Nchi za Ulaya, Marekani na Asia; heshimuni matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania

Kabende Msakila

JF-Expert Member
Oct 7, 2020
1,389
1,258
WanaJF, Salaam!

Nimeandika machache tu kuhusu nchi zenye rekodi ya ukosoaji na ufuatiliaji wa masuala ya uchaguzi na matokeo yake barani Africa ikiwemo Tanzania.

Jumuiya za kimataifa zinapaswa kuheshimu matokeo ya uchaguzi mkuu uliowaweka wagombea wengi wa CCM madarakani kwa kuwa utashi wa wengi ni Sheria (The Will of the many people is the best law). Wengi wa watanzania walifuatilia kampeni, walilinganisha wagombea, kisha tarehe 28 Oktoba 2020 walichagua waliyemtaka. Sasa inasikitisha kuona mara Marekani yatahadhalisha! Mara UK yatoa onyo, - tuacheni huru kwa sisi wenyewe tunaamua juu ya viongozi tuwapendao na chama tukipendacho!

Mahakama ya kimataifa ikiingilia Uhuru wetu wa maamuzi basi ni vizuri tujitoe, tuwaachie mahakama yao iliyoundwa kwa ajili ya Africa - iliyoundwa kwa maslahi ya mabeberu na vibaraka wa mabeberu.

Nchini Tanzania zipo mahakama, kama kuna jambo basi lipelekwe kwenye mahakama hizo lkn si kutumia migogoro kidogo iliyojitokeza kwenye uchaguzi kuharalisha watu kwenda ICC - kesi ya Baganda (Police) mbn ilisikilizwa nchini na shauri Kutolewa kwa haki! Kesi ya Eng Chiza kupinga matokeo na ushindi dhidi ya Bilago mbn ilisikilizwa nchini na CDM walishinda!

Kesi ya mauaji ya Mwangosi mbn ilifunguliwa na wahusika kuwajibishwa - kwa ufupi tu ifahamike kwamba migogoro iliyojitokeza kabla, wakati, na baada ya uchaguzi kama nchi tunaimudu kuitatua - UK, US nk tuacheni tuitatue wenyewe!

Note:
Dkt Magufuli hajawahi kushindwa na asingeshindwa ktk uchaguzi mkuu huo
 
Ule haukuwa uchanguzi, bali maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. Tuombe tu hizo nchi za nje zisichukue hatua, lakini zikichukua hatua tutawaunga mkono, na tutakwenda kutoa ushahidi wa ushenzi uliofanyika kwenye uchaguzi huu. Hatuko tayari kuongozwa kwa shuruti na CCM.
 
Ziheshimu matokeo ya uchaguzi ambao kura halali hazijaamua mshindi bali kura na matokeo yaliyoandaliwa na TISS na NEC???

Ziheshimu matokeo ya uchaguzi ambao kura zilipigwa na wanafunzi walio chini ya miaka 18 kwenye mashule ya boarding na kupelekwa usiku kwenye vituo chini ya ulinzi wa polisi?

Ziheshimu matokeo ya uchaguzi ambao mlikataa mawakala wa upinzani kuingia vituoni na kwa wale walioingia mliwafukuza kwenye kuhesabu kura?

Ziheshimu matokeo ya uchaguzi ambao mliengua wagombea wa upinzani kwa maelfu na mkakataa kuwarudisha huku wengine mkiwarudisha bila kupewa barua hivyo kukataliwa kufanya kampeni?

Ziheshimu uchaguzi ambao tangu kwenye kampeni mlikataza radio na television channels kurusha live mikutano ya mgombea wa upinzani mwenye nguvu Tundu Lissu uhuru siku kadhaa kabla ya kampeni mkiziamuru kampuni za simu ku censor Jina lake kwenye messages ???? Tena mbaya zaidi mkazima internet siku ya uchaguzi na matokeo ili matukio yenu ya sisi wa kura yasirushwe?

