Nchi Zenye kutumia Ubabe kulinda Mipaka yake na Maeneo Jirani, hata kama Nchi Jirani haitaki kulindwa italindwa tu

Nchi Zenye kutumia Ubabe kulinda Mipaka yake na Maeneo Jirani, hata kama Nchi Jirani haitaki kulindwa italindwa tu

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
2,563
Reaction score
7,321
The Monroe Doctrine sio dhana ya kipekee tu kwa Taifa la Marekani. Kwa wasiofahamu Monroe Doctrine ni sera inayokataza Mataifa ya kigeni hasa ulaya na kwingineko wasipeleke au kusogelea Nchi zozote zilizoko katika mabara ya America kusini na America kaskazini. Na nchi yoyote itakayojaribu kufanya ushawishi au kuweka kambi za kijeshi huko Amerika inatafsiriwa kama ni jaribio hatari la kutishia usalama wa Marekani. Nchi kama Venezuela na nyinginezo zote zimeingia katika sera hiyo na kujikuta mpaka Rais wao anatekwa na mafuta yanachukuliwa kinguvu kwa sababu china ilijaribu kutaka kuishawishi Venezuela kumkataa Mmarekani kwa hali na mali. Lakini sasa sera hii haiko tu kwa Marekani kuna Nchi nyingine nyingi tu zenye mfumo huo.

Kuna baba lao 🇷🇺 Russia yeye ana “Near Abroad Doctrine” katika maeneo ya zamani ya kisovieti (Former Soviet space) mfanoUkraine, Belarus, Caucasus, na Central Asia. Lengo kuu ni hakuna nchi nyingine kuweka Kambi na mazoezi ya kijeshi au muunganiko wa kijeshi karibu na Mipaka au nchi zilizopakana na Urusi. Nchi kama Ukraine, Georgia, Moldova → hizi uchukuliwa kama mstari hatari wa mwisho ambao nchi nyingine hasa kubwa hazitakiwi kuweka kambi za muungano wa kijeshi (Red lines enforced). Kupanuka kwa majeshi ya NATO ukanda huu karibu na Urusi inachukuliwa kama ni Tishio kwa warusi. Ukrein ilikiuka hizi sera na kutaka kujiunga na NATO ndio maana inapata kisago.


🇨🇳 China nayo ina mfumo wa “Core Interests Doctrine” katika maeneo ya Mashariki na Kusini Mwa Bahari ya Uchina (East & South China Sea) na eneo la Taiwan. Lengo kuu inapinga muingiliano wa nchi za kigeni katika maeneo yote ya kihistoria yaliyokuwa yanamilikiwa na china. Issue kama ya Taiwan kutaka kuwa na ushirikiano na Marekani ni jambo hatarishi kwa China, na ulinzi mzima wa bahari ya kusini mwa china.

🇮🇳 India nayo haiko nyuma ina “Indian Ocean & Subcontinent Doctrine” katika maeneo ya kusini mwa bara la Asia (South Asia) hasa katika maeneo kama Nepal, Sri Lanka, Maldives, na Bhutan. Lengo ni kupinga utawala wa mataifa ya Kigeni yenye nguvu karibu na mipaka ya India. Moja wapo wa mikakati ni kuzuia ushawishi wa Taifa la China hususani kwenye mambo ya mikopo na matumizi ya bandari katika nchi hizi zilizokaribu na India. Kuweka shinikiza la kisiasa katika nchi hizi jirani. Kudhibiti mikondo yote ya bahari ya Hindi hususani karibu na maeneo ya mipaka ya India.


🇫🇷 France (Ufaransa) nayo ina “Françafrique Doctrine” katika makoloni yake yaliyoko Africa, na yanayozungumza kifaransa (Francophone Africa). Lengo ikiwa ni Makoloni yote ya Ufaransa yabaki katika mzunguko wa kimkakati wa Kifaransa. Mara nyingi wafaransa uweka Kambi za kijeshi katika Makoloni haya yake ya zamani hasa maeneo ya Afrika Magharibi na Afrika ya kati. Pia Wafaransa wanadhibiti Sarafu za nchi hizi, unaweza kusema Currency control (CFA Franc). Pia wanatabia ya kuingilia maamuzi ya nchi hizi pale ambapo inabidi au endapo itatokea shida inayoathiri maslahi ya ufaransa.


