DP World waje, tusiogope kushitakiwa nje ya nchi

deblabant

JF-Expert Member
Oct 7, 2022
899
1,331
DP World waje, tusiogope kushitakiwa nje ya nchi

Na Deodatus Balile, Los Angeles, California, USA

Hapa Los Angeles kuna tofauti ya saa 10 na Dar es Salaam. Sasa hivi wakati naandika makala hii ni saa 8:30 usiku, wakati huko Tanzania ni saa 6:30 mchana. Najikuta usingizi unakwisha mapema kwa sababu ya kubadili muda wa kulala kwa hapo kwetu, ila kwa masuala ya kitaifa, inanibidi kuamka na kufanya kazi hii ambayo ina utume wa pekee.

Nimejikuta nalazimika kuandika tena juu ya Mkataba wa Serikali ya Dubai na Tanzania, katika uendeshaji wa Bandari ya Dar es Salaam na nyingine. Mkataba huu una mengi. Nimeona watu wakihoji mahakama ya kutolea uamuzi wa mkataba huu ikiwa utatokea mgogoro itakuwa wapi na mengine mengi. Ni kweli katika mkataba mashauri yataamuliwa Afrika Kusini kwa Sheria za Uingereza.

Sitanii, watu wanajiuliza kwa nini iwe hivyo? Ikumbukwe nchi yetu tangu tulipopata Uhuru, tulianzisha Sera ya Ujamaa na Kujitegemea na Mwalimu Nyerere akasema madini yetu (na mafuta) yaendelee kukaa ardhini hadi tutakapopata akili kwa maelezo kuwa alikataa mikataba aliyoiita ya kinyonyaji.

Tanzania ilitangazwa kuwa nchi ya Wakulima na Wafanyakazi, hivyo biashara ikawa ni uasi machoni pa watawala. Kwa msimamo huu, nchi yetu ikawa haina cha kuuza nje ya nchi na hivyo ikawa haipati fedha za kigeni, ila ikawa inakopa kuendesha uchumi kwa maana ya matumizi ya kawaida (mishahara na posho) na matumizi ya maendeleo (ujenzi wa miundombinu - maji, reli, shule, hospitali, barabara, viwanja vya ndege...). Matumizi haya yanaitwa kibajeti recurrent and development expenditures.

Nini kilitokea? Mwaka 1967 Serikali ya Tanzania ilitaifisha biashara na mali za wafanyabiashara. Nyumba karibu 26,000 zinazomilikiwa na National Housing (NHC) na Msajili (maeneo ya Upanga, Posta - Dar es Salaam na mengine nchini zilikuwa za watu binafsi). Baadhi zinamilikiwa na Msajili wa Hazina kwa sasa. Wamiliki walikimbilia Canada, India na kwingine duniani.

Kilicholifuata, pamoja na vita ya Uganda ya Pili (1978/79), nchi yetu iliendelea kufilisika kidogo kidogo. Mwaka 1980 nikiwa shuleni hadi 1985, bidhaa ziliadimika madukani. Sabuni ilipotea tukawa tunafulia (oruzinga na mapapai). Chakula na bidhaa muhimu kama sukari, unga, sabuni, dawa ya meno, mchele, nguo... (mention them) zikapotea kabisa. Wanafunzi sare za shule (shati, sketi na kaptula) ikawa tunashonea viraba baada ya kuchanika (siku hizi watoto wetu hawajui kaptula yenye rastika ya mpira wa baiskeli kiunoni (orukoba)!

Sitanii, dhana ya kutothamini biashara ilifanya uchumi wa taifa letu kuwa mgumu na hii ilikuwa moja ya mambo yaliyomfanya Mwalimu Nyerere atake kustaafu Urais mwaka 1980, ila Kamati Kuu ya CCM ikamkatalia kwa maelezo kuwa nchi imetoka kwenye vita angeondoka ingevamiwa tena na Idi Amini. Kwa tabu, tukiwa na madini yetu, bandari zetu, benki zetu... Mwalimu Nyerere aliendesha nchi hadi mwaka 1985 alipoikabidhi kwa mzee Ali Hassan Mwinyi.

