Ndesamburo anunua helkopta za kampeni Chadema

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
*Zitaanza uchaguzi wa serikali za mitaa

Boniface Meena, Moshi

MBUNGE wa Moshi Mjini,Philemon Ndesamburo(Chadema), amenunua helkopta mbili kwa ajili ya kukisaidia chama hicho katika kampeni za chaguzi mbalimbali hapa nchini.

Moja ya helkopta hizo tayari iko hapa nchini na nyingine itawasili Jumatatu (kesho) na tayari mbunge huyo ameshapata vibali vya kuziruhusu helkopta hizo kutumika hapa nchini.

Akizungumza na Mwananchi Jumapili jana, Ndesamburo alikiri kuwa amenunua helkopta hizo, ili kukipunguzia chama chao gharama kubwa za kukodi wakati wa kampeni.

Hatua hiyo ni kubwa zaidi kwa Chadema, chama ambacho kimekuwa kikijitahidi kujiimarisha na kuongeza nguvu hasa wakati wa uchaguzi.

Tangu mwaka 2005 wakati wa Uchaguzi Mkuu, Freeman Mbowe alipogombea urais kwa mara ya kwanza, chama hicho kilitumia helkopta ya kukodi.

Hata katika baadhi ya chaguzi ndogo za ubunge zikiwemo za jimbo la Busanda na Tarime, chama hicho kilitumia helkopta za kukodi kwa ajili ya kufanyia kampeni.

Lakini safari hii, chama hicho kimeamua kumiliki helkopta yake huku Ndesamburo akisisitiza: "Vibali vyote nimeshapata kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga na vile vile vya kuitoa hiyo moja Nairobi na kuifikisha hapa Jumatatu".

Alisema kuwa helkopta hizo zitaanza kufanya kazi katika kampeni za serikali za mitaa katika majimbo yote ya Mkoa wa Kilimanjaro na baadaye katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani.

Kwa mujibu wa habari zilizopatikana ni kuwa Chadema imesimamisha wagombea zaidi ya robo tatu katika kila jimbo mkoani Kilimanjaro.

Katika Jimbo la Moshi Mjini, chama hicho kimesimamisha wagombea 60Â na Jimbo la Rombo kimesimamisha wagombea 52.

Uchaguzi wa serikali za mitaa unatarajiwa kufanyika Jumapili ijayo huku idadi ya wapigakura ikiwa ndogo kinyume na matarajio.

Hali hiyo imesababisha baadhi ya vyama kujipanga kikamilifu ili kuhakikisha wanakwepa kile wanachoita hujuma dhidi ya CCM.

Uchaguzi huo ni muhimu kwa vyama vya siasa kujipatia mtaji na kujiimarisha kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, ambao unatarajiwa kuwa na mchuano mkali.

Viongozi wa serikali za mitaa wana nguvu na ushawishi mkubwa wa kimaamuzi katika uchaguzi mkuu wa wabunge na Rais, kwani wapigakura wengi wako kwenye maeneo yao. Pia ngazi ya uchaguzi wa serikali za mitaa ni muhimu katika maamuzi ya maendeleo ya nchi kutokana na watu wengi kuishi vijijini ambako pamoja na mambo mengine kuna shughuli nyingi muhimu za uchumi hasa kilimo ambacho ni uti wa mgongo wa taifa.

Wamechoka kukodisha?
 
In return ndesa anapata nini kutoka CHADEMA...bure bure hafanyi hiyo biashara mchagga?
 
Itakuwa ngumu sana kumlalamikia mfadhili aisee.Ni sawa na CCM wanavyowaonea haya mafisadi(wengi wao ni wafadhili wa chama).....

hili litakuwa ni jibu la wiki! kwani kina Somaia si wameigawia CCM na serikali yake misaada kibao? na kina Rostam na Lowassa je? sasa tunashangaa kwanini kina JK wanashindwa kung'ata? mtu atang'ata mvipi mkono unaomlisha?

Chadema labda wanafuata nyayo tu za CCM...
 
Mkuu nimekupata,sitaki kuwa negative kwasababu malengo ya choppers hizo ni kuwafikia wananchi na kuwaelimisha kuhusu umuhimu wa mabadiliko ya uongozi kwa muda mfupi iwezekanvyo.

Ukweli ni kwamba "Wadau" wa chama ni lazima wawepo,hata hivyo tatizo ni wadau hao wanapo affect maamuzi muhimu ya viongozi hao....Mkuu MKJJ,ukweli ni kwamba hata hao wadau wa CCM kama kusingekuwa na ufisadi basi ni wazi hakuna ambaye angejisumbua kujiuliza ni kwanini wanachangia massively like the always do ndani ya chama...Mfano wa mchango wa millioni mia nne hivi majuzi kutoka kwa mfadhili wa CCM...Unless kuwe na mabadiliko makubwa,hatuwezi kukwepa kuchagua kati ya wafadhili mafisadi na wale safi ama wenye characteristics za kizalendo,wale wasiofadhili kwa malengo binafsi.

