Mkuu wangu samahani sana sikuweza kukuijibu haraka kutokana na wapuuzi fulani waliokuwa wakinihemea karibu kwa mashuzi ya mdomo.. Nashukuru sana tumefika mahala labda tuelimishane ktk maswala muhimu zaidi ya kijamii kati ya Uhafidhina na Wajamaa wa Kidemokrasia..Mkuu,
Nimefurahi sana kutambua rasmi kwamba Mkandara ni Mhafidhiana. Hili litatusaidia sana kubadilishana mawazo humu ki-tikadi. Nadhani unakubaliana na mimi kwamba Siasa za vyama vyetu Tanzania – CCM, Chadema, CUF, etc, haziendeshwi kwa itikadi. Lakini tuliache hilo kwa sasa.
Kwanza kuanzia, nakubaliana na wewe kwamba Uhafidhiana na ubepari ni vitu viwili tofauti, ingawa wengi hawalifahamu hilo. Lakini muhimu lingine ni kwamba, ubepari na soko huria ni vitu vyenye uhusiano tu, lakini havifanani, kwani Soko lipo katika mifumo mingine yoyote, kinachobadilika chini ya mfumo wa ubepari ni kwamba tu, soko sasa linakuwa la ‘huria'.
Lakini kabla sijaenda mbali, naomba kujitambulisha rasmi leo kwako kama Mjamaa wa Kidemokaria (a Social Democrat). Kwa maana hii, wakati wewe ni muumini wa mrengo wa kulia, mimi ni muumini wa mrengo wa ‘kushoto-kati', kwa kuendana na mpangilio wa itikadi hapa chini, ambapo eneo la KATI ni lile kati ya Uliberali na Ujamaa wa Kidemokrasia likiwa ndio mrengo wa kati, ambayo pia ndio itikadi ya Chadema.
Ukomunisti>Ujamaa=>Ujamaa-wa-Kidemokrasia=Uliberali=>Conservative Liberals=>Uhafidhiana
Sisi na nyinyi tuna tofauti nyingi za msingi, lakini muhimu zaidi ni kwamba pia tuna mambo mengi ya msingi tunayofafana. Naomba unielewe naposema SISI sina maana ya CCM,kwani CCM haina dira. Nikisema sisi maana yangu sisi waumini wa itikadi ya ujamaa wa kidemokrasia, itikadi ambayo bado hakuna hata chama kimoja Afrika inaifuata.
Nianze na tofauti kati ya sisi wajamaa wa kidemokrasia na nyinyi wahafidhiana: Sisi na nyie tunatofautiana juu ya kiwango cha ushiriki wa serikali katika umma na uchumi, kupitia aidha huduma za kijamii kama vile afya elimu, n,k, au mashirika ya umma, katika shughuli za utoaji wa huduma na na uzalishaji. Nyinyi mnahimiza sekta binafsi kuwa mstari wa mbele zaidi, na ikiwezekana, serikali kutojiingiza kabisa. Ni wenzenu chini ya itikadi ya "Conservative Liberals", ndio wana ka-uvumilivu kidogo na serikali katika masuala haya, Sio nyinyi. Lakini pamoja na tofauti hizi, sisi na nyinyi tunafana katika kitu kimoja cha msingi sana: Sote tunaamini juu ya umuhimu wa kuwepo kwa mfumo wa kibepari, na tunapinga itikadi za kijamaa na kikomunisti ambazo lengo lake kuu ni kuusambaratisha na kuutokokomeza mfumo wa kibepari katika jamii.
