Anusuriwe kabla kesi haijawa ngumu, mapenzi shikamoo!

Panctuality

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2019
Posts
1,155
Reaction score
1,736
Habari na poleni na uwajibikaji!

Kuna jirani yangu (Mtanzania) ndoa ya miaka 3 mpaka sasa, na alimuoa huyo mwanamke (raia wa Zambia) tayari mke akiwa na mtoto aliyezalishwa akiwa nyumbani kwa wazazi na mwanaume mwingine.

Wakiwa wameoana mtoto aliachwa kwa wazazi wa mwanamke, kufikia mwanzoni mwa mwaka 2025 (mwaka jana) mtoto alianza kuugua ugonjwa usiojulikana kwa maana ya kukosa matibabu sahihi japo si kwa uhaba wa pesa za matibabu, wazazi walimtaka baba mzazi wa mwenye mtoto amchukue mwanae naye akamhangaikie matibabu baada ya jitihada za matibabu kushindikana.

Isivyokawaida na cha kushangaza, mke akiwa kwenye ndoa yake alipewa taarifa na baba wa mtoto (mvuvi na raia wa Zambia) kuwa "Mama P njoo uchukue mzoga wako", aliambiwa hivyo si kwa maana ya tayari mtoto kuwa amefariki baada ya yeye kushindwa matibabu na lugha iliyotumika si rafiki na haifai.

Mke alimfuata mtoto wake na hatimaye kuja naye huku waishiko na mme wa ndoa, jirani yangu kwa huruma aliyokuwa nayo na mahusiano mazuri aliyokuwa nayo dhidi ya wakwe zake, jamaa amepambana iwe usiku iwe mchana, iwe jua iwe mvua na sehemu kubwa kama siyo yote ya fedha za malipo ya Ufundi ujenzi (yeye ni fundi) alizitosa kuokoa uhai wa mtoto wa mke wake, amethubutu kumpeleka mpaka hospital kubwa lakini bado hali ya mtoto haikuwa sawa, aliamua kuzifuata tiba mbadala zilizo na ramli chonganishi aliambiwa kuwa mtoto karogwa/ndagu kwa ajili ya baba yake mzazi kuwin kwenye uvuvi, na hatimaye mwezi October mwaka jana mtoto aliumaliza mwendo (R.I.P).

Baada ya mtoto kufariki mama alibadilika kabisa kitabia, hapiki, hatulii nyumbani na kuna muda anarudi asubuhi, hafui nguo za mmewe, hafanyi usafi wa mazingira hapo walipopanga na hata kumzalia tu mtoto kwa miaka 3 waliyoishi hayuko tayari. Kipigo mara kadhaa amekipokea na hajirekebishi japo kipigo sio suruhu. Mwanamke hajutii fedha nyingi alizozitoa kwa awamu tofauti kugharamia matibabu ya mtoto wake.
Majirani tunasikia tu mara anatembea na dreva bodaboda, mara maafisa usafirishaji wa stand yaani ni taflani tupu.

Baada ya kusimuliwa na jirani huyo leo hii nimeumia sana kwa anachopitia mwanaume mwenzangu, na hata mimi kutoa ushauri amtafutie nauli mguu kwa mguu amrudishe kwao japo si ushauri bora kwa wana ndoa kuachana lakini enough is enough!!

Wanaosema hii chai tupilia uko na tuwapuuze! kinachotakiwa ni kushare mawazo namna bora ya kufanya kumnusuru huyu jirani, muda huu tena mkewe katoka kaenda anakoshinda, na marafiki zake inasemekana ni wauza bar, grocery na wahudumu wa guest houses.
Jamaa alipanga leo akifika amtupie kila kilicho chake nje ajiendee kwao lakini tumempoza kuwa asifanye hivyo bali ampeleke kwao ili kuepuka kesi ya wazazi kudai kupotelewa na mtoto wao akiwa kwa mme.

Ndoa ngumu jamani japo sisi wenye wake wawili hayatufiki haya.

Vijana sishauri mkatae ndoa kwa kuhofia hizi changamoto, oeni tu ila kwa kufanya upembuzi wa kina kwa kufuatilia historia ya ukweni kwao endapo kama ni familia zenye maadili au laah!
 
Hatari sana

Pole yake kama ni kweli

Mwanaume usioe asiyekupenda utajuta

Mapito mazito haya
Mwanzo mwanamke alionekana ana upendo usio na kifani, lakini kwa sasa loooh!
Nimemcheki muda fulani huyo mwanamke kama karogwa hivi, sijui pepo la ngono hili! Duuh
 
Wanandoa wengi wanapitia unyama ndani ya ndoa….tena bora mwanamke atapiga kelele ila mwanaume anakufa kiume 😭

Ee Mwenyezi Mungu nilindie wanangu 🙏🏽
So sad! Unajua mwanaume mpaka ifikie hatua anamsimulia mtu mwingine, ujue kavumilia mpaka yamemshinda kabisa.
 
Aisee pole yake jirani yako
Ila sielewi nini kinachomfanya mpka sasa hajamrudusha kwao huyo mwanamke ni kitu gani hasa mapenzi?

Au anahisi atabadilika?
Hii issue ya kuogopa kuanza moja baada ya kushindwana inawatesa wengi

Kwa tabia za huyo mwanamke hakuna sababu yoyote huyo mwanaume kumvumilia mpaka dakk hii
 
Kateseka muda mrefu leo kaona vyema anipe mkanda, kutwa amekuwa mtu wa kushinda kiakili akiwa hayuko sawa kabisa.
 
