Nchi haina NDEGE ila Rais ana NDEGE

Mtatia tu akili maisha kwanza yawatwange sikunyingine mkielezwa na mafullbright kama Slaa muwe mnaelewa aliwaambia kumchagua Jk ni janga la kitaifa hamtaki mtatia tu akili hebu maisha endelea kuwa magumu ilihawa waTz wakome kabisa.
 
Jamani hivi kuna mtu ashawahi kufikiria kitu kama hiki? naomba mchangie bila kumtukana rais wala watawala wake , kama huna fact unataka kutukana naomba ukae kimya tu kwa sababu kila mtu an ahasira zake, na hawa viongozi.
hii ndege ndio inayomfanya kila siku kiguu na njia kwenda kwenye matamasha , ndio! hizi ni kodi zetu hizi kwa nini tunyamaze?
nchi yenya watu mili 40 , haina vita ina madini na migodi mbali mbli ,ina maziwa na bahari ina vivutio vya utalii
lakini haimiliki ndege, suitaki kusema kuwa kuwa na ndege ndio uchumi wako una kuwa strong but this is the source of employment also , tunashindwa kufikiria .
hakua faida ya hii ndege zaidi ya kuktutia hasara tu kwa safari zake za mara kwa mara.unafikiri ndege isingekuwepo si angekuwa nchini anafuatilia bunge? iaal hajui hata kitu gani inachoendelea na
VIJANA WA SIKU HIZI WANASEMA MWACHE ALE BATA:

Ndege ya Raisi ya nini? Akija Raisi mwenye uchungu na nchi ataiuza na kuimarisha shirika la ndege. Sidhani kama hata Raisi mwenyewe anapokuwa nje ya nchi na 'ndege yake' na huku wasaidizi wake wakitegemea ndege moja isiyoaminika anajisikia vizuri. Au Air Tanzania inahujumiwa? Sipendi viongozi wanaopenda matanuzi wakati hali ni mbaya nyumbani.
 
[h=3]ATCL: Shirika La Ndege Lisilo Hata Na Ndege Moja Inayoruka![/h]
Na Richard Makore


11th April 2012



Sasa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) halina ndege hata moja inayoruka. Hali hiyo inatokana na kuanguka wa ndege yake pekee juzi katika uwanja wa ndege wa Kigoma wakati ikiruka kutoka Kigoma kwenda Dar es Salaam kupitia Tabora.

Abiria 35 na wafanyakazi wanne wa ndege hiyo waliokuwemo ndani ya ndege hiyo Ft.119 waliponea chupuchupu kufa katika ajali hiyo.

Hali hiyo imeifanya ATCL kubaki bila ndege kutokana na ndege yake nyingine moja kuwa katika matengenezo kwa muda mrefu sasa.

Kutokana na hali hiyo, sasa shirika hilo halitatoa huduma za usafiri hadi hapo litakapopata ndege nyingine.

Juzi baada ya kutokea ajali hiyo, Naibu Waziri wa Uchukuzi, Athuman Mfutakamba, alisema wizara yake imewapa mamlaka ATCL ya kwenda katika shirika lolote kukodi ndege ili kuziba upungufu huo.

Mfutakamba alisema ATCL inaweza kutoa mapendekezo kwa wizara kuhusiana na hatua gani zichukuliwe kama ni matengenezo ya ndege ama kutafuta ndege mbadala.

Jana shirika hilo lilisema kuwa limepata hasara kufuatia ndege yake kuanguka mkoani Kigoma juzi na kuharibika.

Shirika hilo lilisema kuwa, ndege hiyo haifai tena kwa ajili ya kubeba abiria na kwamba linafanya mpango wa kupata ndege za kukodi ili ziendelee kutoa huduma.

Kadhalika, shirika hilo lilisema kuwa licha ya kupata ndege za kukodi, lakini pia lina mpango wa kufanya biashara kwa ushirika na watu wengine ili kuhakikisha linaendelea kutoa huduma kwa wateja wake.

Akizungumza na NIPASHE jana jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Paul Chizi, alisema ndege hiyo haifai tena hata ikifanyiwa matengenezo.

Kuhusu abiria waliokuwa wamekata tiketi kwa ajili ya kusafiri na ATCL, Chizi, alisema watatumia ndege za kukodi za shirika la Precision Air ili kuhakikisha wote wanasafiri kama ilivyokuwa imepangwa.

“Hawa abiria wetu waliokuwa wamekata tiketi za shirika letu watasafirishwa kama ilivyopangwa kwa kuwa hatuwezi kuwaacha na tutawaleta kwa kutumia ndege za shirika la ndege la Precision Air,” alisema Chizi.

Akizungumzia uhai wa shirika hilo, Chizi, alisema haliwezi kufa kwa kuwa wana mipango mingi ya kuhakikisha linafufuka, ikiwemo kumalizia matengenezo ya ndege moja waliyobaki nayo ambayo inatajaria kuanza kutoa huduma zake baada ya wiki tatu zijazo.

