Ndoa miaka 11 naomba ushauri

Ndoa miaka 11 naomba ushauri

Iwe ni chai au true story, hivi inakuaje kuaje hadi mkeo anakupiga??? Labda kama ni vile vimakofi vya kimahaba🥰

Mkuu hui sio chai na why nidanganye sasa??hii ni kweli kabisa....Na amefanya kama mara kadhaa ila nimetulia sema nchi ambayo mipo nikimshika tu atakuwa amemaliza maisha yangu maana atawapigia police nitakuwa arrested na kuaribu kila kitu....
 
Andaa jeneza lako tuje kukuzika kama hutaki kuondoka, Umelogwa, rudi kwenu Huko kakae na Wazee wako au kama ni muumini mzuri omba Mungu.

Wazee walishaniambia tayari nirudi nyumbani mara kibao mungu anaona....Watu wengi wameniambia unacheza na maisha yako kuwa makini sanaaa....sema mpaka sasa nawaza ndoa tu....
 
Kuamini kwamba anaweza kubadilika na kumuonea sana huruma ndipo kunafanya wanaume tunapata maumivu makali kwa mwanamke.

Ni kweli kabisaa na mimi ndio nipo hapo sasa hivi mkuu hivyo unavyosema upo sawaa kabisaa huyo ndio mimi kwa sasa....Huruma huruma....ila yeye hakuwa na huruma na mimi kipindi napitia matatizo yote hii miaka yote....
 
Pndikizi. Hakuna mwanaume anaweza kueleza ama kufanyiwa haya uliyoandika. Hii ni stori ya kitunga

Asante sana mkuu nimeambiwa mda mrefu ila sijasikiliza kabisaa ushauri nimepewa nashukuru sana na hamna neno kabisaa....Nitaufanyia kazi na nitarufi tena...
 
Ushauri wangu ni uachane na huyo mwanamke vinginevyo mpo kwenye hatari kubwa sana ya kudhuriana.

Asante sana mkuu ndio hivyo nataka nifanye juzi wakati tumegombana mpaka akaniambia mwanaume alikuwa ana mtreat vizuri kuliko mimi....Hivi naongea nimerudi kutoka dubai ilikuwa birthday ya mtoto wake na wakati huyo mtoto ana baba yake ila mimi ndio nimetoa kila kitu na hela zote...
 
Wewe ndio mpumbavu, mpaka unakuja kuomba ushauri kitu ambacho maamuzi yanajulikana, na ndio maana anakutukana anajua huna maamuzi

Mi kweli kabisaaa na nimejuwa hicho kitu anasema muda wote weka maamuzi nijue nini unataka tena kwa dharau sana tena sanaaaa...
 
Aiseee, pole

So unampenda sana au mnapendana sanaaa bado?

Ningekuwa na Kaka, akakutana na yako ningemwambia aende akaishi mbali naye. Ila why bado unauliza na kupitia yote ya kuwa na mume mwenza pia? Unataka kuzikwa mapema? Ndoa yako imekufa zamani..shirikisha ndugu zako usione aibu wakuambie sababu wanakujua wewe... ila duh

Kama hauna maamuzi Sali usubiri maono ufanyaje..

Kila tukigombana anasema ndoa imeisha mda mrefu sana kama sijui basi nijue sasa ndio alivyosema yeye.....Sasa hata unyumba hatoi tena anakataa kabisaa...Anasema anajuta hata baba wa mtoto wake alikuwa ana mtreat vizuri kuliko mimi....Na jamaa alikuwa anampiga vibaya sanaa sio kidogo.....ila amejaribu kwangu na ni professional nikimgusa ataniharibia kazi ambayo nafanya....
 
Ndugu zangu ambao mpo kwenye ndoa naombeni ushauri kabla sijafanya maamuzi yangu mwenyewe.

Nipo kwenye hii ndoa kwa miaka 11 ila mwanamke ambaye nilikutana nae alikuwa na mtoto tayari ila naomba niseme alikuwa mwenyewe na mtoto wa miaka 2 mwanaume wake alimkimbia, sasa baada ya hapo mwanaume wake wa zamani kufahamu huyu mwanamke ana mwanaume mwingine siku moja akaniambia kwamba huyu mwanamke huwezi kuja kumzalisha maisha yako yote hata iweje.

