La Bandari kuuzwa, Uongo umefika mwisho. Tujisahihishe tujenge Nchi

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
LA BANDARI KUUZWA, UONGO UMEFIKA MWISHO, TUJISAHIHISHE TUJENGE NCHI.

Na Yericko Nyerere

Kabla sijaanza kujadili kuhusu sakata la bandari ya Dar kubinafsishwa milele (Hadi Mwarabu atakapomaliza kazi yake kama MoU inavyosema), Naomba twende taratibu turudi nyuma kidogo, Mwezi April 2021, Dakika chache tu baada ya kufariki Rais Magufuli, aliyekuwa mfuasi kindakindaki wa hayati John Magufuli bwana Job Ndugai akiwa spika wa bange la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliyeapa kumuongeza muda wa kutawala kidikteta Tanzania atake asitake, alimgeuka mchana kweupe na kulitangazia taifa kuwa serikali ya Rais John Magufuli ilikuwa ya UONGO MKUBWA kuhusu mradi wa Bandari ya Bagamoyo. Mimi nilimuunga mkono Ndugai kwa asilimia miamoja kuhusu mradi huu. Miezi 7 baadae serikali ya Rais Samia nayo ikatangaza rasmi kuwa serikali ya Rais Magufuli ilikuwa ya UONGO kuhusu mradi wa Bandari ya Bagamoyo, Haya yalitamkwa November 2021 kama kauli rasmi ya Serikali ya Tanzania chini ya Waziri Mwambe katika kuhitimisha uongo wa serikali ya awamu ya tano kuhusu mradi huu, na kutangaza rasmi kuwa mradi wa Bagamoyo utaanza rasmi.

Historia ya mradi wa Bagamoyo ni ndefu, inaanzia katika Serikali ya awamu ya nne chini ya Jakaya Kikwete iliyoanzisha mradi wa kimkakati kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha biashara duniani, mradi huu ilikuwa ni kujenga bandari ya Mtwara kwa UBIA kati ya Tanzania, China na Omani wenye thamani ya dola bilioni 10 kwa wakati huo, Serikali ya Tanzania katika mradi huu ilikuwa haiweki pesa yoyote isipokuwa ardhi na raslimali zingine, huku Uchina na Omani wakiweka mtaji na utaalamu.

Kwamjibu wa mapendekezo ya "mkataba wa awali" wa mradi huo, ni kwamba kungeundwa chombo maalumu cha nchi zote tatu ambacho kingeendesha na kusanya mapato ya mradi huu na kusimamia gawio la pande zote, hii inamaana kwamba TRA ya Tanzania isingekuwa na haki ya kukusanya mapato moja kwa moja kutoka katika mradi badala yake ingekusanya gawio toka kwa chombo cha wabia kinachokusanya mapato ya mradi wa nchi zote tatu.

Huu ni moja ya mradi ambo kimsingi ulikuwa umeitangazia dunia vita vya kiuchumi toka kwa washindani wetu ambao ni nchi jirani na zinazotuzunguka. Kwakuwa Afrika yote ingepokelea bidhaa zake toka ulimwenguni hadi Mtwara, sawa na ilivyo Dubai ambayo ndio mlango wa Afrika kupokelea bidhaa zake. Ilitumwa timu ya wataalamu kutembelea Dubai, Singapore na kwingine, kisha ikaja kuandika ripoti ya upembuzi yakinifu (feasibility study). Ripoti ilipofikishwa mbele ya serikali, ghafla mradi ukapunguzwa ukubwa wake na kupelekwa bagamoyo, lakini wabia wakibaki wale wale na ikasainiwa MOU (Mkataba wa awali).

Afrika inaingiza bidhaa toka Uchina kwa 88.8% na kiwango cha 98% ya bidhaa hizo zinapita Dubai. Hivyo kujengwa kwa Bandari ya Bagamoyo kungefunga nyia ya Dubai na bidhaa zote za Afrika kutoka China kupita Bagamoyo. Hii inamaana kwamba uchumi wa Dubai na Marekani ambayo ndio MBIA mkuu ungemegwa. Mradi huu ulikuwa ndio msingi halisi wa kuanzisha mradi wa reli ya kisasa ya SGR, bila Bandari itakayozalisha mizigo kwa wingi SGR itakuwa ni kwakubeba abiria tu badala ya mizigo.

