Ndoa yangu ipo ICU !dah

simon baker

JF-Expert Member
Oct 5, 2017
519
690
Binafsi nipo kwenye ndoa takribani miaka mine na tumebarikiwa watoto wawili. Changamoto zilianza mke alipohamishwa kikazi mwaka juzi kutoka Dar kwenda Morogoro.

Kutokana na ukaribu nikawa najituma sana kutwa kwenda halafu isitoshe huyu mtoto wa pili alikua mwaka mmoja. Umbali ukasababisha mimi niwe mnywaji kidogo kuondoa upweke kuliko niwe nachepuka. Nikawa napunguza safari za kwenda weekend na yeye akazidisha mahusiano ya simu na mfanyakazi mwenzie(sijui kama walitembea ila nilijua wana uhusiano baada ya kunasa chat maana ilifika kipindi anajua weekend nalala ndo anakua busy kwa simu wakiongea na huyo mpaka nilivyombana na chats aka admit wanamahusiano via simu na huyo mtu yupo Dar).

Siku moja nikaenda Moro ghafla nikakuta anachat nae bado na isitoshe kuna mwingine wa Moro; nilimdunda hatari. Tukasuluhishwa na familia baada ya hapo kila tukikwaruzana kidogo anakimbilia kusisitiza tuachane yaani ndo ukawa wimbo.

Sasa nikaona kuondoa usumbufu na yeye kuhamia Dar aligoma kwa kusema maisha nafuu Moro nikatafuta kazi Moro nikahamia(nilipata kazi half the pay ya Dar) ila nilimweleza la msingi tuwe pamoja tuweze nusuru ndoa.

Sasa tangu tumeamua kukaa pamoja mambo hayajawa mepesi. Mimi na-cover basic needs kama kawaida yangu na napambana na biashara ila mwenzangu amekuwa amepotea kabisa kimapenzi. Tangu mwaka huu tunaweza kuwa tumesex si zaida ya mara 15 am sure maana mwenzangu hayupo kabisa anaona nimembana sana.

Kila kitu anatupia lawama nivomdundaga na matatizo ya nyuma. Nimejitahid kumpa space sana ila naona kitu kidogo anakimbilia kutaka talaka.

Sasa kilichonipelekea kuandika uzi huu ni majuzi nilimwambia naenda Dar maana alikua yupo moody sikujua ni sababu yangu au lah. Nikamwambia tu nina safari ya Dar week nzima; aisee alifurahii sana.

Safari ilikuwa ya siku mbili nikarejea jioni nikamtafuta kwenye simu akawa hapokei alivyotoka kibaruani. Jirani yetu ni mfanyakaz mwenzie akarudi tukapishana nikamuuliza vipi shoga yako akasema tumeachana amesema anapita sokoni mara moja (nikaona very rare kutorudi na shoga yake).

Wife akanitumia meseji akasema ametoka outing na shoga zake. Nikasema fine mimi nikanyuti nje mtaa wa pili kuona nani angerudi nae.

Kuna gari ikaja ikapaki kwa jirani ikakaa dakika kama 15 akashuka halafu gari ikaondoka. Alivyoingia ndani nami nikamfwata kwa nyuma
akashtuka sana. Nikamuuliza nani akasema rafiki yake tu walienda pata wine.

Nikamwambia naomba uwe makini tu kuna maradhi. Kama tumefikia huko naomba basi uwe na amani ufanye yako na si hapa kwangu na isitoshe tuna watoto wadogo usilete jazba kwenye haya mambo(maana tulivoingia ndani akaanza kuwaka kama simuamini alivyosema yupo outing nikamweleza outing sio issue ishu umetoka huko mkaweka kambi kwenye gari mie nawaona tu mnapiga story hamkumaliza huko outing)

Nimegundua hana mapenz kwa sasa na nimevumilia sana vituko vyake ila nawaza niwashirikishe wazazi wake na wadhamini wetu nataka niwachukue wanangu nirudi Dar nimpe nafasi tu.

Mkewangu ananiuma sana kila nikikumbuka nilivyompata, mahusiano yetu nk. Yeye ndo alikuwa kipaumbele kunitia sana moyo pale nilipokwama au kusita jambo(hii naandika kwa majonzi sana)

Umri wake haujazidi 30 bado na kuna muda naamini alingia ndoani akiwa mdogo sijui kuna mambo hajafanya? Ila mimi ni mtu wa kuwa huru sana namwambiaga nishirikishe nikupe kibali sina hiyana wala nini cha msingi ni imani tu kwamba hatavuka mipaka.