Ndugu zangu mpaka leo huyu mwanamke amepata mimba mara 3 ila zote zimetoka. Sasa baada ya hapo mwanamke akaanza kunidharau na kuniambia kwamba sina mbegu za kumzalisha. Me kama mwanaume nikapoteza confidence nikaenda kupiga nje na nimepata mtoto vizuri bila shida kabisa

Sasa amekuja kugundua kwamba me nimezaa nje ila nilivumilia mateso yote na maneno yote ya mateso na alikuwa muda wote ananidharau sana na kusema hata iweje umenikuta na mtoto na taka usitake siwezi kuacha kuongea na baba wa mtoto.

Akinikuta nakunywa anamwaga drinks zote kwenye sink.

Sasa jana usiku nimepigwa vyupa vibaya sana damu nyingi zimetoka sababu anataka tuwe tunatumia password moja, ameingia kwenye simu amekuta yule mwanamke mwingine mwenye mtoto amenitumia picha za mtoto.

Baada ya hapo akanitukania wazazi wote na kuwaita Idiots familia nzima pamoja na mimi...

Nilikuwa tu naomba ushauri nini cha kufanya ila tumeenda hospitali tumegundua zile mimba 3 alipata moja imeziba mirija yake ya uzazi so hawezi pata mimba kwa njia ya kawaida.

Naombeni ushauri wenu tafadhali kwa hili suala.

Je, bora niondoke?
HIvi uko katika ndoa hii kwa sababu gani? Unatukanwa, unatukaniwa wazazi wako, unapigwa na juu ya yote unalea mtoto sio wako! kinachokufanya uwe katika ndoa hii ni nini hasa? Unauliza kama ni bora uondoke? Hapana usiondoke baki hapo hapo uwe joke of the street na usubiri siku akupige kisu badala ya chupa!!!!!
 
Ndugu zangu ambao mpo kwenye ndoa naombeni ushauri kabla sijafanya maamuzi yangu mwenyewe.

Nipo kwenye hii ndoa kwa miaka 11 ila mwanamke ambaye nilikutana nae alikuwa na mtoto tayari ila naomba niseme alikuwa mwenyewe na mtoto wa miaka 2 mwanaume wake alimkimbia, sasa baada ya hapo mwanaume wake wa zamani kufahamu huyu mwanamke ana mwanaume mwingine siku moja akaniambia kwamba huyu mwanamke huwezi kuja kumzalisha maisha yako yote hata iweje.

Ndugu zangu mpaka leo huyu mwanamke amepata mimba mara 3 ila zote zimetoka. Sasa baada ya hapo mwanamke akaanza kunidharau na kuniambia kwamba sina mbegu za kumzalisha. Me kama mwanaume nikapoteza confidence nikaenda kupiga nje na nimepata mtoto vizuri bila shida kabisa

Sasa amekuja kugundua kwamba me nimezaa nje ila nilivumilia mateso yote na maneno yote ya mateso na alikuwa muda wote ananidharau sana na kusema hata iweje umenikuta na mtoto na taka usitake siwezi kuacha kuongea na baba wa mtoto.

Akinikuta nakunywa anamwaga drinks zote kwenye sink.

Sasa jana usiku nimepigwa vyupa vibaya sana damu nyingi zimetoka sababu anataka tuwe tunatumia password moja, ameingia kwenye simu amekuta yule mwanamke mwingine mwenye mtoto amenitumia picha za mtoto.

Baada ya hapo akanitukania wazazi wote na kuwaita Idiots familia nzima pamoja na mimi...

Nilikuwa tu naomba ushauri nini cha kufanya ila tumeenda hospitali tumegundua zile mimba 3 alipata moja imeziba mirija yake ya uzazi so hawezi pata mimba kwa njia ya kawaida.

Naombeni ushauri wenu tafadhali kwa hili suala.

Je, bora niondoke?
Daaah kaka kakupa na dharau huna uwezo wa kumzalisha halafu yeye anataka aendeleee kuwasiliana na baba wa mtoto ambaye sio wako🥲

Halafu anakunyanyasa kwa kukupiga tena na chupa basi mkuu wewe ni mpole sanaaaaa

USHAURI WANGU FANYA KILE UNACHOONA POA WEWE
 
Back
Top Bottom