Kuna ndege ya asili iliyotengenezwa na watanzania na yenye uwezo wa kumbeba abiria mmoja tu imepata ajali maeneo ya Sakina Arusha usiku huu, kwa mujibu wa Radio 5 Arusha kupitia mwandishi wake Davis Rhonyagira, ndege hiyo ilikua na rubani tu na kwa bahati nzuri hakuumia kabisa japo ndege yake imesambaratika vipande vipande.
Amedai kuwa ametokea Msumbiji akielekea jiji la Tanga. Wakazi wa Sakina wamempa msaada wa nguo na bado wanaendelea kumfanyia mahojiano!
Ndege zao hupata hitilafu kama ndege za kawaida tunazopanda hivyo kwao ni jambo la kawaida,kinachonishangaza zaidi mpaka leo ni inawezekanaje mtu kusafiri toka Msumbiji mpaka Arusha kwa haraka?Kwanini wasifanye usafiri huu kuwa wa kusaidia zaidi kuliko wanavyowanga?