Kiboko ya Jiwe
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 12,709
- 36,166
Ukiuliza sera ya serikali kwa sasa ni nini hata viongozi wenyewe hawajui. Wataanza kukutajia SGR, Bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere, watakutajia Bandari na kadhalika.
Kwa ufupi hata viongozi hawajui Tanzania na Watanzania wanahitaji nini.
Watanzania wenyewe pia hawajui wanahitaji nini kwasasa, miaka na miaka kazi kulalama kuwa maisha magumu.
Ukimuuliza Mtanzania kwanini maisha magumu utamsikia anasema serikali ndio sababu.
• Kwa wingi huu wa rasilimali sikutarajia mpaka sasa kuona wamama wajawazito Dar es salaam wakienda kujifungua na mapegi mgongoni yaliyojaa vifaa vya kujifungulia.
• Kwa wingi huu wa rasilimali sikutarajia kuona a baadhi ya shule za msingi Dar es salaam darasa Moja kurundikana wanafunzi zaidi ya mia moja.
• Ardhi yenye rutuba ipo , viwanda vya sukari vipo lakini sasa mwaka wa 8 bei ya sukari si himilivu.
Kwa ufupi Watanzania watapata taabu mpaka mwisho wa Dunia.
Anayebisha abishe lakini akumbuke matumaini waliyopewa Watanzania 2012/2013 jinsi gesi ya Mtwara itakavyoondoa umaskini. Leo hii ni miaka 10 tangu mradi uanze.
Kiko wapi?