Ndesamburo anunua helkopta za kampeni Chadema

vyama vyote vya siasa duniani vina wafadhili wake, na ndio wafadhali wakubwa wana sauti zaidi kwenye vyama hivyo na huzawadiwa nafasi mbalimbali tena kwa uwazi. Lakini kwenye nchi za kidemokrasia mfadhili ni lazima awe yule ambaye hana tuhuma za ufisadi au uvunjaji wa sheria au kuhusishwa na mambo yaliyo kinyume. Ndio maana kwenye nchi kama Marekani mfadhili akigundulika kuwa si "msafi" mgombea au kiongozi hulazimika kurudisha ufadhili wake!

hata kwenye kampuni mwenye hisa kubwa ndio mwenye sauti ati. . . .
Muhimu kusiwa na nia mbaya katika ufadhili huo. Ndio maaana hata mabalozi wetu wakikohoa mkulo anatetemeka. Money talks bwana. . .
 
elewa kwanza ndo ukoment mkuu
nimetumia kigezo hicho cha albino kuwa ndo current problem ya TZ kuliko helkopta
kila chama cha upinzani kina sera nzauri tatizo kuzitekeleza
Mbona chadema ni chama cha demokrasia lakini ndani hamna demokrasia?

Nafikiri una-matatizo kidogo kwenye kuprocess taarifa....yani huelewi kabisaaaaaa! Naona error code tu kwenye posts zako, hamna kitu.

Fisadi ni nani? Ndesa yupo kwenye list yako a mafisadi??---- mfanyabiashara ambaye hana record chafu

CCM ilinunua magari (walifadhiliwa na mafisadi)- Mahandra kutoka India kwenye kampeni za 2005, magari kibao tu, kila wilaya nafikiri ilipata gari mbili. Kwa nn wasingejenga health centres au hata dispensaries vijijini? haikuwa kazi yao, hiyo ni kazi ya serikali......kama chama, wanahitaji kujiimarisha.

kama hujaelewa mpaka hapo sijui tukusaidiaje!
 
huu nao ukweli eti. think people, think.

kwa hiyo chama kiendeshwe kwa fedha ya kadi sh 1000 sijui? au wafadhili wawe nguruwe kwasababu hatuwezi kuwapa nafasi za upendeleo, labda tuwale tu!!

do you have problems with thinking?
 
Nafikiri huyo mzee kama kweli anataka kuki imarisha chake ni vizuri akaanza kukifadhili chama chake kuanzia ngazi za nchini!sina uhakika sana ni mikoa mingapi chadema wana usafiri wa gari,lakini kwa uelewa wangu wa baadhi ya mikoa chadema haina hata ofisi achilia mbali usafiri wa watendaji wake!ni vizuri hizo pesa za helkopta angewanunulia watendaji wa mikoa magari au hata piki piki waweze kufanya kazi zao kiufanisi zaidi!

Uendeshaji wa hizo helkopta zina gharama sana pia zitatumiwa kwenye kampeni baada ya hapo zitasimama tu!Kuna mtendaji mkuu mmoja wa Chadema alifanya ziara mkoa mmoja alipelekewa kusaini kitabu cha wageni hotelini kwa kuwa mkoa huo hauna ofisi!!!

Chadema ikiwa wanataka kukiimarisha chama chao ni bora wawe na vitendea kazi kuanzia wilaya mpaka mikoa!Viongozi wakuu wanatumia usafiri wa Helkopta huku katibu wa wilaya au mkoa hana hata baiskeli kuwafikia wanachama wake au hata wapiga kura!!!Watendaji hawana hata chumba cha ofisi kufanyia kazi za chama sijui huwa wanawasiliana vipi na makao makuu ya chama chao!au wanatumia Simu za Mikononi na sms!!!

Hapa tunamzungumzia Ndesamburo kanunua helkopta kwa ajili ya CHADEMA soma hiyo headline vizuri ili uache kujibu PUMBA.