Aidha, Chizi alisema ATCL inatarajia kupata mshirika wa kibiashara atakayekuwa anatoa huduma katika mikoa ya Mwanza na Kilimanjaro.

Chizi alifafanua kuwa biashara ya ndege inahitaji utalaamu, kujituma na uaminifu vinginevyo shirika haliwezi kukua na kuendelea.

Ndege ya ATCL iliyotapa ajali juzi mkoani Kigoma ilinasa kwenye tope na kuvunjika bawa la kulia na matairi yote ya mbele na nyuma yalipasuka.

Shirika hilo lilirejesha huduma ya usafiri wa ndege Novemba mwaka jana na kuanzisha safari za kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma kupitia Tabora.

Miaka ya nyuma shirika hilo lilikuwa likitoa huduma bora za usafiri wa ndege katika maeneo yote nchini.

ATC kabla ya kuitwa ATCL lilianza na ndege 11 ilizopata baada ya kuvunjika kwa jumuiya ya kwanza ya Afrika Mashariki (EAC) mwaka 1977.

Kenya ambayo kwa sasa inatoa huduma bora za ndege ndani na nje ya nchi hiyo kwa kutumia shirika lale la ndege la KQ wakati EAC ikivunjika ilibaki bila ndege.

Rwanda mwanachama mpya katika EAC na nchi ambayo haina rasilimali, kwa sasa ina ndege nyingi zaidi zinazotoa usafiri wa uhakika katika nchi mbalimbali za Afrika na nje ya Afrika kama Dubai na Doha.

Wakati ATCL likibakia hoi, biashara ya huduma za ndege inalipa zaidi na ndiyo maana Precision Air linachangamkia fursa hiyo.




CHANZO: NIPASHE

I do not mean to be rude but Mwandishi alipaswa kutumia jina zima la huyo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji throughout the article kwa sababu anapoandika 'Chizi' peke yake ananikwaza.
Tukumbuke tunaongelea ATCL kubaki shirika la ndege bila kuwa na vitendea kazi vya kufanikisha utolewaji wa huduma ya usafiri wa anga ambayo ndiyo core b'ness.
Halafu unasoma maelezo ya utetezi yanatolewa na 'Chizi'.I've failed to tame my sense of humor.

Nautakia kila la kheri uongozi wa ATCL katika kuendelea kuitia serikali gharama ya kukodi ndege kutoka kwa mashirika binafsi kwa kodi za watanzania ili kujionyesha kwamba wako hai ilhali ni maiti.
Pia ukarabati mwema wa hiyo scrap moja iliyobakia.

Miaka 50 ya uhuru.Wamethubutu kufilisi ATCL kwa ufisadi na hujuma,wanaweza kuendelea kuwabebesha mzigo walipa kodi na wanasonga mbele bila ya kuwa na ndege.
CCM Oyeee!!
 
Mimi kilaza? Haya, nime google. Sabena hili hapa kutoka Wikipedia:

SABENA was the national airline of Belgium from 1923 to 2001, with its base at Brussels National Airport. After its bankruptcy in 2001, the newly-formed SN Brussels Airlines took over part of SABENA's assets in February 2002

Kwa hiyo hilo shirika la serikali ya Belgium lillishakufa toka 2001 kama ATC inakokwenda! Umeleta kimchongo kimepitwa na wakati, shirika lishakwenda bankrupt, haikaisii pointi yako kwa sababu umeleta shirika la serikali ambalo lilikufa, sasa kilaza nani hapa? Eti SABENA, dunderhead mkubwa wewe!

Rais wa Tanzania ana ndege, Tanzania haina ndege. Kweli. Rais wa Marekani ana ndege, Air Force One, Marekani ina ndege?

Cool down Muzee!
 
jamani hivi kuna mtu ashawahi kufikiria kitu kama hiki? Naomba mchangie bila kumtukana rais wala watawala wake , kama huna fact unataka kutukana naomba ukae kimya tu kwa sababu kila mtu an ahasira zake, na hawa viongozi.
Hii ndege ndio inayomfanya kila siku kiguu na njia kwenda kwenye matamasha , ndio! Hizi ni kodi zetu hizi kwa nini tunyamaze?
Nchi yenya watu mili 40 , haina vita ina madini na migodi mbali mbli ,ina maziwa na bahari ina vivutio vya utalii
lakini haimiliki ndege, suitaki kusema kuwa kuwa na ndege ndio uchumi wako una kuwa strong but this is the source of employment also , tunashindwa kufikiria .
Hakua faida ya hii ndege zaidi ya kuktutia hasara tu kwa safari zake za mara kwa mara.unafikiri ndege isingekuwepo si angekuwa nchini anafuatilia bunge? Iaal hajui hata kitu gani inachoendelea na
vijana wa siku hizi wanasema mwache ale bata:


mgawanyo mbaya wa mali za taifa hili
 
mataifa mengi yanatucheka na kutushangaa sana unapowaambia hakuna shirika la ndege la taifa (flag carrier)
 
Hapa ****** ni kutanua tu hizo habari za nchi kuwa na ndege hana habari nazo, namuonea huruma atakayerithi mikoba 2015 kwani nchi itakuwa imebaki mifupa mitupu, sina uhakika deni litakuwa limeongezeka kiasi gani.
 