Suala la muhimu sana kusisitiza hapa ni kwamba, sisi "Wajamaa wa Kidemokrasia", tunaamini umuhimu wa Ubepari, ili mradi tunapewa uwezo wa kuukemea pale unapoenda mrama - hasa pale ubepari unapoumiza watu wa hali ya chini. Iwapo tunapata nafasi ya kuunda serikali, ni muhimu kwetu sisi ubepari utuvumilie, kwani ili kuepusha chuki kama zile za kikomunisti au Kijamaa dhidi ya ubepari, sisi hatuna tatizo na uwepo wake ilimradi serikali yetu inapata nafasi ya kuweka muundo thabiti wa kugawanya utajiri wa taifa, mfano kupitia kodi za aina mbali mbali, lakini pia uwepo wa huduma za kijamii – afya, elimu, makazi n.k, kwa wananchi wote wasiojiweza. Hilo likishindikana, sisi na ubepari hatuwezi kukaa meza moja kwani tuta twangana ngumi.
Sasa tuje kwenye hoja yako nyingine, pale unaposema:
.
Itikadi nyingi za kushoto, ikiwa pamoja na yetu ya Ujamaa wa Kidemokrasia zinakerwa na sera zenu nyingi ambazo kwa kweli hazijali watu maskini katika jamii. Sera zenu nyingi zinachangia sana kuongezeka kwa pengo kati ya watu wa kipato cha juu na kipato cha chini. Lakini hamkosi kuja na hoja kukinga msimamo wenu. Mnadai kwamba – pengo kati ya watu wa juu na wa chini ni kichocheo muhimu kwa wananchi kufanya kazi kwa bidii na kuongeza ubunifu ili na wao wafanikiwe katika maisha. Na ndio maana, in the same vein, mnaamini kwamba huduma za bure za serikali zinajenga muundo unaolea wavivu, ambao wanaishi kwa kutegemea government handouts. Ni kwa sababu hizi, nyinyi huwa hamkubaliani na huduma bure za afya, elimu, n.k, kwa umma.
Kuna hoja yako nyingine unasema kwamba:
Hoja hii ni ya kawaida sana miongoni mwenu, na inasisitiza kwamba ni muhimu kwa serikali kuwaachia wananchi wachague/wawe na choice, sio kuwafunga wategemee huduma za serikali pekee. Suala hili kwa kiasi fulani nakubaliana nalo, kwani ushindani ndio msingi wa ufanisi. Lakini kwa kiasi fulani nina reservation juu ya suala hili katika mazingira yetu ya Tanzania.
Naomba nikuulize:
Je kwa Mtazamo wako, katika mazingira ya Tanzania ambako tuna hospitali nyingi tu za binafsi, mfano kwa Dar-es-salaam zipo Agha Khan, Hindu Mandal, TMJ, Trauma Center, Regency n.k, kwanini hatuoni wakazi wengi wa Dar-es-salaam wakifurika kwenye hospitali hizi, na badala yake wanafurika kwenye hospitali za Mwananyamala, Ilala (Amana)na Temeke, kiasi cha kulala hata sakafuni wakati kuna vitanda wazi vingi tu Agha Khan, Hindu Mandal, TMJ, Trauma Center, Regency?
Unapendekeza suala la mfuko maalum wa ruzuku ambapo hospitali binafsi ambazo zitaweza kutoa huduma kwa gharama karibia na bure, kama sio bure, zitapewa fedha kutoka katika mfuko huu. Hili ni wazo zuri sana. Lakini je, hauoni kama hapo ni mgongano wa ki-itikadi? Iwapo unagombea uongozi, kwa msimamo huo, wahafidhiana hawatakupa kura, kwani, suala la mfuko wa ruzuku ya afya maana yake ni Serikali kuendelea kuwepo katika sekta hii, kwani hizi bado ni fedha za walipa kodi. Vinginevyo, tafisri yangu kuhusu hoja yako ya mfuko wa ruzuku ya afya ni kwamba, ni muhimu kwa serikali kuendelea kushiriki kutoa huduma za afya, lakini njia ya ruzuku ya afya, ndio njia ya ufanisi zaidi, kwani njia hii itaipunguzia serikali mzigo (walipa kodi), tofauti na mfumo wa sasa wa serikali kutoa huduma za afya moja kwa moja, ambao unaendeshwa kwa ufanisi wa hali ya chini sana. Nakubaliana na wewe katika hili.
