Ndege mpya za serikali ziko njiani kuja

Ndege mpya za serikali ziko njiani kuja

Hata msemeje hayo madege atayannua tu,mikodi inaongezeka kila sehemu,wafanyabiashara wenye akili wanaondoka...kile kiwanja cha chato kinahitaji ndege za kutua kama hizi sababu fastjet au precision hawawezi peleka ndege zao kusikokua na faida.
 
Yaani hawa Fastjet waliowezesha % kubwa ya Watanzania kupanda ndege ndio unasema wakatafute pengine ? Ushajiuliza bila uwepo wao hali ingekuwaje ?

Aliyetuloga Watanzania sijui atafufuka lini

Sina tatizo na Magufuli kufufua shirika letu lakini nitakuwa mpumbavu nisipoheshimu revolution waliyoleta Fastjet kwenye airlines industry
Umepotea
 
Je hizo fedha ziliwekwa kwenye budget na kupitishwa na bunge?
 
Juzi Msajili wa Hazina, Lawrence Mafuru amesema kupotea kwa fedha katika mzunguko kunasababishwa na serikali kupeleka fedha nyingi kwenye maendeleo kama kununua ndege na kujenga reli na Barabara. Matokeo yake siyo ya leo wala kesho. Mtasubiri sana
 
Kununua ndege sio tatizo, tatizo ni kwamba hao abiria wako wapi? Nguvu ya soko ndiyo inayokufanya upeleke bidhaa sokoni. Sasa kinachofanywa na hapa Tanzania ni kupeleka bidhaa gulioni wakati huna uhakika wa kuwepo wanunuzi wa kutosha wa hizo bidhaa.
 
Jaman haya madude aachane nayo kwanza aboreshe maslai kwa wafanyakazi wa uma na kuajiri watu. Tunafingua shule january kukiwa na ongezeko kubwa la watoto na upungufu mkubwa wa walimi ingawa walioko vyuoni wamefutiwa ruhusa za masomoni na kutakiwa kurudi kazini
Acha uzushi aliyefutiwa ruhusa na kurudi kazini nani, mbona watu wapo nje ya nchi na wanasoma na wanapata haki kama kawa
 
unabana matumizi maana yake watu na wenyewe watabana matumizi hivyo watu wachache zaidi watapanda ndege kipindi hiki kuliko zamani, ndio maana fast jet wamepunguza route
Sasa unaongeza ndege huku watu hawana income ya kupanda hizo ndege biashara itafanyikaje?
Ni kama una biashara yako kisha wafanyakazi wakapunguziwa mishahara yao, na wakati huo huo ukawaletea bidhaa za bei ghali na luxury unategemea wananunue

Kasome "economies of scale" utapata jibu. Ila kwa kifupi kadiri uzalishaji unavyoongezeka ndivyo gharama za uzalishaji zinavyopungua.

Kuhusisha dhana hiyo na ununuzi wa ndege na kupungua kwa abiria ati kwa sababu kipato chao pia kinapungua, si sahihi kiuchumi. Kuwepo kwa ndege nyingi kutapelekea kushuka kwa nauli na kuongezeka abiria na bado faida inapatikana.

ATCL kuongeza ndege maana yake itaongeza uwezo wa kusafirisha, hadi nje ya nchi, na hivyo kupunguza gharama za usafirishaji.

Naamini menejimenti ya ATCL imejipanga vizuri kwa hilo na kukabiliana na ushindani.
 
Ni vizuri kwa nchi yoyote duniani kuwa na shirika au mashirika ya ndege, ni jambo jema. Tatizo hapa kwetu ni kwamba vipaumbele vya serikali hii au niseme vya Magufuli ni vipi. Ni sawa na mtoto mdogo aliyeingia ndani ya supermarket na kutaka anunuliwe kila kitu anachokiona na anunuliwe muda huo huo.
Kama walivyosema wengine hapatakuwa na maendeleo ya watu awamu hii bali ongezeko la vitu hasa hasa kwenye maeneo ya miundombinu ambapo ndipo baba mtakatifu aliko na uzoefu nako.
Tutaona flyovers, barabara, ndege na reli - zaidi ya hapo hakuna kitu zaidi ya kufoka majukwaani.
Anawaiga Rwanda, watu ambao wanakwenda kwa kufuata national strategic plan tofauti na yeye anawaza mwenyewe na kutekeleza kwa fikra zake bila kuwa na mpango unaopimika.
Ndege ni vyema kuwa nazo lakini siyo kwa gharama ya mahospitali kukosa dawa, watoto kukosa chanjo, wanafunzi kukosa mikopo, waajiriwa kukosa uhakika wa kesho na kadhalika. Hizi siyo nyakati za kutafuta sifa na kushindana na wenzio walioanza mikakati yao siku nyingi huku wakishirikisha mawazo mbadala na ya kitaalamu.
 
