Serikali yaanza kuwapiga Msasa Mawakili kujiandaa na Uchaguzi Mkuu

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Serikali ya Tanzania imeanza kuwajengea uwezo mawakili wake ili kuzikabili kesi zitakazojitokeza baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2024 na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Mafunzo kwa mawakili hao yanatokana na kile kilichoelezwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Dk Eliezer Feleshi kuwa kuna matarajio ya mabadiliko ya sheria za uchaguzi, hivyo inabidi kuwaandaa mawakili mapema.

Kamati ya Bunge imekamilisha hatua ya kupokea maoni ya wadau kuhusu mabadiliko ya sheria mbalimbali za uchaguzi, ambazo miswada yake iliwasilishwa bungeni tangu Novemba 10, 2023.

Dk Feleshi ametoa kauli hiyo mkoani Pwani leo Jumatano, Januari 17, 2024, katika hotuba yake ya kufungua mafunzo ya siku tano yanayowahusisha watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kutoka mikoa 16 nchini.

“Tulichokifanya ni kuangalia kwa pamoja kwamba, sasa hivi huenda kukawa na mabadiliko ya sheria zetu (za uchaguzi) huwezi kuacha mawakili wako wasubiri kinachotokea kwa sababu itakuwa tumechelewa sana,” amesema alipotafutwa na Mwananchi Digital kufafanua zaidi kuhusu mafunzo hayo.

Amefafanua kuwa kazi ya ofisi yake ni kuhakikisha kunakuwa na utawala wa sheria, hivyo kuwaandaa mapema mawakili hao ni jambo muhimu.

Katika mafunzo hayo, Dk Feleshi amewataka mawakili hao kujifunza maarifa mapya na stadi za kazi na kufanya utafiti bila kukoma, kujilinda na uovu na kuwa waaminifu muda wote.

Kwa kuwa teknolojia zinabadilika, amesema ni wajibu wa mawakili hao kuongeza maarifa mapya yatakayoboresha utendaji wa kazi zao na kuwa waangalifu katika maneno na mawasiliano wanayofanya.

"Tunajifungia na kukumbushana wajibu ili hata hapo tutakapolazimika kuchukua hatua kwa wanaokwenda kinyume kusiwe na lawama, hili lipo hata kwenye vitabu vitakatifu waliposema mkulima alishauri mti umwagiliwe mbolea na usipozaa mwakani utakatwa,” amesema.

Wakili Mkuu wa Serikali, Dk Boniphace Luhende amesema mafunzo hayo yataboresha ufanisi wa watendaji hao na kusaidia kutatua changamoto mbalimbali.

Amesema kwa kipindi cha miaka mitatu ofisi hiyo imekuwa ikitoa mafunzo kwa menejimenti yake.

Akizungumzia mafunzo hayo, mkazi wa Pwani Said Mselem amewataka mawakili pia kuweka utaratibu wa kutoa elimu ya sheria za uchaguzi kwa baadhi ya wananchi hususa wenye nia ya kugombea uongozi ili waepuke makosa yanayoweza kuvuruga amani.

“Kuna baadhi ya wanachama wamekuwa wakijiingiza kwenye mkumbo wa kushabikia mambo ya siasa na kuvunja sheria, hususan unapokaribia uchaguzi na kusabaisha mlundikano wa kesi kwenye mahakama.

“Ni vema wakapewa elimu ili wasijiingize kwenye hatari hiyo kwa kuwa inachangia kuvuruga amani ya nchi, jambo ambalo si jema.
 
serikali makini inaona mbali na kujiandaa 🐒
 
Back
Top Bottom