Kwa upande wa Ndesamburo,ameshajitolea mara nyingi tu hata hapo kwenye jimbo lake la moshi mjini,mfano hospital ambulances nk. Alikuwa akijitolea kabla hata hajawa mbunge,hatujui kama atabadilika na kuwa fisadi kama CHADEMA wakifanikiwa kuchukua nchi,kuna wanaosema the same thing will happen kama wakichukua nchi,wanaodai hivyo wanatolea mifano ya kwamba kuna mambo ya undugu ndani ya CHADEMA yanayochochewa na ufadhili wa chama,na kwamba maamuzi yako affected kutokana na hilo,kuna watakaokuja na mfano wa Zitto alipotaka uenyekiti nk.....Ukweli hauwezi kupingika kuwa watanzania watapewa nafasi ya kuchagua either zimwi walijualo ama wasiolijua....Kazi tunayo.
 
vyama vyote vya siasa duniani vina wafadhili wake, na ndio wafadhali wakubwa wana sauti zaidi kwenye vyama hivyo na huzawadiwa nafasi mbalimbali tena kwa uwazi. Lakini kwenye nchi za kidemokrasia mfadhili ni lazima awe yule ambaye hana tuhuma za ufisadi au uvunjaji wa sheria au kuhusishwa na mambo yaliyo kinyume. Ndio maana kwenye nchi kama Marekani mfadhili akigundulika kuwa si "msafi" mgombea au kiongozi hulazimika kurudisha ufadhili wake!
 
je helkopta ni muhim sana, na inahitajika kwa kampeni za serikali za mitaa? fedha izo zingesaidia albino wangapi waliokatwa mkono? yatiima wangapi? au hata shule ya kuwahifadhi albino wasome kwa amani?
sio eti kwaajili CCM inawafadhili mafisadi wanapotumia pesa vibaya basi napo Wafadhili wa CHADEMA nao watumie pesa vibaya....to me kama anauchungu wa taifa lake ondoa hizo hospitali nk, kuna mambo mengi kwa sasa angechangia ningefrahi zaidi ya hizo helkopta hususan asaidie walemavu wanaoishi kwenye mazingira ya shida sana
 
je helkopta ni muhim sana, na inahitajika kwa kampeni za serikali za mitaa?

Yawezekana inahitajika kwani uchaguzi si una gharama..? ulitaka waendelee kutumia baskeli na kutembea tu kwa miguu. Akili ni pamoja na uwezo wa kuitumia.

fedha izo zingesaidia albino wangapi waliokatwa mkono? yatiima wangapi? au hata shule ya kuwahifadhi albino wasome kwa amani?

Fedha zilizoenda Meremeta, Mwananchi Gold, Deep Green, IPTL, Dowans, Richmond, ATCL, n.k zingetumika kuinua maisha ya watu wetu unafikiri tungekuwa na mauaji ya maalbino namna hii. Badala ya kuibana Chadema ibane CCM ambayo inauza utajiri wa nchi yetu kwa wageni kama njugu, huku Watanzania wakiendelea kutumikishwa katika uombaomba wa milele!

sio eti kwaajili CCM inawafadhili mafisadi wanapotumia pesa vibaya basi napo Wafadhili wa CHADEMA nao watumie pesa vibaya....

Inategemea unaangalia nini; kama helikopta zitasaidia kupata wawakilishi wengi mitaani ambao wataweza kutekeleza agenda za Chadema.. basi kuwekeza huko kunalipa. Siasa ni pamoja na kuwekeza katika kugharimia nafasi za kisiasa na hakuna nafasi za kisiasa ambazo ni bei chee.

la maana ni kuona jinsi gani uwekezaji huu utalipa. Hili litaoonekana baada ya matokeo ya uchaguzi. Na hapo ndipo tunaweza kwa haki kuhukumu kama ulikuwa ni uwekezaji makini. Lakini vile vile.. kwenye maeneo mengine yawezekana hizo Helikopta zikatumika katika mambo mengine zaidi ya kampeni za kisiasa. Fikiria.

to me kama anauchungu wa taifa lake ondoa hizo hospitali nk, kuna mambo mengi kwa sasa angechangia ningefrahi zaidi ya hizo helkopta hususan asaidie walemavu wanaoishi kwenye mazingira ya shida sana

Na njia mojawapo ni kupata wawakilishi au viongozi kwenye mitaa wanayoishi walemavu hao.. think about it!
 
je helkopta ni muhim sana, na inahitajika kwa kampeni za serikali za mitaa? fedha izo zingesaidia albino wangapi waliokatwa mkono? yatiima wangapi? au hata shule ya kuwahifadhi albino wasome kwa amani?
sio eti kwaajili CCM inawafadhili mafisadi wanapotumia pesa vibaya basi napo Wafadhili wa CHADEMA nao watumie pesa vibaya....to me kama anauchungu wa taifa lake ondoa hizo hospitali nk, kuna mambo mengi kwa sasa angechangia ningefrahi zaidi ya hizo helkopta hususan asaidie walemavu wanaoishi kwenye mazingira ya shida sana
Hii ni kazi ya serikali iliyoko madarakani, ni kazi ya NGO, ni kazi ya wananchi wote...siyo kazi ya chama cha siasa (chadema) ni kushika nchi kwanza ndio watumia peasa za wananchi kusiaidia uliyoyasema..angalizo usitake chadema iwe ka-NGO kama NCCR mageuzi ya....
 
