MAGEUZI KWELI
JF-Expert Member
- Jul 16, 2011
- 1,947
- 254
Bibi yangu Sukari ananunua alfu tatu. leo umwambie serikali inajipanga kuleta maendeleo inaleta ndege tatu mpya, Bibi lazima aulize ndege za kwenda ahera au?
Kasome "economies of scale" utapata jibu. Ila kwa kifupi kadiri uzalishaji unavyoongezeka ndivyo gharama za uzalishaji zinavyopungua.
Kuhusisha dhana hiyo na ununuzi wa ndege na kupungua kwa abiria ati kwa sababu kipato chao pia kinapungua, si sahihi kiuchumi. Kuwepo kwa ndege nyingi kutapelekea kushuka kwa nauli na kuongezeka abiria na bado faida inapatikana.
ATCL kuongeza ndege maana yake itaongeza uwezo wa kusafirisha, hadi nje ya nchi, na hivyo kupunguza gharama za usafirishaji.
Naamini menejimenti ya ATCL imejipanga vizuri kwa hilo na kukabiliana na ushindani.
Nadhan kuna uelewa tofauti ya dhana mzima ya ubanaji. Kuna vitu kweli amefanya ni vizur llkn mengine ni mabaya na hayataleta tija.unapobania watu shule, unatengeza Bomu. Kuna maaumuz mengi ameyafanya bila kuangalia effects zake na pia matamko mengi ya watendaji wake hayawez jenga zaid yatabomoa. Mfano wa makonda sio mtekelezaji ni mdomo tu.
Ni vizuri kwa nchi yoyote duniani kuwa na shirika au mashirika ya ndege, ni jambo jema. Tatizo hapa kwetu ni kwamba vipaumbele vya serikali hii au niseme vya Magufuli ni vipi. Ni sawa na mtoto mdogo aliyeingia ndani ya supermarket na kutaka anunuliwe kila kitu anachokiona na anunuliwe muda huo huo.
Kama walivyosema wengine hapatakuwa na maendeleo ya watu awamu hii bali ongezeko la vitu hasa hasa kwenye maeneo ya miundombinu ambapo ndipo baba mtakatifu aliko na uzoefu nako.
Tutaona flyovers, barabara, ndege na reli - zaidi ya hapo hakuna kitu zaidi ya kufoka majukwaani.
Anawaiga Rwanda, watu ambao wanakwenda kwa kufuata national strategic plan tofauti na yeye anawaza mwenyewe na kutekeleza kwa fikra zake bila kuwa na mpango unaopimika.
Ndege ni vyema kuwa nazo lakini siyo kwa gharama ya mahospitali kukosa dawa, watoto kukosa chanjo, wanafunzi kukosa mikopo, waajiriwa kukosa uhakika wa kesho na kadhalika. Hizi siyo nyakati za kutafuta sifa na kushindana na wenzio walioanza mikakati yao siku nyingi huku wakishirikisha mawazo mbadala na ya kitaalamu.
Biashara kichaa ndio maaana jk aligoma kununua ndege
Mkuu fastjet wamepunguza route au wameachia route?
Hizo route walizokuwa wanatamba nazo zote ni za ATCL,Twiga kafufuka hawana jinsi ni kuachia tu.
KQ wana safari 49 kwa wiki,asilimia 90 ni za ATCL,wataachia tu.
Kuna route ya Dar London,Dar -Beijing,Dar-Comoro,Dar-Lusaka,Dar Lubumbashi,Dar -J'burg zote hizi zilikua zinashikwa aidha na precision au Fast jet watazitema tu
Moja ya sababu inayopelekea hiyo hali mbaya kwa fastjet ni kunyanganywa tonge (yani soko) pamoja na kuzidiwa ujanja mwingine wa kibiashara na ATCL. Kwa hiyo kwa ATCL mambo ni SUPER na kuongeza ndege hakukwepeki.
Msisahau kuwa baada Precision Air kukumbwa na madeni na hasara fastjet wakaja nchini na wakatumia hiyo loophole kuwapiku Precision Air, na leo hii fastjet yamewafika na Air Tanzania ndo hiyo ishafufuliwa na wenyewe ATCL watatumia hiyo loophole kuwatoa fastjet nje ya ulingo. Kwa kifupi hizo ndizo changamoto za biashara hazikwepeki.
-Hao fastjet ni moto wa ATCL ndio unaowatikisa
-Pia kulikuwa na tetesi kwamba wanataka kuhamisha Head Quarter yao kutoka London kwenda Johannesburg kule South Africa, sasa kama Head Quarter ikihamia jiji la Johannesburg ambalo liko Africa hata hii hub yao ya Africa (ambayo ni Dar es Salaam) itafutwa tu, sasa huenda ndo maandalizi hayo ya kuhamia kabisa Johannesburg.
Akili yako ni kama ya tikiti. Lenyewe hulala popote pale. Hivi una elimu gani. Ulichozungumza ni expenditure pasee. Yaani matumizi tuu. Vipi kuhusu mapato. Unategemea fedha za hayo yote zitatoka.wapi. labda tuambie kiasi cha kudharau hawa wanaojaribu kutengeneza njiaa kuu za uchumi za mapato in the long run.bila kuwa na shughuli za maendeleo ni lini unadhani tutatoka hapa tulipo. Wewe unawaza kula tuuu. Wajameni wajameni. Tuulize kwanza kabla ya kukurupukaSiku zikitoa Bongo nazima tv yangu siku nzima maana kufanya mambo bila priority ni zaidi ya kero na maudhi matupu.
Ni kero na maudhi kumsikia mtu anajisifu kununua ndege kwa cash wakati wanafunzi wanakosa mikopo,madaktari na waalimu hawajiiriwa,madawa hospitalini shida,watumishi stahiki zao hawalipwi,watu wamesitishiwa ajira zao,wahanga wa tetemeko wanateseka,n.k.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]Chato hakuna dawa
Soko LA abiria wa ndege ni kubwa ukiangalia kenyaairways au south Africa airways wananchi wao ndo upanda zaid kuonyesha uzalendo na kuchangia uchumi wa nchi yao hivo Atcl wakileta ndege za kutosha za kwenda nje na ndani uhakika wa soko ni mkubwa
Mimi sizungumzii Mnyika au Sugu nazungumzia msingi wa biashara Demand and Supply.National carrier antakiwa awe namba moja halafu waje watu wa kumchallenge
Hivi umesahau akina Mnyika na sugu walipiga sana kelele tunakosa mapato kwa kutokuwa na national carrier?