Hadi mwaka 1979, Tanzania na China uchumi wetu ulikuwa hautofautiani hata chembe na sera zetu zilifanana neno kwa neno. Ndiyo maana Mwalimu Nyerere na Mwenyekiti wa China Peoples Party (CPC), Mao Zedong walielewana mno. Kwa China, waliona mwenendo huu unaiua nchi yao. Mwanasiasa Deng Xiaoping akabadili sera za China mwaka 1979. Wakaruhusu uwapo wa Ujamaa wenye Tabia za Uchina (Socialism with Chinese Characteristics). Wakaanza safari ya kufanya biashara mwaka 1979. Leo China ni taifa Na. 1, kwa uchumi mkubwa duniani.

Sitanii, China walifanya kama tunayofanya sasa. Walibadili sheria zao kuruhusu mitaji na uwekezaji (Foreign Direct Investment-FDI). Waliruhusu migogoro ya kibiashara kutatuliwa kwa usuluhishi nje ya China, mitaji ikamiminika kutoka kila kona wakiwamo Marekani wanaojuta leo kwa kuwekeza nchini China kwa wingi.

Kwa hofu ileile kwa wawekezaji nchini China baada ya uzoefu wa kutaifisha mali binafsi uliofanywa na Mwenyekiti Mao, walilazimika kuongeza imani ya wawekezaji kwa kubadili sheria zao kuruhusu mwekezaji mwenye malalamiko kufungua kesi nje ya nchi kwa maana mahakama za ndani haziaminiki.

Hilo lilifungua milango na uwekezaji ukawa mkubwa kwa kiwango ambacho hata hapo ulipo mpendwa msomaji wangu jaribu hesabu bidhaa unazotumia kutoka China kuanzia mavazi hadi vifaa vya ujenzi uone ni asilimia ngapi kulinganisha na nchi nyingine. Na kama hatuna mpango wa kuwadhulumu wawekezaji, tunaogopa nini kuruhusu usuluhishi kufanyika nje ya nchi?

Nikirudi hapo nyumbani, mwaka 1987 Mzee Mwinyi ilibidi akubali masharti ya Benki ya Dunia kurekebisha masharti ya kufanya biashara nchini na uendeshaji wa serikali (Structural Adjustment Programmes -SAPs). Kati ya masharti haya ilikuwa ni kushusha thamani ya sarafu yetu, maana haikuwa na uhalisia ilipangwa na serikali kutokana na ukweli kwamba hatukuwa na cha kuuza nje ya nchi kwani wawekezaji wote walioshaondoka.

SAPs ilikuja kama kulikoa taifa letu kutokana na ukweli kwamba mwaka 1978 Tanzania ilikuwa na kila dalili ya kufulisika (Debt Default?) Ila WB wakaikingia kifua (rejea kitabu cha Moyo Dambisa - Dead Capital). Mzee Mwinyi alianza kazi ya kubinafsisha na kujenga imani ya wawekezaji upya kupitia sera yake ya "RUKSA".

Ukisoma kitabu cha Rais Benjami Mkapa, anasema alipochukua nchi alikuta haina fedha za kigeni kabisa (foreign reserves) zinazotumika kuagiza bidhaa na huduma nje ya nchi. Kama alivyokuwa amesema Horace Kolimba (marehemu) nchi yetu ni kweli haikuwa na Dira ya Maendeleo muda wote huo. Rais Mkapa aliandaa Dira ya kwanza (National Vision 2025) iliyoanza kutumika mwaka 2000 na akajenga Mamlaka na Wakala nyingi.

