Ndoa yangu ipo ICU !dah

Ndoa yangu ipo ICU !dah

Binafsi nipo kwenye ndoa takribani miaka mine na tumebarikiwa watoto wawili. Changamoto zilianza mke alipohamishwa kikazi mwaka juzi kutoka Dar kwenda Morogoro.

Kutokana na ukaribu nikawa najituma sana kutwa kwenda halafu isitoshe huyu mtoto wa pili alikua mwaka mmoja. Umbali ukasababisha mimi niwe mnywaji kidogo kuondoa upweke kuliko niwe nachepuka. Nikawa napunguza safari za kwenda weekend na yeye akazidisha mahusiano ya simu na mfanyakazi mwenzie(sijui kama walitembea ila nilijua wana uhusiano baada ya kunasa chat maana ilifika kipindi anajua weekend nalala ndo anakua busy kwa simu wakiongea na huyo mpaka nilivyombana na chats aka admit wanamahusiano via simu na huyo mtu yupo Dar).

Siku moja nikaenda Moro ghafla nikakuta anachat nae bado na isitoshe kuna mwingine wa Moro; nilimdunda hatari. Tukasuluhishwa na familia baada ya hapo kila tukikwaruzana kidogo anakimbilia kusisitiza tuachane yaani ndo ukawa wimbo.

Sasa nikaona kuondoa usumbufu na yeye kuhamia Dar aligoma kwa kusema maisha nafuu Moro nikatafuta kazi Moro nikahamia(nilipata kazi half the pay ya Dar) ila nilimweleza la msingi tuwe pamoja tuweze nusuru ndoa.

Sasa tangu tumeamua kukaa pamoja mambo hayajawa mepesi. Mimi na-cover basic needs kama kawaida yangu na napambana na biashara ila mwenzangu amekuwa amepotea kabisa kimapenzi. Tangu mwaka huu tunaweza kuwa tumesex si zaida ya mara 15 am sure maana mwenzangu hayupo kabisa anaona nimembana sana.

Kila kitu anatupia lawama nivomdundaga na matatizo ya nyuma. Nimejitahid kumpa space sana ila naona kitu kidogo anakimbilia kutaka talaka.

Sasa kilichonipelekea kuandika uzi huu ni majuzi nilimwambia naenda Dar maana alikua yupo moody sikujua ni sababu yangu au lah. Nikamwambia tu nina safari ya Dar week nzima; aisee alifurahii sana.

Safari ilikuwa ya siku mbili nikarejea jioni nikamtafuta kwenye simu akawa hapokei alivyotoka kibaruani. Jirani yetu ni mfanyakaz mwenzie akarudi tukapishana nikamuuliza vipi shoga yako akasema tumeachana amesema anapita sokoni mara moja (nikaona very rare kutorudi na shoga yake).

Wife akanitumia meseji akasema ametoka outing na shoga zake. Nikasema fine mimi nikanyuti nje mtaa wa pili kuona nani angerudi nae.

Kuna gari ikaja ikapaki kwa jirani ikakaa dakika kama 15 akashuka halafu gari ikaondoka. Alivyoingia ndani nami nikamfwata kwa nyuma
akashtuka sana. Nikamuuliza nani akasema rafiki yake tu walienda pata wine.

Nikamwambia naomba uwe makini tu kuna maradhi. Kama tumefikia huko naomba basi uwe na amani ufanye yako na si hapa kwangu na isitoshe tuna watoto wadogo usilete jazba kwenye haya mambo(maana tulivoingia ndani akaanza kuwaka kama simuamini alivyosema yupo outing nikamweleza outing sio issue ishu umetoka huko mkaweka kambi kwenye gari mie nawaona tu mnapiga story hamkumaliza huko outing)

Nimegundua hana mapenz kwa sasa na nimevumilia sana vituko vyake ila nawaza niwashirikishe wazazi wake na wadhamini wetu nataka niwachukue wanangu nirudi Dar nimpe nafasi tu.

Mkewangu ananiuma sana kila nikikumbuka nilivyompata, mahusiano yetu nk. Yeye ndo alikuwa kipaumbele kunitia sana moyo pale nilipokwama au kusita jambo(hii naandika kwa majonzi sana)

Umri wake haujazidi 30 bado na kuna muda naamini alingia ndoani akiwa mdogo sijui kuna mambo hajafanya? Ila mimi ni mtu wa kuwa huru sana namwambiaga nishirikishe nikupe kibali sina hiyana wala nini cha msingi ni imani tu kwamba hatavuka mipaka.

