Unajua tumefika mahala jamani tutazame kwanza maslahi ya wananchi. Sote hapa tunaweza kubaliana na madaktari ktk hoja yao lakini maamuzi waliyofikia kuyafanya kusema kweli binafsi siyakubali kwa sababu wanawatumia wananchi maskini ya Mungu wagonjwa kupigania haki yao. Ni sawa kabisa na Al qaeda ambao wanaenda angusha jumba la Twin Tower ili ipate kusikilizwa na serikali ya Marekani kwa madai ya kuwatakaWaamerika waondoke Saudi Arabia.
Ukiweza kunisoma mtazamno wangu nadhani hatutakuwa na ubishi mkubwa hapa. Mimi ningeomba san madaktari pamoja na asasi zote za utumishi na ajira iwe serikalini au masirika ya Umma waungane na madakatari kufanya maandamano ambayo yatakuwa ya Taifa zima kupinga na kuweka madai kama yao maana sehemu zote za utumishi zina matatizo hayo. Lakini wagonjwa wataendelea kuhudumiwa na hasa wale walioko ICU, wodi ya watoto, na wanawake wajawazito, HIV na cancer, pamoja na upasuaji.
Nasikitika tu kusema kwamba wengi ya watu hapa wanadshabikia lakini hawajui madaktari wanalipwa kiasi gani na kwa mwezi daktari anaweza kuingiza kiasi gani. Nashukuru Mungu mimi nina jamaa zangu ambao ni madaktari na najua vizuri jinsi wanavyotengeza mbali kabisa na mishahara. halafu kibaya kuliko yote ambacho kimenisikisha zaidi ni kugoimbea ongezeko la Posho!...
Jamani posho kweli unaweza ijengea hoja na kufanya mgomo au ilitakiwa usifike ktk vikao ambavyo ulitakiwa kufika na kulipwa Tsh 10,000. Yes, kama kuna dawa ya kutaka posho zaidi acha kuhudhulia vikao vya posho unless serikali inakulipa kiasi unachokitaka. Na kama swala la viongozi mkwenda India.. msiwapokee waacheni watafute safari za India hata wakiumwa mafua halafu watawajibu wananchi..
Kusema kweli nimezisoma sababu zote walizozitoa madaktari haziniridhishi kiasi cha wao kugoma kutoa huduma kwa wananchi kwa madai ya haki yao. Hivi kweli kuna mtu anaweza kunipa hesabu kamili ya Daktari anatakiwa kulipwa kiasi gani? hivi kweli tunaweza kuweka mahesabu ya fedha kwa malipo ya Madaktari au Walimu na kusema huu ndio mshahara au posho wanazotakiwa kupewa!. Mimi sidhani ila najua fika kwamba mishahara yote nchini haifai na haitoshi ktk sekta zote za utumishi na kwa ujumla wa watumishi hawa kupitia Union zao wangepanga maandamano ya pamoja na wakaomba kibali ikajulikana wazi kwamba maandamano ya madaktari yatatokea siku kadhaa wakadhaa..
Hapa Canada mgomo wa madaktari ni kinyume cha sheria. Daktari hawezi kugoma kwenda kazini na kwa kupitia union yao wana hatua kama 4 za kupitia kbala ya kufikia makubaliano... mara nyingi kama sii zote huwa hawafiki hata hatua ya 3 na kama kuna mgomo basi huenda kwa vitengo lakini zipo sehemu ambazo hawaruhusiwi kabisa kuziacha wazi bila kuhudumia. Na pengine kinachowasaidia hapa ni kwamba serikali inalipa mishahara mikubwa kuliko sehemu yoyote ya binafsi iwe udaktari au hata front desk secretary ktk ofisi ya serikali.
Madaktari wanaweza kuomba ongezeko au punguzo la kazi kulingana na masaa wanayofanya kazi. Mishahara yao imepangwa kwa saa ambazo wanakuwa kazini na the more wanavyokuwa na masaa mengi ndivyo mshahara wake unapanda kama Ma pilot wa ndege.. Hivyo pengine tubadilishe mfumo wa mishahara iwe daktari atalipwa Tsh 5,000 kwa saa, kisha wajitume wenyewe kulitumikia Taifa kwa kuweka masaa mengi saidi wanaongeza pia pato lao.
Kwa hiyo kufanya mjadala hu uwe mfupi, Nyie wananchi mnaowaunga mkono madakati? kwa nini hamko nao pamoja kufanya nayi mgomo kama wenzenu. Kwa nini Tanzania ya leo kila mtu anabeba msalaba wake. Ule umoja wenye nguvu umeishia wapi kiasi kwamba mnawatazama tu madaktari wakigoma na kesho wakifunkuzwa kazi mtawacheka na kuwaita wajinga, na hata wakiomba maji ya kunywa majumbani mwenu mnawafukuza..Je huu sii unafiki wa Mtanzania!