Vinginevyo nakubaliana na wewe kwamba matumizi ya ovyo ya serikali ya sasa, katika vitu visivyokuwa na maana yamechangia sana nchi kufilisika, hivyo kuathiri shughuli nyingi sana za kiuchumi na kijamii zilizokuwa chini ya serikali.
Kwanza kabisa naomba nikusahihishe ktk Ubepari maana hapa hili swala la Soko huria ni Azimio lililopitishwa majuzi tu ktk kuboresha nguvu ya Ubepari lakini Ubepari ulikuwepo toka enzi za mitume kina Abraham wakichunga kondoo na kuwauza nchi za jirani nao wakirudi na makasha ya dhahabu na kadhalika. Mesopotamia ilijengwa kwa biashara kubwa na elimu yetu letu asili yake imetoka huko..Ubepari kama ubepari una athari zake na ndio maana miiko inatakiwa kuwepo pasipo kujali Uhafidhina wala Ujamaa maana tunapozungumzia Biashara sidhani kama Ujamaa wa leo unapingana na dhana ya biashara na soko huria isipokuwa kwa uzito wa masharti ndipo tunapogongana...
Sasa nirudi ktk Uhafidhina wangu, binafsi kitu cha mwanzo natazama TULIPOTOKA.. sababu ya kuutaka Uhuru wetu na kisha baada ya hapo natumia Uhafidhina wangu kuweza kuulinda Uhuru kama haki yangu maana tatizo la Wajamaa mara nyingi husahau kwamba HAKI (Justice) na UHURU (Freedom) ni wa WATU sio wa viongozi au serikali. Na hawa watu wanatakiwa kulindwa kwanza kabla hujatazama nje ya mipaka hii. Ujamaa kwa aina fulani unataka kuwapangia watu maisha, kuwapangia Uhuru wao na kuwapangia hata elimu na afya zao kama vile wakati wa Nyerere ukimaliza darasa la 14 unaambia wewe unakwenda UDSM kusomea Udaktari wakati hukutaka kuwa Daktari bali Lawyer. Ujamaa wa demokrasia bado nao unawapa wananchi Haki na Uhuru kwa mafungu, hivyo Mwananchi anakuwa sii Huru bali Uhuru wake ni wa kupakuliwa ktk sahani kama unanunua biriani pale Chef Pride..Ujamaa unajenga fikra za Uhuru wa serikari au chama iliyoingia madarakani kama ndiye mdhamana wa Uhuru na Haki ya wananchi. Na ndio maana hamtaki kuondoka madarakani mnaposhindwa huwa kazi sana kuwaondoa..
Umezungumzia swala la Uhafidhina kuwakera watu wa mrengo wa kushoto na kati ati kwamba Uhafidhina hautazami watu maskini.. Kweli tunawakera lakini kwa sababu hamtazami HULKA ya binadamu na walivyojaaliwa. Katika Uhafidhina hatuamini Umaskini kuwa ni kilema au ugonjwa sugu bali ni mtu kutowezeshwa ktk hali na mali. hakuna mtu aloumbwa maskini wala kuomba kuzaliwa maskini..Mtu yeyote akipewa ELIMU bora bila shaka utapata kazi nzuri na maisha ya binadamu yanategemea kufanya kazi. Mwenyezi Mungu alisema sisi wote watoto wa Adam - Tunaishi kwa jasho letu.
Hivyo, mnapomwandaa biandamu kuboresha maisha yake ni jukumu la serikali kuhakikisha linaweza sera bora za kuzalisha ajira ua Uwekezaji..Uhafidshina unatambua hilo kwanza na Uhafidhina hauweki binadamu ktk makundi kama mnavyofikiria, japokuwa yapo kweli lakini tunachoamini ni kwamba kila mmoja wetu ameumbwa na uwezo na kipaji na anastahili kupewa nafasi kuwezeshwa na atafika popote anapotaka kufika bila kumtazama kama maskini au kilema.
