Ndoa miaka 11 naomba ushauri

Ndoa miaka 11 naomba ushauri

Ndugu zangu ambao mpo kwenye ndoa naombeni ushauri kabla sijafanya maamuzi yangu mwenyewe.

Nipo kwenye hii ndoa kwa miaka 11 ila mwanamke ambaye nilikutana nae alikuwa na mtoto tayari ila naomba niseme alikuwa mwenyewe na mtoto wa miaka 2 mwanaume wake alimkimbia, sasa baada ya hapo mwanaume wake wa zamani kufahamu huyu mwanamke ana mwanaume mwingine siku moja akaniambia kwamba huyu mwanamke huwezi kuja kumzalisha maisha yako yote hata iweje.

Ndugu zangu mpaka leo huyu mwanamke amepata mimba mara 3 ila zote zimetoka. Sasa baada ya hapo mwanamke akaanza kunidharau na kuniambia kwamba sina mbegu za kumzalisha. Me kama mwanaume nikapoteza confidence nikaenda kupiga nje na nimepata mtoto vizuri bila shida kabisa

Sasa amekuja kugundua kwamba me nimezaa nje ila nilivumilia mateso yote na maneno yote ya mateso na alikuwa muda wote ananidharau sana na kusema hata iweje umenikuta na mtoto na taka usitake siwezi kuacha kuongea na baba wa mtoto.

Akinikuta nakunywa anamwaga drinks zote kwenye sink.

Sasa jana usiku nimepigwa vyupa vibaya sana damu nyingi zimetoka sababu anataka tuwe tunatumia password moja, ameingia kwenye simu amekuta yule mwanamke mwingine mwenye mtoto amenitumia picha za mtoto.

Baada ya hapo akanitukania wazazi wote na kuwaita Idiots familia nzima pamoja na mimi...

Nilikuwa tu naomba ushauri nini cha kufanya ila tumeenda hospitali tumegundua zile mimba 3 alipata moja imeziba mirija yake ya uzazi so hawezi pata mimba kwa njia ya kawaida.

Naombeni ushauri wenu tafadhali kwa hili suala.

Je, bora niondoke?
Amekupasua na chupa, utaka ushauri gani mkuu? KIMBIA usigeuke nyuma tena.
 
Ni kweli kabisaa kabisa kama sasa hata unyumba hataki kunipa kabisaaa nikimuomba ila hapo kama ulivyosema inabidi ni remove hisia kabisaa hujakosea na hapo wametuzidi kwa kiasi kikubwa sana tena sana nakubaliana na wewe...
Nimejikaza nisicheke nimeshindwa 😹😹😹
Wabongo tunapenda chini, yani una matatizo bado unawaza kula papa..!!
 
Asante sana mkuu ndio hivyo nataka nifanye juzi wakati tumegombana mpaka akaniambia mwanaume alikuwa ana mtreat vizuri kuliko mimi....Hivi naongea nimerudi kutoka dubai ilikuwa birthday ya mtoto wake na wakati huyo mtoto ana baba yake ila mimi ndio nimetoa kila kitu na hela zote...
Achana nae mwanamke akishakupa reference ya mwanaume mwingine piga chini
 
HIvi uko katika ndoa hii kwa sababu gani? Unatukanwa, unatukaniwa wazazi wako, unapigwa na juu ya yote unalea mtoto sio wako! kinachokufanya uwe katika ndoa hii ni nini hasa? Unauliza kama ni bora uondoke? Hapana usiondoke baki hapo hapo uwe joke of the street na usubiri siku akupige kisu badala ya chupa!!!!!

Kaka najuta sana tena sanaaa sio kidogo.....Umeniambia kitu ambacho nashukuru sana tena sanaaaa...Najuta sio kidogo...
 