Suala la uwezo sijalitilia uzito maana yeye binafsi ana kazi na mshahara wake kwakweli huwa simgusiagi hata kidogo anafanya atakavyo. Mimi nina nyumba Dar ndo nimepangisha kuja kuishi naye huku. In short majukumu yangu nayajua na nayamudu.

Suala la kitandani lilikuwa zuri tu sote tunafurahi nk. Mwaka huu lilianza kususasua penzi la kubembeleza yeye ata enjoy ila mpaka nimemuandaa nimemconvince mbona shughuli.

Kwa upande wangu sio mnywaji sana na anajua. Nikinywa tu wine nikiwa nae ntajitahid kumueleza kiu yangu juu ya mambo ambayo hanitimizii hapo nae atarukia "si uniache"bas mkibishana atasema mlevi tatizo.

Weekend ndo tunakaa na kujadili mambo ila mara chache sana maana katikati ya wiki akirudi home yeye kachoka ni kula kulala tu.

Mimi ni mwanadamu pia naweza kuwa na mapungufuyangu ila all i know kuachilia mbali kila jambo nimekuwa nikijitahid kuomba msamaha ninapokosea nk.

Ndugu zangu ndo wanaona nimekamatwa kwelikweli ila nakuwa najitahid niishi ki maadili maana mke mwenyewe mmoja.

Nimesali sana mpaka nimeona kama ni watoto hata nikisema nimpotezee nitahitaji kuwaona wanangu ambapo itapelekea nimwone labda na yeye kitu ambacho mda mwingi kinaniwia ngumu kuvunja familia. Ila nikisema nibebe watoto(namjua kwa sasa majibu yake atasema nenda nao tu la msingi tuachaneee nk) nitabeba ila nataka niombe nisingependa kusikia pua yake na wakwe ndo watakua gia ya kuwaona. Ninataka full right ya wanangu nina uwezo wa kuwalea vizuri. Yani naumia sana ila naona ndo best option kwa sasa.