Sitanii, tangu tumepata Uhuru hadi mwaka 2005, nchi ilikuwa na mtandao wa barabara za lami wa kilomita 2,800 kati ya mtandao wa kilomita 86,000 nchini kwani hatukuwa na fedha za kujenga lami. Nchi yetu ilikuwa ya "Wakulima na Wafanyakazi". Utakumbuka hadi mwaka 2008 ilikuwa tukitaka kusafiri Dar - Bukoba, tulipitia Namanga, Nairobi, Busia, Kampala - Bukoba. Barabara ya Dar - Morogoro - Dodoma - Singida - Shelui - Kahama - Lusaunga - Biharamulo - Muleba - Bukoba ilikuwa haipitiki.

Ni chini ya Rais Mkapa baada ya kukaribisha wawekezaji alianza ujenzi wa barabara kwa utaratibu wa Build Operate and Transfer (BOT). Barabara ya kwanza ilikuwa ni Morogoro-Dodoma-Singida- Igunga- Tinde-Shinyanga -Mwanza iliyosimamiwa na Dk. John Magufuli akiwa Naibu Waziri, chini ya Mama Anna Abdallah na baadaye Waziri kamili wa Ujenzi. Tukajenga kwa fedha za ndani.

Rais Jakaya Kikwete alipoingia madarakani mwaka 2005, alifungua milango zaidi kwa wawekezaji, ambapo kwa barabara pekee alijenga kilomita 11,600 za lami. Ndipo tukaacha kabisa kupitia Kenya na Uganda kwenda Bukoba. Rais Magufuli alipoingia madarakani mwaka 2015 akarejesha Sera za Mwalimu Nyererere. Mwaka 2017 akatunga sheria ya Resources Sovereignty, ambayo pamoja na mambo mengine, inataka kesi zote ziamuliwe hapo nchini (kama ilivyokuwa mwaka 1979).

Rais Magufuli alipoingia alikuta uchumi unakua. Alikusanya hadi Sh trilioni 1.4 (bila kujali mbinu alizozitumia kwa kuweka vikosi kazi vilivyokuwa vinapora fedha kwenye akaunti za watu). Kilichoendelea miaka ya mwisho ya uhai wake, hamkusikia tena TRA ikitangaza makusanyo kila mwezi. NaambiwayYalishuka hadi bilioni 550 kwa mwezi. Kariakoo na maeneo mengi nchini biashara zilifungwa ndani ya miaka 6, tukiaminishwa kuwa wanaofunga biashara ni wapiga dili.

Rais Magufuli aliliona hili. Yeye aliyekuwa anasema; "Atawageuza matajiri wanaoishi kama malaika waishi kama mashetani", kwenye hotuba yake ya kufungua Bunge Novemba 2020 alisema: "Atajenga mabilionea 100." Unajua hii maana yake ni nini? Alikuwa na mkwamo wa kutosha. Alielewa umuhimu wa kuruhusu biashara zikafanyika bila vikwazo.

Sitanii, Rais Magufuli hakuwa tena na mwekezaji anayelipa kodi kubwa kati ya aliotaka kuwashitaki kwa sheria za ndani wote alikwishawafikisha Kisutu Mahakamani, hakuwapo mpya wa kumshitaki. Nchi ilikuwa inaelekea kufilisika tena kama mwaka 1978 kwani haikuwa tena na kodi za kukusanya baada ya wawekezaji kuondoka.

Alipoingia Rais Samia Suluhu Hassan amekuta madeni makubwa ya kibiashara yaliyokopwa na Awamu ya Tano. Miradi kama ununuzi wa ndege, SGR, upanuzi wa barabara na mingine, Rais Magufuli alikuwa anakopa, lakini anawambia wananchi kuwa tunatumia fedha zetu.

Siku moja wakati anazindua Uwanja wa Ndege Terminal III hapo Dar es Salaam, alikiri wingi wa madeni ila akahoji: "Wanasema nakopa sana, kwani zamani wao walikuwa hawakopi? Mbona tulikuwa hatuzioni zinakwenda wapi?"