Kosa lilianza pale ulipooa single mama ivi kila siku hamuonagi nyuzi apa kuhusu single mama kuwa sio wa kuweka ndani ni wakuwala mbususu na kusepa
 
Daaah kaka kakupa na dharau huna uwezo wa kumzalisha halafu yeye anataka aendeleee kuwasiliana na baba wa mtoto ambaye sio wako🥲

Halafu anakunyanyasa kwa kukupiga tena na chupa basi mkuu wewe ni mpole sanaaaaa


USHAURI WANGU FANYA KILE UNACHOONA POA WEWE

Asantw sanaaa kaka nashukuru sanaa kaka...Wazazi na familia wote wameniambia ila sijasikiliza kabisaaaa ila sijasikiliza naahukuru sana tena sana sina mengi ya kusema ila ninayo mengi sanaaaaa....
 
Mkuu hui sio chai na why nidanganye sasa??hii ni kweli kabisa....Na amefanya kama mara kadhaa ila nimetulia sema nchi ambayo mipo nikimshika tu atakuwa amemaliza maisha yangu maana atawapigia police nitakuwa arrested na kuaribu kila kitu....
Uko nchi gani? Na kwanini umchekeee sasa kama hata unymba hupewiii achana nae
 
Mwambie aende kwa bwanaake we muoe huyo uliemzalisha.
 
HIvi uko katika ndoa hii kwa sababu gani? Unatukanwa, unatukaniwa wazazi wako, unapigwa na juu ya yote unalea mtoto sio wako! kinachokufanya uwe katika ndoa hii ni nini hasa? Unauliza kama ni bora uondoke? Hapana usiondoke baki hapo hapo uwe joke of the street na usubiri siku akupige kisu badala ya chupa!!!!!

Asante sana tena sanaa kaka hayo maswali yako ya kwanza umenisaidia na nashukuru sana sio kidogo asante sanaaa sasa nimeamkaaaa kiakili asamte sanaaaa....
 
Wazee walishaniambia tayari nirudi nyumbani mara kibao mungu anaona....Watu wengi wameniambia unacheza na maisha yako kuwa makini sanaaa....sema mpaka sasa nawaza ndoa tu....

Kenge kabisa wewe
 
HIvi uko katika ndoa hii kwa sababu gani? Unatukanwa, unatukaniwa wazazi wako, unapigwa na juu ya yote unalea mtoto sio wako! kinachokufanya uwe katika ndoa hii ni nini hasa? Unauliza kama ni bora uondoke? Hapana usiondoke baki hapo hapo uwe joke of the street na usubiri siku akupige kisu badala ya chupa!!!!!

Ndugu yangu mimi mwanaume na nashukukuru sana kaka....Nikiwa sijui ila sasa nashukuru sanaaa ushauri wako kaka umenipa moyo sana tena sanaaa sio kidogo...Asante sana....
 
Pndikizi. Hakuna mwanaume anaweza kueleza ama kufanyiwa haya uliyoandika. Hii ni stori ya kitunga

Mkuu ndio maisha yangu sina la kificha na mimi mtu mianifu nipo humu zaidi ya 17 years siwezi danganya kabisaa hata kidogo...Najuwa hujasema sanaa ila nashukuru sana...
 
Kama mzazi mwenzie alikupa onyo, ni vizuri ukamuacha huyo mwanamke ili kupunguza heka heka za hapa duniani. Ile kukupa onyo, kuna mazingaombwe yamefanyika kwa huyo mke. Nakushauri, muwekee mazingira akuache yeye, kisha oa huyo ulie zaa naye.
 
Asante sana tena sanaa kaka kwa ushauri wako nashukuru sana kwa kila kitu....Nadhani umesoma na kuelewa vizuri nini nimesema hapo....

Hapo kuhusu kumuuliza jamaa kuna siku moja tuligombana akaniamboa kwamba siku moja utakuja kunikumbula unadhani unamjuwa huyu mwanamke kunizidi mimi utakuja kunikumbuka siku moja ila sikujuwa anamaanisha nini.....

Kwa sasa tunapitia mambo mengi sana pia vile vile hatujafanikiwa kupata mtoto mpaka hivi sasa mungu hajaalia kabisa....Na watu wengi sana wanaongea vitu tofauti kila siku atakuka atasema ohhh nimeambiwa hivi na hivi mara hivi na hivi....

Maisha yamekuwa magumu sana tena sanaa na dharau imekuwa kitu cha kawaida kwa sasa....
We ukimuona jamaa hajui ku care?
 
Back
Top Bottom