Nchi zenye Uchumi mkubwa Afrika -Tanzania yaporokoma na kutoka 10 bora

Nawasalimu kwa Jina la JMT.

Kwa Mujibu wa makadirio ya Nchi zenye Uchumi mkubwa yaliyofanywa na shirika la fedha Duniani IMF kwa mwaka 2021,Tanzania imeporomoka na kushika nafasi ya 11.

Kwa miaka zaidi ya 10 ,Tzn imekuwa miongoni mwa Nchi zenye Uchumi mkubwa barani Africa kwa GDP,lakini kwa miaka ya hivi karibuni Uchumi ni kama ulidumaa kutoka ukuaji wa wastani wa 7% 2010-2015 hadi kufikia 4% mwaka 2021.

Hali hii ilichangiwa na sera mbaya za uchumi za Serikali iliyopita na matokeo yake ndio hayo,tumepitwa na nchi kama Angola,Tunisia,Ghana na sasa Ivory Coast.Nchi zote hizo Tulikuwa juu yao.

Mbaya zaidi hata gap la Uchumi Kati ya Mshindani wetu Kenya liliongezeka zaidi tofauti na awali ambapo Tulikuwa tunalifunga kwa kasi.

Kwa mwendo huu hivi kuna matumaini kweli huko tuendako? Nimesikitika Sana kwa hali hii kwa Nchi yenye rasilimali za kutosha .

View attachment 1836795
Kwa hiyo world bank walisema tumeingia uchumi wa kati wakati uchumi unadorora?
 
Wewe ni mtu wa ajabu, Uchumi ulianguka na kudumaa zaidi ndani ya miaka 5 iliyopita,sasa hivi ndani ya siku 100 investors confidence kwa mama ni kubwa na wameanza ku inject pesa za kuzidi.

Ukweli ni kwamba Uchumi wa mama utakuwa na mafanikio kuliko Marais waliopita hususani kwenye mageuzi ya Afya, elimu,maji na miundombinu.

Kwa kuanzia tuu umeona ajira za kuzidi,watumishi kulipwa pesa zao na kupandishwa madaraja, serikali imetenga pesa za kuzidi kwenye barabara hasa Tarura,Umeme,Afya na Elimu huku miradi ambayo ilimshinda mwendazake ikiendelea kutekelezwa.

Sijui wewe ndugu Uchumi wa makaratasi ni upi.
Umesahau umeongelea maziwa tuu .ngombe watoa maziwa umewasahau malisho yao
 
Usilinganishe wananchi wa Nigeria kuwa kwenye taifa sema dogo kiuchumi kwa mantiki yako basi hilo taifa waliopo wana Nigeria lina uchumi mkubwa kuliko wanageria. Hicho ni kichekesho cha mwaka na kuonyesha hujui kupambanua mambo, sijui uelewa wako upoj

Usilinganishe wananchi wa Nigeria kuwa kwenye taifa sema dogo kiuchumi kwa mantiki yako basi hilo taifa waliopo wana Nigeria lina uchumi mkubwa kuliko wanageria. Hicho ni kichekesho cha mwaka na kuonyesha hujui kupambanua mambo, sijui uelewa wako upoje.
Acha uvivu, jaribu ku Google tu upate taarifa za hali ya kiuchumi ya wananchi wa Nigeria. Huo uchimi mkubwa nipesa za watu binafsi wanao miliki visima vichache vya mafuta.
 
Umesahau umeongelea maziwa tuu .ngombe watoa maziwa umewasahau malisho yao
Hakuna watoa maziwa waliosahaulika,shida ya wabongo ni ufinyu wa uelewa.

Mtu asiye kwenye ajira rasmi au aliyejiajiri yeye atawekewa mazingira rafiki na Serikali Ili imrahisishie kwenye Kazi zake.Hapa ni pamoja na kaimalisha maeneo ya kutolea huduma,kuondoa vizingiti kadha was kadha nk Ili lengo kupunguza gharama na kuleta unafuu kwenye shughuli na tija ionekane.

Hayo yakifanyika utaona ustawi wa maisha yako kwa namna nyingi tuu ikiwemo uwekezaji wako kuongeza au kuongeza kiyegauchumi nk nk
 
Wewe ni mtu wa ajabu, Uchumi ulianguka na kudumaa zaidi ndani ya miaka 5 iliyopita,sasa hivi ndani ya siku 100 investors confidence kwa mama ni kubwa na wameanza ku inject pesa za kuzidi.