Na suala la Helikopta kuwa mali yake asingeuambia umma kuwa amewanunulia CHADEMA....tena zitaanza kutumika uchagani. Huoni kama ni coincidence....hiki cha kilichokuwa kikijulikana kama "Chaga Development Man" au hukumbi ile kashfa ya ukabila kujaa kwenye hiki chama.

Ndesa amenunua helikopta yake hajainunulia CHADEMA helikopta. Amenunua helikopta kwa ajili ya kufanya biashara. Hamna Commercial company hapa Tanzania ya kukodisha helikopta, hii ya Ndesa ndio ya kwanza. Ilikuwa ukitaka kukodisha helikopta lazima uende SA au Kenya, na rates zina double unapoitoa nje ya nchi.

Wakati wa kampeni Ndesa anaweza aitoe bure kwa CHADEMA au aikodishie kwa bei nafuu. Helikopta inaingia leo, zimebaki siku chache za Kampeni hiyo helikopta itafikaje huko Kusini? Hata angependa kwenda huko logistics zinagoma.

Wewe bila shaka unahitaji msaada wa kitaalam zaidi.....Hoja yangu iko hivi, hakuna asiyejua kuwa CHADEMA imejijenga sana huko juu, ingekuwa busara kama wangetumia rasilimali hiyo kujenga ngome nyingine ya kushambulia mwaka 2010. Ni sawa na Tajiri anaeamua kumsaidia tajiri mwenzie labda anajua atafaidika pia.

Ndesamburo ni mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Kilimanjaro. Priority yake ya kwanza kama mwenyekiti wa mkoa ni kujenga chama katika mkoa wake. CHADEMA kina mbunge mmoja tu wa kuchaguliwa kutoka Kilimanjaro. Ni busara zipi hizo unazozizungumzia?

So if you want to continue with your silly debate be my guest. My point is not chaga people rather sharing of part cake equally kama ilivyotakiwa gawiwo la ruzuku ya chama hicho ambacho robo tatu ya wabunge wanatoka huko na kalibia wabunge wote wa viti maalum nao wa huko huko ukimtoa Mhe. Mhonga.

Zaidi ya hapo, nitakuona ni MGOGORO tu.

Kwa taarifa yako wabunge wa kuchaguliwa wa CHADEMA ni mmoja tu ambaye ni mchagga - Ndesamburo. Arfi anatoka Mpanda, Mwera anatoka Tarime, Zitto anatoka Kigoma na Slaa anatoka Karatu. Kwa viti maalum - Halima Mdee sio mchaga, ni Mpare na Mama Maulidah Komu alikuwa mgombea mwenza kwa tiketi ya urais 2005. Hivi mpaka leo bado hujui kuwa mgombea mwenza lazima awe anatoka visiwani? Au utasema Tume ya uchaguzi iliipendelea CHADEMA?

.
 
Wakuu ile programme ya online registration and support iko wapi? Chadema tupeni upadates please. Tuna hamu nayo

Namba ni 15710. Sasa hivi inafanya kazi kwa mitandao ya Zain na Vodacom. Tigo na Zantel wataunganishwa baada ya muda sio mrefu.

.
 
Namba ni 15710. Sasa hivi inafanya kazi kwa mitandao ya Zain na Vodacom. Tigo na Zantel wataunganishwa baada ya muda sio mrefu.

.

Kampeni zenu mnaanza lini kwenye huu uchaguzi serikali za mitaa?? sijawaona kabisa, mitaani naona wale wa kijani wanapepea, vipi tupe programme tuwaunge mkono hiki ndo chama mbadala.
 
Ndesamburo tangu zamani hajaonyesha kusaidia watu wake kiufisadi. Wagomvi wake ndio wanadai hayo ya ufisadi. Kila kilicho chema kina gharama. Kama tunataka TZ iwe na vyama mbadala vyenye nguvu ni lazima watu kama kina Ndesamburo wawepo ilhali wanao uwezo kusaidia. Sasa na kina nanihii (Bajaji?) wanaochota pesa ya umma na kuipeleka mabenki ya nje, ndio sampuli tuitakayo?

