Wazo Dokezi: Upigaji wa Uchaguzi Mkuu Utaanza "Soon"...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,478
39,998
Na. M. M. Mwanakijiji

Mojawapo ya vitu ambavyo huwa vinafanywa 'vizuri' na watawala wa watawaliwa unapoelekea mwaka wa uchaguzi ni jinsi gani huwa wanajipanga kujipendezesha kwa wakubwa wa dunia. Unajua pale nchi inapojisema tu kuwa ni ya "kidemokrasia" basi wakubwa wanaanza kuangalia vitu vinavyofanyika hasa linapokuja suala la uchaguzi. Uchaguzi unachukuliwa kama kipimo hasa cha ni jinsi gani nchi imekomaa kidemokrasia.

Inapotokea tu kuwa kuna figisufigisu fulani basi wakubwa wa dunia - US, UK, EU, UN na taasisi mbalimbali huwa na haraka ya kutuamulia kama uchaguzi ulikuwa huru na waki (free and fair). Lakini wao hawaanzii siku ya uchaguzi tu bali wanaangalia hata miezi michache nyuma. Na taasisi za ndani na za nje zote zinaanza kutoa "mafunzo" (training) kwa waangalizi wa ndani na wa nje. Waangalizi wa ndani ni wale wa taasisi za kiserikali na za nje ya serikali ambazo huwa zinafuatilia uchaguzi kuanzia maandalizi hadi utangwazaji wa matokeo ya uchaguzi na hata uapishaji wa uongozi mpya.

Zinapokuwepo taasisi za kidini na zisizo za kidini za ndani. Lakini linapokuja lile la waangalizi wa nje wao wanaweza kushirikiana na taasisi hizi za ndani au wakawa na watu wao wenyewe mara nyingi hawa huanza kuingia nchini kama miezi mitatu kabla ya siku ya uchaguzi mkuu. Wakiongozwa na utaratibu uliowekwa na tume ya uchaguzi basi taasisi hizi hupewa uhuru wa kutembelea sehemu mbalimbali kuona maandalizi ya uchaguzi yanavyokwenda na wanalindwa na sheria na taratibu mbalimbali. Taasisi hizi huwekewa masharti ambayo wanatakiwa wayafuate.

Lakini kubwa linalotuhusu leo - ni jinsi gani - wakubwa wa dunia wanaweza kuizawadia nchi kwa kuandaa uchaguzi mzuri. Hivyo watawala wa watawaliwa hujitahidi saini kupambisha maandalizi ya uchaguzi ili jicho la wakubwa lianze kuangalia kwa mapenzi. Hili linatuleta kwenye mada ya leo.

Tunavyoelekea uchaguzi mkuu mwakani tutaanza kusikia na kuona jinsi watendaji wa serikali wa ngazi mbalimbali wakianza kuonesha na kuahidi jinsi gani uchaguzi wa mwakani utakuwa na tofauti kubwa na ule wa 2020. Unaweza kuamini kabisa - ukiwasikiliza sana - kuwa hiki chama kinachoenda kuandaa uchaguzi ujao sicho kilichoandaa uchaguzi uliopita na kuwa sasa wamepata akili ya kuendesha uchaguzi mzuri, usio kuwa na rabsha wala washawasha.

Kwa vile wakubwa wataanza kuvutiwa basi muda si mrefu tutaanza kusikia wakubwa wakitoa misaada ya kuandaa uchaguzi mkuu. Kuna fedha nyingi - mabilioni- ya maandalizi ambavyo yataelekezwa kwa vyama vya siasa na wanufaika wakubwa wakiwa ni chama cha watawala wa watawaliwa. Ikumbukwe kuwa katika fedha hizo kuna ulaji mkubwa unaofanyika kuanzia kwenye maandalizi ya makabrasha ya mafunzo, mafunzo yenyewe, uchaguzi wa nani atakuwa mwangalizi (ndugu, jamaa, na marafiki) na taasisi zao za NGO zikijiandiksha tume ya uchaguzi kuwa watakuwa ni sehemu ya waangalizi wa ndani au wa kimataifa.

Itaendelea...
 
Tumeshaanza kusikia kauli zikidai uchaguzi wa 2020 ulikuwa ni mbaya kwani uliwagawa na kuwaogofya Watanzania..

Lakini wanaosema hayo ndiyo wale wale siku zote hawajakanusha tuhuma za wizi wa chaguzi kuu zilizopita.

Yetu macho kwenye hizi pilika za maandalizi
 
2020 kulikuwa na uchaguzi gani?
 