Nchi kama 🇹🇷 Turkey (Uturuki) nayo inadhibiti maeneo yote yaliyokuwa chini ya utawala wa Ottoman “Neo-Ottoman Sphere” hususani maeneo kama Balkans, Caucasus, Middle East (Mashariki ya kati). Lengo kuu ikiwa ni kurudisha ushawishi wa maeneo yote yalikuwa chini ya utawala wa Ottoman katika enzi zile. Waturuki mara nyingi utawakuta wanaingilia maamuzi ya nchi kama Syria na Libya. Vilevile kuweka ushawishi katika nchi kama Azerbaijan. Na huku wakiangazia kuweka nguvu za kiutamaduni na kijeshi katika maeneo hayo.

Kuna Mwamba mwingine anaitwa 🇮🇷 Iran yeye uwa ana “Axis of Resistance Doctrine” katika maeneo kama Iraq, Syria, Lebanon, na Yemen. Lengo ikiwa ni kuwazunguka Wapinzani, Maadui, au Wanaopinga utawala wa Iran kwa kutumia nchi wakala, nchi nyingine Wawakilishi, Vyombo vya uwakala, Mabwana kazi, or Watu wanaoweza kutenda jambo kwa maagizo Wakiwa eneo tofauti. Huku wakikwepa kuwajibika moja kwa moja na mashambulizi ya aina yoyote kwa sababu hayatoki katika ardhi yao. Mara nyingi Iran ufanya mikakati yake kwa kuwatumia makundi ya kimgambo kama Hezbollah, Houthis, wengineo kufanya operesheni katika ardhi nje ya Iran. Kwanza Iran inakuwa haihusiki na uvamizi hivyo inakuwa rahisi kukataa haina yoyote ya madai kuwa imehusika

Nchi kama 🇸🇦 Saudi Arabia nayo ina “Arab Peninsula Doctrine” katika maeneo ya Ghuba (Gulf states) na Yemen. Lengo ikiwa ni Sera hiyo inahakikisha kuwa hakuna utawala hasimu (au wenye uadui na Saudia) karibu na mipaka yao. Kuna kipindi Saudi Arabia alikinukisha huko Yemen, pia Saudi Arabia uweka shinikizo la kisiasa katika nchi za ukanda huo wa Ghuba. Huku ikitumia diplomasia za uchumi wa mafuta kama nguvu ya ushawishi.

🇮🇱 Israel nayo ina sera ya “Security Perimeter Doctrine” katika maeneo ya Palestina, Syria, Lebanon, na Jordan na wakati mwingine usogea mpaka maeneo ya uturuki kusini, Sinai na Iraq kidogo… kitaalamu haya maeneo yanaitwa “Levant”. Lengo ikiwa ni Kuhakikisha kuwa hakuna utawala hasimu au utawala adui dhidi ya Nchi ya Israel au Mipaka yao. Mara nyingi wanatumia utawala wa nguvu ya kijajusi kudhibiti utawala wowote ambao ni tishio, pia wanatumia eneo nje ya ardhi yao au miji yao kama eneo la kudhibiti mashambulizi, Waisraeli vita hawaipeleki nyumbani kwao, vita wanaipeleka maeneo nje ya makazi yao (Buffer Zones), au vita wanampelekea adui mwenyewe hili yeye ndio apate athara. mfano Ukanda wa Gaza, na west bank, Lebanon na Syria kama Buffer zones… yani vita inatolewa eneo lao na kuamishiwa eneo lingine au eneo la adui. Ukitaka vita wanakuletea mlangoni kwako hili wewe ndio uwe muanga wa mashambulizi, na sio wao. Pia wanatabia ya kufanya Shambulio la mapema au Shambulio la kuzuia pale wanapohisi una nia ya kutaka kuwashambulia, hivyo wanakuwai kabla wewe hujatoa shambulio lolote.

Vile vile hata Tanzania 🇹🇿 ina sera yake ya Muungano, licha ya Zanzibar imeruhusiwa kujitawala lakini haitakiwi kufanya maamuzi yoyote yale ya Kijeshi bila idhini ya Muungano au Tanzania kwa ujumla. Hakuna nchi nyingine inayoruhusiwa kuweka kambi za kijeshi eneo la Zanzibar bila idhini ya Tanzania licha ya Zanzibar kuwa na serikali yake. Nchi nyingine ikitaka kuweka ushawishi Zanzibar basi mara moja Tanzania itatafsiri kama inaingiliwa katika eneo lake la kuivinjari. Na jeshi litalazimika kuingia katika kutatua changamoto hiyo hili kulinda maslahi ya Tanzania.
 
Kama OIC kutaka kuingia zanzibar, Tanzania ilikataa
 
Back
Top Bottom