Serikali ya awamu ya tano katika hali ya kustaajabisha imeutupilia mbali mradi huo kwakutoa sababu ambazo hazina nguvu na zingine za kushangaza sana, mimi naitafsiri kama ni hujuma kwa taifa, izingatiwe kuwa tayari taifa lilishaingia gharama kubwa kuanzia kwenye upembuzi yakinifu, na kusaini mikataba ya awali. Kitendo cha kusitisha katika hatua hii ni kulitia hasara taifa. Moja ya hoja zilizotolewa na rais kama sababu ni kwamba masharti ya wabia nikuwa TRA hairuhusiwi kukusanya mapato, hoja hii ya Rais alikuwa sahihi lakini bahati mbaya alishindwa kufafanua wazi sababu za TRA kutokuwa miusanya mapato ya ubia. Pengine hili Rais alidanganywa.

Pili rais alisema kuwa masharti ya wabia nikuwa Tanzania hairuhusiwi kuendeleza bandari zake zingine. Hoja hii nayo inautata mwingi sana, Bandari zingine zote ziko kwaajili huduma za ndani, na mradi huu ulikuwa kwa shughuli za kimataifa. Sasa hoja ya kuwa tusikarabati bandari zetu zilizopo ni hoja isiyo na mashiko, Hili inawezekana kabisa Rais hakuambiwa ukweli. Serikali ya Rais Samia ilitutangazia kuwa Rais Magufuli alikuwa MUONGO.

Hoja ya Tatu aliyoitumia Rais Magufuli kukataa mradi ule, ilikuwa kwamba, wabia wanataka wapewe umiliki wa ardhi kwa miaka 99. Hili si la mwekezaji bali la sheria zetu ambazo zinatoa uwekezaji unaogusa katika ardhi uwe kwa miaka 33 hadi 99. Sasa hoja hii haiwezi kuwa kwa wabia wawili tu kati ya watatu ikiwemo Tanzania yenyewe. Hili nalo kuna uwezekano watu waliamua kumpotosha rais wetu.

SASA LEO Serikali ya Rais Samia imekuja na hoja nyingine kabisa, sio ujenzi wa bandari ya bagamoyo tena, Wala sio mambo ya UBIA, Bali ni ubinafsishaji, KUUZA yaani ukodishaji kwa 100% wa bandari ya Dar es Salaam kwa muda usio na kikomo (kwamjibu wa MoU) tofauti na sheria ya ardhi inayohusu pale mtu anapojenga kwa mara ya kwanza mradi huo ndio atapewa miaka 99, Sasa bandari ipo ilishajengwa, hawa Dubai wanaiendeleza usimamizi na uboreshaji tu, Je miaka miaka isiyo na kikomo ya nini? Halafu babdari ya Dar katika hoja za miaka yote zilizofanya tuamue kujenga badari ya Mtwara au Bagamoyo nikuwa bandari ya Dar ni ndogo kulingana na ukuaji wa uwanda wa kiuchumi. MoU ama mkataba wa Awali/preliminary contract uliosainiwa 25 October 2022 pamoja na mambo yote unakabidhi kila kitu kuanzia uendeshaji na usimamizi wa bandari ikiwemo Ulinzi na Usalama kwenda Kampuni ya Emirates Dubai mali ya serikali ya Dubai. Izingatiwe kuwa Dubai na Marekani ndio walikuwa washindani wakiupiga vita mradi wa Bagamoyo kwakuwa mradi ule ungetekelezwa na wa bia Tanzania, Oman na wachina, ungeharibu nusu ya uchumi wa Dubai inayotegemea bandari katika uchumi wake. Sasa Dunia imekuja kuukamata mradi kwa kuuharibu ule wa awali na kushikilia kile kidogo tulichokuwa nacho.

Kwa maoni yangu ninafikiri kubinafsishwa bandari si hatua salama kwa mstakabali wa taifa letu, Ninashauri tubaki kwenye UBIA, na sio uuzaji wa bandari. Serikali iingie ubia na Dubai wa kuendesha kwa pamoja bandari hii, ifagamike kuwa bandari na viwanja vya ndege vya kimataifa ni sehemu ya mipaka wa nchi kwa mjibu wa katiba ya Tanzania, na vitalindwa na vyombo vyetu vya ulinzi na sio kuleta majasusi wa kigeni kutoka kampuni ya Dubai Intelligence agencies. Sijui kama watu wanaelewa unyeti wa bandari, sijui kama watu wanaelewa madhara ya huu mkataba kwa vizazi vyetu. Nimesoma MoU, vipengele vingi vina utata mkubwa sana.