Ubarikiwe tu Ndesamburo, kelele za wapita njia hazimnyimi usingizi mwadhini.

Leka
 
Nafikiri una-matatizo kidogo kwenye kuprocess taarifa....yani huelewi kabisaaaaaa! Naona error code tu kwenye posts zako, hamna kitu.

Fisadi ni nani? Ndesa yupo kwenye list yako a mafisadi??---- mfanyabiashara ambaye hana record chafu

CCM ilinunua magari (walifadhiliwa na mafisadi)- Mahandra kutoka India kwenye kampeni za 2005, magari kibao tu, kila wilaya nafikiri ilipata gari mbili. Kwa nn wasingejenga health centres au hata dispensaries vijijini? haikuwa kazi yao, hiyo ni kazi ya serikali......kama chama, wanahitaji kujiimarisha.

kama hujaelewa mpaka hapo sijui tukusaidiaje!
UNAVYOMTETEA HUYO NDESAMBURO SIYO FISADI, JE SIKU MAFILE YAKE YATAKAPOTOKA NA KUJULIKANA YEYE NI FISADI UTASEMAJE?
ACHA USHABIKI KIJANA
NANI ALIJUA KUWA MENGI KAKOPA MIAKA HIYO HELA ZA WANANCHI MPAKA LEO AJARUDISHA?
ME KWA NDESA KUWA NI FISADI AU SI FISADI SIWEZI SEMA LOLOTE KWANI WATU TULIOWAFIKIRIA KUMBE SIO NA TUSIOWAFIKIRIA KUMBE NDIO WENYEWE

KUHUSU TYPING ERROR computer yangu imeingia kirusi

teh teh thh thh teh
 
JF imejaa viroja kweli.

Kukopa pesa ni ufisadi? Yaani so far hiki ndicho ccm mnaweza kuja nacho?

Kwamba ccm inaiba pesa za wananchi --- mzee chenge ni kiongozi wa juu kabisa wa ccm --- inalinganishwa na mwanaccm mwingine (mengi) aliyekopa na akachelewa kurudisha?!
 
je helkopta ni muhim sana, na inahitajika kwa kampeni za serikali za mitaa? fedha izo zingesaidia albino wangapi waliokatwa mkono? yatiima wangapi? au hata shule ya kuwahifadhi albino wasome kwa amani?
sio eti kwaajili CCM inawafadhili mafisadi wanapotumia pesa vibaya basi napo Wafadhili wa CHADEMA nao watumie pesa vibaya....to me kama anauchungu wa taifa lake ondoa hizo hospitali nk, kuna mambo mengi kwa sasa angechangia ningefrahi zaidi ya hizo helkopta hususan asaidie walemavu wanaoishi kwenye mazingira ya shida sana

Tuache kupanga bajeti ya fedha zilizo kwenye mifuko ya watu wengine.
Sisi fedha zetu tumezitumiaje kusaidia hao albino wapate walau kikombe cha chai bila mkate kila asubuhi? Au hata hicho kikombe kimoja cha chai ni aghari sana kwetu?
Matumizi mazuri ya fedha ni kutatua matatizo yanayoonekana? au ni kung'oa mzizi wa kuyaneemesha matatizo?
Walemavu wanaoishi kwenye mazingira ya shida watasaidiwa tu endapo mfumo uliopo utatupwa jalalani na jamii yote kukubali kwamba matatizo mengi tuliyo nayo ni matokeo ya uhalibifu wa makusudi wa taratibu za kiserikali na kijamii tulio ulea na kuuenzi kwa miaka mingi sana.

Mshangao wako ni sawa na kumshangaa mkulima akifukia gunia zima la mbegu za mahindi na maharage ardhini kwa kisingizio cha kuzipanda wakati wa msimu wa kilimo huku familia yake ikishindia uji tu. Kwa nini asipike kande kile akiitacho mbegu ili wanae wajichane na kujaza matumbo yao??
 
JF imejaa viroja kweli.

Kukopa pesa ni ufisadi? Yaani so far hiki ndicho ccm mnaweza kuja nacho?