Mnafikiri hayo mataifa mliyoyataja ni mazumbukuku kama hao watu wenu wa Lumumba eeeh?

Na Bado mwaka huu , huku vikwazo, huku ICC , lazima muite Maji mmaaaaaa!!
 
Ziheshimu matokeo ya uchaguzi ambao kura halali hazijaamua mshindi bali kura na matokeo yaliyoandaliwa na TISS na NEC???

Ziheshimu matokeo ya uchaguzi ambao kura zilipigwa na wanafunzi walio chini ya miaka 18 kwenye mashule ya boarding na kupelekwa usiku kwenye vituo chini ya ulinzi wa polisi???


Ziheshimu matokeo ya uchaguzi ambao mlikataa mawakala wa upinzani kuingia vituoni na kwa wale walioingia mliwafukuza kwenye kuhesabu kura????

Ziheshimu matokeo ya uchaguzi ambao mliengua wagombea wa upinzani kwa maelfu na mkakataa kuwarudisha huku wengine mkiwarudisha bila kupewa barua hivyo kukataliwa kufanya kampeni???

Ziheshimu uchaguzi ambao tangu kwenye kampeni mlikataza radio na television channels kurusha live mikutano ya mgombea wa upinzani mwenye nguvu Tundu Lissu uhuru siku kadhaa kabla ya kampeni mkiziamuru kampuni za simu ku censor Jina lake kwenye messages ???? Tena mbaya zaidi mkazima internet siku ya uchaguzi na matokeo ili matukio yenu ya sisi wa kura yasirushwe?????

Mnafikiri hayo mataifa mliyoyataja ni mazumbukuku kama hao watu wenu wa Lumumba eeeh????

Na Bado mwaka huu , huku vikwazo, huku ICC , lazima muite Maji mmaaaaaa!!
Na kunyimwa misaada na mikopo.
 
1605471786890.png
 
Umeandika Kama kada, uchaguzi tume tayari ilishakuwa na matokeo yake hata kabla ya upigaji kura, kura zilipigwa Kama formalities za kuhadaa watu. Simple tu Kama walizima internet hayo matokeo walitumia njia ngapi kuyawakilisha. Kusema ICC imeumbwa kwa ajili ya Africa kweli swali je hao wanaopelekwa huko wanaonewa? Awanuki damu za waafrika?

Angalau uwepo wa ICC na hofu ya kukosa misaada uwarudisha nyuma watawala wa kiafrica wasimalize waafrika sababu ya matumbo yao na familia zao, bila hivyo waafrika tungeuliwa Sana usiku na mchana na Hawa watawala, maana ni salama zaidi kumkosoa Mungu kuliko kumkosoa mtawala wa kiafrika.

Uliona wapi mtu apewe Kinga ya kutokustakiwa na akatenda haki.
 
Mahakama za Tanzania hizi ambazo watu wapo rumande kwa kesi za kisiasa wanapewa kesi za money laundering na kesi haisikilizwi hakimu ameenda kwenye kitchen party Iringa anarudi after 2 wks.
Tena Hawa mahakimu zetu kesi za upinzani wanazishughulikia haswaa ili kumridhisha boss wao ili awape teuzi tumeshuhudia wakipewa hadi promotion ikiwemo ujaji kwa kuwafunga wapinzani case study Sugu Mbeya.

Mahakama zetu haziwezi kuwa huru pasipo katiba mpya,zimekuwa ni tools za kuwashughulikia wale wote wasio na chapa 666.Kama wwe huna chapa kuwekwa ndani miaka 8 ukisubiria ushahidi kukamilika.
 
Hivi unaweza kumuheshimu mwizi, maana hizo ndiyo tabia za maaCCM
Hili silishangai nimeona kwa macho yangu jirani yangu kavamiwa katika eneo lake lenye hati miliki kapewa barua yenye nembo ya Jiji ikimtambua mvamizi na kusema apewe sehemu ya eneo alio vamiwa hatari kabisa
 
Back
Top Bottom