Naomba ushauri wenu wakuu
 
Kama kichwa cha habari hapo juu...
Binafsi nipo kwenye ndoa takribani miaka mine na tumebarikiwa watoto wawili...
Changamoto zilianza mke alipohamishwa kikaz mwaka juzi moro...kutokana na ukaribu nikawa najituma sana kutwa kwenda afu isitoshe huyu mtoto wa pili alikua mwaka mmoja...umbali ukasababisha mimi niwe mnywaji kidogo kuondoa upweke kuliko niwe nachepuka...nikawa napunguza safar za kwenda weeknd..yeye akazidisha mahusiano ya simu na mfanyakaz mwenzio(sijui kama walitembea ila nilijua wanauhusiano baada ya kunasa chat maana ilifika kipind anajua weekend nalala ndo anakua busy kwa simu wakiongea na huyo mpaka nivo mbana na chats aka admit wanamahusianp via simu na huyo mtu yupo dar)
Najitahid kusummarise maana iliendelea mpaka siku moja nikaenda moro gafla nikakuta anachat nae bado na isitoshe kuna mwingine wa moro..nilimdunda hatari..tukasuluhishwa na familia baada ya hapo kila tukikwaruzana kidogo anakimbilia kusisitiza tuachane bwana ndo ukawa wimbo..
Sasa nikaona kuondoa usumbufu na yeye kuhamia dar aligoma kwakusema maisha nafuu moro..nikatafuta kaz moro nikahamia na mimi moro(nilipata kaz half the pay ya dar) ila nilimweleza la msingi tuwe pamoja tuweze nusuru ndoa
(Haya yote miezi miwili tu nilikuja na kupata kaz mwanzon wa mwaka huu )...
Sasa tangu tumeamua kukaa pamoja mambo hayajawa mepes mimi na cover basic needs kama kawaida yangu na napambana na biashara ila mwenzangu amekuwa amepotea kabisa kimapenz..tangu mwaka huu tunaweza kuwa tumesex si zaida ya mara 15 am sure..maana mwenzangu hayupo kabisa anaona nimembana sana kila kitu anatupia lawama nivomdundaga na matatizo ya nyuma..nimejitahid kumpa space sana ila naona kitu kidogo anakimbilia nataka talaka nk..
Sasa ilichonipelekea kuandika uzi huu..majuzi nilimwambia naenda dar maana alikua yupo moody sikujua mayb ni mimi au lah nikamwambia tu nasafar ya dar week nzima
Ase alifurahii sana ..safar ilikua ya siku mbili nikarejea jion namtafuta kwenye simu akawa hapokei alivyotoka kibaruani..jiran yetu ni mfanyakaz mwenzie akarud tukapishana nikamuiza vp shoga yako akasema tumeachana amesema anapita sokoni mara moja (nikaona very rare kutorud na shoga yake) wife akanitumia mesej akasema ametoka outing na shoga zake
Nikasema fine )
Mimi nikanyuti nje mtaa wa pili kuona nani angerudi nae (kuna gar ikaja ikapak kwa jirani ikakaa dak kama 15 akashuka afu gar ikaondoka )
Alivyoingia ndan nami nikamfwata kwa nyuma
Akashtuka sana..nikamuuliza nani akasema rafiki yake tu walienda pata wine)
Tukaingia nikamwambia naomba uwe makini tu kuna maradhi nk. Ila kama tumefikia huko naomba basi uwe na amani ufanye yako na si mbelen hapa kwangu..afu isitoshe tuna watoto wadogo usilete jazba kwenye haya mambo(maana tulivoingia ndani akaanza kuwaka kama simuamini alivyosema yupo outing nikamweleza outing sio issue ishu umetoka huko mkaweka kambi kwenye gar mie nawaona tu mnapiga story hamkumaliza huko outing)
To mypoint: nimegundua hana mapenz kwa sAsa ma amini nawaambia nimevumilia sana vituko vyake ila nawaza niwashirishe wazazi wake na wadhamini wetu nataka niwachukue wanangu nirudi dar nimpe nafasi tu
(Samahanini naandika kwa kuruka ila hadi naumia yani)
Note
-jaman mkewangu ananiuma sana kila nikikumbuka nilivyompata!mahusiano yetu nk...yeye ndo alikuwa kipaumbele kunitia sana moyo pale nilipokwama au kusita jambo..(hii naandika kwa majonz sana)
-umri wake haujazi 30 bado kuna mda naamin alingia ndoani akiwa mdogo sijui kuna mambo hajafanya nk..ila mimi ni mtu wa kuwa huru sana namwambiaga nishirikishe nikupe kibali sina hiyana wala nini..cha msingi ni imani tu kwamba hatavuka mipaka
-swala la uwezo sijalitilia uzito maana yeye binafsi anakaz na mshahara wake kwakwel huwa simgusiagi hata kidog anafanya atakavyo
Mimi nina nyumba dar ndo nimepangisha kuja kuishi naye huku
Inshort majukumu yangu nayajua na nayamudu
-swala la kitandani lilikuwa zuri tu sote tunafurahi nk. Mwaka huu lilianza kususa sua penz la kubembeleza yeye ata enjoy ila mpaka nimemuanda nimemkomvins mbona shuhuli
-kwa upande wangu sio mnywaji sana na anajua..nikinywa tu wine nikiwa nae ntajitahid kumueleza kiu yangu juu ya mambo ambayo hanitimizii hapo nae atarukia si uniache nk bas mkibishana atasema mlevi tatizo nk...
-unakuta weekend ndo tunakaa na kujadili mambo ila mara chache sana maana katkat ya week akirud home ye kachoka ni kula kulala tu
-mimi ni mwanadamu pia naweza kuwa namapunguf yangu ila all i know kuachilia mbali kila jambo nimekua nikijitahid kuomba msamaha napokosea nk. Ndugu zangu ndo wanaona nimekamatwa kwel kwel ila nakua najitahid niishi ki maadili mana mke mwenyew mmoja
Anapendeza namuhudumia nk ila kwa sasaa nimesali sana mpaka nimeona kama ni watoto hata nikisema nimpotezee nitahitaj kuwaona wanangu ambapo itapelekea nimwone labda na yeye nk kitu ambacho mda mwingi kinaniwia ngumu kuvunja familia
Ila nikisema nibebe watoto(namjua kwa sasa majibu yake atasema nenda nao tu la msingi tuachaneee nk) ntabeba ila nataka niombe nisinge penda kusikia pua yake na wakwe ndo watakua gia ya kuwaona nina taka full right ya wanangu nina uwezo wakulea vizur )
Yani naumia sana ila naona ndo best option kwa sasa
-kama hujaoa olewa na hujanielewa naomba nisikukwaze maana ntakusababishia povu
Mmm mkuu pole sana ila nakushauri kwa manufaa yako ww na watoto wako itisha kikao na cha wazazi pande mbili na kama umeamua kwa moyo wote kumuachamuache huyo mkeo kachanganywa na mambo ya kishua kishua ,pia angalia magonjwa mkuu nakihisi mwaaache aende mungu atakupa mke mwengine
 
unaona huwezi ku move on,

sababu memories za mkeo kuchepuka ziko still vivid,

trust me bro

wengi wamepitia hayo na wamepita salama

uchungu is understandable but time is the best healer....

