Nchi haina NDEGE ila Rais ana NDEGE

Nchi haina NDEGE ila Rais ana NDEGE

Acha ukilaza wewe, nenda Google utafute SABENA ndio utajua
Mimi kilaza? Haya, nime google. Sabena hili hapa kutoka Wikipedia:

SABENA was the national airline of Belgium from 1923 to 2001, with its base at Brussels National Airport. After its bankruptcy in 2001, the newly-formed SN Brussels Airlines took over part of SABENA's assets in February 2002

Kwa hiyo hilo shirika la serikali ya Belgium lillishakufa toka 2001 kama ATC inakokwenda! Umeleta kimchongo kimepitwa na wakati, shirika lishakwenda bankrupt, haikaisii pointi yako kwa sababu umeleta shirika la serikali ambalo lilikufa, sasa kilaza nani hapa? Eti SABENA, dunderhead mkubwa wewe!

Rais wa Tanzania ana ndege, Tanzania haina ndege. Kweli. Rais wa Marekani ana ndege, Air Force One, Marekani ina ndege?
 
Uingereza hawana ndege ya rais/waziri mkuu. Viongozi wanatumia ndege ya BIASHARA (British Airways) ambalo ni shirika la umma

Mkuu angalia fact zako kabla ya kuweka pumba ...... ........
 
sijui kama zanzibar, somalia, south sudan, zina ndege ya rais.... lakini nadhani the question here had a special meaning kuliko unavyojaribu kuleta ushabiki kivuzi

Halafu nini mkuu naona Zanzibar wanazinguliwa na Tanganyika wangekuwa wao tu Wangekuwa na national flag carrier, fikiria mambo ya national TV wa-zenj long time lakini Tanganyika hadi miaka ya 90's, Kuh Somalia sijui ila South Sudan wana mafuta so ni swala la muda tu watakuwa na shirika lao.

Maoni yangu.
 
Zenji walikuwa wa kwanza kuwa na ndege ya rais kabla ya TZ bara. Alinunua A. Jumbe kama sikosei.
 
Uingereza hawana ndege ya rais/waziri mkuu. Viongozi wanatumia ndege ya BIASHARA (British Airways) ambalo ni shirika la umma
:

The RAF has a fleet of eight jets (the two larger jets carry a maximum of 30 passengers)
[SUP]http://en.wikipedia.org/wiki/Air_tr..._of_the_United_Kingdom#cite_note-raf-bae146-2[/SUP] equipped for VIP transport. All of the VIP fixed-wing aircraft currently operated by No. 32 Squadron RAF were delivered in the mid-1980s and have an out of service date of 2015.[SUP]http://en.wikipedia.org/wiki/Air_tr...nment_of_the_United_Kingdom#cite_note-IATR-14[/SUP] In an Independent Air Review published in June 2006.

Ka google utapata habari zake.
 
nchi zote zinazotuzunguka zinaleta ndege zao hapa bongo lakini cha kustaajisha na kuuzunisha hatuna hata ndege moja ya kupiga mingo ndani kwa ndani bongo. hivi sijui wafanyakazi wa ATC wapo kazini au wameshapigwa panga ,na kama wapo kazini ina maana wanalipwa na nani na kwa vigezo gani wakati hawazalishi hata ndululu. kweli bongo tambarare
 
Zenji walikuwa wa kwanza kuwa na ndege ya rais kabla ya TZ bara. Alinunua A. Jumbe kama sikosei.
Tanganyika wameziua , hawana hata haya hawa watanganyika , zanzibar ndio nchi ya kwanza kuwa na tv kwenye huu ukanda lakini sasa hivi angalia kulivyo... mimi lawama zote nawatupia hawa wazanzibar wenyewe...kwa nini wanalala lala???? watakuja kuuzwa siku moja hapa
 
Saint Ivuga; Tanzania hatuna viongozi wabunifu tofauti na kenya ambako wao wanabuni miradi kwa ajili ya kuzalisha mali, wabongo wanabuni miradi ya kushibisha familia zao.
 
Saint Ivuga; Tanzania hatuna viongozi wabunifu tofauti na kenya ambako wao wanabuni miradi kwa ajili ya kuzalisha mali, wabongo wanabuni miradi ya kushibisha familia zao.
ni kweli kaka... sisi tumeua hata relizetu wakati watu walikuwa haawapandi bure sisi ile pesa badala ya kuitumia kuboresha sijui tunaipeleka wapi aisee
 
[h=3]ATCL: Shirika La Ndege Lisilo Hata Na Ndege Moja Inayoruka![/h]
Na Richard Makore


11th April 2012



Sasa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) halina ndege hata moja inayoruka. Hali hiyo inatokana na kuanguka wa ndege yake pekee juzi katika uwanja wa ndege wa Kigoma wakati ikiruka kutoka Kigoma kwenda Dar es Salaam kupitia Tabora.

Abiria 35 na wafanyakazi wanne wa ndege hiyo waliokuwemo ndani ya ndege hiyo Ft.119 waliponea chupuchupu kufa katika ajali hiyo.

Hali hiyo imeifanya ATCL kubaki bila ndege kutokana na ndege yake nyingine moja kuwa katika matengenezo kwa muda mrefu sasa.

Kutokana na hali hiyo, sasa shirika hilo halitatoa huduma za usafiri hadi hapo litakapopata ndege nyingine.