Watamzania amkeni leteni ile kitu inayoitwa balance of power kunahitajika 2010 Bunge la Tanzania liwe controlled na wapinzani na Ikulu iwe kwa chama tawala hapa ndio tutaweza kupata uwazi kupunguza ubadhirifu pia kwa Zanzibar CUF wa jifunze kutoka Kenya/Zimbabwe ukilishika Bunge basi Chama tawala kitakua na uwezo wa kuakaa chini na kupunguza kiburi na kuwa na tamaduni mpya ya kukubali kuweka uwazi na kuhojiwa sio CCM imeshika kila kitu , Ikulu , Bunge , na Mahakama hapo ndio Rushwa na dulma inapozid i Tanzania kila Mtanzania alieko nje akiongea na dugu yake mmoja huku nyumbani kumelimisha umuhimu wa kuwa wabunge wengi wa Upinzania ni njia moja ya kuikomba Tanzania kutoka kwa mafisadi.
 
halafu watoto wake, wakweze wakipewa viti maalum mtalalamika?
Hayo ni yako Masatu. Hayakuhusu waachie Chadema wenyewe waamue.

Kwani mlipompa Makongoro Nyerere ubunge wa bure kuna mtu aliwalalamikia?
Si mlikuwa mnalipa fadhila? Sasa wacha Chadema waamue kama wanalipa fadhila au la, hayo hayakuhusu baba/mama.
 
Hayo ni yako Masatu. Hayakuhusu waachie Chadema wenyewe waamue.

Kwani mlipompa Makongoro Nyerere ubunge wa bure kuna mtu aliwalalamikia?
Si mlikuwa mnalipa fadhila? Sasa wacha Chadema waamue kama wanalipa fadhila au la, hayo hayakuhusu baba/mama.[/QUOTE]
Duu! kuwaachia bila kuwauliza eti kwasababu hawatuhusu siyo sawa hakuna Chama ambacho hakituhusu labda kama inataka control ya uchaggani tu! lakini as long as wanataka kuongoza nchi nzima..wantuhusu si wao tu wote CUF etc..wanatuhusu..kwahiyo lazima watuambie..Ndesa anatoa ...bila ...kutegemea au ku-fanya ufisadi baadaye?? nakataa mkuu wanatuhusu wote yeyote anayetaka kuchukua nchi...
 
Hayo ni yako Masatu. Hayakuhusu waachie Chadema wenyewe waamue.

Kwani mlipompa Makongoro Nyerere ubunge wa bure kuna mtu aliwalalamikia?
Si mlikuwa mnalipa fadhila? Sasa wacha Chadema waamue kama wanalipa fadhila au la, hayo hayakuhusu baba/mama.

kulikuwa na msemo kuwa kunya anye kuku, akinya bata ...
 
Wapiga kura wengi hawana elimu (in-deep) kuhusu siasa za Tanzania na hali hio imekuwepo tokea tupate uhuru kwani bado televisheni baadhi ya sehemu bado ni ndoto.

Chadema wanastahili pongezi kwa kuwa na mawazo hayo ya kutaka kuwaelemisha wananchi kwamba siasa si kupiga kura tu bali pia ni kuchambua sera za wagombea kwa mapana na marefu.

Helicopter ziongezwe na wengine tutasaidia kujenga helipads nyingi.

Lol
 
In return ndesa anapata nini kutoka CHADEMA...bure bure hafanyi hiyo biashara mchagga?

acha chuki za kikabila wewe, wachagga wamekukosea nini au wanahusikaje hapa?

mijitu mingine bwana ...... pyyyyyyuuuuuuuuu .... ukabila hadi machoni
 
kwani CHADENA ikisaidia albino ni NGO?
CCM wameshafulia wametulia hela zetu tunataka kuona vyama vya upinzani vitumie pesa kwa utaratibu mzuri.
 
In return ndesa anapata nini kutoka CHADEMA...bure bure hafanyi hiyo biashara mchagga?

Umeshasema biashara halafu unasema bure bure, where's the logic?!

Kama wewe umeshajaribu kufanya biashara halafu hiyo biashara haikufanikiwa basi sababu umeshaitaja mwenyewe. Hujui biashara. Hakuna biashara ya bure bure. Hata enzi za barter trade walibadilishana mali na mazao!!
 
Back
Top Bottom