Maamuzi ya Azimio la Mtwara yatakuwa kama yale ya 2019

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,705
36,154
Kitendo kilichofanyika 2019 na 2020 kilinifanya Mimi niione CHADEMA kama chama chenye viongozi matapeli wa kisiasa.

Ni kikundi cha upigaji tu chenye kuangalia maslahi ya viongozi kwanza kisha maslahi ya Taifa inafuatia nyuma.

Ilikuwa 2019 ambapo CHADEMA iliweka Azimio la kugomea uchaguzi wa serikali za mitaa kutokana na rough za wazi zilizofanywa na serikali kwa mgongo wa CCM, pia Sheria za uchaguzi ambazo ni kitanzi kwa chama chochote pinzani. Lakini 2020 kwa Sheria zilezile, kwa CCM ileile, kwa viongozi walewale CHADEMA bila aibu wakaingia kwenye uchaguzi mkuu ingawa nako walupigwa za uso.

Leo nasikia viongozi wa CHADEMA wanajifungia Mtwara kujadili masuala mbalimbali likiwemo la uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mwaka huu.

Kwa akili zangu hizi za kawaida na uzoefu wa siasa za Tanzania CHADEMA watatoa Azimio la kutokushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa miezi michache ijayo mwaka huu 2024.

Ikumbukwe viongozi hawa wengi watakwenda kugombea ubunge 2024 na wengine waligombea 2020.

Uchaguzi wa serikali za mitaa hauwagusi hawa viongozi maana ndoto zao ziko kwenye level ya ubunge, uwaziri na kuendelea.

CCM itachukua mitaa yote katika uchaguzi huu baada ya CHADEMA kususa.

Lakini 2025 kwa sheria hizi hizi viongozi hawa wataondoa vipingamizi na kusema tutashiriki tu kwa damu na kwa jasho.

Kwa hali hii Watanzania wataendelea kuteseka miaka mingi chini ya CCM.

Hakuna chama cha kuindoa CCM, maana watu wanaodhaniwa huenda wanaweza kuthubutu nao wanatanguliza ubunge.
 
Kwa nini usishiriki wewe kuitoa ccm madarakani hadi uilaumu CDM? Wewe umefanya nini kutimiza wajibu wa kuipigania Tz iliyo njema?
 
CHADEMA

CHADEMA inastahili lawama kwasababu inaishi na kulipana mishahara kwa Kodi zetu!!

Mnataka tukae kimya wakati Ruzuku ambazo ni fedha za umma mnazitafuna kama mchwa? Puuzi kabisa
 
Back
Top Bottom