Suala la uwezo sijalitilia uzito maana yeye binafsi ana kazi na mshahara wake kwakweli huwa simgusiagi hata kidogo anafanya atakavyo. Mimi nina nyumba Dar ndo nimepangisha kuja kuishi naye huku. In short majukumu yangu nayajua na nayamudu.

Suala la kitandani lilikuwa zuri tu sote tunafurahi nk. Mwaka huu lilianza kususasua penzi la kubembeleza yeye ata enjoy ila mpaka nimemuandaa nimemconvince mbona shughuli.

Kwa upande wangu sio mnywaji sana na anajua. Nikinywa tu wine nikiwa nae ntajitahid kumueleza kiu yangu juu ya mambo ambayo hanitimizii hapo nae atarukia "si uniache"bas mkibishana atasema mlevi tatizo.

Weekend ndo tunakaa na kujadili mambo ila mara chache sana maana katikati ya wiki akirudi home yeye kachoka ni kula kulala tu.

Mimi ni mwanadamu pia naweza kuwa na mapungufuyangu ila all i know kuachilia mbali kila jambo nimekuwa nikijitahid kuomba msamaha ninapokosea nk.

Ndugu zangu ndo wanaona nimekamatwa kwelikweli ila nakuwa najitahid niishi ki maadili maana mke mwenyewe mmoja.

Nimesali sana mpaka nimeona kama ni watoto hata nikisema nimpotezee nitahitaji kuwaona wanangu ambapo itapelekea nimwone labda na yeye kitu ambacho mda mwingi kinaniwia ngumu kuvunja familia. Ila nikisema nibebe watoto(namjua kwa sasa majibu yake atasema nenda nao tu la msingi tuachaneee nk) nitabeba ila nataka niombe nisingependa kusikia pua yake na wakwe ndo watakua gia ya kuwaona. Ninataka full right ya wanangu nina uwezo wa kuwalea vizuri. Yani naumia sana ila naona ndo best option kwa sasa.

Naomba ushauri wenu wakuu
Mkuu je mama yako yuko hai?
Na mtoto wa pili ana umri gani?
Nakushauri usilazimishe kuishi na mtu asiye na mapenzi na Wewe tambua wewe ni binadamu iko siku atakufanyia kituko ili tu akuvunje moyo muachane na wewe ukashindwa kuvumilia ukachukua maamuzi magumu halafu watoto wataabike na kubaki yatima...
Nakushauri mtoto mkubwa mpeleke shule boarding..
Huyo mdogo Kama umri mdogo zaidi mpeleke kwa bibi yake yaan mama yako akikua kidogo naye mpeleke boarding..

Usilazimishe kuishi na joka ndani ya nyumba iko siku litakudhuru
 
Mkuu ukitaka kuinjoy life hakikisha mwanamke hakusomi akakumaliza alichomic mkeo ni kulia (mwanamke anapaswa asifurahi siku zote siku zingine unamfanyia fujo unakauka kiume hakuna kuomba msamaha ukiomba omba msamaha anakuona wewe ni mama tu)

Wewe achana naye avinjari anavyotaka hawatafika mbali hao
 
hahaha
mkuu nahisi ntakua nime understate kutoka a na stress
But am sure kuanzia last 3months
Mana nikikumbuka mwanzo wa mwaka it was fine ila miez hii ya karibuni bila bila
Imagine huu mwez tu show imepigwa mara mbili tu

halafu show yenyewe waonekana wewe mbakaji tu,anakutengea tu kama kahaba wa buguruni Kimboka ili mradi ukojoesasa hiyo ni show mzee baba???
 
pole sana inabidi tu ufate moyo wako unataka nini uko kwenye wakati mgumu sana ukimuacha ipo siku atarudi kwa magoti
 
Achana nae mbona una kua boya kaka ndoa ndoa ndoa kitugani?! Una teseka sana dingiii achana nae kasha pata mwingine
 