Unajiuliza maswali, ni kweli TISS haikujua kuwa kuna vita vya kiuchumi pale ulipotangazwa meadi wa Bagamo? Ni kweli TISS imeruhusu vita vya washika Dubai + Marekani vs mradi wa Bagamoyo + China + Oman kuanguka na kwenda kuziba njia kwakuishika bandari ya Dar?. Zingatia kwenye MoU ya Dubai na Tanzania kwaajili ya Bandari ya Dar, kipo kipengele kile alichokisema Magufuli kuwa hatutaruhusiwa kuendeleza bandari zingine katika bahari na maziwa yetu, isipokuwa wao Dubai ndio wanapewa haki hizo. Soma tamko la bunge kifungu cha kwanza kabisa. Kilicho tokea kwa Dubai kuinunua Bandari ya Dar, ni sawa na Klabu ya Simba kwenda kunua Hisa zote 100% za Klabu ya Yanga. Ni mbinu ya kumuua mpinzani wako kwa kumnunua!

Nasisitiza, kuna tatizo kubwa kwenye eneo la Ujasusi katika nchi yetu, hasa ujasusi wa Kiuchumi, na hili ndilo lilikuwa msingi wa mimi kuandika Kitabu changu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi. Michakato mingi ya kiuchumi katika nchi hii imekuwa haina mafaa ama inaliacha taifa katika makovu makubwa yasiyozibika. Hii inazaa uhalali wa LAZIMA wa kuhitaji mageuzi makubwa katika Idara ya Usalama wa Taifa nchini kuanzia kwenye ideology, sheria, misingi, kanuni, na mambo anuai ndani ya idara ya usalama wa Taifa nchini. Ujasusi kwa nchi zilizoendelea kama China, Israel, Urusi, Uingereza na Marekani, unafanywa na watu ambao ni smart na wanajengwa kuwa smart ili kuweza kumudu ugumu wa kazi hiyo na kuifanya kazi hiyo kwa mafanikio makubwa. Majasusi katika nchi hizo hawapewi kazi kwasababu ya ujomba ujomba na kujuana. Ni kweli asilimia kubwa ya information's zenye thamani katika kazi ya ujasusi huwa zinaletwa na "human intelligence" badala ya magazeti, TV na source nyingine za habari.

Kwa maana hiyo basi ni lazima kuwe na watu competent ambao wana uwezo wa kukusanya habari za kijasusi ili tuweze kupata information's za maana na kujenga uwezo wa kuzifanyia kazi informations hizo. Imagine wakati ule wa vita baridi jinsi Directorate 16 ya KGB ilivyoweza kufanya kazi ya kununua sensitive navy information za USA na kuweza kutengeneza balance ya navy fleet bila USA kugundua kwa miaka 17 kupitia kwa Johny Walker junior! Leo kampuni ya Dubai tu hapa TISS inashindwa kujua ukweli kwamba Kampuni hiyo ni corrupt na ina migogoro katika maeneo mengi ilikowekeza? Bunge linasema kampuni ya Emirates Dubai wako Msumbiji, huu ni uongo na ni Uzembe wa vyombo vya ulinzi na Usalama kushindwa kupata taarifa sahihi za kampuni hii. Bandari ya Nacala ya Msumbiji ambayo ni moja ya Bandari kubwa sana Afrika, inamilikiwa na wabia watatu ambao ni Vale Logistics (47.5% ownership), Mitsui Co., Ltd. (47.5%), and the Ports and Railways of Mozambique (CFM, 5%). Hawa ndio wanaoendesha bandari hii Msumbiji.