Ukweli ni kwamba Uchumi wa mama utakuwa na mafanikio kuliko Marais waliopita hususani kwenye mageuzi ya Afya, elimu,maji na miundombinu.

Kwa kuanzia tuu umeona ajira za kuzidi,watumishi kulipwa pesa zao na kupandishwa madaraja, serikali imetenga pesa za kuzidi kwenye barabara hasa Tarura,Umeme,maji,Afya na Elimu huku miradi ambayo ilimshinda mwendazake ikiendelea kutekelezwa.

Sijui wewe ndugu Uchumi wa makaratasi ni upi.
Investor confidence my ass! Upuuzi mtupu, Hayo aliyafanya sana Kikwete lakini wapi! Mwisho wa siku akatengeneza mianya ya ufisadi wa kutupwa! Swali ni moja tu! Tanzania iliingia top 10 uchumi bora Afrika awamu ya ngapi? Tanzania imeingia uchumi wa kati awamu ipi?
 
Naongea na mtu timamu au mpumbavu,kwa hiyo kwa akili yako ya kuendeshea chooni Serikali itatoa wapi kodi? Sikujibu tena seems naongea na mpumbavu
 
wametumia kipimo cha GDP yaani thamani ya uzalishaji wa nchi na haihusiani na ubora wa maisha wa wananchi husika. Ndio maana hapo huoni nchi ndogondogo zenye population ndogo ambazo zipo chini kiuzalishaji kutokana na udogo wao

kama wakitumia kipimo cha Human Development Index (HDI) ambacho hupima ubora wa maisha ikiwemo huduma za kijamii, usijeshangaa hata Nigeria isiwepo 10 Bora
Kweli kabisa Mkuu
Nigeria BOKO haram na wale wanaowateka Mabikra kila siku mpaka Serikali ikawakomboe ni ajabu kuwa Raia wako salma kuliko Tanzania, hapo wanapima uzalishaji km mafuta na wizi wao wa kwenda kuhifadhi nchi za nje
 
Nawasalimu kwa Jina la JMT.

Kwa Mujibu wa makadirio ya Nchi zenye Uchumi mkubwa yaliyofanywa na shirika la fedha Duniani IMF kwa mwaka 2021,Tanzania imeporomoka na kushika nafasi ya 11.

Kwa miaka zaidi ya 10 ,Tzn imekuwa miongoni mwa Nchi zenye Uchumi mkubwa barani Africa kwa GDP,lakini kwa miaka ya hivi karibuni Uchumi ni kama ulidumaa kutoka ukuaji wa wastani wa 7% 2010-2015 hadi kufikia 4% mwaka 2021.

Hali hii ilichangiwa na sera mbaya za uchumi za Serikali iliyopita na matokeo yake ndio hayo,tumepitwa na nchi kama Angola,Tunisia,Ghana na sasa Ivory Coast.Nchi zote hizo Tulikuwa juu yao.

Mbaya zaidi hata gap la Uchumi Kati ya Mshindani wetu Kenya liliongezeka zaidi tofauti na awali ambapo Tulikuwa tunalifunga kwa kasi.

Kwa mwendo huu hivi kuna matumaini kweli huko tuendako? Nimesikitika Sana kwa hali hii kwa Nchi yenye rasilimali za kutosha .

View attachment 1836795
Hii listi inawalakini . Bado Tz ipo Kwenye 10
 
TANZANIA haijawahi kuzishinda hizo nchi kwa GDP miaka ya hivi karibuni!
Katiba mpya ni ya lazima sio ombi!
 
TANZANIA haijawahi kuzishinda hizo nchi kwa GDP miaka ya hivi karibuni!
Katiba mpya ni ya lazima sio ombi!
Katiba mpya ndio inaleta GDP? 😄😄😄😄 Toka jf nenda road ukadai Katiba mpya.

Kama umesoma Uzi ni kwamba hadi 2016 Tulikuwa juu ya Ghana na Tunisia wakatupita.Mwaka Jana Tulikuwa juu ya Ivory coast,wametupita mwaka huu
 
Back
Top Bottom