Ujamaa tatizo lake unalea watu ktk umaskini wanatambua umaskini wa watu kama kilema vile.. na kusema aaah maskini hawa tuwasaidie..hivyo kuwalemaza watu hawa ktk umaskini kwa vilio na kuonewa. Tabia ya kuwalea watu kama maskini kunawajengea ukungu akilini wakaamini na kukubali matokeo hivyo wataishi kama maskini wakitegemea kusaidiwa. Haya ndio mazao ya Ujamaa na demokrasia. Tanzania leo ni mfano mzuri sana wa Ujamaa na demokrasia maana wananchi wamekubali kushindwa baada ya serikari kutowafikiria kabisa wao bali wageni ambao wanakuja nchini kuwekeza. Uhafidhina unakupa Ushujaa na ujasiri wa kusimama na kupiganisha malengo uloyaweka, unakupa Haki na Uhuru wewe mwenyewe kuamua unataka kufika wapi hakuna vikwazo bali kikwazo utakuwa wewe mwenyewe.
Kwa Tanzania yetu ya leo hii, hajtujui tumesimama wapi wala tumetoka wapi.. hatujui na ndio maana hatuna hata Historia ya Uhuru wetu isipokuwa kwa Udini na Ukabila..Haya tukiweka na mchanganyiko wa kukubali Ubepari wakati bado kiimani Watanzania wengi ni Wajamaa au Liberal wamekosa HOPE kabisa... Hivyo ili nao watoke wameona UFISADI ndio njia pekee ya kutokea maana serikali haijui imesimama wapi..Kina JK kwa kuchanganyikiwa hawaoni ubaya kwa mwenyezaji kutoka nje ambaye kwa aina fulani anarudhisha UKOLONI mamboleo kuwekeza nchini maadam ati anakuza GDP..Na mimi mhafidhina sikubaliani na uwekezaji wa wageni- GDP nitaikuza mimi mwenyewe toka pale nilipo hata kama ilikuwa -20 ndipo naweza kujipima uwezo wangu kuzalisha..
Sasa Tazama, Nyerere ambaye alikuiwa Mjamaa haswa alifanya nini? alikataa kuwaleta wawekezaji nchini kuchimba madini yetu akisema yabakie huko chini hadi vijana wake watakapoweza kushimba wenyewe.. Huyu Mjamaa lakini katumia Uhafidhina ktk kupinga kukoloniwa tena..Ufafidhina kwa nchi kama Tanzania unautazama kwa mazingira tulipata UHURU wetu, nini zilikuwa itifaki zetu na malengo gani tuloyaweka while fighting the power..Mawazo hayo yanatakiwa kuenziwa na ndipo uhafidhina wangu unapotulia kama maji mtungini..
Kuhusu swali lako la wagonjwa wanaokwenda Mwananyamala, Temeke na Ilala ni mpango wa serikali ambao unawataka wagonjwa waende kwanza Hospital zao kisha wanakuwa reffered Muhimbili au hospital hizo. Huu ndio utaratibu uliopo na ndio maana unaona watu wengi wanakwenda kwanza ktk Hopitalk za majimbo yao kabla hawajapelekwa za Kitaifa. Mimi sioni tatizo kabisa hapa mkuu wangu, huu ni mpango mzuri sana na umeondoa sana mlindikano wa watu Hospital kuu. Isipokuwa tatizo linakuja kwamba hizo Hospital za Temeke, Ilala na Mwananyama zinatakiwa kuboreshwa zaidi ili zipate kuwa na vitanda vingi zaidi..