Mwambie watu kwenye maisha hua wanakuja na kuondoka

Kama vile masika na kiangazi
Asing'ang'anie kupandisha maji mlima

Mwishoni mwa maongezi mwambie asikilize moyo wake na umwambie utamuunga mkono kwa maamzi yake na kuyaheshimu
 
Pole yake, ni huzuni hakika, ajivue gamba tu hakuna namna ni vyema kwake na ustawi wake binafsi, inaonekana baada ya kupata trauma huyo mwanamke ameamua kuonyesha makucha yake halisi, inasikitisha sana
Wanawake wa Zambia ni jinamizi kweli kweli japo si wote lakini asilimia kubwa ni mapicha picha tu.
 
Ni
Habari na poleni na uwajibikaji!

Kuna jirani yangu (Mtanzania) ndoa ya miaka 3 mpaka sasa, na alimuoa huyo mwanamke (raia wa Zambia) tayari mke akiwa na mtoto aliyezalishwa akiwa nyumbani kwa wazazi na mwanaume mwingine.

Wakiwa wameoana mtoto aliachwa kwa wazazi wa mwanamke, kufikia mwanzoni mwa mwaka 2025 (mwaka jana) mtoto alianza kuugua ugonjwa usiojulikana kwa maana ya kukosa matibabu sahihi japo si kwa uhaba wa pesa za matibabu, wazazi walimtaka baba mzazi wa mwenye mtoto amchukue mwanae naye akamhangaikie matibabu baada ya jitihada za matibabu kushindikana.

Isivyokawaida na cha kushangaza, mke akiwa kwenye ndoa yake alipewa taarifa na baba wa mtoto (mvuvi na raia wa Zambia) kuwa "Mama P njoo uchukue mzoga wako", aliambiwa hivyo si kwa maana ya tayari mtoto kuwa amefariki baada ya yeye kushindwa matibabu na lugha iliyotumika si rafiki na haifai.

Mke alimfuata mtoto wake na hatimaye kuja naye huku waishiko na mme wa ndoa, jirani yangu kwa huruma aliyokuwa nayo na mahusiano mazuri aliyokuwa nayo dhidi ya wakwe zake, jamaa amepambana iwe usiku iwe mchana, iwe jua iwe mvua na sehemu kubwa kama siyo yote ya fedha za malipo ya Ufundi ujenzi (yeye ni fundi) alizitosa kuokoa uhai wa mtoto wa mke wake, amethubutu kumpeleka mpaka hospital kubwa lakini bado hali ya mtoto haikuwa sawa, aliamua kuzifuata tiba mbadala zilizo na ramli chonganishi aliambiwa kuwa mtoto karogwa/ndagu kwa ajili ya baba yake mzazi kuwin kwenye uvuvi, na hatimaye mwezi October mwaka jana mtoto aliumaliza mwendo (R.I.P).

Baada ya mtoto kufariki mama alibadilika kabisa kitabia, hapiki, hatulii nyumbani na kuna muda anarudi asubuhi, hafui nguo za mmewe, hafanyi usafi wa mazingira hapo walipopanga na hata kumzalia tu mtoto kwa miaka 3 waliyoishi hayuko tayari. Kipigo mara kadhaa amekipokea na hajirekebishi japo kipigo sio suruhu. Mwanamke hajutii fedha nyingi alizozitoa kwa awamu tofauti kugharamia matibabu ya mtoto wake.
Majirani tunasikia tu mara anatembea na dreva bodaboda, mara maafisa usafirishaji wa stand yaani ni taflani tupu.

Baada ya kusimuliwa na jirani huyo leo hii nimeumia sana kwa anachopitia mwanaume mwenzangu, na hata mimi kutoa ushauri amtafutie nauli mguu kwa mguu amrudishe kwao japo si ushauri bora kwa wana ndoa kuachana lakini enough is enough!!

Wanaosema hii chai tupilia uko na tuwapuuze! kinachotakiwa ni kushare mawazo namna bora ya kufanya kumnusuru huyu jirani, muda huu tena mkewe katoka kaenda anakoshinda, na marafiki zake inasemekana ni wauza bar, grocery na wahudumu wa guest houses.
Jamaa alipanga leo akifika amtupie kila kilicho chake nje ajiendee kwao lakini tumempoza kuwa asifanye hivyo bali ampeleke kwao ili kuepuka kesi ya wazazi kudai kupotelewa na mtoto wao akiwa kwa mme.

Ndoa ngumu jamani japo sisi wenye wake wawili hayatufiki haya.

Vijana sishauri mkatae ndoa kwa kuhofia hizi changamoto, oeni tu ila kwa kufanya upembuzi wa kina kwa kufuatilia historia ya ukweni kwao endapo kama ni familia zenye maadili au laah!
Nice men endeleeni kupigika kisawasawa maana kenge huwa hawasikii hadi damu ziwatoke.

Ubinadamu ni kazi - the humanity is work.
 
Wazazi wako wasingeoana na kuzikabili changamoto za ndoa wewe ungezaliwa?
Ondoa uzwazwa wako hapa, bichwa kubwa akili kisoda.
Ukiona hayakuhusu si lazima u-reply na hujashikiwa bunduki ku-reply.
 
Shushia bilauri moja ya maji ya kunywa ya bariiidi kuepukana na BP za kipuuzi.

Back
Top Bottom