Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Ndege ya Rais wa Tanzania yenye usajili wa 5H-ONE imeonekana kutua Dubai na kuanza safari kuelekea Saudi Arabia!

Bado idara ya habari ya Ikulu haijatoa taarifa yoyote kama Rais Samia yuko ziarani katika nchi hizo mbili za UAE na SAUD ARABIA.
Screenshot_2023-07-28-22-21-52-77_8a6ce7ef6b1c5341b022b20d7fbb4b6e.jpg
Screenshot_2023-07-28-22-23-14-93_40deb401b9ffe8e1df2f1cc5ba480b12.jpg


1690605168257.png


1690605913889.png
 
Tunachokijua
Ndege ya Tanzania yenye usajili wa 5H-ONE inaelezwa kuwa ni ndege inayotumiwa na Rais wa Tanzania. Ndege hii ilinununuliwa Mwaka 2004 Wakati Rais wa Tanzania Akiwa Mhe Benjamin Mkapa na Waziri wa Fedha akiwa Mzee Mramba na Waziri wa Uchukuzi akiwa ni Professor Mark Mwandosya.

Ndege hii imesajiliwa kwa usajili wa namba 5H-ONE, Ina uwezo wa kutembea angani kwa masaa 13, Ina Tembea umbali wa kilomita 12,501 kutokua eneo moja mpaka jingine. Ina Speed ya Kilometer 941 kwa saa, ina Urefu wa mita 15.4. Ndani yake huduma zote za kiofisi na starehe zote, Ina Uwezo wa kubeba abiria 18.

Mnamo Julai 28, 2023 uliibuka uvumi katika mitandao ya kijamii ukiohoji ndege hiyo ya Rais wa Tanzania kuonekana Dubai pasina kuwapo kwa taarifa kutoka kurasa za Ikulu ya Tanzania.

Mathalani, Julai 28, 2023 Mwanachama wa JamiiForums anayeitwa Mpinzire aliweka andiko lake akihoji suala la ndege hiyo kwenda Dubai pasina idara ya habari Ikulu utoa taarifa. Mpinzire aliandika:
Ndege ya Rais wa Tanzania yenye usajili wa 5H-ONE imeonekana kutua Dubai na kuanza safari kuelekea Saudi Arabia! Bado idara ya habari ya Ikulu haijatoa taarifa yoyote kama Rais Samia yuko ziarani katika nchi hizo mbili za UAE na SAUD ARABIA.

Pia katika ukurasa wa Twitter wa @comanchechiefIV nao ulihoji suala la ndege ya Rais wa Tanzania kuonekana Dubai pasina kuwapo kwa taarifa hizo katika ukurasa wa habari wa ikulu ya Tanzania. @comanchechiefIV katika andiko hilo alisema:

Sijasikia @ikulumawasliano ikitangaza safari ya rais Dubai au Saudi Arabia. Lakini flight tracking data zinaonyesha ndege ya rais iliondoka jana ikitumia call sign TANZ01 ambayo ni rais on board. Ndege ilitoka Dubai leo na iko Saudi Arabia.
Baada ya kuwapo kwa fununu hizo JamiiForums imefatilia vyanzo mbalimbali vinavyofuatilia mienendo na safari ya ndege mbalimbali na kubaini mambo yafuatayo:

Katika Ukurasa wa FlightAware ambayo ni Kampuni ya Kidijitali inayofatilia mienendo mbalimbali ya safari za ndege duniani inaonesha mnamo Julai 28, 2023 ndege ya 5H-ONE ilikuwa nchini Dubai muda wa saa 2:35 Asubuhi.

Aidha inaonesha kuwa ndege hiyo pia iliruka muda wa 02:35 nchini Dubai na kuelekea Saudia ambako ilitua saa 03:03 Asubuhi hiyo. Tazama taarifa hiyo kwenye picha hapa chini sehemu yenye kivuli cha rangi ya njano.

1690605168257-png.2701846

Taarifa za FlightAware kuhusu ndege 5H-ONE
Nao, Flightrader24 waliojikita kuonesha mienendo ya safari mbalimbali za ndege ulimwenguni hawatofautiani na FlightAware kwani nao wanaonesha kuwa mnamo Julai 28, 2023 ndege hiyo ya Tanzania ilipaa ikitokea Dubai lakini wao hawajaonesha ilipoelekea. Tazama kielelezo hapa chini:

1690605913889-png.2701849

Taarifa za Flightrader24 kuhusu ndege 5H-ONE

Aidha, JamiiForums pia imepitia katika ukurasa wa Twitter wa @Ikulumawasiliano na ukurasa wa Instagram wa @ikulu_mawasiliano ambako wanaweka taarifa mbalimbali za safari za viongozi wa kitaifa lakini hakuna taarifa yoyote kuhusu safari ya ndege hiyo siku hiyo ya Julai 28, 2023. JamiiForums pia imepitia kurasa Twitter na Instagram za Msemaji wa Serikali Gerson Msigwa lakini hakuna taarifa yoyote kuhusu safari ya ndege hiyo siku ya Julai 28, 2023.

Hivyo, kutokana na vyanzo hivyo vilivyopitiwa na JamiiForums, hoja inayoeleza kuwa ndege ya 5H-ONE ilionekana Dubai mnamo Julai 28, 2023 na ikaelekea Saudia na taarifa hizo hazikuwekwa katika vyanzo rasmi vya ikulu ni ya ukweli.
Katikati ya mjadala mkubwa kama huu na malalamiko ya Wananchi ndio kwanza Rais anafanya safari huko huko kwa tunaowalalamikia.

Rais wetu hatujali kabisa. Hana uzalendo wala uchungu wa lolote lile.

Ni jambo la kusikitisha kwamba kwa sasa hatuna kiongozi mzuri.
 

Similar Discussions

23 Reactions
Reply
Back
Top Bottom