Halafu kama kweli huwa zimejaa lakini kuna vitanda Muhimbili au AghaKhan viko wazi basi hii inaonyesha mipango mibovu ya ushirikiano baina ya hizi Hospital maana Huku majuu kuna utaratibu mzuri sana baina ya daktari wako na Hospital zote zinazohusiana na maradhi yako. Na sababu nyingine inaweza kuwa gharama maana kutokuwepo mfumo bora wa tiba unajenga matabaka ya wagonjwa ayani asiye na uwezo aende Ilala, Temeke na Mwananyamala aliki akiugua Mchambuzi hupelekwa Muhimbili au Lugalo moja kwa moja.
Ndipo mimi napopingana na mpango nzima wa Afya nchini na kusema unajenga matabaka. Wahafidhina hawawezi kunipinga mimi naposema serikali itoe ruzuku kwa wananchi.. Hata kidogo labda huyo mhafidhina kichaa ambaye hafahamu tumefika hatua gani.. Mkuu wangu bado kabisa tupo ktk Transition ingawa kina JK na wasomi wetu wanadai tumeisha toka huko sasa tunaelekea ktk Transformation. Kwanza kabisa Uhafidhina unajali AFYA ya wananchi na pengine tunaweza sema kuliko hata wajamaa kwa sababu tunaenda na mahesabu. Sasa unapokuwa ktk Transition unakutana na vikwazo vingi na kimojawapo ni kwamba wananchi wenyewe wazawa hawana uwezo wa kujenga majengo makubwa kama Hospital iwe hata ya Mwananyamala.. sii rahisi, hivyo hatuwezi kudai hii ni biashara maana majengo haya siyo biashara isipokuwa watoaji huduma za AFYA. Na ndio maana unaona tunakubali sana kutoa fedha za uwekezaji ktk majengo ya Hospital lakini Hospital yenyewe inajiendesha ikiwa na uongozi wake kama shirika binafsi bila kuingiliwa na wanasiasa kama tunavyoona Tanesco. Hospital hizi zinafanya biashara na kuajiri madaktari bingwa hivyo kuwapa mtihani mkubwa viongozi wake hata kama mteja wake mkubwa ni serikali yenyewe - Umenipata hapo!.
Na uzuri wa Demokrasia ni pale pande hizi mbili zinapopambana kisi kwamba hata sisi wahafidhina tunakubali baadhi ya huduma kama hii hasa inapolenga AFYA na wananchi tunachokipinga tu ni kama huduma hii itamgharimu mwananchi zaidi ktk kodi na afadhali angehudumiwa na Private hospital akilipa mwenyewe. Kwa hiyo kwa nchi nyingi za Kibepari zimegundua kwamba huduma kama asfya ni fedha ile ile inatoka mfuko huu na kwenda mfuko mwingine..gharama ambayo ungeilipa wewe kwa tiba serikali inachukua fungu hilo na kukulipia wewe toka ktk kodi yako na ndio maana Canada na nchi nyingi zinazotoa huduma hizi tuna kodi kubwa sana kutokana na maswala ya Afya na Elimu kuwa bure..
Marekani bado wana ugoinjwa wa kufikiria kwamba watumishi wa serikali ni wazembe ukiwapa AFYA na ELIMU wanaziboronga na kuwa huduma mbaya sana kwa sababu in general mfanyakazi wa serikali hana uchungu..Lakini nadhani baada ya kutazama nchi nyingine wanagundua kwamba elimu na AFYA ktk nchi hizo imezidi kuboreka zaidi baada ya kuzifanya mandatory na HAKI ya mwananchi.. na kinachofunga zaidi ni imani yetu ktk HAKI na UHURU. Tunataka mtu achague yeye mwenyewe anataka kusomea nini, shule gani atibiwe na daktari au Hospital gani badala ya kuwa reffered to kama tunavyofanya Tz. Na huwezi kutatua tatizo hili bila kuujua mfuko wa mtu isipokuwa ukimpa mtu jukumu hilo anajua vizuri uwezo wake hivyo kujipangia malengo na sio kupangiwa..
Duh! nimeongea sana mkuu wangu tutaendelea baadaye..