mkuu ila siku zote lazima uhalisia Wa mambo ndio uakisi maamuzi. Kama anaona hali anazopitia anaweza kuendelea na Mke wake , namuomba aendelee na Mke wake. Mimi macho na masikio Yangu natega Redion na habari za magazetini.
Hakika
 
30 mkuu
Mwenzangu 27
Dah kweli halafu mwanamke wa kupishana nae umri kidogo hivyo ndio huwa wanakuwaga viburi sana! At least umuache 5 years and above wanakuwaga na hali ya kuogopa kufanya ujinga!
 
Ndoa ndoa ndoa......

Tangu Jiwe aingie madarakani watu wanalalamika maisha magumu.

Kawaida kwenye changamoto nyingi ukiweza kuzitatua au kuwa na suluhisho unaweka bei ya kutatua na unapiga hela.

Kuna changamoto nyingi sana kwenye ndoa na sio kila mtu anataka au yuko tayari kuvunja ndoa yake kwa namna moja au nyingine......

Akili yangu inanituma kufanya kitu..... ambao hawajaoa na kuolewa wanatamani ndoa ila kiuhalisia hawatamani ndoa wanatamani harusi ndo maana ndoa inakufa baada ya miaka michache tuu tangu wale kiapo.

Akili yangu imenipotea suluhisho la ndoa, ila kwa kuanza nataka nianze na wanaotamani harusi tuba inaanza kabla hawajafanya kiapo au kufunga ndoa.

Ntaisajili rasmi hiyo huduma na itajulikana kama Kasie Matata Co.

Coming Soon, stay tuned wateja wangu.

Mtoa mada pole umepata nyingi, mie nakufariji tuu...... wapende wanao kama hujawahi kupenda. Nguvu na akili yako ihamie kwa watoto. Tuamia muda wako mwingi kuwa na wanao, wapelekwe shule Fanta nao homework nenda nao mahali pa michezo cheza nao waogeshe walishe kabla ya kulala sema nao asubuhi uwahi kuwaamsha. .... be a unique father..... hutojutia in five years to come. Angalia, usijaribu kuyapet nafasi mawazo ya yawezekana hao watoto si wako. .... hata ikiwa sio kiuhalisia wekeza kwa wanao ndo ulichobakiwa nao.

Kuhusu mkeo sina la kusema.

K' Matata.
 
Pole sana mkuu,unajua haya maswala ya ndoa rite kama watu wangekuwa wanaambia ukweli juu ya faida na hasara watakazokuja kuzipata ktk ndoa am sure watu weng wasingeingia humo..ila tatizo watu wengi nj waongo utasikia wanasema ndoa tamu sana hahahaha tena mwenye ndoa ni ngumu sana kumuadithia matatizo ya ndoa mtu ambaye hayuko ndoani ili tu asimvunje moyo na yy siku moja aingie mkenge hahaha,but nakushauri mtoa mada fanya kile ambacho moyo wako unakutuma kukifanya kwa the betterment ya uhai wako na afya ya watoto wako...hebu fikiria siku ukifa kwa pressure mfano watoto wako watapata tabu kiac gani wakiwa yatima?au unadhani siku ukipata hasira na kumtia visu mkeo watoto wako wataishi maisha gani pale utakapopelekwa jera na mama yao kuwa amekufa?huoni kama endapo utatengana nae basi utajihakikishia uhai zaidi na hivyo ku ensure future bora ya watoto wako na familia yako inayokutegmea hasa wazazi???wanawake ktk mapenz siku zote ni wavumilivu sana kama ni kweli anamapenz ya dhati..but ukiona anafika stage ya kukuambia muachane basi huyo achana nae haraka sana..ameshapata watu wa kumuendesha akili zake..na hapo hutakuja kusikilizwa kwa lolote mpaka atakapozinguliwa huko nje alipoweka mapenz yake.
 
Pole mkuu binafsi nilikuwa sielewi kwa nini wanasema wanaume tumeumbwa mateso...but hapo mwisho umeweka vitisho acha watu wakupe nyeusi na nyeupe ili ujue wapi palekebishwe....kwa mfano sijaona sababu ya wewe kuhamia Moro na nyumba unayo Dar hilo tu linaonyesha hukusimama imara....
Mkuusalama?
well mimi kama kiongozi wa nyumba yangu najitahid kuwa mkimya sana wakat wa ugomvi na mwenzangu ili niweze msoma anachotaka na awali alilalamika sana umbali na ye hawez hamia dar mpaka atakohamishwa na kapapenda moro...mimi nikafanya maamuz magumu yakuhamia pia mana juu chini garama za nyumba mbili usawa huu ni mkali kuliko moja
 
Hapa ndipo huwa naukumbuka ule uzi unaosema...WALIOOA STD U NA FORM 4 WANA FURAHA KWENYE NDOA ZAO....
 
Back
Top Bottom