Ndege mpya za serikali ziko njiani kuja

Ndege mpya za serikali ziko njiani kuja

PakavuNateleza

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2009
Posts
1,106
Reaction score
1,297
Serikali ya Tanzania imesaini mkataba na kampuni ya kutengeneza ndege ya Bombardier yenye makao makuu nchini Canada kununua ndege tatu mpya miezi michache tangu iliponunua ndege mbili mpya za Bombardier Q400.

Ndege za CS300 zinauwezo wa kubeba abiria 150 kila moja tofauti na Q400 ambayo inabeba abiria 70.

Mkataba huo mpya unahusisha ununuzi wa ndege moja aina Bombardier Q400 inayotarajiwa kuwasili nchini mwakani na ndege nyingine mbili ni Bombardier CS300 ambazo haijajulikana zitawasili lini.



========

Bombardier CSeries will sell both the Government of Tanzania, which represents its first order in seven months for its new commercial aircraft.


In total, the transaction includes two CS300 and a Q400 aircraft. According to list prices, the order is valued at 203 million US.

The aircraft will be operated by Air Tanzania, the national airline of the United Republic of Tanzania.

The last order of CSeries was in April, when the US carrier Delta Air Lines has confirmed the purchase of 75 CS100 aircraft, a firm order valued according to catalog prices, is estimated at US $ 5.6 billion .

Monday, Bombardier had delivered its first CS300 – the largest device family CSeries aircraft – the Latvian carrier airBaltic, its launch customer.

cwynnlrucaacozw.jpg


This aircraft, which can carry up to 160 passengers, must make its first commercial link between Riga and Amsterdam on 14 December.

Overall, airBaltic ordered 20 Bombardier CS300 devices.

So far, the aircraft manufacturer and rolling stock received 360 firm orders for its new aircraft, including 235 for the CS300.


Source: The Quebec Telegram
 
Jaman haya madude aachane nayo kwanza aboreshe maslahi kwa wafanyakazi wa umma na kuajiri watu. Tunafungua shule mwezi Januari Mwakani kukiwa na ongezeko kubwa la watoto na upungufu mkubwa wa walimu ingawa walioko vyuoni wamefutiwa ruhusa za masomoni na kutakiwa kurudi kazini.
 
Wakati tunapambana kupata maendeleo ya vitu tukumbuke maendeleo ya watu.Maendeleo ya vitu ni Barabara,Reli,Ndege,Meli nk. Maendeleo ya watu ni Elimu bora kwa wote,Huduma bora za afya,Ajira,Makazi,Chakula nk.

Huwezi kutenganisha maendeleo ya vitu na ya watu.

Ukijenga shule ni budi kuweka miundo mbinu ya kuifikia na huduma zingine za kijamii.

Ukihamasisha kilimo, ni budi kuwepo na miundo mbinu ya kufukia mashamba na kusomba mazao.

Na kadhalika
 
Hapa Wachawi wa Maendeleo watakuja tu, na nimeona hapo Juu wameanza kulalamika, mtalalamika sana mwaka huu, na bado mwakani mtalia sana macho ya damu, lakini lazima Tununue Ndege.

Ninyi ndo awamu ya nne mlilalamika sana kuwa eti hata Rwanda wametuzidi, sasa mlidhani fedha za kununulia hizo ndege zingetoka wapi?

Lazima tufunge mkanda hadi malengo yetu yatimie, sasa hatutamsikiliza mtu tena hadi pale Ndege zetu zitakaponunuliwa, na bado Reli ya Standard gauge pesa zote zinaenda kwa kampuni husika, yaan mikanda tuliyojifunga tutaifungua mwaka 2019
 
Siku zikitoa Bongo nazima tv yangu siku nzima maana kufanya mambo bila priority ni zaidi ya kero na maudhi matupu.

Ni kero na maudhi kumsikia mtu anajisifu kununua ndege kwa cash wakati wanafunzi wanakosa mikopo,madaktari na waalimu hawajiiriwa,madawa hospitalini shida,watumishi stahiki zao hawalipwi,watu wamesitishiwa ajira zao,wahanga wa tetemeko wanateseka,n.k.
 
Safi xaanaaa hadi fast jet wakatafute kwinginee. Tanzania mpya inakujaaa
Yaani hawa Fastjet waliowezesha % kubwa ya Watanzania kupanda ndege ndio unasema wakatafute pengine ? Ushajiuliza bila uwepo wao hali ingekuwaje ?

Aliyetuloga Watanzania sijui atafufuka lini

Sina tatizo na Magufuli kufufua shirika letu lakini nitakuwa mpumbavu nisipoheshimu revolution waliyoleta Fastjet kwenye airlines industry
 
unabana matumizi maana yake watu na wenyewe watabana matumizi hivyo watu wachache zaidi watapanda ndege kipindi hiki kuliko zamani, ndio maana fast jet wamepunguza route
Sasa unaongeza ndege huku watu hawana income ya kupanda hizo ndege biashara itafanyikaje?
Ni kama una biashara yako kisha wafanyakazi wakapunguziwa mishahara yao, na wakati huo huo ukawaletea bidhaa za bei ghali na luxury unategemea wananunue
 
Siku zikitoa Bunge nazima tv yangu siku nzima maana kufanya mambo bila priority ni zaidi ya kero na maudhi matupu.

Ni kero na maudhi kumsikia mtu anajisifu kununua ndege kwa cash wakati wanafunzi wanakosa mikopo,madaktari na waalimu hawajiiriwa,madawa hospitalini shida,watumishi stahiki zao hawalipwi,watu wamesitishiwa ajira zao,wahanga wa tetemeko wanateseka,n.k.
Ndio shida ya kuongozwa na kilevi...maskini!
 
Hali zenyewe mifukoni mwa wananchi ni mbaya, ni uchumi gani tulionao utatuletea faida?.

Tungeongeza moja kwa ajili ya route za kimataifa. Tukasikilizia

Kwa soko la ndani hizi mbili tulizonazo tungezisikilizia kwanza
 
Back
Top Bottom