Juzi baada ya kutokea ajali hiyo, Naibu Waziri wa Uchukuzi, Athuman Mfutakamba, alisema wizara yake imewapa mamlaka ATCL ya kwenda katika shirika lolote kukodi ndege ili kuziba upungufu huo.

Mfutakamba alisema ATCL inaweza kutoa mapendekezo kwa wizara kuhusiana na hatua gani zichukuliwe kama ni matengenezo ya ndege ama kutafuta ndege mbadala.

Jana shirika hilo lilisema kuwa limepata hasara kufuatia ndege yake kuanguka mkoani Kigoma juzi na kuharibika.

Shirika hilo lilisema kuwa, ndege hiyo haifai tena kwa ajili ya kubeba abiria na kwamba linafanya mpango wa kupata ndege za kukodi ili ziendelee kutoa huduma.

Kadhalika, shirika hilo lilisema kuwa licha ya kupata ndege za kukodi, lakini pia lina mpango wa kufanya biashara kwa ushirika na watu wengine ili kuhakikisha linaendelea kutoa huduma kwa wateja wake.

Akizungumza na NIPASHE jana jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Paul Chizi, alisema ndege hiyo haifai tena hata ikifanyiwa matengenezo.

Kuhusu abiria waliokuwa wamekata tiketi kwa ajili ya kusafiri na ATCL, Chizi, alisema watatumia ndege za kukodi za shirika la Precision Air ili kuhakikisha wote wanasafiri kama ilivyokuwa imepangwa.

“Hawa abiria wetu waliokuwa wamekata tiketi za shirika letu watasafirishwa kama ilivyopangwa kwa kuwa hatuwezi kuwaacha na tutawaleta kwa kutumia ndege za shirika la ndege la Precision Air,” alisema Chizi.

Akizungumzia uhai wa shirika hilo, Chizi, alisema haliwezi kufa kwa kuwa wana mipango mingi ya kuhakikisha linafufuka, ikiwemo kumalizia matengenezo ya ndege moja waliyobaki nayo ambayo inatajaria kuanza kutoa huduma zake baada ya wiki tatu zijazo.

Aidha, Chizi alisema ATCL inatarajia kupata mshirika wa kibiashara atakayekuwa anatoa huduma katika mikoa ya Mwanza na Kilimanjaro.

Chizi alifafanua kuwa biashara ya ndege inahitaji utalaamu, kujituma na uaminifu vinginevyo shirika haliwezi kukua na kuendelea.

Ndege ya ATCL iliyotapa ajali juzi mkoani Kigoma ilinasa kwenye tope na kuvunjika bawa la kulia na matairi yote ya mbele na nyuma yalipasuka.

Shirika hilo lilirejesha huduma ya usafiri wa ndege Novemba mwaka jana na kuanzisha safari za kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma kupitia Tabora.

Miaka ya nyuma shirika hilo lilikuwa likitoa huduma bora za usafiri wa ndege katika maeneo yote nchini.

ATC kabla ya kuitwa ATCL lilianza na ndege 11 ilizopata baada ya kuvunjika kwa jumuiya ya kwanza ya Afrika Mashariki (EAC) mwaka 1977.

Kenya ambayo kwa sasa inatoa huduma bora za ndege ndani na nje ya nchi hiyo kwa kutumia shirika lale la ndege la KQ wakati EAC ikivunjika ilibaki bila ndege.

Rwanda mwanachama mpya katika EAC na nchi ambayo haina rasilimali, kwa sasa ina ndege nyingi zaidi zinazotoa usafiri wa uhakika katika nchi mbalimbali za Afrika na nje ya Afrika kama Dubai na Doha.

Wakati ATCL likibakia hoi, biashara ya huduma za ndege inalipa zaidi na ndiyo maana Precision Air linachangamkia fursa hiyo.




CHANZO: NIPASHE
 
Tuige mfano wa Zanzibar ambayo haina ndege wala rais wake hana ndege. Kimsingi kama rais asingekuwa na ndege na akapata adha za kupanda ndege za abiria za nchi nyingine huenda angetia akilini na kupambana na mafisadi wake walioua Air Tanzia. Unashangaa ndege tu? Mbona hata hospitali zetu zinatelekezwa na wanapougua wanakwenda zao Apollo? Hiyo ndiyo Danganyika bint Bongolalaland usishangae. Huoni ajabu tunakosa pesa ya kuwekeza kwenye elimu lakini tunapata pesa ya chaguzi ndogo na kuwalipa watu wasiostahiki kama Edward Lowassa anayelipwa pesa ya kustaafu wakati aliachia ngazi kutokana na kashfa?
 
Mle majani mle mizizi hajalishi ndege ya rais lazima inunuliwe full stop. sasa mnalalamika nini?
 
wameagiza zile boeing 777 nasikia 5 zinakuja

Zikija lazima baadae ujekusikia palikuwa na ufisadi ambayo kwa sasa tunaichukulia kama nembo ya viongozi wetu waliopo madarakani
 
Mkomo mmezidi kilakitu mmelala usigizini fofofo wajanja wanawaamsha kumepambazuka hamtaki kuamka tuwafanyeje mkome kwanza mkija kwetu nikuandika tu dawa mkanunue kwenye vifamasi
 
Back
Top Bottom