Unaweza kuamini kabisa - ukiwasikiliza sana - kuwa hiki chama kinachoenda kuandaa uchaguzi ujao sicho kilichoandaa uchaguzi uliopita na kuwa sasa wamepata akili ya kuendesha uchaguzi mzuri, usio kuwa na rabsha wala washawasha.
Once a liar always a liar..
Kuamini hicho chama baada ya yale madhila ya 2020 ni ngumu, watu wanalazimika kutulia tu kwa shuruti
 
Uchaguzi mkuu haujawahi kuwa huru na haki nchi hii, kinachoenda kutokea 2025 tutarudishwa kwenye ule wizi wa kura tuliozoeshwa miaka ya nyuma.

Naamini hata wapinzani nao walishauzoea ule wizi wa zamani ndio maana sasa wanaamua kushiriki uchaguzi kwa tume hii mbovu iliyopo.

2020 inatumika kama kipimo cha juu kabisa cha uharibifu uliowahi kufanyika kwenye historia ya chaguzi zetu, pale ndipo Magufuli aliharibu kwa kiasi kikubwa sana mpaka akawaogopesha wezi wenzake ndani ya CCM akishirikiana na kina Makamba.
 
Tumeshaanza kusikia kauli zikidai uchaguzi wa 2020 ulikuwa ni mbaya kwani uliwagawa na kuwaogofya Watanzania..

Lakini wanaosema hayo ndiyo wale wale siku zote hawajakanusha tuhuma za wizi wa chaguzi kuu zilizopita.

Yetu macho kwenye hizi pilika za maandalizi
Kwakweli ulikua mbaya na wenye dhuluma kuu

Tunaomba Mungu hali ile isijirudie
 
Kauli zishaanza kutoka-ndio maandalizi hayo.

CCM wanadai 2025 hakutakuwa na Uzuzu wala Mazuzu, yani full no mazingaombwe, kwamba hakuna "goli la mkono" wala nini.

Huku, hawa wanaharakati, ukiondoa ACT-Wazalendo NCCR- Mageusi, UDP n.k n.k washaanza kusema kuna mbinu zinaandaliwa ili kura ziibiwe.

Ila sijayasikia ya "Wasimamizi" au ya "Waangalizi" zaidi ya ripoti ya Profesori Mukandala kuhusu Uchaguzi wa 2020, walakini tunaeza sema aligusia kidogo "concerns" kuelekea 2024-2025

Report of the 2020 General Election in Tanzania

Aliandika katika Utangulizi[Foreword]

"...There was, and still is, suspicion regarding the sincerity of the state and the neutrality of election management bodies..."

Tume huru ishapatikana, tunaamini hivyo, ingawaje CHADEMA wanadai bado tume hiyo haina 'uhuru' ama kwa lugha nyingine, matakwa yao yalipuuzwa, ila basi, watashiriki.

Wakishindwa itakuwaje? Wanachagulika?

NB:
R.I.P J.P.M , Comrade, Wanakuzodoa huku, wanadai uliondoa nyota yao kwenye medani za kisiasa.

Sasa kumewiva, sijui itakuwaje...

Wakishindwa watakuja kuandamano CHATO?
 
Tumeshaanza kusikia kauli zikidai uchaguzi wa 2020 ulikuwa ni mbaya kwani uliwagawa na kuwaogofya Watanzania..

Lakini wanaosema hayo ndiyo wale wale siku zote hawajakanusha tuhuma za wizi wa chaguzi kuu zilizopita.

Yetu macho kwenye hizi pilika za maandalizi
Kuna mmoja-kapanda Boda Boda huko Lindi
 
Tayari harambee za kuchukua fomu zimeanza, milioni 120 ipo na fomu itakuwa Moja tu.
 
Nusu mkate fc wameshafika bei!

Lengo la katiba mpya na tume huru limekufa,Sasa naonaupinzani ukiwaza Santa idadi ya wabunge na halmashauri watakazoshika!!
 
Tanzania hakuna uchaguzi, bali Kuna maonyesho ya ujinga wa mtu Mweusi kwenye box la kura. Mtu mjinga tu, au anayefaidika na chaguzi hizi za kishenzi, ndio ataendelea kujitokeza kushiriki kwenye chaguzi katika mifumo hii hii.
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Mojawapo ya vitu ambavyo huwa vinafanywa 'vizuri' na watawala wa watawaliwa unapoelekea mwaka wa uchaguzi ni jinsi gani huwa wanajipanga kujipendezesha kwa wakubwa wa dunia. Unajua pale nchi inapojisema tu kuwa ni ya "kidemokrasia" basi wakubwa wanaanza kuangalia vitu vinavyofanyika hasa linapokuja suala la uchaguzi. Uchaguzi unachukuliwa kama kipimo hasa cha ni jinsi gani nchi imekomaa kidemokrasia.