Kwa hali iliyokuwapo mwaka 2021 wakati anafariki dunia, Tanzania haikuwa na namna, isipokuwa kurejea kilichofanyika mwaka 1987 chini ya SAPs kwa kulegeza masharti na kuwaiga China walichofanya chini ya Xiaoping mwaka 1979. Tulikuwa na uchaguzi wa kubaki na ‘Resource Sovereignty’ nchi ikafilisika au kubadili sheria zetu na kurejea alipotuacha Rais Kikwete, tukajenga nchi.

Kwa Rais Samia kuwajengea upya imani Wafanyabishara, Desemba 2022 TRA walikushanya Sh trilioni 2.75. Hili linaonyesha imani ya wafanyabiashara kurejea na biashara kurejea nchini. Nchi zote ikiwamo hapa Marekani zinajiendesha kwa kukusanya kodi, ikiwamo viwanda vikubwa vya wafanyabiashara vinavyolipa kodi kubwa kama Kampuni ya kutengeneza ndege ya Boeing na nyingine nyingi zinazolipa kodi kubwa baada ya kuuza bidhaa na huduma nje ya nchi.

Sitanii, mambo ni mengi naomba nihitimishe na hili la Bandari. Ni kweli hadi mwaka 2005 Bandari lilikuwa suala la Muungano kimaandishi tu, ila si kwa vitendo. Mwaka 1997, Baraza la Wawakilishi Zanzibar chini ya uongozi wa Komandoo, Dk. Salmin Amour (Mwalimu Nyerere akiwa hai), walitunga Sheria ya Shirika la Bandari Zanzibar (ZPC) No. 1.

Mwaka 2004 Tanzania (Tanganyika) ikatunga Sheria ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Na. 17 ya Mwaka 2004. Haya hayasemwi! Ni ukweli mchungu au usiotamkwa kuwa Bandari si suala la Muungano kitambo. Nafahamu bado kuna watu wana mning'inio (hangover) wa Ujamaa wa kusadikika, hivyo kwao kila tajiri ni mwizi au mla rushwa.

Nafahamu pia kwa uchanga wetu katika sekta ya biashara iliyopewa kisogo tangu Uhuru - ujuzi, maarifa na maadili ya biashara vipo katika kiwango cha chini hapo nchini. Swali ni je, tujenge ujuzi, uadilifu, maarifa na kufuata misingi ya kufanya biashara ikiwamo kujenga imani kwa wafanyabiashara nchi ipate fedha za kigeni na kukuza uchumi kama ilivyofanya China au tuendelee kusubiri hadi tutakapopata akili kama alivyopendekeza Mwalimu Nyerere enzi hizo? Uchaguzi ni wetu.

Ikiwa hatuna mpango wa kuwadhulumu wawekezaji (kama ilivyotokea mwaka 1967) tunaogopa nini kusuluhishwa nje ya nchi? Binafis naona acha DP World waje waendeshe bandari tupate mtaji, ujuzi na maarifa. Jambo moja tu, tusiwape kila kitu. Tusiweke mayai yote kwenye kampu moja. Turuhusu ushindani kati ya DP World na waendeshaji wengine. Mungu ibariki Tanzania.

+255784404827

Ends…
 
Ok kwako.. kulwa jilala.....!
 
This idiot is very corrupt, left, righ, up, bottom!! Ubongo wake umeshashashika kutu ya kupenda kulamba vya bure kama nzi anavyolamba vidonda. Watu kama hawa kipindi cha kupigana na makaburu walikuwa wanapata special treatment! Kweli waafrika tunakuwa kama tuna laana. Ndiyo maana watu weusi ndiyo race pekee iliyochukuliwa kwa wingi utumwani kwa sababu tulikuwa tunauzana wenyewe. Ulaaniwe wewe Balile.
 
Kama upo San Francisco itakuwa hofu ya wizi na vibaka wa huko tu. Los Angeles imejaa vilima na walevi wanao zurura mitaani tu.
 
