Bukyanagandi
JF-Expert Member
- Jun 24, 2009
- 11,626
- 18,228
Uraisi wa spares kwa sababu ya economy of scale.Uraisi katika gharama za kufundishia marubani na mafundi, kwa sababu rubani wa bombardia hawezi rusha Boeing mpaka kwa mafunzo marefu,wakati ni mafupi kwa ndege zilizotengenezwa na kiwanda kimoja kwa sababu ya mfanano wa instruments na Aircraft systems .Utahitaji mafundi na marubani wachache kwa vile wanaweza zungushwa kiurahisi katika ndege zilizotoka Kwenye source moja. Uzoefu huja haraka zaidi kwa ndege zilizotoka kiwanda kimoja kwa hiyo rubani au fundi waweza kuhitimu haraka zaidi na wakawa na uwezo sana kwa sababu ya task repeatition.
Mkuu unaweza kutufafanulia kwa nini Mapilot wa ndege za vita uajiliwa kirahisi kuendesha ndege za kiraia?
Linapo kuja suala la Instruments/avionics zote zinafuata same basic principles bila kijali type ya ndege, instruments/avionics zinaweza kutofautiana kwenye display i.e analogue au digital (LCD) lakini marubani wenye uzoefu haziwapi shida ku adopt in no time.
Madhumuni ya mimi kuhoji kwa nini tunanunua ndege zote kutoka source moja nilikuwa na wasi wasi kwamba,je, kampuni ya kuhunda ndege ikifirisika ikafunga kiwanda sisi tutakuwa wageni wa nani - huo ndio ulikuwa wasi wasi wangu.