Naona different emotions kwako,sad,angry, guilty

hio ni normal

ni mechanism ya ku deal na tatizo kama lako

Watoto wangebaki na mama yao,ila kama yuko irresponsible fanya jitihada uwachukue,sio upoteze mke na watoto..,

pole sana..
 
Mmm mkuu pole sana ila nakushauri kwa manufaa yako ww na watoto wako itisha kikao na cha wazazi pande mbili na kama umeamua kwa moyo wote kumuachamuache huyo mkeo kachanganywa na mambo ya kishua kishua ,pia angalia magonjwa mkuu nakihisi mwaaache aende mungu atakupa mke mwengine
mkuu to be honesy kila nikifikiria hii road naumiaga sana na niombe niwe imara kwa hili
Kuna siku nilikuta vyakujipimia ngoma anavyo..niliishiwa pozi kumuuliza nilisubir tupo outing tukiwa tume refresh nikamuuliza angependa tukapime sote maana nilikuta kachukua hatua mwenyew maana sijajua kama either mimi nilisababishia ahofie au yeye tu mwenyewe aliniuliza umeaza lin kupekua vitu vyangu..nikachoka
 
mkuu to be honesy kila nikifikiria hii road naumiaga sana na niombe niwe imara kwa hili
Kuna siku nilikuta vyakujipimia ngoma anavyo..niliishiwa pozi kumuuliza nilisubir tupo outing tukiwa tume refresh nikamuuliza angependa tukapime sote maana nilikuta kachukua hatua mwenyew maana sijajua kama either mimi nilisababishia ahofie au yeye tu mwenyewe aliniuliza umeaza lin kupekua vitu vyangu..nikachoka
Mkuu ninachosikitika binadamu wa sasa hawana tumaini na kuingia peponi,nakuomba uwe na moyo imara simama katika bwana mkuu ,achana nae mungu aktakuongoza ,nayajua maumivu ya mke sio siri mkuu .Wakati mwingine unajiona kama upo ndotoni
 
unaona huwezi ku move on,

sababu memories za mkeo kuchepuka ziko still vivid,

trust me bro

wengi wamepitia hayo na wamepita salama

uchungu is understandable but time is the best healer....

Naona different emotions kwako,sad,angry, guilty

hio ni normal

ni mechanism ya ku deal na tatizo kama lako

Watoto wangebaki na mama yao,ila kama yuko irresponsible fanya jitihada uwachukue,sio upoteze mke na watoto..,

pole sana..
Yani ndugu umeread direct through me clearly sana..naposhindwa mimi kumsoma sitaki kum judge careness yake kwa wanangu najua ipo safi..but i feel like tukimpq nafasi apitie ki phase anachopitia mwwnyew tu bila wanangu kum comfort her actions
I want her to sleep and wake up with her actions...
Yani nawazaga tu angesema tulee kwanza tuoane baadaye ila tumeoana na ndo nimeisha ladha sijui dah
 
Mkuu ninachosikitika binadamu wa sasa hawana tumaini na kuingia peponi,nakuomba uwe na moyo imara simama katika bwana mkuu ,achana nae mungu aktakuongoza ,nayajua maumivu ya mke sio siri mkuu .Wakati mwingine unajiona kama upo ndotoni
Aliniambia wewe saiz ndo wakumjua mungu
(Pindi namwambia tuombeane mema na mioyo yakufuta majonz niliyomsababishia kwenye kipigo)
 
Mkuu Wewe ni mwanaume shupavu sana..Hongera sana mke wako angejua amepata lulu asingeichezea.
Kiukweli ningekua Mimi ningeshaachana nae long time Ago!! Sitaki shida mimi kisa mwanamke ndo maana wanaume wengi wanafariki kabla ya wakati kwa mambo kama haya.
Mimi kukushauri Naomba Uachane nae ili awe huru Mara nyingi watu kama hawa Dunia ndo huwa inawafunza. mpe uhuru anaoutaka wewe sepa kafanye yako Akija siku maisha yamempiga Mfungie vioo kabisa usije ukamwonea huruma.
 
Back
Top Bottom