Kwamba ccm inaiba pesa za wananchi --- mzee chenge ni kiongozi wa juu kabisa wa ccm --- inalinganishwa na mwanaccm mwingine (mengi) aliyekopa na akachelewa kurudisha?!
mengi sio kama kakopa kachelewa, ni HAJARUDISHA MKOPO MPAKA SASA
mimi siisemei CCM wao wamesha chemsha kwenye hilo swala la ufisadi
kuhusu ndesa vyanzo vyake vya mapato hatuvijui so tukae kimya kuliko kumdeclare sio fisadi..
 
Mzee Ndesa si fisadi.
Welcome to JF Semenya naona umejiunga juzi juzi tu.
 
mengi sio kama kakopa kachelewa, ni HAJARUDISHA MKOPO MPAKA SASA
mimi siisemei CCM wao wamesha chemsha kwenye hilo swala la ufisadi
kuhusu ndesa vyanzo vyake vya mapato hatuvijui so tukae kimya kuliko kumdeclare sio fisadi..

Mkuu Semenya vipi tena?

Mbona unaamuru watu hapa cha kusema na/au cha kutosema? Kwa nini unataka maoni yako ndiyo yawe ya jumuia au jamii nzima?

Punguza jaziba na mapovu mkuu na maisha yatakuwa rahisi tu. Kumbuka kuwa Ndesamburo hana hatia (sio fisadi) mpaka ithibitishwe vingenevyo - au wewe unasemaje?
 
Ndio maana nimemkaribisha upya JF. Huenda alipoingia hakukaribishwa kwa hiyo anamalizia hasira za kutokaribishwa kwenye kiibodi.
 
Ndio maana nimemkaribisha upya JF. Huenda alipoingia hakukaribishwa kwa hiyo anamalizia hasira za kutokaribishwa kwenye kiibodi.

Asante sana Jasusi,

Huyu Semenya amekuwa na hasira sana hapa jamvini for a while now. Juzi alimwaga madai chungu nzima hapa kuwa vyama vya upinzani havikosolewi hapa jamvini. Ilibidi SteveD atoe shule kwa kipindi kizima (bila maswali wala pop quiz).

Labda kwa kuwa umemkaribisha sasa atatulia na kufuatilia mijadala yote ya JF kwa umakini zaidi).
 
Mkuu Semenya vipi tena?

Mbona unaamuru watu hapa cha kusema na/au cha kutosema? Kwa nini unataka maoni yako ndiyo yawe ya jumuia au jamii nzima?

Punguza jaziba na mapovu mkuu na maisha yatakuwa rahisi tu. Kumbuka kuwa Ndesamburo hana hatia (sio fisadi) mpaka ithibitishwe vingenevyo - au wewe unasemaje?
nani anathibitisha kuwa mtu ni fisadi me najua ni Court of law kama hivyo basi hata akina Lowasa et all tuwachukulie hivyo hivyo innocent till proved guilty
 
nani anathibitisha kuwa mtu ni fisadi me najua ni Court of law kama hivyo basi hata akina Lowasa et all tuwachukulie hivyo hivyo innocent till proved guilty

Ukitaka kusema kuwa Lowassa sio fisadi, unaweza kusema hivyo mkuu. Uzuri ni kuwa utapingwa kwa hoja na sio kulazimishwa kusema vinginevyo.
 
Asante sana Jasusi,

Huyu Semenya amekuwa na hasira sana hapa jamvini for a while now. Juzi alimwaga madai chungu nzima hapa kuwa vyama vya upinzani havikosolewi hapa jamvini. Ilibidi SteveD atoe shule kwa kipindi kizima (bila maswali wala pop quiz).

Labda kwa kuwa umemkaribisha sasa atatulia na kufuatilia mijadala yote ya JF kwa umakini zaidi).
lakini ujumbe si niliufikisha mkuu
kama tunataka kuweka upinzani uwe strong lazima tukosoe nao wanapokosea ili wanaojiita CCM wasiwe napakukimbilia
 
Back
Top Bottom