BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,769
- 288,332
Vikao vya baraza la Mawaziri ambavyo Rais ni Mwenyekiti wake huwa havifanywi kwa siri. Waandishi wa habari na wapiga picha wa kutoka vyombo mbali mbali vya habari nchini huitwa kuandika yaliyojadiliwa katika vikao hivyo wakachukua na picha na pia video, lakini hakuna kitu kama hicho katika awamu hii. Hakuna picha ya kuonyesha vikao vya baraza la mawaziri hata habari kuhusiana na vikao hivyo labda viwe vinafanyika kwa siri na yanayojiri pia katika vikao hivyo yanafanywa siri.
Angalia haya matamko ya hovyo hovyo ya Mawaziri mbali mbali katika awamu hii. Baadhi Mawaziri wanakurupuka na kuja na matamko ya ajabu ajabu ambayo mengi ya matamko hayo baadaye huyakanusha au kudai "mlininukuu vibaya" Kungekuwa na vikao vya baraza la Mawaziri hali isingekuwepo.
Angalia sakata la Dangote na kiwanda chake cha Saruji. Kungekuwa na vikao vya baraza la Mawaziri sakata hili lingemalizwa ndani ya vikao vya Baraza la Mawaziri na Wananchi tusingejua chochote kama kulikuwa na sakata kati ya Serikali na Dangote lakini kutokana na kutokuwa na vikao sakata hili kubwa likaibuka hadharani huku Serikali ikitudanganya Watanzania kwamba kiwanda kimefungwa kwa matengenezo ya kawaida tu wakati ni uongo mtupu sasa wamebaki kufukia mashimo ya uongo wao. Juzi Muhongo kafanya mkutano na waandishi wa habari na kuwaalika viongozi wa juu wa viwanda wa Saruji nchini lakini wale wa Dangote wakasusia kwa kuchoshwa na usanii wa Serikali hii.

BAK unajuaje hakuna vikao kati ya Raisi Na mawaziri? Hata kama mambo yote mazuri kiuchumi ungekuwa huna zuri juu ya awamu ya JPM.