THINGS SPEAK FOR THEMSELVES.................
wa kujilaumu ni sisi wenyewe kwa kukosa muelekeo na dhamira ya kweli katika maendeleo
 
yes, nyingi mno.... kuna kitu kinaitwa states flag carrier na sisi tunalazimishwa kununua ticket za delta, northwest airline etc

je tanzania tuna national flag carrier??

au ulielewaje neno ndege?? ulidhani shorwe au tongwa??
Hakuna shirika la ndege lenye jina hilo siku hizi US!.
 
KWELI AISEE... precision is also majorly owned by Kenya and not Tanzania....

Si kweli kuwa Precision Air Services inamilikiwa kwa kiasi kikubwa na Kenya Air Ways. Kenya Airways wana miliki asilimia 32 na Mtanzania Mzalendo Michael Ngaleku Shirima anamiliki asilimia 36. Zilizobaki zinamilikiwa na Watanzania walionunua hisa kupitia Initial Public Offer
 
Obama ana ndege. Marekani ina ndege?

Obama kama maraisi wengine wana ndege inaitwa Airforce one ndo hiyo nayoitumia kwenye avata yangu.Na marekani kama marekani wana shirika la ndege strong linaitwa America Airline
 
Uingereza hawana ndege ya rais/waziri mkuu. Viongozi wanatumia ndege ya BIASHARA (British Airways) ambalo ni shirika la umma

Lakini Queen ambaye ni mkuu wa nchi ana ndege zaidi ya moja kwa ajili yake na loyal family si hilo tu wana mpaka YATCH na helicopter. Nakubaliana nawe Waziri Mkuu na viongozi wengine Uingereza wanatumia British Airways kwa usafiri, tusimseme vibaya Kikwete tutakuwa tuna muonea, ndege yenyewe alikuta imekwisha nunuliwa na nina hakika kam ndege za ATC zingekuwa zinafanya kazi kwa ufanisi sioni kam Kikwete ange sita kuzitumia. Tujilaumu sisi kwa kukosa uzalendo kwa kuihujumu AIR TANZANIA, tulikuwa na ndege zaidi ya kumi sasa hivi hakuna hata moja, serikali iliwahi kumteuwa mtu kutoka mashirika ya kijamii eti awe mkurugenzi wa ATC, katika hilo mtu utegemee nini!

Kuna wakati fulani ndege yetu ya Boeing iliyokuwa imebaki iliwahi kupata ajali ya kijinga pale Kiwanjani Mwanza wakati inatua, rubani aliye sababisha ajali hiyo hakuchukuliwa hatua yoyote; we fikilia hata madereva wa magari wanajuwa hatari ya kuendesha gari kwa kasi na kukatiza dimbwi la maji - usukani utajigeuza kwa nguvu ya ajabu ambazo dereve hawezi kuzihimili na unaweza kupata ajali mbaya sana, na hiki ndicho kilicho tokea pale MWANZA, je huyu rubani alikuwa alijuhi hilo?
 
Nimegundua kwamba kuna vodafasta humu wengi wanajifanya kuchangia kumbe ni wale wenye elimu ya idadi ya vyumba vya madarasa na siyo ubora wa elimu.Shirika la ndege la Taifa hata kama serikali itamiliki share kidogo ni muhimu sana.Mataifa makubwa na madogo ya Afrika yana makampuni yao ya ndege.Kwa Tanzania usafiri wa ndege ni muhimu sana na bado soko la ndani ni kubwa sana.Shirika kama Precision la binafsi na ambalo sasa limesajiriwa DAR STOCK Exchange linafanya vizuri japo linalemewa na wateja.Marekani usiulize mashirika ya ndege ni ya kumwaga tu zaidi.Ni aibu pia kulinganisha Tz na somalia.Rwanda shirika lao linakuwa kwa kasi japo halina zaidi ya miaka mitano tangu kuanzishwa.Uganda nao UgandaAir inazidi kujiimairsha ukanda huu na hakuna shida kwenda Kampala na Entebe kupitia hata Mwanza na bei very cheap kama nauli ya kutoka Dar-Kigoma.Tanzania is poorly managed
 
Jamani rais ni lazima awe na ndege ya kusafiria. Tatizo la nchi kutokuwa na ndege ni tatizo lililotokana na watu ambao sio wazalendo. Hivyo lawama hizi hazitakiwi kwenda kwa rais japo na yeye anayo sehemu kubwa na kuweka dira ya nchi.
 
Back
Top Bottom