Naunga mkono Ubia wa uendeshaji wa miradi mikubwa ambayo ni roho ya nchi kama babdari, Reli (SGR), Airports, nk, lakini napinga vikali UBINAFSISHAJI wa roho ya nchi, miradi hii ndio usalama wa nchi wenyewe. Tuache kuishi kwa mazoe kuwa Watz ni wajinga kwamba wao wanazipa kipaumbele habari za Yanga na Simba tu hivyo hawatajali mambo nyeti kama haya. Tumwambie Ukweli Rais kwamba anakosea anaangamiza kizazi hiki na kijacho. Serikali hiyohiyo inayomnyima Bakhresa Kuendesha Huduma ya Vivuko Kigamboni na badala yake imeng'ang'ania kuendesha yenyewe, ndio hiyo hiyo inayoona imechoka kuendesha bandari hivyo inampa mwarabu kusimamia. Ni Bakhresa aliomba kuanzisha huduma ya boti za abiria kutoka Mtongani hadi Bagamoyo maarufu Teksi, Lakini wakamkatalia kwa visababu vidogovido vya kijinga kabisa, eti mambo ya usalama! Hao Dubai kwao bandari zao zote wanaziendesha kwa Ubia na Marekani, hawajawauzia wamarekani kama kwetu, kwanini kwetu wanataka kununua miaka mia?.

NASISITIZA, UONGO WA KISERIKALI UMEFIKA MWISHO, TUJISAHIHISHE
IMG_20230607_204533_388.jpg
FB_IMG_1686158104130.jpg
FB_IMG_1686158107564.jpg
 
Hili Jambo sisiem watalizima kwa kitu kidogo sana Kisha maisha yataendelea. Ngoja wanawaandalia Basi Kali kutoka south kwa ajili ya parade ya kombe la Yanga kutembezwa Dar nzima Kisha tuanze kujadili mpira kila masaa 24 kuanzia kwenye maredio,Twitter na mitandao mingine yote kisha swala la bandari linazimika.

Hii nchi ina laana ya CCM na Simba na Yanga.

Hawana uchungu na watanzania Hawa watu.
 
Ujasusi wa kidola na kiuchumi! hakuna aliyeelewa uchumi ni silaha ya vita na vita ya sasa duniani n uchumi.
Huu mkataba na hizo MoU zimeandikwa namajasusi wa kiuchumi, ukasomwa na akina Mzanzibar Mbarawa

Bandari za Zanzibar zipo salama1 haziguswi kabisa ingawa mapato ya bandari za Tanganyika ndiyo ynalipia gharama za muungano. Kuna nini?

Tuwekeni rekodi sawa kwa akina Kassim Majaliwa na Philipo Mpango na Wabunge wote. Ipo siku isiyo na jina wala tarehe tutawauliza wakiwa wastaafu au wanawania nafasi za juu. Tutawauliza walifanya nini kuitetea Tanganyika.

Wale wote mnokaa kimya Tanganyika ikisubulubiwa, tutawauliza, na majina yenu kwa watoto wenu yatabaki kuwa mzigo. Mliitetea vipi Tanganyika!

JokaKuu Pascal Mayalla
 
Umeichambua vizuri sana ili suala.

Kama nchi tunakosa mwongozo wa kisera hasa ni kitu kipi tubinafsishe , tuingie ubia au tuache sekta binafsi.

Kwenye madini sehemu kubwa, tumeacha sekta binafsi hasa ya nje. Walau wachimbaji wadogo wanajitutumua

Gesi, utalii nako pia hali ni hiyo hiyo

Hili la bandari linastaajabisha kutoka kufikiri PPP hadi ubinafsishaji?



Kwa tafakari zaidi, inaonekana makubaliano hayo ni ya jumla (kama katiba fulani).

Kinachofuata ni kuingia mikataba ya mradi mmoja mmoja kwa kila bandari watakayoitaka hao DiPU Weldi. Hii sina hakika kama wataiweka wazi , humo ndio kuna pesenti na tenda ndogondogo.

Bila ya shaka miezi 12 inayosemwa na TipiEE ni kipindi hiki tokea huo Mkataba Mkuu kusainiwa hadi sasa. Bila ya shaka wako chemba wanagawana hayo maeneo ya kuyaendeleza.

Cha ajabu kwa nini wamechukua muda mrefu tokea wasaini hadi sasa kuuleta mkataba kilingeni bongeni
 
Mimesoma mstari kwa mstari na kwa makini sana., Chief Mangungo wa Musovero anisamehe bure kumlaum kwa kusaini mikataba ya uraghai., maana yeye naamini hakujuwa kusoma na kuandika.
Hawa watawala wa leo wanaojuwa kusoma na kuandika, tena wana mbwembwe nyingi zenye matamshi ya kingereza wanafamya nin., wamekuwa WALAFI wakubwa wanaolinyonya Taifa bila huruma, naamini kabisa mtoto wa Masiki atakuja kukubali vita kuliko amani yenye manufaa kwa Mtawala.
 
Back
Top Bottom