Semenya
JF-Expert Member
- Sep 5, 2009
- 572
- 51
Nimeipenda hii line of thought, na ingekuwa bora kuiangalia vizuri. Swali la Ufadhili wa vyama vya siasi ni muhimu sana katika nchi inayofuata mfumo wa demokrasia. Ishu inakuja hasa kwenye swali la wafadhili na remuneration. Mara nyingi wafadhili watapenda kupata something in return na ndio kilicholeta hili swali la kwanza...
Jibu la Balantanda ni zuri lakini limeacha mengi wazi...
Kwa mfano: Je ni haki ya mfadhili kuwa remunirated? Na kama ni haki/sawa, ni remuniration gani inayokubalika?
Umejibu swali kwa kusema jirani(CCM) anafanya, hivyo ni haki kwa Chadema nao kufanya hivyo. Okay...Lakini katika jibu umeingiza neno UFISADI. This takes the conversation katika direction nyingine.
Kwanza, kwangu mimi neno UFISADI = the use of public funds for private benefit. Hivyo katika jibu lako, ume-imply kuwa ni haki kuwarudishia Wafadhili chao hata kama itafikia kiwango cha kuwapa Mali ya Umma. Nadhani hapo tunakuwa tumevuka mpaka. Kuendesha vyama vya siasi ina cost kubwa, na ndio maana kila chama kina power base yake, ambayo kwa mara nyingi ndio wafadhili wao. Kwa mfano katika nchi zilizoendelea kisiasi, unakuta chama chenye policies za kibepari huwa na wafadhili wengi kutoka watu wa business class - yani watakao faidi matunda ya policies za chama. Hivyo hii relationship kati ya Chama na Wafadhili inakuwa ipo katika level ya 'strach my back and i will scratch yours'. Lakini relationship hii inafikia kikwamo pale Chama kitakapotumia Mali ya Umma katika kuwa-remunerate Wafadhili. Nadhani jibu la MWJJ limeongelea hichi:
comment of the weekvyama vyote vya siasa duniani vina wafadhili wake, na ndio wafadhali wakubwa wana sauti zaidi kwenye vyama hivyo na huzawadiwa nafasi mbalimbali tena kwa uwazi. Lakini kwenye nchi za kidemokrasia mfadhili ni lazima awe yule ambaye hana tuhuma za ufisadi au uvunjaji wa sheria au kuhusishwa na mambo yaliyo kinyume. Ndio maana kwenye nchi kama Marekani mfadhili akigundulika kuwa si "msafi" mgombea au kiongozi hulazimika kurudisha ufadhili wake![/quote]
Solution ya hili tatizo:
1. Kuweka expenditure limits katika kampeni
2. Ku-fund Vyama vya Siasi kwa pesa ya Umma pekee.
3. Kuweka hesabu za vyama wazi kwa lengo la kujua wafadhili wao, na kuweka heavy penalties kwa vyama vitakavyoficha hesabu kwa mfano kushindwa kushiriki katika uchaguzi mkuu ujao, nk.
Kuchukulia hili swala ki-lele mama ni kuonyesha kutokukomaa kisiasi. Ni wazi kuwa Wafadhili ni watu muhimu sana, hasa ukizingatia gharama za kuendesha vyama, na cost za kampeni. Lakini, kesho kutwa mtoto wa Ndesa akipewa Contract ya ku-supply umeme, nk nchi nzima, msishangae. Kwa maoni yangu, hii ndio mbegu ya Ufisadi. Na tukikaa kimya ni kuipalilia. Kama kutakuwa na uwazi na uwezo wa ku-trace hizi relationship, itakuwa step kubwa sana ya kupambana na Ufisadi.
stunning
safi sana