Siku zikitoa Bongo nazima tv yangu siku nzima maana kufanya mambo bila priority ni zaidi ya kero na maudhi matupu.

Ni kero na maudhi kumsikia mtu anajisifu kununua ndege kwa cash wakati wanafunzi wanakosa mikopo,madaktari na waalimu hawajiiriwa,madawa hospitalini shida,watumishi stahiki zao hawalipwi,watu wamesitishiwa ajira zao,wahanga wa tetemeko wanateseka,n.k.
Wewe unadhani huto tu milioni 200$ ndito tungetatua matatizo yetu hayo uliyoorodhesha? Very poor thinking capacity. Hata huko kwenye nchi zilizoendelea kama USA kuna matatizo kama hayo hususani affordable huduma za afya (hence Obama care & the like), ukosefu wa ajira na kadhalika lakini serikali zao zinatumia mabilioni ya dolla kupeleka vyombo kuvinjari sayari zingine kama Mars and Jupita, kutengeneza silaha za maangamizi and so forth. Wewe umebaki na wimbo huo huo - tetemeko la Kagera, mikopo ya wanafunzi, ajira na uhaba wa madawa.
 
Kasome "economies of scale" utapata jibu. Ila kwa kifupi kadiri uzalishaji unavyoongezeka ndivyo gharama za uzalishaji zinavyopungua.

Kuhusisha dhana hiyo na ununuzi wa ndege vs kupungua kwa abiria ati kwa sababu kipato chao piankinapungua, si sahihi kiuchumi. Kuwepo kwa ndege nyingi kutapelekea kushuka kwa nauli na kuongezeka abiria na bado faida inapatikana.

ATCL kuongeza ndege maana yake itaongeza uwezo wa kusafirisha, hadi nje ya nchi, na vivo hivyo kupunguza gharama za usafirishaji.

Naamini menejementi ya ATCL imejipanga vizuri kwa hilo na kukabiliana na ushindani.
pointi hapa ni biashara ya ndege inahitaji watu wawe na fedha, nadhani tungeweka sawa mambo mengine haya ya ndege yafuate,
 
Hapa Wachawi wa Maendeleo watakuja tu, na nimeona hapo Juu wameanza kulalamika, mtalalamika sana mwaka huu, na bado mwakani mtalia sana macho ya damu, lakini lazima Tununue Ndege, ninyi ndo awamu ya nne mlilalamika sana kuwa eti hata Rwanda wametuzidi, sasa mlidhani fedha za kununulia hizo ndege zingetoka wapi? lazima tufunge mkanda hadi malengo yetu yatimie, sasa hatutamsikiliza mtu tena hadi pale Ndege zetu zitakaponunuliwa, na bado Reli ya Standard gauge pesa zote zinaenda kwa kampuni husika, yaan mikanda tuliyojifunga tutaifungua mwaka 2019
ILE ILIYOKWAMA ARUSHA ISHAAMKA? HEHE VIVUKO CHAKAVU NDEGE MBOVU MBELE KWA MBELEEEEEEEEE
 
Biashara kichaa ndio maaana jk aligoma kununua ndege
 
Wakati tunapambana kupata maendeleo ya vitu tukumbuke maendeleo ya watu.Maendeleo ya vitu ni Barabara,Reli,Ndege,Meli nk. Maendeleo ya watu ni Elimu bora kwa wote,Huduma bora za afya,Ajira,Makazi,Chakula nk.
Ni kweli, lakini vitu kama hivi ndivyo vitakavyosaidia kuongeza wigo wa income ambayo itaenda kuboresha maendeleo ya watu. Huwezi kuwa na maendeleoa manzuri ya watu wakati huna income ya kuwezesha hayo maendeleo.
 
Naomba mungu yatue salama yasiue marubani wetu na yasije yakashindwa kugeuka kwa kuacha runway.
 
Back
Top Bottom