Umeongelea kusuruhishwa nje ya nchi tu . Vipi kuhusu
1. Ukomo wa mkataba?
2. Kupewa mamlaka ya kufanya chochote kiwe kibaya au kizuri bila kusumbuliwa na serikali?
3. Maslahi yetu ni yapi yaani watalpaje ?
4. Kodi atakusanya TRA au wao?
5. Kama hakuna ukomo maanake si nchi imeuzwa?
 
Umeandika vyema
 
This idiot is very corrupt, left, righ, up, bottom!! Ubongo wake umeshashashika kutu ya kupenda kulamba vya bure kama nzi anavyolamba vidonda. Watu kama hawa kipindi cha kupigana na makaburu walikuwa wanapata special treatment! Kweli waafrika tunakuwa kama tuna laana. Ndiyo maana watu weusi ndiyo race pekee iliyochukuliwa kwa wingi utumwani kwa sababu tulikuwa tunauzana wenyewe. Ulaaniwe wewe Balile.
Ukishahgaa ya Musa utaona ya firauni
 
Balile hakuwa kati ya kundi la Waandishi Mamluki walioalikwa na DP Dubai??
Kwa tunaomjua Balile tangu akiwa pale SAUT jamaa ni anaendekeza njaa kuliko kitu chochote.Sitoshangaa kama mgawo wa safari ya Dubai aliupata
 
Naunga mkono kichwa chako cha habari, nimeshindwa kulisoma andiko lako lote kwa sasa. Ntalisoma baadae.
Naamini kama tuna nia njema ya biashara tusiogope kabisa kushitakiwa. Kuogopa-ogopa kushitakiwa maana yake hatuna nia njema, tuna nia ya kufanya dhambi, simpo.

Halafu hivi kwa bandarini tunaogopa kwani tunawauzia nini Dubai?
Mizigo watafute wao,
vifaaa vya kutendea kazi walete wao,
mifumo ya TEHAMA walete wao, kwa pesa zao.

Wafanyakazi wazoefu walete wao,
Mafunzo wafanye wao,
vijana wetu watapata fursa za kufanya kazi hapa na duniani walipo DP World.
Pesa watulipe wao, jinsi tutavyokubaliana.

Watuletee na wawekezaji wengine kwenye miradi mingine.
Yote hayo sisi yametushinda miaka yote.
Faida inatarajiwa kupanda mara kibao.
Halafu sisi ndiyo tujidai tunaogopa kushitakiwa.
Mbona wao hawaogopi kushtakiwa?

Mimi naamini sisi ni taifa la wanga.
 
Issue mkataba wa kuuza nchi ni upumbavu na Sa100 keshatukosea heshima Watanganyika nani amamuamini tena? katugusa pabaya Mama... anatakiwa ajiuzulu kabisa... Alipokuwa na Jiwe walikuwa wanajifanya wanataka kufufua kila kiwanda na shughuli zote zilizokuwa za maendeleo Tz sasa yeye katugeuka kama dalali na hajaanza na hili la bandari tu keshatupiga na amenogewa anaunua hizo Application na mitambo mipya tuongoze weyewe kwa mikataba yenye ukali kabisa mtu akiiba ni kitanzi na kufilisiwa mali zake zote... hebu rejesheni heshima ya uafrica kuwa tunaweza na sio kuwezeshwa kama na sio kurejesha wakaloni upya...

Hata madhara ya kuteuana kila siku ndio yanatuletea matatizo kila kukicha... wekeni ma HR wawafanyie interview nyanja zote za uongozi kama Kagame na kila kiongozi account ziwe zinasoma live pure and open procurement za serikali kila raia ajue tuone majizi ni kina nani yanaogopewa hadi Mama anaamua kuwapa waarabu sensitive area za nchi...
 
😂😂UVCCM Kazini
IMG_20230622_131053.jpg
 
Back
Top Bottom