Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,331
33,141
Rais Samia atamani JKT ya kisasa zaidi.jpg
Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajab Mabele leo Julai 10, 2023 wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) yaliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma. Picha na Ikulu.

Muktasari:​

  • Rais Samia Suluhu Hassan ameshiriki maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) katika viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma huku akionesha matamanio yake kwa jeshi hilo kuwa la kisasa zaidi.
Dodoma. Amri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais Samia Suluhu Hassan amesema ni matamanio yake kuona Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) linakuwa la kisasa lenye kuwalea vijana katika uzalendo.
Rais Samia ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Julai 10,2023 wakati akihutubia kilele cha miaka 60 ya JKT katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Amesema vijana wanaotoka JKT wanapaswa kuwa wazalendo katika nchi yao na hata wanaobaki katika majeshi na vyombo vya ulinzi wawe watu wenye weledi wa kupigiwa mfano.

Rais amesema Serikali iko tayari kusimama na JKT na ikibidi kuwadhamini hata katika mikopo ili waweze kuimarisha vikosi vyao kwenye uzalishaji.

“Katika miradi mikubwa mmefanya vizuri sana ikiwemo ujenzi wa Ikulu ya Chamwino, sisi Serikali tutaendelea kuwaunga mkono na ikibidi mpate mikopo ili kuongeza nguvu ya uzalishaji tuko tayari kuwadhamini,” amesema Rais Samia.

Amesema vijana wanaopita JKT wanapaswa kubeba dhima ya uzalendo mioyoni mwao siyo katika midomo kwani jeshi linawafanya vijana kuwa wamoja na wenye kuithamini nchi yao katika kuonyesha uzalendo.

Kuhusu JKT ametaka waendelee na malengo yao ya kupunguza umasikini na utegemezi kwani ndiyo malengo makuu na kwamba Serikali itaendelea kuongeza nguvu ya kuwa na idadi kubwa ya vijana wanaopitia mafunzo hayo kuliko idadi ya sasa.

Kwa mujibu wa taarifa, idadi ya vijana waliokwenda JKT kwa mujibu wa sheria ni 52,000 ikiwa ni ongezeko kubwa kutoka 30,000 walioitwa mwaka jana baada ya kumaliza kidato cha sita. chanzo.
 
Back
Top Bottom