Inapotokea tu kuwa kuna figisufigisu fulani basi wakubwa wa dunia - US, UK, EU, UN na taasisi mbalimbali huwa na haraka ya kutuamulia kama uchaguzi ulikuwa huru na waki (free and fair). Lakini wao hawaanzii siku ya uchaguzi tu bali wanaangalia hata miezi michache nyuma. Na taasisi za ndani na za nje zote zinaanza kutoa "mafunzo" (training) kwa waangalizi wa ndani na wa nje. Waangalizi wa ndani ni wale wa taasisi za kiserikali na za nje ya serikali ambazo huwa zinafuatilia uchaguzi kuanzia maandalizi hadi utangwazaji wa matokeo ya uchaguzi na hata uapishaji wa uongozi mpya.

Zinapokuwepo taasisi za kidini na zisizo za kidini za ndani. Lakini linapokuja lile la waangalizi wa nje wao wanaweza kushirikiana na taasisi hizi za ndani au wakawa na watu wao wenyewe mara nyingi hawa huanza kuingia nchini kama miezi mitatu kabla ya siku ya uchaguzi mkuu. Wakiongozwa na utaratibu uliowekwa na tume ya uchaguzi basi taasisi hizi hupewa uhuru wa kutembelea sehemu mbalimbali kuona maandalizi ya uchaguzi yanavyokwenda na wanalindwa na sheria na taratibu mbalimbali. Taasisi hizi huwekewa masharti ambayo wanatakiwa wayafuate.

Lakini kubwa linalotuhusu leo - ni jinsi gani - wakubwa wa dunia wanaweza kuizawadia nchi kwa kuandaa uchaguzi mzuri. Hivyo watawala wa watawaliwa hujitahidi saini kupambisha maandalizi ya uchaguzi ili jicho la wakubwa lianze kuangalia kwa mapenzi. Hili linatuleta kwenye mada ya leo.

Tunavyoelekea uchaguzi mkuu mwakani tutaanza kusikia na kuona jinsi watendaji wa serikali wa ngazi mbalimbali wakianza kuonesha na kuahidi jinsi gani uchaguzi wa mwakani utakuwa na tofauti kubwa na ule wa 2020. Unaweza kuamini kabisa - ukiwasikiliza sana - kuwa hiki chama kinachoenda kuandaa uchaguzi ujao sicho kilichoandaa uchaguzi uliopita na kuwa sasa wamepata akili ya kuendesha uchaguzi mzuri, usio kuwa na rabsha wala washawasha.

Kwa vile wakubwa wataanza kuvutiwa basi muda si mrefu tutaanza kusikia wakubwa wakitoa misaada ya kuandaa uchaguzi mkuu. Kuna fedha nyingi - mabilioni- ya maandalizi ambavyo yataelekezwa kwa vyama vya siasa na wanufaika wakubwa wakiwa ni chama cha watawala wa watawaliwa. Ikumbukwe kuwa katika fedha hizo kuna ulaji mkubwa unaofanyika kuanzia kwenye maandalizi ya makabrasha ya mafunzo, mafunzo yenyewe, uchaguzi wa nani atakuwa mwangalizi (ndugu, jamaa, na marafiki) na taasisi zao za NGO zikijiandiksha tume ya uchaguzi kuwa watakuwa ni sehemu ya waangalizi wa ndani au wa kimataifa.

Itaendelea...
yaliyopita si ndwele tugange ya sasa na yajayo 🐒

Jambo muhimu zaidi ni uchaguzi wa amani, huru, wazi na wa haki kwa waTanzania wote🐒
Nadharia nyingine labda ni katika kukumbushana mambo na tahadhari muhimu za kua nazo makini...

Ile muhimu zaidi, ifahamike tu kwamba Tanzania tunaelekea kwenye chaguzi bora, makini na credible zaidi duniani siku si nyingi zijazo 🐒
Ni vizuri kujipanga kutumia fursa hiyo muhimu sana kwa waTanzania wote 🐒
 
Nusu mkate fc wameshafika bei!

Lengo la katiba mpya na tume huru limekufa,Sasa naonaupinzani ukiwaza Santa idadi ya wabunge na halmashauri watakazoshika!!
Ulitaka wapinzani wafanya nini ili kupata katiba mpya na tume huru ya uchaguzi? Je,jukumu hilo nila umma wote au kundi la wachache.

Vipi wale wanao jifanya Wazalendo (DP) wamefika wapi au wamezidiwa akili na wanasiasa.
 
yaliyopita si ndwele tugange ya sasa na yajayo 🐒

Jambo muhimu zaidi ni uchaguzi wa amani, huru, wazi na wa haki kwa waTanzania wote🐒
Nadharia nyingine labda ni katika kukumbushana mambo na tahadhari muhimu za kua nazo makini...

Ile muhimu zaidi, ifahamike tu kwamba Tanzania tunaelekea kwenye chaguzi bora, makini na credible zaidi duniani siku si nyingi zijazo 🐒
Ni vizuri kujipanga kutumia fursa hiyo muhimu sana kwa waTanzania wote 🐒
Labda Tanzania nyingine siyo hii
 
Back
Top Bottom