The best option ni kuachana nae. Huyo ashakuchukia lolote anaweza kukufanya coz hakupendi tena. Anza maisha upya utaumia lkn yataisha
 
mwanamke anaweza kukufanyia ushenzi na kuwa mkaidi labda kwa siku nne au ikizidi san wiki kutokana na wewe kumboa au yeye kuwa na stress zake,lakini huyo wa mwaka mzima hapoi mzee nakushauri uachane naye na utafute mpenzi mwingine ili usiendelee kuumiza moyo wako na ukaishi mbali naye kabisa ikiwezekna rudi dar badilisha na simu time will tell
 
mkuu kuanzia uhusiano wetu yeye ndo alikomaa tuwe serious(kipind hiko alikua anatoka kwenye uhusiano na mimi nilikua nipo nipo tu)nilikua namkwepesha nakuwa nae karibu sana kwasabab nilielewa maybe ni maumivu aliyotokea nayo..basi kiutani utani kweli niliamua kudate nae maana nilikua nampenda pia -nilimpenda awali nikajenga ukaribu nae nilivyogundua anapitia a break up nikapunguza mazoea apite salama ila yeye akazidisha eventually tukadate
Kwenye mahusiano alikua sio mtu wa vizinga
Yani huyu mwanamke hela sio kipaumbele ila ana ujana nahisi hajafanya bado ndo anapigania sana afanye kwa


Mmh hilo janga sijui kanga gani ulibebee, nlikuuliza hivyo coz nlihisi labda huyo mkeo hakukupenda tokea mwanzo (aliolewa na ww basi tu kwa vile hakuwa na option) ndo maana sahiv anakufanyia vitimbi simon baker
 
Ndoa zina mengi sana. Talaka kwa mkeo sio suluhisho. Akishaachika kwako unadhani huyo mchepuko atakaa naye basi? Lazima atarejea tu. By the way kumpiga mnaposhindwa kuelewana sio suluhisho. Angalia alternative solution.
 
Mkuu,
Pole Sana Kwa Maswahibu Hayo! Mungu Anasema Njooni Kwangu Ninyi Nyote Msumbukao Na Mizigo Nami Nitawapumzisha! Mungu Ni Mwaminifu Siku Zote, Hata Asipojibu Sawasawa Na Upendavyo Bado Yeye Ni Mwaminifu!
Watu Wengi Wanakwambia Umwache Mkeo,but I Beg To Differ With The Following Reasons!
1. Mara Nyingi Over 90% Ukivunja Ndoa Yako Ya Ujanani Ni Nadra Sana Ku Stabilize Kwenye Ndoa Zinazofuata,fanya Tafiti Utakubaliana Nami!
2. Katika Maisha Strength Ya Mtu Haipimwi Kwa Kukimbia Tatizo Bali Kulikabili Na Kulishinda. Msamaha Ni Pale Unaposamehe Jambo Ambalo Ki Binadamu Ni Ngumu Lakini Kwa Uwezo Wa Mungu Anakupa Neema Ya Kusamehe. Hatuchagui Mambo Ya Kukoseana, Sisi Sote Ni Dhaifu Sana,tofauti Yetu Na Wazee Wa Zamani Ni Kuwa Wao Walisameheana Sana Na Kuvumiliana Ambazo Ndo Traits Hasa Za Kuwa Katika Ndoa,forget The YOLO Saying Huo Ni Msemo Wa Teenagers Sio Adults!

SULUHISHO LA MUDA MFUPI
1.Tafuta Kazi Dar,rudi Dar Na Watoto Wote! Ikishindikana Hamia Mtaa Mwingine Hapo Moro Mwache Peke Yake!
 
Pole sana ndugu yangu,kwanza nikupe pongezi kwa kupambana kunusulu familia yako na kuhakikisha wanoa unawalea vizuri kwa maisha yao ya badae.Kaka hawa watu mara nyingi wanaitaji huwe na uvumilivu na maono ya badae kwa familia yako(watoto).Nina mfano kuna rafiki yangu mmoja, mke wake alinganganiza na kumfanyia vituko vya kutosha hadi jamaa akaamua kuondoka na kubeba mwanae,lakini kwa sasa huyu mama licha ya kuwa na kazi anateseka sana,hivyo nachokushauri mwambie ndoa haijaribishwi na ukiingia lazima mengine ya dunia hayaache ili apate thawabu kutoka kwa mwenyezi mungu,vinginevyo ataaribu ndoa yake kwa mikono yake.Asubuhi njema na mungu akubariki wewe na familia yako.
 
Mkuu kwanza nikupe pole na hongera kwa uvumilivu. Mpaka kwenye point hyo the Best Option achana Naye , tena kama bado yupo under 30 bado hajui life inaendaje. Let her go bro, ipo siku atakuja anatembelea magoti kuomba msamaha.
 
Back
Top Bottom